Mkandarasi wa SGR (Yapi Merkezi) anawaondoa Wafanyakazi kwa gia ya kuwapa likizo ya lazima, pia hajaingiza malipo ya NSSF

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Sisi Watumishi wa SGR ambao tupo chini ya Mkandarasi Mkuu wa mradi huo, Yapi Merkezi tunasikitishwa na kitendo cha Muajiri wetu kupunguza Wafanyakazi kwa gia ya kuwapa likizo ya lazima.

Uongozi wa SGR Lot One inayoanzia Dar es Salaam kwanza ulitutaka kwenda likizo ya miezi minne, wengine wanaambiwa waende miezi sita na wengine zaidi ya hapo. Tulivyopiga kelele wamepunguza muda wa likizo na kusema ni wa mwezi mmoja lakini kiuhalisia hiyo ndio njia ya kuondolewa mazima.

Lakini kinachotokea baada ya hapo ni kama vile ndio inakuwa gia ya kuondolewa kwenye mfumo wa ajira, kuna wenzetu zaidi ya 200 hayo yamewakuta.

Kibaya zaidi wanafanya hivyo bila kuwa wametukamilishi stahiki zetu za NSSF, tumekuwa tunakatwa katika mishahara kwa ajili ya kiasi hicho kipelekwe NSSF lakini tukiangalia kwenye mifumo inaonekana mara ya mwisho kuingiziwa fedha hizo ni zaidi ya miezi 10.

Tunaomba Serikali ambao ndio wamempa tenda Yapi Merkez afuatlie kinachoendelea kwani hii sio mara ya kwanza kuripoti kuhusu Yapi kutolipa Watumishi wake na kutowaingizia malipo ya NSSF wakati tunakatwa kama kawaida kwenye mishahara yetu.
 
Soma vizuri mkataba wako wa ajira. Mwajiri ana haki ya kukupumzisha pale asipohitaji huduma yako
 
Noma imeanza huko!?
Tafadhali hamia kule kwa wakandarasi wa kichina chap pindi unapumzishwa.
Ila, mpange afisa mwajiri aweke jina lako ktk mkono wake wa kulia.
 
Huu ni wizi kama sheria za nchi zinavyosema ukimuajiri mtu hata kama ni timely projects lazima NSSF michango yote uende.Kwanini hawakupeleka ikatunzwe kule! ? Wahini haraka kwenye mamlaka za idara ya Kazi na ajira jambo hili lifuatiliwe? Mtalia au mmeshalizwa
 
Sisi Watumishi wa SGR ambao tupo chini ya Mkandarasi Mkuu wa mradi huo, Yapi Merkezi tunasikitishwa na kitendo cha Muajiri wetu kupunguza Wafanyakazi kwa gia ya kuwapa likizo ya lazima.

Uongozi wa SGR Lot One inayoanzia Dar es Salaam kwanza ulitutaka kwenda likizo ya miezi minne, wengine wanaambiwa waende miezi sita na wengine zaidi ya hapo. Tulivyopiga kelele wamepunguza muda wa likizo na kusema ni wa mwezi mmoja lakini kiuhalisia hiyo ndio njia ya kuondolewa mazima.

Lakini kinachotokea baada ya hapo ni kama vile ndio inakuwa gia ya kuondolewa kwenye mfumo wa ajira, kuna wenzetu zaidi ya 200 hayo yamewakuta.

Kibaya zaidi wanafanya hivyo bila kuwa wametukamilishi stahiki zetu za NSSF, tumekuwa tunakatwa katika mishahara kwa ajili ya kiasi hicho kipelekwe NSSF lakini tukiangalia kwenye mifumo inaonekana mara ya mwisho kuingiziwa fedha hizo ni zaidi ya miezi 10.

Tunaomba Serikali ambao ndio wamempa tenda Yapi Merkez afuatlie kinachoendelea kwani hii sio mara ya kwanza kuripoti kuhusu Yapi kutolipa Watumishi wake na kutowaingizia malipo ya NSSF wakati tunakatwa kama kawaida kwenye mishahara yetu.
Huyu yapi lazima atalipa hizo statutory rights kwa mujibu wa sheria…. Hana ujanja wa kukimbia au kukwepa

Btw, Mnatamani sana kuweka negativities kwenye efforts ya uwekezaji mkubwa unaoendelea

Au basi
 
Back
Top Bottom