Mkandarasi wa ujenzi wa SGR Tanzania, Yapi Merkezi adaiwa kuwa na hali ngumu kiuchumi

Mkandarasi wa ujenzi wa SGR Tanzania, Yapi Merkezi adaiwa kuwa na hali ngumu kiuchumi

Hali ya Mkandarasi YAPI MERKEZ ya Uturuki ambaye anajenga reli ya SGR si shwari hata kidogo kwa maana ameishiwa fedha na kushindwa kuwalipa Wazabuni wanaotoa huduma katika mradi huo. Wazabuni ni pamoja na wanatoa ya magari, Mashine na vifaa mbalimbali ya kujengea reli hiyo.

Hadi sasa imefikia miezi saba bila Wakandarasi hao kupata malipo yao huku Wazabuni hao wakilalamika kwamba kutokana Makadarasi hiyo kushindwa kuwalipa na wao wanashindwa kuwalipa Wafanyakazi wao ambao ni waendasha mitambo kama Escavetor, madereva wa malori, mabasi nk. Hali kadhalika Wazabuni hao pia wamedai kwamba wanashindwa kuwasilisha na kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na kutokupwa.

Wazabuni hao wameendelea kudai kwamba wamefanya juhudi mbalimbali za kukutana na Uongozi wa Yapi Merkez lakini hawajafanikiwa kutokana na uongozi huo kutoa visingizio vya COVID 19. Hata hivyo baadhi ya wazabuni wamedai wamefikisha malalamiko yao kwa Shirika la Reli nchini (TRC) lakini hadi sasa hawajapata ufumbuzi wowote wa malipo yao.

Kutokana na hali hiyo Wafanyakazi YAPI MERKEZ nao mwezi huu wa Saba watalipwa mshahara nusu.
Hiyo Reli haiwezi Kwisha ng'o...Kenyatta na akili zake zote za biashara na Uchumi mkubwa wa Kenya ameshindwa kumalizia SGR yake, itakuwa Huyu Kilaza Kamasi wa Kolomije🤧
 
Mwezi Nov Mwaka jana kwa hesabu zipi? Mradi umeanza May 2017 na ni mradi wa miezi 36(Miaka 3)...hujaweka atleast 3 month ya Mobilization...hio Nov mradi unaishaje?...sometime tuache unafiki nafiki
Tarehe iliyoandikwa ni hiyo hapo kwenye bango. Kama kulikuwa na nyongeza ya muda ni mpaka lini?, mwaka umepita sasa
Screenshot_20201216-202942_Facebook.jpeg
 
Mwezi Nov Mwaka jana kwa hesabu zipi? Mradi umeanza May 2017 na ni mradi wa miezi 36(Miaka 3)...hujaweka atleast 3 month ya Mobilization...hio Nov mradi unaishaje?...sometime tuache unafiki nafiki
Ndio umeshakwama sasa
Kazi za Umma mnataka kuzifanya kama mnajenga Nyumba zenu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Chuki kwa JPM haitafanya Tanzania isiendelee.
 
Waturuki tupo nao mtaani daily tunakula nao fegi.
 
Wanasaccos mnahangaika sana. Miradi hiyo yote itamalizika salama salimini. Mjiandae kufa kwa stress baada ya kukamilika.
Stress lazima. Hayo madeni mnayoingia mnadhani ni dunia hii?
 
Waturuki waliopo kwenye mradi wanaishi Kama wamekuja tour Yaan,full Bata level ya [emoji294][emoji294][emoji294][emoji294][emoji294]..yaaann...kwa jinsi wanavyolipana..
Wamejisahau kabisa.. wazawa na sub company wanakoma na kusanda kuhusu malipo...
 
Back
Top Bottom