Mkandarasi wa Uturuki, Yapi Merkezi athibitisha pengo la $1.8bn katika ufadhili wa Tanzania SGR

Mkandarasi wa Uturuki, Yapi Merkezi athibitisha pengo la $1.8bn katika ufadhili wa Tanzania SGR

Hii Tenda bora angepewa Mchina rafiki yetu wa dhati kwa miongo mingi.Angetupa mpaka mabehewa na vichwa vya kisasa vile vya mchongoko.
Kwanza sio swala la urafiki Bali ana hela.Kina Kadohosa walilazimisha sana huyu mkandarasi wao apewe kazi nyingi wakati hana pesa , kiufupi amefilisika Sasa anatafuta wa kumuuzia mradi au wa kumpa Mkopo wa kustabilise uwezo wake Ili amudu kazi.
 
Wakati serikali ya Tanzania ikiendelea kuficha ukweli, Kampuni ya ujenzi ya Uturuki ya Yapi Merkezi imeripoti pengo la dola bilioni 1.8 (zaidi ya shilingi trilioni 4.5 za kitanzania) katika ufadhili wa mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa nchini Tanzania huku ikiendelea kuwezesha Dodoma kutafuta ufadhili wa mradi huo kote Ulaya.

Makamu Mwenyekiti wa Yapi Merkezi, Erdem Arioglu, ambaye hivi karibuni alimuongoza Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na ujumbe wa Serikali katika nchi za Hispania, Sweden na Poland kutafuta ufadhili wa mradi huo, aliliambia gazeti la The EastAfrican kuwa harakati za kuchangisha fedha hizo ni ufuatiliaji wa ahadi mbalimbali zinazofikia dola bilioni 2.2. kuelekea mradi wa dola bilioni 10.4.

Alikanusha kuwa Yapi iliongoza misheni hiyo walipochunguza Mpango B - ufadhili mbadala ili kushughulikia matatizo yake yenyewe ya mtiririko wa pesa - lakini walifanya hivyo katika nafasi zao kama mkandarasi mkuu kwa awamu nne za kwanza za mradi.

Source: THE EASTAFRICAN
Turkey contractor confirms $1.8bn gap in funding Tanzania SGR
 
kwa maana hio ni sawa na kuleta fundi akujengee nyumba halafu kila kitu agharamikie yeye na sio wewe mwenye nyumba kwa unavyo manisha
Mwenye nyumba unamlipa pesa badala aziingize kwenye ujenzi ikiwa ni pamoja na kulipa mafundi na vibarua anaenda kulipia Madeni kwingine mradi wako unakwama.

Usiwe mjinga siku zote cheap is expensive ndio maana kigeso Cha mkandarasi mojawapo ni financial stability yake.
 
Mkandarasi ana jenga kwa hela za nani?
Anajenga Kwa hela yake na ya serikali,kama amefilisika hawezi Jenga na akilipwa za serikali anaenda kulipia wanaomdai huko kwao ilhali Wafanyakazi na subcontractors wanabakia kulia njaa mradi unakwama.

Punguza upumbavu ndugu ndio maana kigeso Cha uwezo wa kigedha wa mkandarasi ni muhimu kuliko kawaida.
 
Huyo Yapi kapewa Lot 4 juzi tu hapa huku tayari kuna migomo ndani yake na anasuasua kule Lot 3!

Yaani mkandarasi aliye nyuma kwa 10% kwenye Lot 3 mnampaje Lot nyingine kama siyo nyie ndiyo tatizo.

Kakubali kutumiwa tu na wanasiasa ila shida ni serikali yenyewe kutopeleka pesa kule na wataendelea naye sababu wameona ni toilet paper.
 
Tunaseme hana hela, na selikali nayo haina?

Mnapokuwa machawa msinye akili zote.

Ni hivi bwana lichawa, mamako hana hela za huu mradi
 
Kwa miundo mbinu yafaa sasa tushikane na Mchina tu.Huko Serikalini yapaswa wajue CCM na Communist Part ni Pete na Kidole hivyo wasingetuacha njiani.
 
Ni Bora expensive but sure ila cheap siku zote lazima usue sue ,waliojenga wanafahamu hili.
Kwa sasa sijajua ni mradi upi mchina kaboronga.Standard ni standard tu ukiboronga kwenye kandarasi ni ngumu kupata kandarasi nyingine na project kubwa Mchina akubali kufeli.Ndio manake project zao nyingi ziko funded na Chines Government au China Exim Bank.
 
Tunaseme hana hela, na selikali nayo haina?

Mnapokuwa machawa msinye akili zote.

Ni hivi bwana lichawa, mamako hana hela za huu mradi
Yaani Serikali impe mkandarasi pesa badala ya ajenge harafu aombe malipo ndio imlipe? Toa upumbavu.

Na kjvunja mkataba ningumu na bahati mbaya mikataba hii ya Kimataifa Huwa inafanyiwa sattlements Kimataifa na ni ngumu ndio sababu atasubiriwa Hadi atengamae kifedha.
 
Back
Top Bottom