Mkanganyiko chanzo cha mgogoro wa Mgodi wa Msasa, Runzewe, Geita

Mkanganyiko chanzo cha mgogoro wa Mgodi wa Msasa, Runzewe, Geita

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wakati Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Pasikas Mulagiri akisema chanzo cha mgogoro uliotokea leo Januari 22, 2026 katika mgodi wa Msasa, Runzewe mkoani Geita umesababishwa na kujaa kwa maji yaliyoletwa na mvua, Ofisi ya Ofisa Madili Wilaya ya Mbogwe amesema chanzo ni mvutano unaohusisha kiwango cha umiliki hisa wa maduara ya uchimbaji.

Kutokana na mzozo huo, leo Januari 22, picha za video zilionyesha wananchi wakikimbia huku milio ya mabomu ya machozi ikisikika kuashiria polisi waliokuwa wakiwatanya wananchi kwenye mgodi huo.
Akizungumza kwa simu na waandishi wa habari akiwa jijini Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Paskasi Mulagiri amesema suala la mvutano wa umiliki kwa wa asilimia 50 kwa 50 lilishatatuliwa.

“Ule mgodi uko kwenye mbuga lililokuwa wanalima mpunga, kwa hiyo kiusalama wakasema kazi leo isifanyike ili watoe maji. Kwa hiyo mmiliki wa mgodi alitangaza kwamba mtu asiingie kwenye mgodi, sasa tangazo lile ndio lilizua taharuki.

“Tatizo sio umiliki wa 50 kwa 50, kwa sababu ilikuwa sorted na walishasaini mikataba, kwa sababu hata jana uchimbaji uliendelea, waliosaini 50 kwa 50 walichimba na ambao hawakusaini mkataba walibaki nje na hapakuwa na vurugu yoyote.

“Leo hakuna aliyeruhusiwa kuchimba, mweye mkataba hakuruhusiwa kuchimba na wasio na mkataba hawakuruhusiwa na sababu ndio hiyo niliyosema ni maji,” amesema Mulagiri.
Hata hivyo taarifa iliyotolewa na Ofisa Madini mkazi wa Mbogwe imesema chanzo ni mvutano unaohusisha kiwango cha umiliki hisa wa maduara ya uchimbaji.

“Baadhi ya wamiliki wa maduara wamekubali kusaini na kuendelea na kazi huku wengine wakikataa. Wakurugenzi wamechukua hatua ya kuzuia wale ambao hawajasaini mikataba wasiingie katika eneo hilo maalum lililowekewa uzio. Wachimbaji waliozuiwa kuingia wameanzisha fujo katika eneo la mgodi,” imesema taarifa hiyo.

Kuhusu hatua zilizochukuliwa, Ofisa madini amesema baada ya malalamiko haya kumfikia Mkuu wa wilaya na KU ya wilaya, waliitisha Kikao na kuunda Kamati iliyojumuisha pande mbalimbali ikiwemo FEMATA, Ofisi ya Madini, Mwanasheria ofisi ya DC. Kamati hii imekusanya maoni toka pande zote na yatawasilishwa kwa Mhe DC ili yaweze kufanyiwa kazi.

“Polisi wameendelea kuimarisha ulinzi katika eneo la Barabara kuu iendayo Rwanda inayopita katika eneo la mgodi na kuzuia uvunjifu wa amani unaoweza kutokea kwa raia wengine wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo.”

Ofisa huyo alidai kuna upotoshaji unnaoeleza kwamba vurugu zinazotokea kwenye mgodi wa Msasa ni kwa sababu wachimbaji wanalalamikia Serikali kuchukua asilimia Hamsini (50%) ya uzalishaji.
“Tunapenda kukanusha jambo hili la upotoshaji lenye nia ovu ya kuichafua Serikali na kutoa onyo kwa wale wote wanaofanya opotoshaji huo na hatua kali za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Vurugu zilizotokea kwenye mgodi huo ni kutokana na kutokubaliana mgawanyo wa hisa baina ya Wakurugenzi wa mgodi na Wamiliki wa Maduara,” amesema.
 
Nawashauri wachimbaji wafuate mamlaka za serikali kuepusha mgogoro zaidi.
 
Back
Top Bottom