Mkanganyiko katika Gharama za Vocha za Simu

Mkanganyiko katika Gharama za Vocha za Simu

Ninavyojua mimi Zain & Zantel wametoa matangazo kwenye magazeti yote kuwa bei ya vocha inabaki palepale.

Tigo na Voda wamenyamaza kimya ikimaanisha kuwa wamebariki kupanda kwa bei ya voucher zao.

Inakera sana kwa hawa wauza vocha,pamoja na matangazo yaliyotoka kwenye gazeti wanaendelea kuuza vocha kwa bei ya zaidi ya thamani ya vocha yenyewe.

Mimi binafsi nimekorofishana na muuza vocha alipotaka kunichaji 1100 kwa voucher ya 1000 ya Zantel. Huu ni wizi wa wazi makampuni husika yanatakiwa kuhakikisha wauza wote wanauza voucher kama zamani.
 
TCRA yapiga marufukuvocha kupanda
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 10th July 2009 @ 08:59

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imepiga marufuku wafanyabiashara wa rejareja kupandisha bei za vocha za kuongeza muda wa maongezi kwa maelezo kuwa hakuna kodi iliyoongezwa na serikali inayosababisha kupanda kwa vocha hizo. TCRA imetoa tamko hilo baada ya juzi kukutana na kampuni zote za simu na baada ya majadiliano ya kina ilibainika kuwa hakuna kodi ambayo inachangia kupanda bei kwa vocha hizo.

Mamlaka hiyo imeainisha kodi hizo kuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), imepunguzwa kutoka asilimia 20 hadi asilimia 18 hali inayolazimu thamani ya kodi kushuka. TCRA imeeleza kuwa licha ya serikali kuweka kiwango cha kodi cha asilimia 10 kama ushuru bado kiwango chake hakiwezi kubadilisha bei ya vocha hasa kutokana na kiwango cha VAT kupungua.

“Kwa hali hiyo hakuna mabadiliko ya bei kwenye vocha za maongezi,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na mkurugenzi mkuu wa TCRA Profesa John Nkoma. Profesa Nkoma alisema mamlaka yake inaendelea kushauriana na Mamlaka ya Mapato (TRA) pamoja na kampuni za simu kuhusu suala hilo.

“Hata hivyo, ilikubalika vocha zote lazima ziuzwe kwa bei iliyoko kwenye vocha husika na sio vinginevyo, tunawaomba wananchi wakatae kulipa kiasi zaidi ya kilichoko kwenye vocha,” alisema.

Wiki iliyopita, wananchi wameonja machungu ya kupandishiwa bei za vocha. Vocha ya Sh 500 iliuzwa kwa Sh 550, ya 1,000 iliuzwa kwa Sh 1,100 na ile ya 5,000 iliuzwa kwa Sh 5,500. Wauzaji hao wamekuwa wanadai kuwa wamepandishiwa na mawakala wanaouza vocha hizo kwa bei ya jumla, hali inayowalazimu kupandisha kwa vile wakiuza kwa bei ya sasa, hawapati faida yoyote.


Source: Habari Leo
 
"Hata hivyo, ilikubalika vocha zote lazima ziuzwe kwa bei iliyoko kwenye vocha husika na sio vinginevyo, tunawaomba wananchi wakatae kulipa kiasi zaidi ya kilichoko kwenye vocha," alisema.

Hiki ndicho kinachotakiwa, lakini mbona wananchi wenyewe hawatekelezi hilo? Na bado wanaendelea kununua vocha kwa bei ya juu?

Badala ya TCRA kuwakaba koo wauzaji wa rejareja basi iwakabe koo Hao mawakala wanaopandisha bei maana hao ndio chanzo cha vocha za simu kupanda bei.

Kwa hali ilivyo mpaka hivi sasa mimi nikiwa kama muuzaji wa vocha wa rejareja hakuna atakayeuza vocha hasa za Vodacom kwa bei iliyoandikwa na vinginevyo haziwezi kuuzwa kabisa. Si umesikia kule Mwanza kuwa wauza vocha wameanza mgomo kupinga suala la mawakala kuwapandishia vocha bei.

Aluuuuu hii imekaa vyema.
TCRA kaba koo mawakala sio wauzaji wa rejareja.
 
Hiki ndicho kinachotakiwa, lakini mbona wananchi wenyewe hawatekelezi hilo? Na bado wanaendelea kununua vocha kwa bei ya juu?

Badala ya TCRA kuwakaba koo wauzaji wa rejareja basi iwakabe koo Hao mawakala wanaopandisha bei maana hao ndio chanzo cha vocha za simu kupanda bei.

Kwa hali ilivyo mpaka hivi sasa mimi nikiwa kama muuzaji wa vocha wa rejareja hakuna atakayeuza vocha hasa za Vodacom kwa bei iliyoandikwa na vinginevyo haziwezi kuuzwa kabisa. Si umesikia kule Mwanza kuwa wauza vocha wameanza mgomo kupinga suala la mawakala kuwapandishia vocha bei.

Aluuuuu hii imekaa vyema.
TCRA kaba koo mawakala sio wauzaji wa rejareja.


Wakuu huku morogoro jana kuna jamaaa alichapwa kibao kwa kumuuzia vocha bei tofauti na ile halali.
Kwa hiyo kikubwa ni kuwalamba vibao tu kwenda mbele
 
Katika hili kuna unafiki mkubwa tu unaendelezwa na serikali. Kitendo cha kubadilisha mfumo wa kutoza kodi ya ongezeko la thamani katika usambazaji wa vocha kimeongeza gharama kwa wauzaji wa jumla.

Hivyo kama wauzaji hawa wanataka kuendelea kupata faida ileile ya mwanzo ni wazi wataongeza bei zao (kama hawawezi kupunguza matumizi) na vivyo hivyo kwa wauzaji wadogo na mwishowe watumiaji wa simu watanunua vocha kwa zaidi ya bei iliyoandikwa kwenye vocha. TRA wanalijua/wanapaswa kulijua hili lakini nadhani wameamua kuchagua unafiki!

Labda hapa hoja ni kiasi gani kimeongezeka na vipi ongezeko hilo linaakisi ongezeko la gharama lililosababishwa na mabadiliko katika mfumo wa kutoza kodi ya ongezeko la thamani.
 
Sunday, 12 July 2009 16:53
Na Benjamin Masese

WAUZAJI wa vocha za simu wamesitisha utoaji huduma hiyo siku chache baada ya tamko la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwataka wateja kununua vocha kwa mujibu wa bei zilizoandikwa juu ya kadi hizo.


Hatua hiyo imetokana na taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi TCRA, Bw.John Nkoma aliyeagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mawakala na wauzaji wa rejareja waliopandisha bei kinyume cha utaratibu.

Wakizungumza na Majira Dar es Salaam jana wafanyabiashara hao, walisema wameamua kusitisha huduma hiyo kutokana na bei wanayonunulia wao kuwa juu huku wao wakizuiwa kupandisha bei.

"Vocha zimepanda kutoka sh.450 hadi sh. 490 katika maduka ya jumla (mawakala) tofauti na ilivyokuwa awali hivyo haiwezekani tukafanya biashara kwa faida ya sh. 10, kinachotakiwa bei irekebishwe kuanzia kwa mawakala,"alisema muuzaji wa reja reja, Bw. Sadiki Ndege.

Alisema kuwa wao kama wauzaji wadogo wanashindwa kuelewa nani mkweli kuhusu bei halisi ya vocha hizo hivyo kuzitaka kampuni husika kubainisha bei halisi za vocha zake.

Alisema bei za jumla wanazouziwa na mawakala ni; Vodacom sh. 490, Tigo sh. 485, Zantel sh.480 na Zain sh.483 ambapo faida ni kati ya Sh.10 hadi 20.

Naye mteja mwingine, Bw. Godfrey Emanuel alisema wamelazimika kuachana na biashara hiyo kutokana na kulazimishwa kuuza bei isiyokuwa na faida kwao.

"Sisi tunazilaumu kampuni za simu kwani zinatambua kabisa kiwango kilichopanda na hata risiti za mawakala zinaonesha lakini wao wameshindwa kututetea badala yake wanatugandamiza," alisema Bw. Emanuel.

Duh! Hii ingefanyika nchi nzima si ingekuwa balaa, maana mtu anahitaji mawasiliano ya haraka anaenda kununua vocha anakuta hamna.

Nadhani hii inaweza kusaidia maana hawa mawakala hasa hasa wa VODACOM hatakaki kabisa kupunguza.
 
Toka suala la vocha kupanda bei kampuni za simu zimekuwa hazimsemi ukweli wala jambo hili...ukweli ni kwamba WAO WENYEWE WAMEAMUA KUPANDISHA KWELI BEI HIZO...
kilichotokea:
Miaka mingi seriklai imekuwa inapoteza mapato kwakuwa makampuni mengi ya simu yanadai kupata hasara au kuweka pesa kwenye upanuaji huduma na huduma za jamii...na mara zote Vocha zimekuwa nikitozwa VAT kabla ya bonus kwa superdealer..yaani operator huwa wanatoa 8% to 9% discount kwa superdealer ambaye nae huwapa either hiyohiyo wauzaji wa rejareja au pungufu, sasa siku zote TRA hatozi VAT kwenye hii bonus, that is kwa mfano vocha ya 2000, operator ataripa (2000-(2000*8%)*20%), kwahiyo hapa operator alikuwa anapata nafasi ya kumpa faida superdealer kidogo kwa kumuuzia kwa bei nafuu.
sasa serikali imeamua kuondoa huo utaratibu, ni kwamba kuanzia july 1, serikali itatoza VAT kwa thamani halisi (2000*18%),
hapo ndio operators walipopagawa...kwahiyo kwa akili ya kawaida tu unaweza ukaona tatizo liko wapi maana ile 8% ya discount nayo inaliwa..
Vodacom waliitisha Board na kujadili na wameshindwa kupata muafaka na kama kawaida yao wamepandisha bei na wameamua waivae serikali, tigo wameamua kukubali hasara na vocha ziuzwe kama ilivyo zamani, zantel bado hawajaamua kitu..zain pia bado hawajaamua pia.

ila ukweli ni kwamba makampuni ya simu yamekuwa wakwepa kodi wakubwa na sababu ni kwamba TRA mpaka leo haijajua jinsi gani ya kutoza kodi, kampuni nyingi zimekuja na mapendekezo tofauti lakini mpaka leo bado haijaamuriwa, ndio maana sasa TRA wameona pakuwabana ni kwenye VAT maana kule hawana ujanja...

lakini kwakushangaza wote na TCRA hawasemi hili...wanawasingizia wauzaji wa rejereja...
 
Aisee hapo umenena kweli. Ndio maana makampuni ya simu wako kimya wanatupooza pooza tu hasa Vodacom.
 
Back
Top Bottom