Mkapa alia na serikali mbili (2)

Mkapa alia na serikali mbili (2)

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
8,199
Reaction score
8,186
WanaJF,

Rais mstaafu wa JMT, ndugu Benjamin Mkapa, ametoa maoni hayo akiwa kwenye hafla fupi ya kuzindua vitabu vyenye hotuba zake zote za kipindi alichokuwa rais wa JMT.

Ndugu Mkapa amesema ili kuendeleza umoja na mshikamano wetu wa kihistoria, ni vyema Watanzania wabaki na muundo huu uliopo wa serikali (yaani serikali mbili).

Aidha, rais huyo mstaafu alitumia nafasi hiyo kutuasa Watanzania juu ya kuenzi amani na utulivu wetu hasa katika kipindi hiki cha kuandaa katiba mpya ya nchi.

My take,

Binafsi bado sijashawishika na wale wanao pendekeza serikali 3 mpaka sasa. Mara nyingi nikijaribu kufuatilia naona wengi wanao shabikia kufufuka kwa Tanganyika ni wafuata upepo wasio na hoja yoyote ya msingi ya kuwapa hamu ya kuitaka Tanganyika!

Kuna haja yoyote ya kuifufua Tanganyika?

Kufanya hivyo kutajibu matatizo yetu ya taifa kama vile ujinga, magonjwa na umaskini?, hell no.

Zanzibar imejitangaza nchi kamili hivi karibuni. Je, wamebadilika nini mpaka sasa?

KILICHO KUFA, KIBAKI KUWA MFU TU.

Hammy-D mtakuja na kila aina ya mbinu na utetezi, hamtaweza kutuondoa katika hoja muhimu sana na tutazijibu hoja bila shaka.

1. Rais Mkapa amekuwepo katika serikali zote kwa miaka zaidi ya 40. Matatizo yaliyopo aliyaona na alikuwa na fursa ya kuyatafutia ufumbuzi kwa miaka 10 alipokuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM. Historia ipo wazi Mkapa hakufanya lolote na matatizo yaliyopo ni zao la yeye kukimbia ukweli wa kuyakabili. Kwa msingi huo Mkapa hana Moral authority ya kuongelea jambo alilo feli na hapa nasema Mkapa shut up!

2. Kwako Hammy D
Kabla hujawalaumu wanaotaka serikali ya Tanganyika lazima uwaeleze kwanini serikali mbili ni muafaka, kwanini miaka 50 serikali mbili hazijatoa jibu la tatizo na kwa vipi kubaki na serikali 2 kutatuliwa.

Ukishatoa maelezo yenye akili, usiishie hapo bali ueleze kwanini Wazanzibar siyo sehemu ya Tanzania isipokuwa wanapotaka mafao tu. Halafu utueleze tatizo la kurudi kwa Tanganyika ni lipi endapo SMZ ipo na hakuna tatizo. Ni vipi ujio wa Tanganyika uwe tofauti na ule wa SMZ.

3. Matatizo ya umasikini na maradhi yapo kwa miaka 50 chini ya serikali 2. Ni jambo la ajabu unapotaka kufanya uvumbuzi kuwa Tanganyika itakuja na matatizo yaliyoshindikana miaka 50 chini ya serikali 2.

4. Kama unakubalii kuwa znz imejitangaza kama nchi kamili, jiulize nchi hiyo imeungana na ipi ili kupata Tanzania. Huoni malalamiko ya wznz kuwa Tanganyika ndio Tanzania yatazidi kutubebesha lawama na mzigo kwa miaka mingine ijayo. Lazima uwe na logic kuwa muungano unatokeaje kukiwa na nchi moja tu.

Kurudi kwa Tanganyika kunatokana na kushindwa kwa sera za CCM na udhaifu wa Rais Kikwete katika ku address matatizo ya kitaifa. Huwezi kuwa na ZNZ kama nchi huku ikichota mishahara Tanganyika. Huwezi kuwa na nchi huku ada zake zikilipwa na Tanganyika n.k.

Ninachotaka kukuambia ni kuwa muungano na znz ni pale wanapokuwa na mafao zaidi ya hapo Mznz hamthamini Mtanganyika.

Muungano ni hiari ya wananchi ambao kupitia tume 5 za watu mashuhuri na waadilifu tena kwa muongozo wa CCM zimeona hakuna muungano isipokuwa kuwa na nchi mbili.
Kwasasa kung'ang'ania serikali 2 kunaweza kuwa ni bendeji baada ya siku 90 nguvu ya umma itarudi kwa kasi sana na muungano utakufa kabisa.

In other words uwepo wa Tanganyika uta sustain muungano ukiwa ICU na dawa ya kudumu ikitafutwa. Kulazimisha serikali 2 ni kuwatuma wananchi tusikohitaji kufika.

Wewe na wenzako akina Nape mkae mkijua kuwa hisyoria ya dunia inaonyesha wazi kuwa HAKUNA MAHALI NA SERIKALI YOYOTE DUNIANI ILIYOWEZA KUKABLIANA NA NGUVU YA UMMA NA KUSHINDA.

cc JokaKuu Bongolander Mchambuzi AshaDii Mag3 Pasco zumbemkuu

Napendekeza katiba mpya iunganishe Zanzibar na mkoa wa pwani kama ilivyo Mafia na mkuu wa mkoa awe Ameir Pandu Kificho ili kuleta utangamano na kuondoa chokochoko za kuwa na serikali zaid ya 1.
 
Napendekeza katiba mpya iunganishe Zanzibar na mkoa wa pwani kama ilivyo Mafia na mkuu wa mkoa awe Ameir Pandu Kificho ili kuleta utangamano na kuondoa chokochoko za kuwa na serikali zaid ya 1.

Kwa hiyo na Msata iwe ndani ya Zanzibar.... Au Chalinze ndo iwe makunduchi....??? Au unataka Mailimoja iwe ndo mchambawima...???
 
Yaan kwa lugha rahisi ZNZ yote iwe mkoa wa Pwani wenye wilaya kadhaa mf. Wilaya ya Unguja Kaskazini, Unguja kati, Chake Chake etc. Hapo ndo adabu itarudi.
 
Wenyewe wanataka kuungana na falme za kiarabu,we unataka uwaunganishe huku,nkifikiria swala la mabomu wanayolipua huko kwao,hao watu c wa kuwalazimisha kuwa na Muungano heri tuwaache tu wakajiunge kwenye umoja wa upendao
 
HI ndyo product ya BRN...Haya sasa tutaona mambo mengi sana
 
Unasemaje!?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Una hatari sana wewe! Kwa hiyo unataka tuwe tunapata urojo hata tukiwa Chalinze....
 
Zanzibar haina hata sifa ya kuwa wilaya ndani ya tanzania, subirini vijana tushike hatamu!
 
Unguja na pemba sio zanzibar...zanzibar ni pamoja na mikoa yote ya pwani na pembezoni mwake na uelewe waswahili ndio wanaopigwa changa la macho. Tafuteni historia sahihi.
 
Napendekeza katiba mpya iunganishe Zanzibar na mkoa wa pwani kama ilivyo Mafia na mkuu wa mkoa awe Ameir Pandu Kificho ili kuleta utangamano na kuondoa chokochoko za kuwa na serikali zaid ya 1.

Pendelea kunywa chai asubuhi badala ya mnazi,zanzibar si tanganyika.
 
Zanzibar haina hata sifa ya kuwa wilaya ndani ya tanzania, subirini vijana tushike hatamu!

Huku zanzibr vijana tayari wameshika hatamu,akipatikana mdada wa kitanganyika lazima vijana wamle0713.
 
Nchi zetu ni Tanganyika na Zanzibar hakujawahi kuwepo Tanzania Bara naomba tusikerane hapo. Dhambi aliyofanya Nyerere ni hiyo ya kuiua Tanganyika na atakua ameshatubu. TANGANYIKA TU. Spika weka hiyo sawa hapa tunaanza upya.
 
Pum....fxxx
 
Hoja ya nani? Ukitaja Tanzania Bara taja na Tanzania Visiwani na Ukitaja Zanzibar taja na Tanganyika hakuna namna nyingine.
 
tanganyika imejificha kwnye vichaka vya jamhuri ya muungano,ila zanzibar ipo
 
Wa ccm wanatuchafua akili zetu. Kwa kuwaogopa hao Wapemba tu wanaogopa kuwaita watu wa Tanzania Visiwani, ili kuwafurahisha wanawaita Wazanzibari. Wakifika kwa Tanganyika wanatutusi kuwa Watanzania Bara. Mmemtoa wapi huyo Mtanzania Bara? Tupeni Taifa letu, Tanganyika Baasi
 
WanaJF,

Rais mstaafu wa JMT, ndugu Benjamin Mkapa, ametoa maoni hayo akiwa kwenye hafla fupi ya kuzindua vitabu vyenye hotuba zake zote za kipindi alichokuwa rais wa JMT.

Ndugu Mkapa amesema ili kuendeleza umoja na mshikamano wetu wa kihistoria, ni vyema Watanzania wabaki na muundo huu uliopo wa serikali (yaani serikali mbili).

Aidha, rais huyo mstaafu alitumia nafasi hiyo kutuasa Watanzania juu ya kuenzi amani na utulivu wetu hasa katika kipindi hiki cha kuandaa katiba mpya ya nchi.

My take,

Binafsi bado sijashawishika na wale wanao pendekeza serikali 3 mpaka sasa. Mara nyingi nikijaribu kufuatilia naona wengi wanao shabikia kufufuka kwa Tanganyika ni wafuata upepo wasio na hoja yoyote ya msingi ya kuwapa hamu ya kuitaka Tanganyika!

Kuna haja yoyote ya kuifufua Tanganyika?

Kufanya hivyo kutajibu matatizo yetu ya taifa kama vile ujinga, magonjwa na umaskini?, hell no.

Zanzibar imejitangaza nchi kamili hivi karibuni. Je, wamebadilika nini mpaka sasa?

KILICHO KUFA, KIBAKI KUWA MFU TU.
 
  • Thanks
Reactions: cpt
Back
Top Bottom