Mkapa alia na serikali mbili (2)

Mkapa alia na serikali mbili (2)

Mimi naona wewe ndiye huna hoja za msingi, zitoe hoja zako hapo tuone za serikali mbili ili tuzijadili vizuri. Wewe unatoa tu porojo na kukariri fikra za zidumu fikra za Mwenyekiti wa Chama. Jaji Warioba alishatoa hoja nzito na za msingi za kwa nini walifikia maamzi yale. Ungezijibu kwanza ndio uendelee kutoa hoja zako maana mpaka sasa hamjazijibu ninyi mnaotaka serikali mbili. Hoja za msingi zipo kwa serikali tatu kuliko wewe unayesema serikali mbili bila kutoa hoja. Hizo ni porojo tu wala huna jipya!
 
WanaJF,

Rais mstaafu wa JMT, ndugu Benjamin Mkapa, ametoa maoni hayo akiwa kwenye hafla fupi ya kuzindua vitabu vyenye hotuba zake zote za kipindi alichokuwa rais wa JMT.

Ndugu Mkapa amesema ili kuendeleza umoja na mshikamano wetu wa kihistoria, ni vyema Watanzania wabaki na muundo huu uliopo wa serikali (yaani serikali mbili).

Aidha, rais huyo mstaafu alitumia nafasi hiyo kutuasa Watanzania juu ya kuenzi amani na utulivu wetu hasa katika kipindi hiki cha kuandaa katiba mpya ya nchi.

My take,

Binafsi bado sijashawishika na wale wanao pendekeza serikali 3 mpaka sasa. Mara nyingi nikijaribu kufuatilia naona wengi wanao shabikia kufufuka kwa Tanganyika ni wafuata upepo wasio na hoja yoyote ya msingi ya kuwapa hamu ya kuitaka Tanganyika!

Kuna haja yoyote ya kuifufua Tanganyika?

Kufanya hivyo kutajibu matatizo yetu ya taifa kama vile ujinga, magonjwa na umaskini?, hell no.

Zanzibar imejitangaza nchi kamili hivi karibuni. Je, wamebadilika nini mpaka sasa?

KILICHO KUFA, KIBAKI KUWA MFU TU.
Hammy-D mtakuja na kila aina ya mbinu na utetezi, hamtaweza kutuondoa katika hoja muhimu sana na tutazijibu hoja bila shaka.

1. Rais Mkapa amekuwepo katika serikali zote kwa miaka zaidi ya 40. Matatizo yaliyopo aliyaona na alikuwa na fursa ya kuyatafutia ufumbuzi kwa miaka 10 alipokuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM. Historia ipo wazi Mkapa hakufanya lolote na matatizo yaliyopo ni zao la yeye kukimbia ukweli wa kuyakabili. Kwa msingi huo Mkapa hana Moral authority ya kuongelea jambo alilo feli na hapa nasema Mkapa shut up!

2. Kwako Hammy D
Kabla hujawalaumu wanaotaka serikali ya Tanganyika lazima uwaeleze kwanini serikali mbili ni muafaka, kwanini miaka 50 serikali mbili hazijatoa jibu la tatizo na kwa vipi kubaki na serikali 2 kutatuliwa.

Ukishatoa maelezo yenye akili, usiishie hapo bali ueleze kwanini Wazanzibar siyo sehemu ya Tanzania isipokuwa wanapotaka mafao tu. Halafu utueleze tatizo la kurudi kwa Tanganyika ni lipi endapo SMZ ipo na hakuna tatizo. Ni vipi ujio wa Tanganyika uwe tofauti na ule wa SMZ.

3. Matatizo ya umasikini na maradhi yapo kwa miaka 50 chini ya serikali 2. Ni jambo la ajabu unapotaka kufanya uvumbuzi kuwa Tanganyika itakuja na matatizo yaliyoshindikana miaka 50 chini ya serikali 2.

4. Kama unakubalii kuwa znz imejitangaza kama nchi kamili, jiulize nchi hiyo imeungana na ipi ili kupata Tanzania. Huoni malalamiko ya wznz kuwa Tanganyika ndio Tanzania yatazidi kutubebesha lawama na mzigo kwa miaka mingine ijayo. Lazima uwe na logic kuwa muungano unatokeaje kukiwa na nchi moja tu.

Kurudi kwa Tanganyika kunatokana na kushindwa kwa sera za CCM na udhaifu wa Rais Kikwete katika ku address matatizo ya kitaifa. Huwezi kuwa na ZNZ kama nchi huku ikichota mishahara Tanganyika. Huwezi kuwa na nchi huku ada zake zikilipwa na Tanganyika n.k.

Ninachotaka kukuambia ni kuwa muungano na znz ni pale wanapokuwa na mafao zaidi ya hapo Mznz hamthamini Mtanganyika.

Muungano ni hiari ya wananchi ambao kupitia tume 5 za watu mashuhuri na waadilifu tena kwa muongozo wa CCM zimeona hakuna muungano isipokuwa kuwa na nchi mbili.
Kwasasa kung'ang'ania serikali 2 kunaweza kuwa ni bendeji baada ya siku 90 nguvu ya umma itarudi kwa kasi sana na muungano utakufa kabisa.

In other words uwepo wa Tanganyika uta sustain muungano ukiwa ICU na dawa ya kudumu ikitafutwa. Kulazimisha serikali 2 ni kuwatuma wananchi tusikohitaji kufika.

Wewe na wenzako akina Nape mkae mkijua kuwa hisyoria ya dunia inaonyesha wazi kuwa HAKUNA MAHALI NA SERIKALI YOYOTE DUNIANI ILIYOWEZA KUKABLIANA NA NGUVU YA UMMA NA KUSHINDA.

cc JokaKuu Bongolander Mchambuzi AshaDii Mag3 Pasco zumbemkuu

Ila kwel nimeamin macc wote ni mambumbumbu ,wananchi tunataka Muundo wa serekal tatu nyie mnataka wa serekal mbil.Lengo kuu nikutaka kutafuna pesa zetu kupitia kutatua mnachoita kero za mungano,kupitia serekal tatu hakuna kero za mungano
 
Hana credibility ya kutoa maoni ya hivi. Ni katika uongozi wake tulishuhudia uzembe mkubwa kwenye kushughulikia kero za muungano. Ni yeye aliyeamuru kuuawa kwa mamia ya Wapemba mwaka 2001. Bora hata aongee Kikwete kuliko huyu dikteta...
 
"cc wtanganyika wao wa z'bari" hakuna haja ya kuendelea ku2piana vijembe. Muungano uvunjwe kila m2 afe kivyake. 2mechoka!
 
ajabu ya mwaka ibilisi kumuombea neema malaika wa mungu,
 
WanaJF, Rais mstaafu wa JMT, ndugu Benjamin Mkapa, ametoa maoni hayo akiwa kwenye hafla fupi ya kuzindua vitabu vyenye hotuba zake zote za kipindi alichokuwa rais wa JMT. Ndugu Mkapa amesema ili kuendeleza umoja na mshikamano wetu wa kihistoria, ni vyema Watanzania wabaki na muundo huu uliopo wa serikali (yaani serikali mbili). Aidha, rais huyo mstaafu alitumia nafasi hiyo kutuasa Watanzania juu ya kuenzi amani na utulivu wetu hasa katika kipindi hiki cha kuandaa katiba mpya ya nchi. My take, Binafsi bado sijashawishika na wale wanao pendekeza serikali 3 mpaka sasa. Mara nyingi nikijaribu kufuatilia naona wengi wanao shabikia kufufuka kwa Tanganyika ni wafuata upepo wasio na hoja yoyote ya msingi ya kuwapa hamu ya kuitaka Tanganyika! Kuna haja yoyote ya kuifufua Tanganyika? Kufanya hivyo kutajibu matatizo yetu ya taifa kama vile ujinga, magonjwa na umaskini?, hell no. Zanzibar imejitangaza nchi kamili hivi karibuni. Je, wamebadilika nini mpaka sasa? KILICHO KUFA, KIBAKI KUWA MFU TU.
chezeeni utulivu huu kwa mikono yenu! Kama dhamira ya kweli ni Umoja iwe kweli serkali.1! Serkali mbili si Umoja tena bali utengano! Unapo sema aliyekufa amekufa, huo ni ujinga wa kumchezea simba makalio eti amelala! Tatizo la ujinga na umaskini usilihushe na Utaifa wake mtu!
 
Hivi wakuu kwanza habari za asbh, naomba kuuliza hivi hakuna maisha nje ya "Muungano "..? Sbb kiukweli wazenj hawataki kabisa hichi kitu kinachoitwa Muungano lkn sisi tunang'ang'ania kweli utadhani wazenj ndo wanatupa oxygen. Je mnajua kuwa mtu yeyote kutoka bara kule zenj anaitwa kafiri? Cjui ni udini au chuki tu lkn ukitaka kuamini haya nisemayo nenda Zanzibar kajionee
 
Nimefuatili sana tena kwa ukaribu mno kuhusiana na suala la aina ya muungano unaotakiwa.katika huu mjadala kumetokea pande kuu tata zinazotofautiana kuhusiana na aina gani ya muundo wa serikali tuufuate au kutengeneza kwenye katiba yetu mpya.kundi la kwanza ni la wasomi ambao wana pendekeza ilikuwa na muungano imara na mzuri tuwe na serikali moja.kwa maana ya kwamba baada ya tanganyika na zanzibar kuungana izaliwe serikali na nchi moja itkayoitwa jamhuri ya muungano wa tanzania na hii serikali itakuwa na rais mmoja atakekuwa amri jeshi mkuu wa jamhuri.kundi la pili lina pendekeza kuwe na serikali mbili kwa maana ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar itakayokua na rais wake na bunge lake na katiba yake,alafu kuwe na serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania yenye serikali yake,bunge na rais wake alafu hili kundi linapendekeza kuwe na bunge la tanganyika lakini serikali ya tanganyika isiwepo.kwa maana hiyo watendaji wa serikali ya tanganyika wategemee uteuzi wa rais jmt.kwa maudhui yaliyomo kwenye hii hoja ni kwamba kischotakiwa hapa kwa uelewa ni kutkuwepo kwa serikali na nchi ya tanganyika yenye mipaka ya ke na katiba yake kama ilivyo kwa watu wa zanzibar.kundi la tatu linataka pawe na serikali tatu kwa maana ya serikali ya zanzibar yenye katiba,bunge na rais wake alafu na serikali ya tanganyika yenye katiba,bunge na rais wake ya tatu iwe ni serikali jmt yenye bunge na rais ambae ndie atakae kuwa amri jeshi mkuu. Kwangu mimi nakubaliana sana na kundi la kwanza maana mapemdekezo yao serikali moja ndio ya ngeleta pich na maana halisi ya muungano,kuhusu mapendekezo ya kundi lapili yana mapungufu kidogo kwa sababu haiwezekani wananchi wa upande mmoja wapewe haki ya kuunda serikali yao,katiba yao na kuwa na rais wao alafu upande mwingine wanyimwe haki hiyo.maana katka hali ya kawaida ni lazima tujiulize kwamba je watu wazanzibar wanahaki sana kuliko watanganyika?ndio maana mimi nakubaliana na kundi la tatu lakutaka tuwe na serikali tatu.maana kuwa na serikali moja kwa sasa haitawezekana tayari zanzibar ni nchi kamili yenye katiba,bunge,serikali na rais kwa hiyo suluhisho kamili na watanganyika mamlaka ya kuunda serikali yao,bunge lao,katiba yao na rais wao.na ndipo tufikie mahala pakuunda serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania.kwanini wa tanganyika wasipewe nchi yao wakati wenzao wazanzibar tayari wanayo?maana tanganyika+zanzibar=jmt.sasa kwa kuwa zanzibar tayari ni nchi hatunabudi kuitambua nchi ya tanganyika.nawasilisha.tuonane tanganyika.
 
Mwambie HATURUDI NYUMA.. Tanganyika Haiepukiki..

Nyie CCM Vp? Mwenyekiti Wenu Alisha waambia mjiandae KISAIKOLOJIA, Vingine Mtakufa na vihoro vyenu, MUDA WA MABADILIKO UMEFIKA, TANGANYIKA HAIEPUKIKI..
 
Serikali ya Tanganyika iliondoshwa kwa nguvu na bila hoja zenye mantiki tangu kuasisiwa kwa muungano.Leo hii serikali ya Tanganyika ni muhimu ipatikane kwa jinsi muungano wenyewe ulivyo.Machungu yamewakuta wengi kwa ajili ya kuidai serikali ya Tanganyika na kudai uhalali wa Muungano mmojawapo akiwa Abod Jumbe.February mwaka 1995 Jumbe akihojiwa na gazeti la The East African alipoulizwa kuhusu muungano,alisema;"There is no doubt that the Tanganyika government was unjustifiably,unfairly,and unconstitutionally eliminated.Tanganyikans have a right to demand it".
 
WanaJF,

Rais mstaafu wa JMT, ndugu Benjamin Mkapa, ametoa maoni hayo akiwa kwenye hafla fupi ya kuzindua vitabu vyenye hotuba zake zote za kipindi alichokuwa rais wa JMT.

Ndugu Mkapa amesema ili kuendeleza umoja na mshikamano wetu wa kihistoria, ni vyema Watanzania wabaki na muundo huu uliopo wa serikali (yaani serikali mbili).

Aidha, rais huyo mstaafu alitumia nafasi hiyo kutuasa Watanzania juu ya kuenzi amani na utulivu wetu hasa katika kipindi hiki cha kuandaa katiba mpya ya nchi.

My take,

Binafsi bado sijashawishika na wale wanao pendekeza serikali 3 mpaka sasa. Mara nyingi nikijaribu kufuatilia naona wengi wanao shabikia kufufuka kwa Tanganyika ni wafuata upepo wasio na hoja yoyote ya msingi ya kuwapa hamu ya kuitaka Tanganyika!

Kuna haja yoyote ya kuifufua Tanganyika?

Kufanya hivyo kutajibu matatizo yetu ya taifa kama vile ujinga, magonjwa na umaskini?, hell no.

Zanzibar imejitangaza nchi kamili hivi karibuni. Je, wamebadilika nini mpaka sasa?

KILICHO KUFA, KIBAKI KUWA MFU TU.
Acheni unafiki hivi hizo serikali mbli ni msaafu au ni kanuni ya kiihisabati? Mbona hamtaki serikali moja ambayo kwa maoni yangu ni bora zaidi kuliko hayo maserikali mbili, tatu au hata mia. Sababu ya kutotaka serikali moja ni ipi?
 
Hammy-D mtakuja na kila aina ya mbinu na utetezi, hamtaweza kutuondoa katika hoja muhimu sana na tutazijibu hoja bila shaka.

1. Rais Mkapa amekuwepo katika serikali zote kwa miaka zaidi ya 40. Matatizo yaliyopo aliyaona na alikuwa na fursa ya kuyatafutia ufumbuzi kwa miaka 10 alipokuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM. Historia ipo wazi Mkapa hakufanya lolote na matatizo yaliyopo ni zao la yeye kukimbia ukweli wa kuyakabili. Kwa msingi huo Mkapa hana Moral authority ya kuongelea jambo alilo feli na hapa nasema Mkapa shut up!

2. Kwako Hammy D
Kabla hujawalaumu wanaotaka serikali ya Tanganyika lazima uwaeleze kwanini serikali mbili ni muafaka, kwanini miaka 50 serikali mbili hazijatoa jibu la tatizo na kwa vipi kubaki na serikali 2 kutatuliwa.

Ukishatoa maelezo yenye akili, usiishie hapo bali ueleze kwanini Wazanzibar siyo sehemu ya Tanzania isipokuwa wanapotaka mafao tu. Halafu utueleze tatizo la kurudi kwa Tanganyika ni lipi endapo SMZ ipo na hakuna tatizo. Ni vipi ujio wa Tanganyika uwe tofauti na ule wa SMZ.

3. Matatizo ya umasikini na maradhi yapo kwa miaka 50 chini ya serikali 2. Ni jambo la ajabu unapotaka kufanya uvumbuzi kuwa Tanganyika itakuja na matatizo yaliyoshindikana miaka 50 chini ya serikali 2.

4. Kama unakubalii kuwa znz imejitangaza kama nchi kamili, jiulize nchi hiyo imeungana na ipi ili kupata Tanzania. Huoni malalamiko ya wznz kuwa Tanganyika ndio Tanzania yatazidi kutubebesha lawama na mzigo kwa miaka mingine ijayo. Lazima uwe na logic kuwa muungano unatokeaje kukiwa na nchi moja tu.

Kurudi kwa Tanganyika kunatokana na kushindwa kwa sera za CCM na udhaifu wa Rais Kikwete katika ku address matatizo ya kitaifa. Huwezi kuwa na ZNZ kama nchi huku ikichota mishahara Tanganyika. Huwezi kuwa na nchi huku ada zake zikilipwa na Tanganyika n.k.

Ninachotaka kukuambia ni kuwa muungano na znz ni pale wanapokuwa na mafao zaidi ya hapo Mznz hamthamini Mtanganyika.

Muungano ni hiari ya wananchi ambao kupitia tume 5 za watu mashuhuri na waadilifu tena kwa muongozo wa CCM zimeona hakuna muungano isipokuwa kuwa na nchi mbili.
Kwasasa kung'ang'ania serikali 2 kunaweza kuwa ni bendeji baada ya siku 90 nguvu ya umma itarudi kwa kasi sana na muungano utakufa kabisa.

In other words uwepo wa Tanganyika uta sustain muungano ukiwa ICU na dawa ya kudumu ikitafutwa. Kulazimisha serikali 2 ni kuwatuma wananchi tusikohitaji kufika.

Wewe na wenzako akina Nape mkae mkijua kuwa hisyoria ya dunia inaonyesha wazi kuwa HAKUNA MAHALI NA SERIKALI YOYOTE DUNIANI ILIYOWEZA KUKABLIANA NA NGUVU YA UMMA NA KUSHINDA.

cc JokaKuu Bongolander Mchambuzi AshaDii Mag3 Pasco zumbemkuu

Nguluvi una hakika gani kwamba watanzania wote ,ama asilimia kubwa wanahitaji muundo wa serikali 3? jambo hili sanasana linakuzwa na wanasiasa kuliko mwananchi wa kawaida ambaye yeye kikubwa kwake ni yale mahitaji yake ya msingi, kama yanaweza patikana ndani serikali moja au mbili au tatu siyo tatizo.

Wanasiasa wanatumia fursa hii vibaya kwa sababu ndani ya ile rasimu kuna mambo mengi sana ya msingi lakini ebu angalia watu walivyoacha mambo hayo na kujikita kwenye muundo wa muungano tu, usijeukapatwa na mshangao pale itakapolazimika swala la muundo wa muungano wakaulizwa watanzania wenyewe na wengi wakasema wanataka serikali 2, au moja.

Kwa maoni yangu nadhani jambo hili la muundo wa muungano lingepaswa kujadiliwa lenyewe tu, na sanasana wananchi waulizwe, lakini wajumbe wakajikita katika mambo mengine ya msingi.
 
Hivi wakuu kwanza habari za asbh, naomba kuuliza hivi hakuna maisha nje ya "Muungano "..? Sbb kiukweli wazenj hawataki kabisa hichi kitu kinachoitwa Muungano lkn sisi tunang'ang'ania kweli utadhani wazenj ndo wanatupa oxygen. Je mnajua kuwa mtu yeyote kutoka bara kule zenj anaitwa kafiri? Cjui ni udini au chuki tu lkn ukitaka kuamini haya nisemayo nenda Zanzibar kajionee
ndo hapo uwashangae viongozi wetu,zanzibar huruhusiwa kununua kiwanja lakini wao huku kwetu wananunua wanavyotaka
 
Tumezoea kusema uongo na kujidanganya. Kila tunaposema Muungano wa serikali mbili tunajidanganya kwa kuwa kuna serikali moja ya Zanzibar na kiini macho cha serikali ya muungano ambayo ndani yake imeficha serikali ya Tanganyika. Hata sasa ziko serikali tatu ila tunapenda kujidanganya kwa kufichaficha hii ya Tanganyika. Wakati umefikawa kuwa wakweli na kusema kweli kuwa Muungano wetu nikati ya serikali ya Tanganyika na ya Zanzbar,. Tuseme kweli kuwa ni lazima kuwe na Serikali ya Tanganyika kwa mambo ya Tanganyika na ya Zanzbar kwa mambo ya Zanzbar na ndipo ya Muungano kwa yale mambo yanayotuunganisha. Ni kiini macho kuchagua wabunge kutoka Zanzbar kuja Dodoma kujadili mambo ya Tanganyika. Ni kujidanganya kuliita bunge la Muungano wakati zaidi ya 80% ya yanayojadiliwa yanahusu Tanganyika. Ni kujidanganya kuwa ni bunge la Muungano wakati maamuzi yake hayawezi kutekelezwa Zanzbar hadi yajadiliwe na kupitishwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzbar! Watanzania, tutaendelea kujidanganya hadi lini? Misahafu ya dini zetu inasema kuwa Waongo hawataingia peponi. Tuvunje huu uongo sasa! Tanganyika irudi na serikali yake na tuwe na Muungano wa usawa na ndugu zetu wa Zanzbar.
 
WanaJF,

Rais mstaafu wa JMT, ndugu Benjamin Mkapa, ametoa maoni hayo akiwa kwenye hafla fupi ya kuzindua vitabu vyenye hotuba zake zote za kipindi alichokuwa rais wa JMT.

Ndugu Mkapa amesema ili kuendeleza umoja na mshikamano wetu wa kihistoria, ni vyema Watanzania wabaki na muundo huu uliopo wa serikali (yaani serikali mbili).

Aidha, rais huyo mstaafu alitumia nafasi hiyo kutuasa Watanzania juu ya kuenzi amani na utulivu wetu hasa katika kipindi hiki cha kuandaa katiba mpya ya nchi.

My take,

Binafsi bado sijashawishika na wale wanao pendekeza serikali 3 mpaka sasa. Mara nyingi nikijaribu kufuatilia naona wengi wanao shabikia kufufuka kwa Tanganyika ni wafuata upepo wasio na hoja yoyote ya msingi ya kuwapa hamu ya kuitaka Tanganyika!

Kuna haja yoyote ya kuifufua Tanganyika? Kufanya hivyo kutajibu matatizo yetu ya taifa kama vile ujinga, magonjwa na umaskini?, hell no. Zanzibar imejitangaza nchi kamili hivi karibuni. Je, wamebadilika nini mpaka sasa?

KILICHO KUFA, KIBAKI KUWA MFU TU.

Mkuu kuna mazingira yanayofanya hoja kuhusu Tangayika irudi. Kwasasa kama ni kujen ga hoja ni kuwa kwanini Zanzibar iwepo na Tangayika isiwepo, wanaotaka Tanganyika isiwepo na Zanzibar iwepo maana yao hasa ni nini?
 
Kuna haja yoyote ya kuifufua Tanganyika?

Kufanya hivyo kutajibu matatizo yetu ya taifa kama vile ujinga, magonjwa na umaskini?, hell no.

Na hizi serikali mbili tullizonazo zimetatua hayo matatizo?
 
WanaJF,

Rais mstaafu wa JMT, ndugu Benjamin Mkapa, ametoa maoni hayo akiwa kwenye hafla fupi ya kuzindua vitabu vyenye hotuba zake zote za kipindi alichokuwa rais wa JMT.

Ndugu Mkapa amesema ili kuendeleza umoja na mshikamano wetu wa kihistoria, ni vyema Watanzania wabaki na muundo huu uliopo wa serikali (yaani serikali mbili).

Aidha, rais huyo mstaafu alitumia nafasi hiyo kutuasa Watanzania juu ya kuenzi amani na utulivu wetu hasa katika kipindi hiki cha kuandaa katiba mpya ya nchi.

My take,

Binafsi bado sijashawishika na wale wanao pendekeza serikali 3 mpaka sasa. Mara nyingi nikijaribu kufuatilia naona wengi wanao shabikia kufufuka kwa Tanganyika ni wafuata upepo wasio na hoja yoyote ya msingi ya kuwapa hamu ya kuitaka Tanganyika!

Wewe ndiye bendera fuata upepo, hujiulizi kwanini Waziri Mkuu hajawahi kwenda Zanzibar hata kufungua shuke ya chekechea?
 
April 26 mwaka 1964, Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda nchi iitwayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...

Lakini jambo la kushangaza leo hii, eneo lijulikanalo kama Zanzibar lina vitu vifuatavyo:

1. Wimbo wa Taifa

2. Bendera

3. Katiba

4. Rais na Baraza la Mawaziri

5. Jina la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar

6. Mengineyo

Halafu bado kuna watu wanaona kama hili ni sawa na wala halihitaji juhudi yoyote ya kulirekebisha.

Itafika kipindi ndugu zetu hawa wataunda jeshi na mengineyo halafu kukazuka taharuki ambayo haijapata kutokea...
 
Back
Top Bottom