Mkapa aliamini kwenye Vetting, Kikwete Vetting na uswahiba, Magufuli uzandiki na uchawa, Rais Samia...

Mkapa aliamini kwenye Vetting, Kikwete Vetting na uswahiba, Magufuli uzandiki na uchawa, Rais Samia...

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Niko na mzee wangu aliyefanya kazi serikalini kwa muda mrefu sana.

Ananiambia Marehemu Mzee Mkapa kwenye teuzi zake aliangalia sana Vetting uliyofanyiwa inasemaje hasa kwenye uwezo wako kikazi, na Mambo ya msingi tu.

Kwa kikwete yeye alimix Vetting inasemaje na uswahiba

Kwa magufuli hapa hakuzingatia Vetting zaidi ya uchawa na jinsi anavyomuona mtu anaweza yeye binafsi.

Sijui mama yangu samia anazingatia mambo gani ila naomba sana asiendeshwe na majungu na fitna.
 
Raia wa USAA aliwezaje kuwa wazrrr wizara Ile????

Kiongozi wetu ana mamlaka makubwa kiasi kuwa anaweza kataa ushauri wa yeyote na hamna la kumfanya.

KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA irudi mezani mjadala uanzie hapo hatimaye tupate KATIBA mpya.

Ameeeen.
 
Kwako tofauti ya "uswahiba" na "uchawa" ni ipi?

Naona umemkwepesha mmoja hapo unayempenda kusema nae alitumia uchawa, ilimradi umtofautishe na yule usiempenda.

Hebu tuambie, nani aliyeanza kumpa cheo Makonda serikalini kwasababu ya kumpiga ngumi Mzee Warioba?

Nakuona hata wewe nawe umeshageuka chawa wa mama unayejidai haujui mama yenu anaendeshaje nchi.
 
Niko na mzee wangu aliyefanya kazi serikalini kwa muda mrefu sana
Ananiambia Marehemu Mzee Mkapa kwenye teuzi zake aliangalia sana Vetting uliyofanyiwa inasemaje hasa kwenye uwezo wako kikazi, na Mambo ya msingi tu...
Yeye ni kwa kupitia "trial & error"
 
Nchi haiwezi kuendelea kwa kutegemea hisani ya kiongozi na maoni yake binafsi pasi kuzingatia sheria nichele kusema kwamba Watanzania tunataka kuvuka viwango vya ujinga na kuwa wapumbavu
 
Uongozi wa kuangukiwa KWA Bahati una changamoto zake!

Ndicho kinachomsumbua Mama!!

Yaani anajikuta KWENYE kazi ngumu na kubwa ya kutengeneza jina KWA KIPINDI KIFUPI KWA Hiyo hata kama washauri wakamuingiza chaka hawezi gundua coz Muda hautoshi wa kumjua yupi ni yupi na nani anafaa nani hafai KWA ajili yake!unaweza ikawa unafaa KWA Taifa LAKINI hufai KWA maslahi yake kama kiongozi alieingia KWA Bahati!!

KAZI nni ngumu na kubwa Sana kwake!!!
 
Kwa JK ilikua enzi ya vimemo, ukiwa mdau wa pale msikiti wa kwa mtoro na manyema umeula.
 
Vetting ingefanyika bungeni tena liwe bunge lenye weledi (sio hili la ccm) hapo tungeweza kupata watendaji wenye weledi na viwango.
 
Nchi ina hitaji “ MERITOCRACY SYSTEM " narudia tena nchi ina hitaji “ MERITOCRACY SYSTEM ” mwisho wa kusema.
 
Niko na mzee wangu aliyefanya kazi serikalini kwa muda mrefu sana.

Ananiambia Marehemu Mzee Mkapa kwenye teuzi zake aliangalia sana Vetting uliyofanyiwa inasemaje hasa kwenye uwezo wako kikazi, na Mambo ya msingi tu.

Kwa kikwete yeye alimix Vetting inasemaje na uswahiba

Kwa magufuli hapa hakuzingatia Vetting zaidi ya uchawa na jinsi anavyomuona mtu anaweza yeye binafsi.

Sijui mama yangu samia anazingatia mambo gani ila naomba sana asiendeshwe na majungu na fitna.
Rais Samia Suluhu anazingatia watu wachapakazi, waadilifu na wananosimamia katiba ya nchi ndio maana unaona sasa Tanzania inaendelea kwa kasi
 
Sasa Mkapa huyu waziri wake mkuu mpaka akaitwa ziro, ni vetting ipi alizingatia?
Huwa najiuliza yule zero alipokelewaje CDM?

Watu wengine ni LIABILITY kuwapa chance ni kijidhoofisha.

Tujisahihishe.
 
Back
Top Bottom