WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Mie naomba Mmuache Mkapa kwa hili,Kosa la Mkapa Hapa ni lipi kama siyo wivu tu ambao umewajaa watanzania wengi.Na wakati mwingine huwa nahisi maneno aliyoyasema Mkapa ni kweli,Watananzania ni Wavivu wa Kufikiri.
Yeye alichaguliwa kuwa Msuluhishi tu,Na kuhusu Malipo yeye yalikuwa hayamhusu kama Alilipwa na Serikali au alilipwa na UN au AU,Mpaka kieleweke hiyo siyo habari ya kujadili humu ndani na haina maana yeyote ila inajadilika kwa maana ingine ila siyo kwa kumhusisha Mkapa.
Mkapa kama Rais Mstaafu lazima apewe Ulinzi akiwapo sehemu yoyote ambayo kuna Machafuko na hata akiwa Nchini,Deligate yake ya TISS na Daktari wake wanalipwa na Serikali.Kwa kfupi kama ana Watu kumi na walikaa Nairobi kwa Muda huo wote ulitegemea watumie Sh. Ngapi.Mkapa kama Rais lazima akae katika Hoteli ya 5 stars.
Pia Wakati akienda Nairobi aliondoka na Wasaidizi ambao ni wataalam wa ambao mbali mbali waliokuwa wakifanya majadiliano ya Hapa na pale kabla ya kufikia hitimisho.Hapa Kuna mambo mawili AU ina utaratibu ambao Nchi huchangia gharama mbali mbali za Umoja huo na inawezekana Tanzania iliombwa kufanya hivyo.
Tuwe tunaongea hivyo na vigezo na kwa mpangilio unaofaa na siyo kisa mkapa.Wewe ulitaka Afanye kazi Bure.Amesoma na lazima alipwe kutokana na anachofanya
Gembe,
You have look at this issue objectively. There could be poor resources governance..na kwa msingi huu.. tatizo si la msuluhishi bali ni la mfumo mzima unaoruhusu uchotaji wa fedha kutoka coffers za serikali..( huenda kama walivyofafanua wengine ni kuwa gharama zimebebwa aidha na UN au AU).Kweli kiwango hicho kinatisha lakini lawama zisimwendee msuluhishi ( Mstaafu Mkapa) bali walioweka huo utaratibu wa kuchota hiyo hazina ambayo ingeweza " kusuluhisha" matatizo lukuki waliyo nayo watanzania kwa mamilioni.Iweje ukatengeneze kwa jirani ilhali kwako kunateketea?