Mkapa kaondoka, je nani atamfunga paka Kengele?

kwa upande wa Mzee Ruksa, dogo kala shavu huko Zenji..... hutamsikia kukemea hadi siku ya kiama!
 
Ni mzee Mkapa aliyekemea ile waliyoanza nayo, serikali yangu na wengine waliita mikoa yao na hata watu wao. Sasa hivi hakuna hili kweli ndio aliwaokoa katika CCM.
 
Mtoa maada umezungumza point sana,Mkapa alitoa msimamo wake kuhusu raisi kujiongezea muda,lakini waliobaki kazi kujikomba kwa mkuu sijui itakuwaje
 
Acha woga we,

Magu anajielewa! Ila tu Kama ni mmoja wa mafisadi, Sasa ujiandae maana mahakana ya mafisadi imepata njaa ya ghafla! Waliokuwa wakikingiwa kifua na Nkapa mkae mkao wa kunyolewa! Kwa watz, neema imefunuliwa!
Comment hii imenikosha
 
Lazima katiba atabadilisha
 
Mama Anna Abdalla, Mzee Mangula, Dr. Shein na Jaji Warioba nao wanaheshimika sana kwa Magu. Nadhani wanaweza kumkanya kiutu uzima.

Magu ashawahi elezea jinsi Mzee Mangula na Shein walivyokuwa wakimfuata mwanzoni alipokuwa akiwaka sana. Wakimwambia atulize munkali. Alisemaga hii kwenye moja ya mikutano ya CCM.
 
Magufuli atakuwa huru zaidi kufanya maamuzi wala hakuna impact kubwa kwani mara nyingi tumeona akitoa maamuzi papo kwa papo bila kushirikisha watu wengine.
Lakini ikibidi yupo Jakaya Kikwete atapoza kwa kiasi chake.
 
Aliondoka Nyerere Kuna watu wakasema sasa shamba la bibi, lakin ashukuriwe Mungu yu nasi kila wakati na udhibiti wa amani ukaendelea vzr. Tunaye kiongoz JPM tunaamini Nchi iko salama.
 
Umeandika vizuri sana.hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho walikuwepo wakina idd amin na Mobutu wapo wapi now
 
Mwinyi na Kikwete hawana influence yoyote kwa Marais wa nchi hii?
Wana Umuhimu wao Mkubwa tu Sema binadamu mpaka mambo yatokee ndo tunajuaga kusifia...........Utajua kila kitu lakini mpaka itokee shida ndivyo tulivyo Walimwengu.
 
Nyie subirieni muone show.

Bahati mbaya huwa hamjui mshike lipi,siku moja atakuja mtu miongoni mwenu na kuandika afadhali magu angeendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…