Hiii ndo ushahidi kua wabongo bado tupo mbali saana katika kutafakari mambo huyu jamaa hajui kabisa analo changia na madhara yake.Angalia madhara ya Rushwa ndogo ndogo kama kanga, Tshirt na sherehe kubwa ambazo kipindi hicho ziliitwa TAKRIMA na kubalikiwa na viongoz umezaa vingozi mafisadi coz wametokana na mfumo wa Rushwa hivyo wakiwa madarakani wanarudisha pesa yao kwa namna yoyote madhara yake kila Raia sasa hivi anajua kua kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake so jamii nzima HOSPITALINI,MASHULENI,BARABARANI,BANDARINI,MAHAKAMANI yaani kila sehemu kama huna ndugu bila Rushwa hufiki kokote kifupi niseme TAKRIMA ZA UCHAGUZI ZIMEZAA MFUMO FISADI.Tuje issue ya ulimboka madhara ya vitendo vya serikali kuwateka Raia wake (kama kweli make nachukulia kauli ya dk Ulimboka mwenyewe kua anamtambua vizuri afisa wa serikali aliemteka Lakini pia kule zanzibar kiongozi wa uamsho awali polisi ilikana baada ya wananchi kutishia kutembeza mapanga mitaani wakamuachia) madhara yake ni kua Hata raia wenyewe wanaiga unyama wa namna hii tena kuliko serikali yenyewe kama walivyoiga Takrima mfano halisi Vitendo vya kuwateka watu na kupotezwa kisha kukutwa wamekufa vimeongezeka lakini pia mauaji ya KITOVU CHA USALAMA MWANZA (RPC MWANZA) ni mfano tena mpaka sasa polisi hawajui nani kafanya ndo maana nikasema kua Raia wakiiiga wanapanga vizuri make akina ulimboka na Shakh wa Zanzibar iliwachukua Raia masaa tu kuwajua wliofanya unyama ule hadi mwanahalisi ikafungiwa kwahiyo serikali Lazima ilaumiwe kwa namna yoyote ile kwani Ulimboka kaitaja lakini ndie Baba wa nyumba ambae wanae wanamhisi kushiriki umafya ambao tayari na watoto wameiga kwahiyo ukiona wnaolaumu wajinga ujue ipo siku jamii nzima ikishakua ya kimafya hata ww au katika nduguzo hamtasalimia sawasawa na vita ya wenyewe kwa wenyewe inaua aliekuwemo na asie kuwemo ndege ikiachia Bomu toka angani likfika ardhini linaua nyasi,sisimizi wanyama hadi wanadamu halichagui Mungu isaidie Tz tusifike huko hapa panatosha.