KUNENA KWA LUGHA
Inaendelea……….
- KUHUSIANA NA SWALA LA KUNENA KWA LIGHA KAMA ISHARA YA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU
UZOEFU ALIOUPATA MHUSIKA KUHUSIANA YA DHANA YA KUNENA KWA LUGHA, PINDI ALIPOKUWA UHAMISHONII KANISA B
Mhusika aliwahi kukaa uhamishoni Kanisa B kwa takribani miaka mitatu (3). Katika kipindi chote alipokuwa huko alikutana na mambo kadhaa yafuatayo ambayo hakuwa amewahi kuyaona kabla, na ambayo baadhi yake (mengi) hajawahi kuyaona tena tangu aondoke Kanisa B
- Hakuwahi kumuona mtu akinena kwa lugha kwenye maombi yoyote yale.
- Ukiondoa hili la kutokumuona muumini yeyote akinena kwa lugha , yafuatayo hapa chini hajawahi kuyaona tena tangu aondoke huko.
- Aliwahi kuwa aanwaona baadhi ya waumini (wa kike wawili na baadhi ya wachungaji akiwemo Mchungaji Kiongozi (wa kiume)) wakiendesha maombi huku wakiongea maneno kutoka kwenye maandiko matakatifu kwa mfululizo kwa muda hata wa taktibani saa nzima bila kupumzika au kukatiza
- Lugha walizokuwa wanatumia ni Kiswahili na Kiingereza tu basi
- Walikuwa wanaendesha maombi kwa lugha hizo, katika namna ambayo mtu anaweza akadhani kuwa ndiyo lugha ambazo walizaliwa wakiwa wanaongea
- Iwe ni kwa Kiingereza au kwa Kiswahili, wachungaji hawa au waumini hawa wa kawaida, wataendesha maombi kwa takribani saa nzima, wanaongea Biblia tupu bila kupumzika hata sekunde moja na kwa mojawapo ya lugha hizo mbili, yaani Kiswahili au Kiingereza
Hiki kitu kwa Kanisa A, mhusika hajawahi kukiona hata mara moja kikifanyika kwenye maombi yoyote yale, kwa muda wote wa takribani miaka 7 ambayo amekuwepo Kanisa A.
Hawa watu wanaofanya maombi kwa jinsi hii, je ni kweli kwamba wao hawana RM kwa sababu hawaneni kwa lugha ngeni? Hawa kabisa walikuwa hawaneni kwa lugha ngeni lakini wana uwezo wa kuendesha maombi kwa takribani saa nzima bila kupumzika, wakitamka maneno kutoka kwenye Maandiko MJatakatifu utafikiri kuna Biblia ya Kiingereza au ya Kiswahili imefichwa mahali fulani ambapo hapaonekani na macho ya wengine, halafu wao wanasoma mfululizo baadhi ya mafungu hayo, randomly kutoka kwenye Biblia hiyo bila kupumzika, kwa lugha hizo. Je ni kweli hawa wao hawana RM kwa sababu hawaneni kwa lugha ngeni?
Hata hivyo, mhusika yeye katika swala hili la RM, mpaka muda huu anaamini kuwa mtu akikosa RM lazima afe, kwa sababu mtu yeyote yule awe ni muumini ama la. hawezi akaendelea kuwa hai wakati hana RM kabisa. Yeye anaamini kuwa kila mtu aliye hai ana RM isipokuwa tu kwa wale waliopo Kanisani, RM wao yuko activated zaidi kuzidi wale ambao huwa hawaendi. Ndiyo maana mtu anaweza akaongozwa sala ya Toba leo na akajazwa RM hapo hapo. Hii ina maana kuwa mtu huyu alikuwa naye RM tangu mwanzo isipokuwa tu alikuwa hawezi kumtumia katika kiwango kilichokuwa kinatakiwa. Mtu yeyote akikosa kabisa RM lazima afe kwa sababu RM ndiye anayemlinda kila mwanadamu, bila kujali binadamu huyo ni muumini wa Mungu ama la!
JE, KUNA UWEZEKANO KUWA HUWA KUNA PEPO LA UTAMBUZI WA LUGHA NGENI WANAZONENA WATAKATIFU WA MUNGU
Bila kuficha ukweli ulivyo, ukizingatia hali tete ya kiroho iliyopo Kanisa A kwa sasa na kwamba kuna mapepo yanendelea kurushwa, kwa muumini halisi kabisa aliyejazwa RM kunena kwa lugha kunaweza kukawa na risk kubwa iwapo tu kunaweza kukawa na uwezekano wa mapepo ya utambuzi wa lugha wanazoweza kunena watakatifu wa Mungu
Pepo linaweza kurushwa halafu likawa linatafsiri kila wanachonena waumini halafu linakifuta kwenye ulimwengu wa roho na kuzuia maombi yao kwenye ulimwengu wa roho, kama ilivyowahi kutokea kwa Daniel. Vile vile inaweza ikatokea scenario kama iliyomtokea mhusika ambayo ameshailelezea hapo nyuma. Unafuta ulichonena kwa lugha kama alivyokuwa akifuta yeye mhusika alipokuwa anasoma Zaburi yote ya 119 pale tu alipokuwa anaufikia na kuusoma mstari wa Zabuti 119:130. Pindi alipokuwa anaufikia, mstari huu ulikuwa unafuta kila kitu alichokuwa anasoma mhusika, juu na chini ya mstari huo. Hali kadhalika alivyokuwa akisoma Wakolosai 3:1-17, kuna kigingi kiliwekwa kwenye mstari wa 16, ambacho ilikuwa kila akiufikia na kuusoma mstari huo, ulikuwa unafuta mafungu yote juu ya mstari huo, na vile vile fungu moja la 17 lililokuwa chini ya mstari huo
Kama pepo anaweza kumfutia muumini alichosoma kutoka kwenye maandiko matakatifu, je atashindwa kufuta kila nachoweza kukinena kwa lugha ngeni?
Mhusika mpaka muda huu anamini kuwa pepo la utambuzi wa lugha likirushwa na likafanikiwa kuwepo ndani ya nyumba ya Ibada, wanenao kwa lugha wote wana uwezekano wa kupoteza kila kitu kwenye maombi yao.
Mhusika anashuri kuwa kama mtu anao ujazo huo, bora akautumie zaidi akiwa kwenye maombi ya faragaha, kuliko akiwa Kanisa A
HITIMISHO:
Kwa hiyo katika miaka yote mitatu ambayo mhusika alifanikiwa kuwepo Kanisa B, hakuwahi hata siku moja kusikia mtu ananena kwa lugha wakati wa maombi, lakini msisitizo uliopo Kanisa A kwa sasa juu ya unenaji kwa lugha umekuwa ni wa kiwango cha juu muno, kiasi kwamba mantiki iliyopo Kanisa A kwa sasa ni kuwa wale wote wasionena kwa lugha hawana RM.
Je hiki kitu ni kweli?
Hii kwa upande mwingine inamaanisha kuwa kule alilkowahi kuwepo mhusika, yaani Kanisa B,
AIDHA hakuna hata mtu mmoja kwenye nyumba hiyo ya Ibada aliye na ujazo wa RM
AU wapo waliojazwa na ambao wanao uwezo wa kunena kwa lugha ila kwa bahati mbaya MAOMBI YAO NI YA KIWANGO CHA CHINI SANA kwa sababu huwa wanaomba si kwa kunena kwa lugha, japo wanao uwezo huo wa kunena kwa lugha ngeni
MUBARIKIWE TENA NA BWANA
Yohana 14:6
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Malaki 3:5
Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.
WAEBRANIA 6:4-6 SUV
Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu kwa mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
MwiH
elly obedy