TATU:
BAADA YA TUKIO LA FLUIDS ZA J2 KANISANI KUPITA
J4 tarehe 09/01/2024 ndiyo ukafanyika utekelezaji wa PLAN A ya kum-
scare mhusika kuwepo mazingira ya ofisini kwa kumtumia binti anayefanya kazi kwenye maabara ya MRX
Kesho yake tena J5 tarehe 09/01/2024 likatekelezwa plan nyingine yenye lengo hilo hilo, safari hii kwa kutumia
vifaa vya electronics vilivyoletwa ofisini kwao mhusika kwa ajili ya kuchajiwa, na wahusika wakuu tukio hilo walikuwa ni OM-1 na MWG
Maelezo ya kina ya plans zote hizi mbili tayari yapo kwenye posts zilizopo hapo juu
MATUKIO BAADA TA PLANS A NA B KUWA ZIMEPITA
NNE UPEPO WA TAIR ZA GARI LA MHUSIKA KUPUNGUZWA ALHAMIS YA TAREHE 11/01/2024, GARI LIKIWA LIMEPAKI OFISINI
Alhamis ya tarehe 11/01/2024, akiwa maeneo ya ofisini, mhusika alilazimika kwenda kupaki kwenye parking zilizopo kwenye jengo la CHAMA CHA WAFANYAKAZI, baada ya kukuta parking za kwenye jengo la ofisi yake zimejaa
Mara ya mwisho mhusika alipaki kwenye parking zilizo nje ya jengo la ofisi yake ilikuwa possibly mwaka jana kabla ya July 2023, na baada ya hapo, amekuwa akitumia parking za kwenye jengo la ofisi yake siku zote hadi ilipowadia Alhamis hiyo ya tarehe 11/01/2024
Gari nyingine aliyoikuta ikiwa imepaki kwenye parking hizo siku hiyo ilikuwa ni ya SMKE, ila mhusika hakupaki jirani na gari hiyo kwa sababu parking zilikuwepo za kutosha
Jioni hiyo wakati mhusika anataka kuondoka ofisini kurudi nyumbani,
alikuta UPEPO WA MATARI hasa yale ya nyuma, umepunguzwa sana. UPEPO NI FLUID PIA
Kutokana na hali hiyo, mhusika aliondoka ofisini siku hiyo na kupitiliza moja kwa moja kwenda kujaza
FLUID hiyo kwenye SHELL iliyopo karibu na maeneo ya Mwenge Mpakani
TANO: J2 YA TAREHE 14/01/2024 MHUSIKA ALIPOKUWA YUPO KANISANI
Kama ilivyo kawaida yake, J2 hiyo, mhusika alihudhuria Ibada ya pili
Mhusika aliwahi na kukuta Ibada ya kwanza bado inaendelea, ila ilikuwa mwisho kwenye matangazo
Akiwa yupo amesimama nyuma ya lango kuu la kuingilia kanisani, alimuona MR X akiwa anatokea sehemu ambayo ilionekana kuwa washrooms
Mhusika na MR X walisalimiana hapo mlangoni na hatimaye MR X kuingia tena ndani Kanisani kwenda kuhitimisha muamala wa Ibada ya kwanza aliyokuwa amehudhuria J2 hiyo
BAADA YA DAKIKA KADHAA KUPITA, KM-A ALITOA TANGAZO LA GHAFLA UHAMISHO WA KIONGOZI AMBAYE ALIHITAJI KULIAGA KANISA
KIONGOZI HUYO ALIHITAJI PIA KUTOA SADAKA YA SHUKRANI KWENYE IBADA HIYO YA KWANZA
Baada ya Sadaka ya Shukrani kutangazwa, mhusika aliamua kushiriki kwenye sadaka hiyo
WAKATI MHUSIKA ANAELEKEA MBELE KWA AJILI YA KWENDA KUTOA SADAKA YA SHUKRANI
Kule mbele kwenye viti vya pembezoni kabisa jirani na PATHWAYS, aliwakuta MR X na MRS X wakiwa wamekaa pamoja,
huku MRS X akiwa amekaa kiti cha pembezoni kabisa, akifuatiwa na MR X
Hapo mhusika alimgusa MRS X peke yake begani kama ishara ya kumsalimia, na kumwacha MR X kwa sababu mhusika na
MR X walikuwa tayari wameshasalimiana
Kwa muumini mwingine ambaye hakuwa amewaona MR X na mhusika wakisalimiana kule nyuma ya lango kuu la Kanisa, possibly angeweza kupata ishara
kama ya mhusika kum-signal MRS X na si kumsalimia, possibly ili baadaye waonane na kuongea
na kweli muda mfupi baadaye wawili hawa walionana na kuongea
TUKIRUDI NYUMA KIDOGO KWENYE MAZINGIRA YA OFISINI KAMA MIEZI MIWILI ILIYOPITA
Mhusika aliwahi kumuuliza MR X kuhusiana na binti amabye kwa sasa haonekani tena mazingira ya Kanisani hapo
- Kipindi alipokuwepo, binti huyu alikuwa anaonekana kuwa alikuwa ni swahiba wa karibu sana na MRS X na alikuwa hakosi kuwepo Kanisani kila J2
- Baada ya mhusika kumkosa binti huyu, siku moja wakiwa wapo ofisini, mhusika alijaribu kumuuliza MR X kuwa binti huyo alienda wapi kwa kudhani kuwa pengine MR X angeweza kujua kwa sababu alikuwa ni swahiba sana wa MRS X
Baada ya swali hilo, MR X alishindwa kumtambua binti huyo, na maongezi yao yaliishia hapo, huku mhusika akiwa na nia ya kumuuliza MRS X siku atakapofanikiwa kuonana naye
TANGU SIKU MHUSIKA ALIPOMUULIZA SWALI MR X, MHUSIKA NA MRS X HAWAKUWAHI KUONANA TENA KANISANI HADI ILIPOFIKA J2 HIYO YA TAREHE 14/01/2024
J2 hiyo, baada ya mhusika kuingiza gari lake na kulipaki ndani ya uzio wa Kanisa yo huku Ibada ya pili ikiwa tayari imeanza,
ndipo mhusika alipomuona tena MRS X kwa karibu wakiwa wapo nje ya nyumba ya Ibada, na kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu sana
Huyu MRS X ndiye ambaye dakika chache zilizokuwa zimepita, mhusika alionekana akim-
signal kwenye bega ndani ya Kanisa wakati wa Sadaka ya Shukrani
Baada ya kumuona,
mhusika alimfuata MRS X na kumuuliza huyo rafiki yake siku hizi yuko wapi ambapo MRS X alijibu kuwa wala hamkumbuki
Wakati huo Ibada ilikuwa imeanza na vyombo vya muziki vilikuwa vinapiga,
Baada ya kuachana na MRS X na hatimaye mhusika kuelekea ndani ya nyumba ya Ibada, ndiyo pale alipoweza kuuona mpangilio wa matukio kuanzia wakati ule aliposalimiana na MR X kabla ya Ibada ya kwanza kumalizika, wakati wa Sadaka ya Shukrani na hadi wakati alipoonana na kuongea na MRS X kwenye parking
KWA NINI MHUSIKA ALIKUWA ANA HAJA YA YA KUJUA HUYU BINTI SWAHIBA WA MRS X ALIENDA WAPI
Ni kwa sababu wakati mwingine walikuwa wakikutana na binti huyu, binti alikuwa anaweza akakwepa kusalimiana na mhusika bila sababu yoyote ya msingi, halafu baadaye tena tuseme mhusika alipokuwa anakuwa yupo maeneo ya nje kwenye parking anataka kutoa gari nje aliingize ndani ya uzio wa kanisa,
binti huyu alikuwa akionekana maeneo hayo na kupita karibu na gari la mhusika huku akimpungia mhusika
Wakati wa Ibada vile vile, japo si kwa mara zote, binti huyu alikuwa anakaa maeneo jirani na mahali anapokaa mhusika
Haya ndiyo mambo pekee yaliyopelekea mhusika akawa anatamani kujua binti huyu alienda wapi
……………………………inaendelea