KUHUSIANA NA FUNDI MEKANIKA (FME) WA GARI LA MHUSIKA
MAELEZO YA UTANGULIZI
Kwa matukio ya hivi karibuni kuhusiana na FME, tunaweza kuanzia mwaka jana kwenye siku ambayo gari la mhusika lilipata hitilafu akiwa mtaani sehemu jirani na mahali pale anapoishi;
siku ya Ijumaa jioni mara baada ya kuwa ametoka ofisini.
Kwa hiyo kwa sasa, tutatembea na matukio muhimu tu kuanzia kipindi hicho hadi leo, halafu baadaye tena ndiyo tutayarudia tena yale yaliyowahi kutokea kabla, focus yetu ikiwa ni kwa huyu FME tu
Tukirudi sasa kwenye mada yetu, hitilafu hiyo iliyowahi kutokea siku ya Ijumaa jioni baada ya mhusika kutoka ofisini, ilisababisha usukani wa gari kuwa mgumu na hivyo mhusika kushindwa kuendesha gari kawaida.
Na kwa sababu siku hiyo ilikuwa ni Ijumaa tena jioni, kama ageamua kulipeleka gari gereji, ingebidi liende likalale huko kitu ambacho alikuwa hataki kwa sababu matukio ya kabla ya siku hiyo tayari yalikuwa yameshampa indicator za wasiwasi kuhusiana na FME; kwamba fundi huyu hakuwa na nia njema na gari la mhusika. Kwa hiyo hadi kufikia siku hiyo, matukio ya nyuma yalikuwa tayari yameshamfanya mhusika kupoteza kabisa imani na FME; japo mhusika hakuwa ameidhihirisha hali hii kwa FME; na hajui kama labda FME mwenyewe alikuwa amegundua hilo ama la; pamoja na yeye (mhusika) kujitahidi kuificha hali hiyo
Hata hivyo hadi kufikia muda huo, na mhusika mwenyewe pasipo kuwa na ufahamu kuwa alichokuwa anajaribu kukikwepa kilikuwa kimeshatokea lakini ukweli ulikuwa ni kwamba tayari watu walikuwa wameshafanya kazi; na engine hiyo ilikuwa tayari imeshaibiwa tangu mwanzoni mwa mwezi wa tatu; na possibly hicho ndicho kilichopelekea tatizo hili la usukani kuwa mgumu. Uwezekano mkubwa ni kwamba kuharibika kwa kifaa hicho siku hiyo (kilichohusiana na usukani) kulisababishwa na engine nyingine iliyowekwa kwenye gari la mhusika kutokuwa imefungwa vizuri baada ya kutolewa ile iliyokwepo mwanzo
Baada ya kutokea tatizo la kifaa hiki ambcho yeye kwa lugha ya ki-
layman alikiita
“steering wheel belt roller” mhusika aliamua kwenda kulipaki gari nyumbani kwanza Ijumaa hiyo
- Kesho yake Jumammosi mhusika hakulitumia gari hilo
- J2 pia hakulitumia gari hilo na hivyo ilibidi aahirishe kwenda Kanisani
Siku ya J3 asubuhi ndiyo alilitumia gari hilo kwenda ofisini na baada ya muda asubuhi hiyo hiyo, ndiyo aliamua sasa kulipeleka gereji kwa FME. Gari lilirekebishwa na haikuchukua muda mrefu, na baadaye mhusika aliondoka baada ya dakika kadhaa kupita akarudi ofisini na kuendelea na kazi zake zingine
BAADA TENA YA SIKU KADHAA KUPITA…………
- J3 asubuhi rectifire ya umeme ikaharibika, betri illikataa kupiga
- Jana yake J2 baada ya mhusika kuwa ametoka Kanisani alipaki gari ikiwa salama kabisa, halafu ghafla kesho yake J3 asubuhi betri ikawa haiwezi kupiga
Kwa experience yake aliyonayo mhusika kwa sasa, uwezekano mkubwa ni kwamba uharibifu huu ulifanyikia kwenye parking za Kanisani J2 alipokuwa yupo kanisani
Baada ya kutokea hitilafu hiyo, mhusika aliipeleka tena gari gereji siku hiyo kwa ajili ya marekebisho ya ku-replace kifaa kilichokuwa kimeharibika, na ilikuwa ni lazima kufungua boneti la gari kwanza na hatimaye COMMPRESSOR ya AC halafu ndiyo kifaa hicho kiweze kufungwa.
BAADA YA BONETI KUWA LIMEFUNGULIWA KWA MUDA MREFU, NDIYO PALE MHUSIKA ALIBAINI KUWA ENGINE ILISHABADILISHWA
Swali lililomjia kichwani ni je, engine imebadilishwaje wakati gari haijawahi kulala gereji hata siku moja?
Baadaye mhusika alikuja kubaini window moja mwanzoni mwa mwezi wa tatu ambapo taa za kwenye parking kwa maghorofa mawili yaliyo jirani likiwemo lile analoishi yeye mhusika, zilizimwa kwa siku kadhaa kukawa na giza totoro. Mbali na hivyo, mita ya umeme wa taa za kwenye parking kwa ghorofa lile analoishi mhusika ilikuwa imeondolewa kabisa
Hata hivyo kitu hiki kuhusiana na engine hii nacho aliamua kukificha pia kwa kujua kuwa pengine hata FME naye atagundua pia tatizo hilo
- Tofauti na matarajio yake mhusika, FME hakuweza kugundua wakati hata muonekano wa radiator tu ambayo alikuwa siku zote akicheza nayo akiisafisha au kubadilisha coolant; ulikuwa tofauti mno
- Engine iliyokuwepo awali ilikuwa almost mpya, hadi rangi yake ilikuwa ni mpya na ilikuwa safi kabisa bila vumbi jingi na matope yaliyogandamana siku nyingi
- Hii iliyokuwepo siku hiyo ilikuwa kuukuu hadi rangi; na ilikuwa ni chafu mno.
Mhusika anaweza kuwa ni mchafu kwenye vitu vingine, lakini haikuwa hivyo kwa gari lake ikiwa ni pamoja na engine ya gari hilo
Kwa hiyo, wakati utaratibu wa kutafuta kifaa kilichokuwa kimeharibika ili kiweze kufungwa kwenye gari ukiwa unaendelea siku hiyo; FME alimshauri mhusika afunge pia COMPRESSIOR nyingine ya AC na kwamba yeye anawajua watu wanaoweza kumletea COMPRESSIOR nyingine nzuri pale pale gereji walipokuwapo. Actually haikuwa mara ya kwanza kwa FME kutoa ushauri huu siku hiyo, bali hapo awali FME alikuwa amewahi pia kutoa ushauri wa aina hiyo siku ya kwanza mhusika alipokuwa amepeleka gari kwa ajili ya kurekebisha
“steering wheel belt roller”; sema tu kitu unique alichokuwa anafanya FME wakati anamshauri mhusika ni kwamba alikuwa anahakikisha kuwa hakuna fundi mwingine yoyote yule pale gereji, anayesikia wanachoongea. Kwa hiyo ushauri wa mwanzo aliwahi kuutoa katika mazingira ambayo walikuwa pia wawili tu na katika muda ambao mhusika alikuwa tayari ameshawasha gari anajiandaa kuondoka na alikuwa ameshafika getini kabisa anatoka nje ya uzio wa gereji. Hapo ndipo FME alimsogelea mhusika na kuteta naye pale getini; gari ikiwa inaunguruma tayari
MHUSIKA AKUBALI USHAURI WA KUFUNGA COMPRESSOR NYINGINE
Baada ya FME kushauri mhusika afunge COMPRESSIOR nyingine ya AC; mhusika alikubaliana na uamuzi huo kwa sababu
- Ili fundi aweze ku-replace kifaa kilichokuwa kinahitaji matengenezo siku hiyo, ilikuwa ni lazima pia COMPRESSIOR ya AC ifunguliwe
- ilikuwa ni tayari mwisho wa mwezi; mhusika
Mpaka hapa mhusika akawa hana shaka kabisa kuwa engine iliyokuwa kwenye gari haikuwa ile ya kwake.
Kazi sasa ikabaki kuwa anaweza kuthibitisha hilo kwa watu wengine na mafundi wengine waliopo hapo gereji? Atathibitishaje?
Akiwa anachekecha akili yake, hatimaye mhusika alifikia uamuzi wa jambo moja kubwa kwamba kama akikosa kabisa namna ya kuthibitisha kuwa engine iliyoko kwenye gari siyo ile yake,
itabidi akae kimya, ………..kimya kimya kimya kabisa; unless anapata namna ya kuthibitisha hilo
Zaidi ni kuwa kipindi mhusika anabaini swapping ya engine hizo kufanyika; alikuwa hana hata idea ya kama engine hiyo iliyokuwa imewekwa inaweza kuwa haikufungwa vizuri kiasi cha kuwa loose; hakuwa na idea hiyo. Idea hiyo alikuja kuipata kutoka na kubabaika kwa FME mwenyewe; kwenye tukio jingine siku nyingine ambapo mhusika alikuwa sasa ameirudisha gari makusudi kwa FME na kijanja kwa ajili ya kumpima ili kupata taarifa zaidi kama aliyehusika na tukio ni yeye ama la.
Test simple aliyoitumia siku hiyo ni kumuomba fundi abadilishe COOLANT na hapo ndipo alipopatia zaidi ya asilimia 200% halafu na ushahidi mwingine wa ziada wa kutosha na usio shaka yoyote (BEYOND REASONABLE DOUBT) ukapatikana
Taarifa zaidi za namna FME alivyopaniki na hivyo kupelekea mhusika apate ushahidi mwingine mkubwa wa ziada kuhusiana na engine hiyo, zitafuata baadaye
…………….inaendelea