Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa
Sehemu ya 10
Michakato ikawa inaendelea huku duka likizidi kupanuka nami kwa upande wangu nikawa bize sana kiasi cha kunifanya kutoweza dukani kwa muda mwingi kwahiyo nikamchukua mmoja wa wanafamilia na kumuweka kusimamia shughuli za pale dukani akiwa kama muuzaji nami nitakuwa nikipita kutazama mahesabu lakini kaka alimzuia na akasema "kwanini tunauliza maswali yasiyo na majibu,kama wewe ni ndugu yetu kweli na unataka tuwe washirika na vitu vyako kweli kwanini unashindwa kutuambia ukweli?" Ilinipa shida sana hiyo na naamini hata wewe leo hauna pesa na watu wanakuna katika maisha ya kawaida siku ukapata pesa katika mazingira yoyote kwa sababu pesa inaweza kumjia yoyote yule,tizama mimi zimenijia katika mazingira haya sikuwahi kuwaza,sikuota ndoto na zimekuja nyingi katika maisha yangu hata wewe utakapopata pesa watu wakaona mabadiliko yako lazima kuna vitu watazungumza,kama hawatazungumza umejiingiza kwenye mambo mabaya,umejiingiza kwenye ushirikina utawatoa sadaka kuna shuhuda shuhuda za uongo watakwambia kuhusu wewe kumbe sio,mimi hizi pesa sijapata kwa njia zozote watu wanaweza wakanijudge nazo,nimepata katika mazingira ambayo nakueleza lakini siwezi kuzungumza,ni vitu ambavyo havizungumziki,nikamwambia kaka "mtakapokataa sitapoteza hata dakika moja,nina uwezo wa kuajiri mtu na nitamlipa tena nafikiri ntafanya nae kazi kwa mazingira mazuri kwa sababu atafanya vizuri na nitamlipa vizuri pia" lakini huyo ndugu yangu yeye alikuwa na utayari "mi nafanya bwana,kaka yeye ndio anazuia mi nafanya bwana" nikamwambia "tulia hapa fanya kazi,hufanyi kazi kama ndugu tu,unafanya kazi nakupa mshahara,wapi unaweza ukapata laki mbili mwisho wa mwezi na nakupa mahitaji yote laki mbili yaani umebaki nayo,chakula nakupa nauli nakupa utapata wapi kazi kama hiyo na natakaka kuona mwendo wako mwanzo na kama utaenda vizuri biashara inalipa ntakuongeza mshahara,tulia ufanye kazi achana na maneno ya kaka".
Nilizidi kugawa majukumu kwa sababu kuna jukumu kubwa liko mbele yangu,kuna biashara kubwa iko mbele yangu sasa ambayo naenda kuitazama,sikuishia hapo kwani nikaenda tena kwa yule mama ambaye ana watoto wa yule mshkaji kule gerezani,nilienda kama nilivyosema mapokeo ya yule mama yalikuwa yamebadilika sana ,pesa imefanya mapokeo ya mama yabadilike,mama sasa hivi anatabasamu na anaongea na mimi kwa sauti tofauti kabisa na ile ya mwanzo,yaani sasa hivi naipata sauti flani nzuri nzuri kwa huyu mama na nakumbuka sana nilipofika kwa mara ya pili kwani mara ya kwanza nilimwambia ntafika kuchukua majibu na nikawa busy nilipopata nafasi nikaenda tena hadi aliniandalia chakulaπ! Unaona? Pesa inakupa heshima,inakupa kibali,pesa inakupa vitu ambavyo hauwezi kuvipata kama huna pesa,ni kweli kabisa,nikapata chakula nikafurahi nikiwa na hawa watoto na nikamwambia "vipi kuhusu mawazo ambayo nilishea na wewe" akanambia "lolote utakalosema mimi nimeona iwe sawa,iwe sawa kwani siwezi kujua uliishi vipi na mzazi mwenzangu,siwezi kujua lakini ninachojua umekuja kwetu kwa mema tu" nikamwambia "ni kweli nimekuja kwa wema tu" nakumbuka tulizungumza mengi na akanipa michakato ambayo anataka kuifanya akasema yeye anapenda mambo ya vinywaji,anapenda mambo ya vinywaji yaani akifungua kama glocery inaweza ikamfaa,mimi nikamwambia "usiwaze kufungua glocery waza kufungua bar kubwa kabisa" akasema "kweli mi nifungue bar? Nimiliki bar ntaweza wapi?"
Nikamwambia "kwani wanaoweza wanawezaje,hata wewe utaweza" akasema "sijui,ntawezaje kupata huo mtaji wakuweza kufungua bar kubwa" nikwamwambia "wala usiwaze kuhusu hilo,kwenye bar uwa kuna namna yake unaweza usichukue bar nzima,unaweza kuwa na wenzako wewe ukachukua eneo la vinzaji wengine wakachukua eneo la chakula inategemea vile nyie wenyewe mnajipanga" akanambia "una mawazo kweli mazuri,umeniwa wazo zuri na umenipa akili nimekuwa sasa hivi nawazawaza vitu vingi lakini nimeona eneo la vinywaji mimi linanitosha kabisa lakini mtaji wake ni mkubwa sijui yani,sijui kama itawezekana" nikamwambia "wewe sema unachotaka,hicho unachotaka mimi kwangu itawezekana" aisee mama alifurahi sana,mama alifurahi sana kwa sababu sasa nimeshamaliza nataka kuondoka mama anatamani nibakiπ! Nabaki nafanya nini? Nabaki nafanya nini kwa huyu mama,nikamuaga na nikamuahidi ntakapokuja awe na majibu na ikiwezekana atafute hilo eneo liwe zuri,asitafute eneo ambalo hakuna biashara,atafute location nzuri nami nikamuahidi "nami nazidi kukutafutia uko kama nitapata eneo zuri nitakujuza mapema" tulizungumza na huyu mama haya manen kwa uzuri kabisa lakini najua huyu mama ana maswali mengi sana lakini alipokea ombi langu nililopeleka kwake.
Nakumbuka nimeondoka na kuendelea na mishe nyingine huyu mama akaanza kunitumia meseji "vipi Rojas uko poa? Wadogo zako huku ni wazima kabisa wanakusalimia sana" hakuishia hapo akawa ananipigia simu niongee nao,"ongea nao basi" nikamwambia "sawa" naongea nao nikawa mwenye furaha napiga nao story lakini akawa ananipigia simu majira hata ya usiku,majira hata ya usiku wa saa 4 ananipigia simu unaona,na hii ni nilipotoka round ya pili hii ambayo nilienda kuzungumza nae kuhusu kutafuta eneo la bar na nini,simu za usiku ananipigia ananiambia nini? Ananisalimia,ananitakia usiku mwema,basi tutaongea asubuhi,uko na nani,ananitumia meseji au tunazungumza kwenye simu na mazungumzo kama hayoπ
Mimi najua huyu mama anapotaka kwenda na kama nilivyosema awali kuwa pesa inaweza kumbadilisha kabisa mtu mawazo na kwa mtu unampa kwa lengo wewe wewe unalolijua na silo analowaza yeye,yeye anawaza vitu vingine kwa sababu huyu mama kwa jinsi nilivyoongea nae anavyowaza labda mimi nimefall in love na yeye,ndivyo akili yake ndivyo inavyomwambia na labda anaona ninavyoonesha nia yakutaka kumpa mtaji basi kabisa kwanini asiwe na mimi,ndivyo nilivyoendelea kuisoma akili ya huyu mama lakini mimi wala siko uko,yaani sijawahi kumtazama kwa huyu mama kwa umakini,sijawahi,yaani namuona ni mama ninayemheshimu,sijawahi ku pay atention kutazama chochote kuona kitanivutia kwenye upeo wa macho yangu kwake hata siku moja,nazungumza hiyo kwa ukweli kabisa,sijaona chochote kwa sababu nimebeba ile heshima ambayo mshkaji alinambia na mimi niko karibu na huyu mama kwa ajili ya hawa watoto ili nitimize ahadi ambayo rafiki yangu alinambia,nikasema ni akili zake tu ataelewa,atanielewa baadae wala sina haraka na hili.
Wakati michakato ikiwa inaendelea nikapata bahati kwa sababu niliwaambia watu wanitafutie eneo ambalo naweza kufungua bar,kuna mtu akanipa hiyo taarifa na nikamwambia huyo mama kuna eneo nimepata naye akanambia kuna eneo amepata akanambia "njoo Rojas ungekuja kwanza kuliona hili" nikamwambia sawa nikafunga safari nikaenda kuliangalia nikamwambia "sawa lakini lile mimi nililoambiwa naliona ni bora zaidi na ukilipenda wewe mwenyewe utakuwa na choice" akanambia "sawa" kweli tulienda pale na uzuri huyu mama ana uelewa sana yaani ameishi kwenye ulevi mpaka akawa na experience kubwa sana kwa sababu huyu mama ni mlevi mlevi sanaπ. Tulizungumza mengi hapa na makubaliano tulizungumza nao hapa katika hii bar,walizungumza mambo ya biashara,mwanzo wa kufanya biashara kilibainika nami ikabaki ni kutoa tu pesa sawasawa na uhitaji wa huyu mama aliokuwa nao na nakumbuka tumezungumza sasa tumerudi nimdrop mahali ili mimi niendelee na mishe zangu nakumbuka huyu mama akanambia "sijawahi katika maisha yangu kukutana na mtu akanisuprise kama ulivyonisuprise wewe,yaani mpaka natafuta eneo hadi wenzangu wananiuliza ni nini umekutana nacho,ni muujiza gani nimekutana nao,wananiambia mimi ni muongo,nawaambia ni rafiki wa mzazi mwenzangu wananikatalia wanasema wewe ni mtu wako" nikamwambia "huna hata sababu ya kujieleza kwao kwa sababu hata ukijieleza,hata ukijitetea watakuwa na majibu yao ila wewe baki na unachokijua kuwa ni rafiki wa mzazi mwenzio,mimi ninachokuombea ni ufanikiwe,unajua biashara haitaki uweke mbele urafiki na usipageuze pale marafiki wanakuja wanakunywa wanakopa" akasema "siwezi kufanya hayo makosa,nimeangaika sana kutafuta mtaji,siwezi kufanya hayo makosa yaani siku unanipa pesa na kusema nifanye biashara na ndio mwanzo wa mimi kutoka katika umaskini,sitaishi tena kuwa mwanamke wakuombaomba,sitaishi tena kuwa mwanamke wa kukutana na mtu aniambie kwamba atanipa pesa niende nikampe furaha,sitaishi tena hayo maisha kwani nimekuwa nikiangaika kwa ajili ya watoto wangu ili wale,ili wavae na ndio maana nimekuwa hata na tabia ambazo najua unajua" nikamwambia "hata wala mimi sijakuhukumu kwa chochote kile naamini hata iki unaenda kusimama nacho kitawafaa pia na watoto" akasema "kabisa,nakushukuru sana" nikamwambia "sawa,kesho ntapita benki na nitakuletea pesa zote unazozihitaji" akesema "kweli" nikamwambia "kweli namaanisha" nilizidi kumchanganya akili ya huyu mama kiukweli nikachanga akili yake isivyo kawaida.
Hapo mimi sikuwa na ukaribu na wanawake kwa kiwango hiki nilicho karibu na huyu mama,nikizungumza hivi najua unaelewa yaani ule uclose wa kuzungumza hivi,mishemishe kama hizi tunatafuta,tunawasiliana,tunaongea,kwa maeneo kama haya yaani ulezi wa mtoto,malezi kwa ujumla sijui nini kwa mara yangu ya kwanza yaani nayaishi hayo,akinambia "watoto wananini,wanahitaji sijui nini yaani moja,mbili,tatu" siunajua hayo ni mambo ya watu wa familia nami bado ni kijana sikuwahi kuishi hivyo,niliachana na huyu mama nami nikaendeleatna michakato yangu kama kawaida.
Nazidi kukimbizana na nikamkamilishia ahadi yake ya pesa yule mama,nilienda kumpa taarifa mshkaji wangu kule gerezani nikimjuza hatua jinsi nimepiga,jinsi ambavyo nimefanikiwa nilimweleza yote "vipi na suala la kuwahamisha kutoka pale wanapoishi kwenda kwenye nyumba nyingine?" Nikamwambia "yote yatakamilika" akafurahi sana na akanambia "kuwa mwangalifu sana na yule mwanamke anapenda sana hela na kwenye hela yule mwanamke anaweza fanya chochote,usije ingia tamaa nae kwani ni mwanake ambaye hajawahi kuwa na utulivu,asije kukushawishi kwa sababu ameona umeanza kuwa na pesa ukajikuta siku umedondoka nae,nakutahadhalisha kwa sababu nakupenda kwani mwanamke mwenye kubadilisha wanaume kama nguo hafai,si ni kweli?" Nikasema "ni kweli,hawezi kufanikiwa kwangu na nimeshamjengea mazingira mazuri sana kwenye akili yake naamini mpaka sasa ameelewa siko upande huo" akasema "ameshakutegatega eeh?" Nikamwambia "sio sana" akasema "lazima ulishinde hilo jaribu mtu mzima yule" nikamwambia "ni kweli " mengi nilimueleza na nikamwambia harakati zote zinazoendelea na alizidi kufurahi sana,alinambia lakini nisimsahau yule mwanamke niwe naenda hata kumjulia hali na nimsikilize nini anawaza ambacho tunaweza kumfanyia,nikamwambia "sawa,hivi ni hawa tu katika maisha yako unaowathamini uliwaza ukifanikiwa katika maisha utawafanya wawe bora zaidi na vipi kuhusu shangazi yake kule kijijini?" Akasema "sasa hayo nakuachia wewe" nikasema "unaniachia mimi vipi wakati hao ni ndugu zako?" Akasema "kama uliguswa na shangazi kwa sababu ya mapokezi yake sawa lakini mbona mimi hawaji kunitembelea? Si kwa sababu wanajua sina kitu,si wanajua nitaozea gerezani? Si hata kama mmoja angetokeza ungechukua hata milioni kumi ukampa imfae kwa biashara lakini wameniacha huku wanajua mimi nimeisha sasa mimi naweza ninkfanyaje,eti Rojas nifanye nini sasa,kama kuna siku kuna mtu ataamka kuja kunitembelea nitakwambia umpe pesa" tukacheka sana na akaniuliza "na wewe vipi kuhusu ndugu zako" nikamwambia "nina changamoto kubwa sana lakini sio kubwa kiasi nishindwe,nitasonga tu" akasema "ahadi yangu itunze,usimwambie mtu siri hii" nikamwambia "nakumbuka sana na nitaitunza siku zote za maisha yangu mpaka siku utakapotoka,utakapokuwa huru tena na tukaungana pamoja" akasema "naingoja kwa furaha sana siku hiyo" nikamwambia "lakini vipi kwa hizi pesa tulizopata haziwezi kubadilisha chochote katika hukumu yako?" Akacheka na akasema "natamani iwe hivyo Rojas lakini nimepoteza matumaini sijui kuna muujiza gani mbele yangu,sijui,sitaki hata kuyazungumzia hayo" nikamwambia "sawa,basi tutangea wakati mwingine" akasema "basi usichelewe sana hata kuja kunisalimia tena najua kuna kipindi utakuwa busy hutakuwa huji kabisa" nikamwambia "haiwezekani lazima nitakuja na nikikumbuka mafanikio yangu kuna mtu hiyo sauti tu yatosha kunikumbusha mi kuja" akanambia "Rojas wajua wewe ni mtu mwema sana,moyo wako ni wenye utu ndani yako lakini endapo ukishea na watu mambo yako ya sirini sana watu watageuza moyo wako utakuwa mbaya kuliko kawaida,basi endelea kutunza wema wako na siri zako ili watu ili wasiweze kukuharibu" kiukweli sikuweza kuelewa kwanini mtu huyu amekuwa akinisisitiza sentensi hii mara nyingi,hii sentensi amekuwa akiniambia toka nikiwa ndani gerezani kwamba watu ni wazuri wengine wana mioyo yenye utu ndani yao lakini watu wanawabadilisha kwa maneno,kwa kuchochea vitu vyenye hila ndani yao,watu wale wanabadilika na kuwa wabaya.
Nimekuwa nikikimbizana sana,michakato imekuwa mingi sana na ukiwa na pesa kuna connection ya watu wenye pesa wanakuja kwako,iki ni kitu cha ajabu sana kwani wakati nikiwa sina kitu watu niliokuwa nazungumza nao,watu waliokuwa wananisogelea katika maisha yangu ni watu wa hali ya chini sana yaani ni mtu ambaye hauwezi hata kumuomba hata kiasi flani cha pesa kwa mfano nikiwa hata na simu naweza kumkosa mtu wa kumpigia kumuomba hata elfu kumi,hao ndio watu waliokuwa wamenizunguka lakini wingu la pesa limekuja katika maisha yangu yaani kuna watu wanakuja kwangu wenye pesa,wenye kuzungumza habari ya pesa,wenye kuzungumza fulsa ya biashara flani,nami maombi yangu kila mtu apate pesa,kila mtu apate pesa kwa mazingira yoyote yale pesa ije kwenye maisha yako,vitu vinabadilika sana kwani hauwi kama mwanzo,ongea yako inabadilika,tembea yako inabadilika,akili zako pia zinabadilika,kuwaza kwako kuna badilika,yaani vitu vyako vinabadilika haviwi kama kawaida.
Nikapata mtu alinambia "kama una hela na uzidi kuwa na hela zaidi kuna eneo la kuwekeza pesa" akanishauri niwekeze pesa kwenye eneo la madini,sasa huo ni mwanga mpana sana,ni mambo makubwa sana mengine sitaweza kuyazungumza yote kwa upana lakini alinambia "chungulia huku uone jinsi michakato inavyofanyika na jinsi watu wanapata pesa,ukiwa na pesa unaweka pesa unapata pesa" mengi nilielezwa nami nilivutiwa sana na uko "nikasema basi ntachungulia uko" mimi ni kijana nimekuwa nikiendesha taxi na sina elimu kubwa ni elimu yangu hii yakujipambania katika maisha lakini nina neema ya kujua jua vibiashara biashara hivi,naona kuendesha taxi kulifanya akili yangu kukua kwa haraka kwahiyo akili yangu sasa inatizama wapi nitupe pesa wapi wapi nitupe pesa,tulifanikiwa kupata magari matano kwa pamoja na yote tukayafanya taxi ambayo yote yalikuja kwa pamoja,yalipofika tu jambo la kwanza kulifanya ni kwenda kule gerezani na kwenda kumwambia habari hizi,nikamwambia "hizi gari ni za kwako" akasema "hapana hizi gari ni za kwako Rojas,kwa sababu hauwezi kuandika jina langu,utaandika majina ya watoto wangu" nakumbuka sana hii sentensi, alinambia "Rojas katika vitu ambavyo unafanya sitakwambia vyote uandike kwa majina ya watoto wangu,tutakuwa tunagawana au unasemaje?" Sikupinga katika maneno haya, basi akanambia "basi katika magari haya mawili tu andika majina ya watoto wangu" nikamwambia "unajua bado uko gerezani na michakato ya nje bado haujajua,kuna process za hapa na pale,kuna vitu vya kuandika nitafanya hivyo lakini kama umekuwa ukiniamini mimi mtu mwema sawasawa neno lako ntalibeba na ntalifanyia kazi" tuliongea mengi na akanipa ushauri kuhusiana na biashara na akanambia "wewe ni mimi,wewe ni mimi niko uraiani sasa,ninafurahia kila hatua yako" nikamwambia "ahsante,nashukuru sana" mimi nimekuwa nikija huku gerezani mara kwa mara kuja kumpa feedback ya nini kimekuwa kikiendelea.
Familia yangu ilizidi kushtushwa mpaka nikaitwa na vikao lakini nakumbuka siku moja kaka yangu alinambia "mdogo wangu njoo tuongee" awamu hii kaka alizungumza mpaka alitokwa na machozi "kama ni mafanikio mdogo wangu mimi sikatai,mimi ni kaka yako sdna neno moja nipate amani moyoni mwangu,tunaangaika,tunateseka,unatusaidia ni kweli lakini sitaki mdogo wangu jambo baya likutokee,sitaki shida ikotekee kwani unajua jinsi ambavyo tunavyokupenda na jinsi ambavyo nakupenda,nimejitoa kwa mangapi kwa ajili yako,kuna siri unanificha mimi?" Unajua huyu kaka yangu na mpenda sana,alilia kwa machozi sana na nikaona SIWEZI KUMFICHA KWELI KAKA YANGU,naweza kuwaficha wote lakini kadri siku zinavyoenda naona hapa panazidi kuwa pagumu kwa kaka ndipo niliposukumwa kutamani kusema ili kaka awe na amani katika hili.
ITAENDELEA!