Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​


Sehemu ya 9


Siku mpya ikafika na mawazo yakiendelea kunitawala kichwani mwangu kwani mzigo wa pesa ulikuwa mkubwa sana pamoja na mawazo aliyonipa ndugu yangu kule jela yakufungua duka la nafaka lakini bado mawazo hayakuondoka kwani nikifikiria wingi wa pesa zile,maneno yale aliyonambia kule kiukweli mtanziko ulikuwa mkubwa tena sikuwa nimesema mwanzoni katika zile pesa kulikuwamo na pesa za kigeni aina ya dola,kiukweli mawazo juu ya chanzo cha pesa hizi hayakwisha kichwani,kiukweli napenda pesa ila nilitaka kujua kama kumefanyika dili hadi kupatikana kwake je ni dili la kiwango gani? Na mtu wa kunambia chanzo chake ni huyu ndugu naye kashanambia nisiulize chanzo nijue tu ni pesa halali,nikaanza kufanyia kazi yale mawazo yakufungua duka la nafaka kwani nikakubali kuwa sitaweza kujua ni kiasi gani cha pesa nilicho nacho na nikaachana na mawazo hayo na nikachukua milioni ishirini zakufanyia zoezi kama tulivyopanga na liwe duka la nafaka la jumla,nilitafuta nyumba nzuri ya kupanga, watu wanajua maisha yetu unajua na hata familia yangu wanajua mwenendo wangu,wanajua wapi napata pesa na kaka alipojua nimekwenda kupanga nyumba ya thamani kama ile aliniuliza "mdogo wangu unawezaje kuishi kwenye nyumba kama ile,naona sasa hivi unatukwepakwepa mishe zako sizielewi,unaweza kunishirikisha lolote?"

Nampenda sana kaka yangu tena ni kaka mwema kabisa hilo ndilo ninalolijua ni kaka mzuri sana lakini nawezaje kumshirikisha hili jambo japo kiukweli ndani yangu natamani kushea na mtu kuhusiana na hili jambo uenda akanishauri kitu kikanifaa kwa leo au kwa siku za baadae maana sasa hivi mawazo yote najiuliza mwenyewe na kujijibu mwenyewe lililo sahihi na lisilo sahihi yote nayawaza mimi mwenyewe kwani zaidi ya yule mtu hakuna mwingine anayeijua hii siri wakusema naweza nikashea nae na amenambia hata siku moja nisitoe siri hii kwa mtu yoyote,nilimwambia kaka "ni mtu tu ndio amepanga sio mimi ila amenambia mimi naweza nikakaa lakini yeye atakuja kukaa siku sio nyingi" akanambia "ni mfanyabiashara gani huyo,yuko hapa hapa nchini? Nikamwambia "ana mishe mishe zake tu anafanya" zaidi kaka alinisisitiza kuwa mwangalifu sana "kuwa makini sana na watu" nikamwambia "ni kweli kaka ila ni mtu mwema" akasema "kuwa mwangalifu unajua kwa shughuli unayofanya unakutana na watu wengi wengine sio wazuri si unaona kwa mfano ishu iliyokukuta kipindi kile ikatuletea taharuki kubwa,usije kuingia kwenye matatizo napenda kushirikisha ndugu katika mambo ambayo unakutana nayo hata katika watu ambao unakutana nao" lakini sikuweza kumwambia chochote kaka zaidi ya haya niliyomwambia.

Kwa wingi wa pesa nilionao yaani nikisema nianze kufanya matanuzi lazima nitaleta taharuki hasa kwa familia yangu na hata jamii inayonizunguka zaidi zaidi nikajikuta ni mtu wa kujiongelesha,nakumbuka niliwaambia familia yangu nina mpango wa kukopa,kuna mtu amenipa connection ya kukopa,wakanambia "unakopa kwa kipi ambacho utakirejesha yaani kwa hazina ipi itatumika kama dhamana ya mkopo maana unapoenda kukopa kuna taratibu zao kwamba una nini" nikasema "kuna mtu uko yupo anafanya kazi anasema kuna namna" "kuna namna ipi?p" ndugu wanahoji kwakuwa wote wanajua kama mimi nafanya deiwaka tu kwahiyo nakosa vitu vya kutetea hoja yangu lakini sikuacha kujisemesha nikaendelea kujisemesha ili mambo yatakapoanza kutokea yasije kuwashangaza wakumbuke matetezi yangu ambayo niliyasema awali kwamba kuna mtu yuko benki anataka kunikopesha,anataka kunifanyia mpango na vitu kama hivyo.

Katika ile nyumba niliyopanga nilifanya mchakato kama nilivyoelekezwa,katika chumba ambacho mimi ndio ninalala nilitindua mwenyewe kwa sababu ilikuwa hauwezi kusema niite mtu aje afanye hilo zoezi lazima atagundua kwamba kwanini huyu anachimba hapa chini anataka kuhifadhi nini na watu ni wepesi katika kushea vitu na watu kwahiyo ataenda kusema mbona yule alichimba hivi kwahiyo wakataka kujua kuna nini,hili zoezi nililifanya mwenyewe na halikuwa gumu kivile na ukizingatia makuzi yangu mimi ni kijana mpambanaji toka kitaa chochote ukinipa nafanya,niite kwenye ujenzi mi naendaa,niite kwenye jambo loloje mimi nafanya kwahiyo nilichimba kwa kadri nilivyoweza mwenyewe inatosha nikaweka sawa mazingira vizuri ili fedha zikikaa zikae vizuri na nikafanikiwa kufunika kwa namna sahihi kabisa ambayo mimi nikitaka naweza kwenda kuzichota sehemu salama na kuwa ngumu mtu kugundua kama mimi nina pesa ndani kwa nilivyohifadhi.

Nikaanza kufatilia mchakato wa suala zima la nafaka kwani nilimpata mtu akanipa mwongozo na nilimwambia mimi nina mtaji wa milioni ishirini na akanambia kwa mwanzo kwa biashara ya nafaka milioni ishirini ni mtaji mzuri kabisa,akasema "pesa hiyo hata ukitaka kuwekeza katika biashara nyingine inaweza kukupush ila wewe umesema nafaka yafaa sana,tutafungua duka na kuuza nafaka za jumla" nikamwambia "basi naomba mwongozo wako,naomba nisaidie katika hili kwa sababu nimekuwa nikitamani sana" ndipo alipofatilia na kupata eneo na kulipa eneo,yaani kulipia flemu na michakato mingine ikaendelea ili kuweza kuanza biashara na mimi ni mtanzania wa asili ya kutoka hapahapa Tanzania na nikalipa jina fremu yangu kwa jina la asili ya kutoka nyumbani kwetu,nilianza kuwa bize sana na kuna muda nilipata wakati nikaenda kuwatizama watoto wa mshkaji na safari hii sikuenda kinyonge kama nilivyokuwa naenda safari za nyuma,nilikwenda na vitu vingi sana kwa sababu nilienda kufanya shopping ya vyakula vya kutosha kabisa na hata yule mama yao alishangazwa sana na kitendo changu chaa mimi kupeleka vyakula vingi kama vile yaani karibu vyote vilivyokuwa vikihitajika nyumbani nilipeleka na akasema "eeh vyote unatuletea sisi? Nikasema "ndio" akasema "kwanini,kwanini? Kwani wewe hauna ndugu?" Na yeye ananiuliza nami nikacheka na kumwambia "hata nyinyi ni sehemu ya ndugu zangu kwa sababu nimeshakuwa marafiki na nyinyi" nikamwambia naomba nitoke na watoto,nikatoka na watoto na kuwapeleka shopping katika maduka na sikuwapeleka maduka madogo madogo ni maduka ya ukweli na kuwapa uhuru wachague wanachotamani kuvaa,yaani watoto walifurahi wakachagua viatu,majinzi,fulana,mashati nami nikalipa kwa ukweli watoto walifurahi sana,walifurahi mno na kikubwa mimi niliwaambia "baba yenu anawapenda sana" na kwakuwa baba yao yupo gerezani na watoto hawa wamekuwa hawapati nafasi kwa baba yao kwahiyo wanapokea tu sio ile usiliasi sana katika mapokeo ya kuhusu baba yao lakini mimi nikawa nimefanya kwa nafasi na niliyakamilisha hayo na nikarudi tena kule gerezani.

Nilipofika gerezani nikampa salamu zake kutoka kwa watoto na nikamuelezea kuwa nimewafanyia shopping na ni kwa kiasi gani watoto wamefurahia naye akafurahi sana kwa maelezo yangu na kusema "nakushukuru sana Rojas,nakushukuru na sina neno jingine zuri lakusema,nakushukuru sana lakini mbona wewe haujavaa mavazi yale ninayotamani kukuona nayo umevaa?" Nikamwambia "unatamani kunionaje?" "Nenda kanunue nguo nzuri sasa maisha yako Rojas yameshabadilika haiwezekani una pesa ndani uwe unavaa hivyo bwana" nikacheka nikamwambia "nimekuelewa" akasema "zile pesa ni za kwako Rojas,nikisema zile pesa ni za kwangu na zangu ujue ni za kwako kwakuwa wewe ndio upo uraiani hata ukisema uniletee haya mimi nafanya matumizi gani hapa? Sina matumizi ya kufanyia hapa ila wewe unayo,furahia maisha Rojas tena uwe na amani kabisa kwani mimi nafurahi unaponiletea habari za watoto wangu mimi moyo wangu unajawa na furaha,sina furaha nyingine zaidi ya watoto wangu mimi,nataka nione wanasoma vizuri sijui una mpango gani sasa?" Nikamwambia nimefanya moja,mbili,tatu nikamueleza mengi ambayo nimefanya akafurahi sana na nikamueleza kuwa kuna haja ya watoto sasa kuwapa elimu iliyo bora na akasema iliyobora sioni kama nimechelewa? Nikasema "kwa mfano huyo mdogo wala usiwaze nitatafuta shule nzuri kwa namna yoyote ile waingie uko" akaniuliza "unawaza nini kingine" nikamjibu "mengi nayawaza kuhusu watoto wake ikiwapo kuwapa elimu bora na maisha mazuri,nataka niwahamishe pale wanapokaa" basi ninapozungumza hivi anafurahi sana,anafurahi kweli kweli,alifurahi sana na katika mazungumzo akanigusia swala ambalo tulilizungumza mwanzoni "Rojas wewe ni bosi sasa,wewe ni tajiri mtoto" nikacheka na akanambia "biashara ya taxi kwakuwa unaifahamu na una uzoefu nayo kwanini usinunue taxi nyingi" nikamuuliza "nyingi ngapi bwana?" Akanijibu " kwa pesa ulizonazo unaweza unaweza kununua ngapi? Nunua gari tano,nunua gari tano alafu zitupe sokoni naamini hautajuta" nikamuuliza "kweli?" Unajua mimi nimekulia kitaa nimekuwa sina connection zozote sifahamu naanzia wapi?" Akanambia "najua,najua na sasa mimi nipo gerezani je nikusaidie kukukutanisha na mtu?"

Nikamwambia "mtu? Kuna mtu uko uraiani unafahamiane nae kwa ukaribu hivyo anaweza kunisaidia?" Akasema "yupo kuna mshkaji mmoja alikuwa anadili na mambo ya magari sasa umekuwa muda umeshaenda sana sijajua kama bado anaendelea kufanya hivyo " nikamwambia "wala usiwaze kwa sababu niko uraiani hakuna sab kitakachoshindikana nitatafuta namna yoyote kujua wapi naweza nikapata na sio mambo ya kutapeliwa" akasema "hilo la msingi sana,sawa,lini tena utaenda kuwaangalia watoto" nikamwambia "naangalia,naangalia namna bora lakini mimi nimewaza jambo moja zuri sana" akasema "jambo gani?" Nikamjibu "ikiwezekana,ikiwezekana kama yule mama atakataa habari ya kuwapeleka watoto boarding ikiwezekana niwachukue nikae nao" akasema "hatakubali yule mwanamke,hatakubali kabisa,hawezi kukuamini hivyo kukupa wale watoto hata kama umekuwa unaenda,hawezi kuruhusu kitu kama hicho,wala usiwaze kuhusu hilo pengine litakuja kufanyika baadae akishajenga imani na wewe na mimi nataka wale wakaa na mama yao pia wala sitaki kumnyang'anya yule mwanamke watoto maana yake na yeye ni faraja yake pia ila waweza watengenezea mazingira mazuri,wakaishi pazuri wakapata mahitaji yote,hilo ndio naona bora zaidi" nikamwambia "sawa,nimetamani kukuletea vitu vingi sana huku gerezani ila vichache hivyo nimeleta" akasema "si unajua hivyo vingi ntaviweka wapi tena lakini nashukuru sana,asante sana" alishukuru saana yaani kiwango cha kushukuru kilikuwa cha juu mno,ile hofu aliyonipa mwanzoni hakunipa safari hii,niliondoka nikiwa na furaha nasikia moyo wangu umeanza kuwa na amani kwa mazungumzo tuliyoyafanya.

Biashara iliposimama sasa na kaka alipojua kuhusiana na hili kiundani kwamba ni mimi ndio nimefungua hili duka alinambia "mdogo wangu njoo tuzungumze,njoo tuzungumze hauwezi kuendelea kunikwepa njoo tuongee" nikapata muda nikakaa na kaka,kaka alinambia "mimi ni nani kwako?" Nikamjibu "wewe ni kaka yangu" akaendelea "unaweza kunificha jambo lolete mimi na ukafanya mambo kwa siri? Pesa ya kufungua duka la nafaka umezipata wapi? Sisi tunajua maisha ya familia yetu,umekuwa unatoa pesa hata mimi nikasema labda ni huyo mfadhili lakini na hili duka ni nani tena? Ni yule mtu aliyekwambia upange ile nyumba kule? Nikamwambia "kaka kwani shida ni nini,inamaana kila kitu katika maisha yangu natakiwa kukiongea kwako? Nilipomwambia kaka alishangaa akanambia "Rojas unanijibu mimi hivyo?" Kwa sababu naweza kumueleza nini kaka kuhusiana na hizi pesa zaidi zaidi nitamdanganya nami sitaki kumdanganya na ndio maana sitaki kuzungumza habari kuhusiana na hizi pesa.

Nampenda sana kaka yangu lakini siwezi kumueleza huu ukweli lakini aliniambia sentensi moja "waweza kuona umewin kwa kutokusema au kunidanganya lakini Rojas wewe ni mdogo wangu na ninakupenda sana na sisi kama familia tunakupenda,hatutaki kukupoteza wala upatwe na matatizo yoyote,usiwaze kunishirikisha mimi naweza kukuharibia dili lako zaidi zaidi ntakushauri yaliyo mema,sijajua unafanya dili gani,sijajua la halali au sio la halali lakini mimi nipo kwa ajili ya kukushauri yaliyo mazuri,mimi ni kaka yako" hatukuelewana na kaka nikaondoka zangu niliendelea na mishe zangu kama kawaida.

Nilipata muda na nikamtafuta yule mwanamke ambaye yule mshkaji wangu wa jela alikuwa anampenda sana (yule mchumba wake),iwapo yule kaka angekuwa uraiani huyu ndio angekuwa mke wake wa ndoa kabisa,anasema "mwanamke wa ndoto yangu,mwanamke ambaye nilimpenda sana" nilipoenda kumtembelea nilimpelekea pia vitu mbalimbali hasa vyakula vya nyumbani,hii ni mara ya pili namtembelea huyu mwanamke na kikubwa nilienda kumwambia "nina salamu zako kutoka kwa mwanaume ambaye anakupenda sana" alicheka na akafurahi nilipompatia zile zawadi na akanambia "kwanini unaniletea hizi zawadi mimi,mimi nilishbmua kuanza maisha yangu mapya,hajakwambia chochote kwani? Nikamwambia pengine anajua umeshaamua kuanza maisha mapya lakini upendo alionao kwako ni mkubwa sana na kwa sababu anaishi anasema upendo wake kwako hauwezi kupotea na amenitumia kuja kukwambia nami ni mjumbe mwema,rafiki mwema nimekuja,nimekuja kukujulia hali,kukupa salamu na kukuletea hivi vitu,akasema "usijisumbue kuingia gharama na kuniletea mimi hivi vitu" nikamwambia "usijali nimekuja kukusalimia kwa upendo" akapokea na nikampatia kiasi cha pesa,nilimuachi laki nne akashangaa na kunambia "kwanini unanipa pesa? Yaani Kwanini?" Angejua kama hizi pesa zinatoka kwa mwanaume ambaye yuko gerezani ila ndio hivyo hauwezi kusema na kwakuwa mimi ni mjumbe tu nimekuwa nikiwatendea wema watu hawa ambao huyu mtu alitamani kama angekuwa uraiani wafurahie maisha,sikuishia hapo kwani nilirudi tena kwa yule mama na kuketi na kuzungumza nae anataka kufanya nini,alicheka sana siku niliyomuuliza hilo swali,alisema "eeh unataka kujua mimi nataka kufanya nini ili wewe ufanye nini?"

Nikamwambia naweza kukushauri kitu au kama unahitaji mtaji au kukukopea mtaji mahali ukafanya biashara" akasema "nina mawazo mengi ila sina tu msingi maisha yangu yamevurugwa,si unaona yule mwanaume yuko kule gerezani anafanya cha maana nini,maisha yake yameishia uko,ndugu zake hawajali lolote kuhusu mimi na siwataki hata kuwaona,watoto hawa naangaika nao mimi ndio kila kitu" nakumbuka nikamwambia "basi angalia biashara gani unaweza ukafanya alafu nishirikishe,kitu kingine pia naona hapa unapoishi naona mazingira sio mazuri kwa watoto,nina jambo nilifikiria na jambo nililofikiria kwanini nisitafute nyumba ambayo itakufaa zaidi wewe pamoja na watoto" akanambia "unitafutie nyumba mimi? Unitafutie nyumba kwa sababu gani? Nikamuuliza "kwanini umestuka nami nimeshakuwa sehemt ya familia" akaniuliza "unamaanisha nini,unataka nini kwangu? Nakumbuka huyu mama aliniuliza hili swali,unajua mimi ni kijana mdogo na huyu kwangu age ilikuwa imeenda kidogo,sio age zangu kidogo sio age zangu lakini kwa jinsi nilivyomwambia akaona labda ni wale vijana wahuni nini (wapenda majimama[emoji23])au kijana anakuja kuja amenitamani nini? Yaani akili kama hizo na nikajua ndio mawazo anayoyawazia hayo,nikamwambia "mimi ninawapenda sana hawa watoto kwa sababu ya rafiki yangu na kama mimi Mungu amenibariki napata chochote kwanini nishindwe kufanya vitu vilivyo bora kwa watoto ambao ni wa rafiki yangu,fikiria kuhusu hilo alafu ntakapokuja utaniambia" huyu mama mara zote nyuma nilizokuwa nakuja uwaga ananikaziaga macho,tukiwa tunazungumza uwaga na maneno flani mfano ni nini? Umekuja kufanya nini na maneno kadha wa kadha ya shombo lakini leo huyu mama hata angalia yake ilikuwa ya uoga na nidhamu,unajua mtu anakuangalia anaona haya flani kwa matendo yake ya nyuma kwako,akanambia "kwahiyo utakuja lini?" [emoji23]
Nikawa naulizwa mimi tena hapo wakati uwaga hana hata swaga hizo wakati ukija atakupa maneno ya shombo kama yote lakini leo nikaliona tabasamu lake,akaniuliza "utakuja lini?" Nami nikamjibu "nitakuja,kwani wewe ulitaka nije lini?" Akanijibu "wakati wowote hata kesho jioni ntakuwa nshapata majibu" nikawa najisemea moyoni mwangu "pesa,pesa ni kitu kingine kabisa katika maisha ya mwanadamu hapa duniani,pesa ina nguvu,pesa inasema,pesa inaongea,pesa ina siri nzito sana mimi katika maisha niliyopitia nikagundua siri ya nguvu ya pesa ni ya ajabu sana" nikaondoka kwa huyu mama nikiwa natabasamu lakini kaka yangu alizidi kunisumbua sana akitaka kujua vyanzo vyangu vya mapato vinatoka wapi,akiwauliza washkaji zangu,watu zangu wa karibu lakini hakuna hata mtu mmoja anayejua chochote kwa sababu sijawahi na mtu yoyote yule,wakati huo nikiendelea na michakato ya kujikita kwenye biashara ya taxi yaani naagiza magari mazuri na natafuta vijana na kwa sababu mimi nina uzoefu si haba hii inaweza kuwa mwanzo wa biashara hii kuweza kufanikiwa.



Itaendelea!



ITAENDELEA!
Hapa nimemkubali kwakweli akitimiza ahadi Mungu atambariki[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​



Sehemu ya 8





Ahadi ambayo nilimuahidi huyu kaka ambaye nilikutana nae gerezani nakunifanyia yote haya sijaitimiza bado yaani kama kungekuwa na mtu angekuwa anaijua hii stori angeniuliza kwanini hadi muda huu sijaenda gerezani kwa mtu aliyenipa mwongozo kuhusu hizi pesa,yaani kwanini naanza kufanya kinyume na makubaliano tuliyoyafanya,kiukweli nilikuwa sina jibu,mipango ikaanza kuwa mingi sana yaani kila ninachofikiria kufanya naona sahihi,kila nikiwaza naona hiki ni bora zaidi ya kile kwa sababu sijawahi kuwaza katika maisha yangu kama naweza kukutana na pesa nyingi kiasi hiki,pengine ningewahi kuwaza ningelishakuwa na mipango thabiti lakini kwa sababu nilikuwa na fight for food yaani maisha ya kupambana kwa ajili ya tumbo tu yaani siku nenda siku rudi na sasa nimepata pesa,nikajiwazia hivi kula ni nini yaani kwa pesa niliyokuwa nazo hizi ni za kwenda kufanya vitu vikubwa sana na wala si za kuwaza tena kuhusu kula,nikajikuta nawauliza watu "hivi kwa mfano ukipata pesa nyingi unaweza kufanya kitu gani?" Kila mmoja ana mawazo yake wengine wanasema "nitajenga nyumba nyingi sana na nitapangisha huku mwenyewe nikiwa nimekaa tu nakula kodi" yaani mawazo ni mengi nawezaje kufanya kiukweli akili ilikuwa inawaka moto.

Katika harakati hizi nakumbuka sana siku moja,naikumbuka sana hiyo siku,nakumbuka ilikuwa ni majira ya saa nne usiku nilikuwa nimechoka sana nikasema ngoja nijiegeshe nipumzike tu,sikuwa nimejipumzisha kitandani bali ilikuwa kwenye kochi,wakati nimejipumzisha nikaota ndoto na uwaga sinaga kumbukumbu mimi ya mambo ya ndoto kwani kile ntakachokiota kinapotelea juu kwa juu lakini ndoto hii kwanini naizungumza pengine naiona kwangu haikuwa ya kawaida kwani nimeota ndoto niko kwenye kijiji kile nilichokuwa nimeenda kwenda kuchukua hizi pesa na nimejiona nipo ndani ya kile kijumba ambacho mshkaji amenielekeza na taratibu zote mpaka kufanikiwa kupata hizi pesa,nikiwa katika hiki kijumba nikawa najiona nimelala katika kile kitanda cha kamba,kitanda ambacho ndicho nilielekezwa kufata zile pesa,yaani nimelala hapo alafu nikawa najiuliza kwanini nimelala hapa ilihali mimi ni mtu mwenye pesa nyingi na nikiwa katika hiki chumba hakikuwa na mwangaza wakutosha yaani kama mshumaa umewashwa yaani mwangaza wake ni hafifu,nilisikia sauti ya mwanamke akinambia maneno haya "geuka huku unione" nami katika ndoto nikageuka,yaani sasa huu mwangaza ambao niliuelezea kuwa ni hafifu na sikujua unatokana na nini na fikara zangu zikawa zinahisi labda ni mshumaa kwa sababu ilikuwa ni ngumu kitu kukiona vyema na nilimuona mwanamke mmoja mnene sana,mnene mno katika kona ya hiki chumba,sauti ya huyo mwanamke naikumbuka siku zote katika maisha yangu kwa sababu alinambia "maisha yako wewe ni ya hapa,hizo pesa unazoziwaza uko nazo ziko wapi? Hizo pesa si za kwako,unajua yeye kazitoa wapi? Kwanini unaingiwa tamaa? Mbona ni mapema sana unaingiwa tamaa? Ni rahisi sana mtu kupata pesa? Mbona wewe katika maisha yako haujawahi kupata pesa kama ni rahisi,unajua huyu alifanya nini mpaka kupata hizi pesa?" Kiukweli katika ile ndoto huyu mwanamke mnene alinifokea sana na alinambia "usile jasho la mtu bila ya ruksa yake,rudisha jasho la mwenzako maana haujui vyanzo vya pesa hizi,fanya haraka rudisha pesa za mwenzako" nimekuja kustuka kwende ndoto niko kawaida nimelala pale kwenye kikochi kiukweli niliogopa sana yaani huyu mwanamke mnene ambaye sura yake sikuiona vyema ambaye kiumbile ni mwanamke sikuwahi kumuona wala kumsikia kabla,yaani ni vitu vipya kabisa kwangu,nikawa najiuliza "ndoto gani hizi au kwa sababu nawaza sana kuhusu pesa?" Yaani kama alarm ikalia kwenye kichwa changu,nikawaza lakini ni kweli mtu azifukie pesa kule mashambani na bila kumpa mtu yoyote ambaye ni ndugu yake,watoto wake wanateseka kule,amesema ana mwanamke wa maisha wake je ameshindwa kumueleza hata huyo mwanamke anayempenda sana pengine hasiteseke kwa maisha anayoishi uko uraiani aje anipe mimi? Au ni pesa za mambo ya nguvu za giza? Hofu iliingia ndani yangu,nilipatawa na hofu sana kwa sababu ni kweli kupata pesa si kitu rahisi mbona mie napambana sana,mbona mie napambana katika kazi nyingi ninazofanya na sijawahi kupata za kusema angalau nipate pesa nijenge,ninunue gari na nipate hivyo vitu angalau moyo wangu unatamani,mbona sijawahi kupata? Yeye hizi pesa alipata wapi? Kiukweli mpaka kumepambazuka sikupata usingizi kabisa yaani nikajiwa na hofu sana kwa sababu kama nilitishwa katika hii ndoto sikujua imekuja katika mazingira ya wema,sijui kwanini ndoto inijie lakini imekuja kunipa hofu.

Nilikaa kama siku mbili nikaamua kwenda kule gerezani,mimi mwenyewe nikaenda kule gerezani na nilipofika nikapata nafasi ya kuzungumza na yule mshkaji wangu na kiukweli aliponiona alifurahi sana,alifurahi sana akanambia "nilijua tu Rojas utakuja lakini mbona umekuja kwa kuchelewa?" Nikamwambia "unaona nimechelewa? Mbona sijachelewa" akasema "hapana nilitegemea ungekuja mapema zaidi kuliko leo ambavyo umekuja" nikatabasamu nikamwambia "nimekuja huu ni wakati sahihi" akanambia "mbona nakuona huna furaha,kwanini hauna furaha kwani haujafanikiwa katika jambo letu? Nikamwambia "nimefanikiwa" akanambia "najua una shauku ya kutaka kujua nini kipo ndani ya ile mizigo,unadhani ulitegemea kukuta dhahabu kama dhahabu zikiwa wazi lakini umekuta vitu vimefungwa na kufuli" nikamwambia "kwani nilitakiwa nisijue kilichomo ndani mpaka ntakapokuja na mzigo mpaka huku? Akanambia "ndio" nikamwambia "ningewezaje kutembea na kitu ambacho sijui kuna nini ndani?" Akanambia "Rojas lakini nilikwambia utakapokuja na huo mzigo utakuja kwangu na mimi ndio ntakupa maelekezo" nikamwambia "ni kitu ambacho hakiwezekani wewe unajua,tazama mambo yalivyo barabarani kukaguliwa na isitoshe mimi nimeenda kule nikiwa siko vizuri kiuchumi kwahiyo sikuweza kuhatarisha maisha yangu ilibidi nijue nini nabeba isije nikabebeshwa maiti za watu au nikabebeshwa viungo vya watu bila kujua nikajikuta nimeingia tena katika matatizo pasipo kujua na si nitaonekana mimi ni kijana mpumbavu" akanambia "mbona Rojas unaongea maneno hayo" nikamwambia " hapana nimekuja,nimekuja kukusikiliza" akasema "sawa,nashukuru sana,nashukuru sana umekuja nilikuwa nasikia sauti ndani yangu ikinambia hautakuja Rojas,hautakuja,ulivyoziona pesa ulijisikiaje? Haukujisikia kuchanganyikiwa?" Nikacheka,.nikamwambia "kwanini" akanambia "ndivyo inavyokuwa kama haujawahi kama mtu haujawahi kukutana na pesa labda katika maisha yako umeshawahi kuona shilingi ngapi,umeshashika shilingi ngapi? Labda milioni tano,milioni kumi,milioni ishirini au thelasini au hata milioni hamsini,sabini au mia lakini pindi unapokutana na pesa nyingi sana unaweza jikuta unachanganyikiwa,haujawahi kuchanganyikiwa?" Nikamwambia "kwanini unambie hivyo,pesa ambazo sijazitafuta nawezaje kuchanganyikiwa nazo zaidi tu yakupewa mwongozo" akasena "vizuri,Rojas umefanya vizuri sana kuja,si nilikuambia? Umeniamini katika kila nililolisema? Basi na wewe timiza ahadi uliyonipa" nikamwambia "kwani nilikosea kufungua yale matranka na kuzitoa zile pesa na kuzihifadhi katika mazingira mazuri?" Akasema "nilitamani uyabebe matranka yote lakini nimekuelewa mambo yamebadilika na ningekuwa mimi ningefanikiwa kuyabeba matranka lakini mambo uko uraiani sijui yakoje wewe ndio unajua siwezi kukupinga unachosema,kuna kiasi cha pesa chochote ulichotumia?

Nikamwambia "ndio,si nilikwambia nimeenda katika mazingira gani nikawa nahitaji pesa kwa ajili ya kuhonga ili nipite,nilitoa zile pesa na kuweka katika visalfeti" akasema "pesa zote zile? Ulizipangaje? Nikamwambia "nilitumia akili ya ziada kama ulivyonielekeza" akanambia "jicho langu lilipokuona mara ya kwanza lilikuwa na imani na wewe,nashukuru sana" nikamuuliza "hizi pesa umezipata wapi,pesa nyingi kiasi hiki na kwanini pesa hizi haukuzihifadhi benki sehemu ambako ni salama,kwanini umezihifadhi pesa kwenye kijumba tena cha zamani" akanambia "nilijenga kile kijumba kwa kusudi sana,kwani ni mimi peke yangu ndio nimefanya hivyo? Ngoja nikusimulie jambo moja,hizi fedha ni fedha halali kabisa,hizi fedha wala si fedha bandia,hizi ni fedha ambazo nimezipata mimi kwa jasho langu,kwa nguvu zangu,kwa kutumia akili zangu na uwezo wangu wote,niliona sehemu sahihi yakuzihifadhi ni pale" nikamwambia "bado haujanipa majibu lakini kwakile nataka kujua,mbona benki zipo ambapo watu wanahifadhi pesa nyingi sana" akasema "unajua mimi nilikuwa nafanya kazi gani? Nikamwambia "sijui" akasema "mimi nilikuwa ni raia tu nilikuwa nafanya shughuli zangu mbalimbali japo nilikuwa na kipaji cha tofauti kidogo ambacho nilikuwa naweza kuwasaidia watu wengine ambao hawana kipaji nilichokuwa nacho mimi" nikamwambia "kipaji gani hicho" akajibu "ni kipaji ambacho naweza kuzungumza hata na watu wenye elimu kubwa sana,watu wenye uwezo mkubwa wanaweza wakanifata na hata wakazungumza na mimi na wakaniuliza nina shauri kipi katika haya,ndipo nilipo pata pesa hizi kwa jasho langu na kwa nguvu zangu,nikazihifadhi pale na wala usiniulize maswali mengi kwa sababu pesa umeshazipata na ni muda wa kutumia pesa,Rojas kuanzia sasa maisha yako yanaenda kubadilika" nikamwambia "naomba niambie chanzo cha wewe kupata pesa ili niwe na amani na hizi pesa" akanambia "pesa hizi zina amani tu kama utafata na kusikiliza yale nitakayosema lakini kama utaenda kinyume na yale unayoyazungumza hizi pesa haziwezi kuwa pesa nzuri sana kwako" nikamwambia "mbona unanitishia? Mbona sentensi hiyo haukuniambia toka mwanzo" akanijibu "nilikwambia,nilikwambia na ndio maana nikakwambia uape au nani aliapa? Wewe si ndio uliyeapa Rojas? Mbona naona sasa hivi sentensi zako na sauti yako vimekuwa kama vimebadilika,kwani Rojas pesa zimekuchanganya? Mbona mimi nakuona una utulivu sana na katika watu niliowaamini ni wewe,kuna kitu kimebadilika kwako? Kuna vitu ambavyo tulizungumza mwanzo unaona hauwezi kuendelea kuvishikilia? Rojas hizi pesa ni zetu sote na mimi nilizitafuta lakini siwezi kuzitumia kwa sababu niko gerezani lakini wewe waweza kuzitumia hizi pesa lakini kwa makubaliano ambayo tumekubaliana" nikamwambia "sawa,nimekuwa na hofu sana kuhusu hizi pesa" akanambia "kwanini" nikamwambia "sijawa na amani nazo" akaniuliza "kwanini hauna amani nazo? Kwanini ukose amani nazo au uliziwazia mabaya? Kama uliziwazia mabaya lakini kama uliziwazia mema hakuna jambo lolote baya Rojas" kiukweli sentensi zake zikaanza kama kunipa ukakasi hivi kwa sababu ni kweli nilianza kuwaza mabaya na mimi nimekuja huku kwa sababu ya ile ndoto tu niliyoota ndio kimenisukuma ndio nimekuja hapa,kwanini aniambie sentensi hizi niliziwazia mabaya na nini hivyo yaani,nikamwambia "nilishafanya ulichonielekeza sasa nipe maelekezo mengine kwa sababu hizi ni pesa nyingi ni hatari zaidi kukaa nazo pengine nitastahili kuzipeleka benki au unanielekeza vipi" akanambia "hata senti moja haitakiwi kwenda benki" nikamwambia "kwanini,kwanini zisiende benki na nawezaje kukaa na pesa nyingi ndani kiasi hicho,vipi kuhusiana na usalama wangu? Nawezaje kukaa na hizo pesa zote? Kama pesa ni halali hakuna shida yoyote kwanini tusipeleke benki? Akanambia "Rojas kumbe hujui? Si utaulizwa maswali mengi ukizingatia wewe ni dereva taxi tena ambaye hata usafiri hauna ni deiwaka unapata wapi pesa kama hizo,unaweza kuthibitisha kuwa pesa umepata wapi? Kama una mahali unaweza kuorodhesha maelekezo yakujitosheleza kuhusiana na hizo pesa basi unaweza ukazipeleka kwa sababu watu wanaweka pesa benki sama sawa na kile wanachokipata kwenye movement za maisha yao ya kila siku,ebu niambie mzunguko wa pesa yako,pesa nyingi kama zile umezipaja wapi,utasema umezipata mashambani,kwenye shamba la nani? Utasema ulioteshwa,ulioteshwa vipi? Unataka pesa zote nilizozipambania kwa maisha yangu yote zishikiliwe kwa ajili ya uchunguzi?"

Nayakumbuka haya maneno aliyonambia huyu kaka,tunazungumzia pesa nyingi ambazo mpaka sasa hivi nimezikusanya idadi yake ya pesa nimezihesabu mpaka nachanganyikiwa,nikatulia na kusubiria maelekezo yaidi kujua nini sasa nafanya na hizi pesa,akanambia "nini unawaza kichwani mwako,kuna kitu ambacho umekuwa ukitamani kufanya pale utakapopata pesa nyingi?" Nikamwambia "hapana,sikuwahi kuwaza hata siku moja kama ntakuja kupata pesa kiwango kama hiki" akanambia "pale ulipofanikiwa kuzileta hizi pesa na kuwa nazo ndani nini ulifikiria kichwani kwako,nini,kufanya kitu gani?" Nikamwambia "vitu vingi sana nimefikiria ila kwa sababu pesa sio yangu nikarudi kwa mwenye pesa anipe maelekezo kwa sababu najua ulihifadhi hizi pesa kwa siku zote ina maana ulikusudia kufanya kitu labda nisikie ulikusudia kufanya kitu gani" akanambia "nyakati hizo wakati nimepata hizi pesa sikuwa na uwezo wakuzitumia kwa nyakati hizo japo kuna vitu niliviwaza ingawa najua kwa sasa hivi mambo uko nje yatakuwa yamebadilika,wewe unaendesha taxi vipi? Unauonaje ulimwengu wa taxi kwa ujumla je niku chenye faida? Unajua kwa pesa zile tunaweza kununua taxi ngapi? Nikamwambia "na ndio maana nikazungumzia habari yakupeleka pesa benki kwa sababu mojawapo ni tujue zile pesa ni shilingi ngapi" akasema "hauwezi kujua idadi ya zile pesa,wewe ni kuzitumia tu" nikamwambia "kwanini unasema hivyo,mbona unanipa wakati mgumu sana na ni pesa gani ambazo hazihesabiki wakati watu wanahesabu hadi mabilioni na mabilioni na mabilioni lakini inajulikana ni kiasi gani cha pesa kwanini zile ziwe shida kuzihesabu?" Nilimuuliza hivyo na mengineyo kadhaa ila kwa sababu muda ni mdogo haujitoshelezi kuzungumza hayo yote na alinambia "muda ni mdogo lakini nikupe muda ukajifikirie,rudi baada ya muda mfupi usikawie sana,utakachokiwaza njoo unishirikishe nakutegemea sana kwa sababu wewe ndio unajua hali ya uko nje,angalia ulimwengu wa udereva wa taxi kwa ujumla uone unaweza kuagiza magari mangapi" nikamwambia "siwezi kuagiza magari ngapi wakati sijui idadi ya kiwango cha pesa,ni dhambi kujua kiasi cha pesa nilichokuwa nacho mule ndani? Akasema "Rojas hauwezi kujua kiasi cha pesa kilichomo mule ni nyingi sana" nikamwambia "naomba hata nipambane nitafute hata mashine nihesabu zile pesa" akasema "uliahidi kunisikiliza kwa kila ntakachokisema mbona tena kama unataka kuzungumza vya kwako wakati pesa ni ya kwangu? Nikamwambia "pesa ni ya kwako lakini usinitumikishe" akanambia "kwanini unanambia hivyo" nikamjibu "hapana kwa sababu unavyozungumza vitu mimi sivielewi" akanambia "nenda nyumbani kidogo pumzika,tafuta nyumba nzuri Rojas,tafuta nyumba nzuri ya wewe kuishi,tafuta kitu uanze kukifanya mapema ili watu watakapoanza kuona macdiliko yako wasihisi vitu vibaya" nikamwambia "una maana gani? Akanijibu "tafuta hata biashara ndogo" nikamuuliza " kwa mfano kama nini" akanambia "fungua duka la nafaka" nikamwambia "sina hobie na hivyo vitu" akanisisitiza "fungua duka la nafaka muweke hata ndugu yako hapo na naamini mtaji unaweza kufika milioni ishirini,mtaji wa milioni ishirini kwenye nafaka unaweza kuuza nafaka za jumla,wewe unauza vitu vya jumla" nikamwambia "kumbe una mawazo" akanambia "nina mawazo,milioni ishirini inaweza kukuwezesha kwanza,tafuta nyumba nzuri,usijenge panga nyumba nzuri haraka sana,usipange kwenye nyumba ndogo kwani zile pesa zinahitajiwa kuchimbiwa chini unakuwa unaweka mazingira mazuri kabisa kwani wewe ndio utakuwa unaenda kuzichukua,ndio usalama na ni lazima uzihifadhi katika matranka"
Baada ya maagizo haya ya mwisho nikayabeba na kuondoka zangu kurejea nyumbani ingawa mara baada ya kutoka katika mazungumzo na huyu mtu hofu ikawa juu zaidi kutokana na majibu aliyokuwa akinipa,hofu ikanijia katika hali ya kibinadamu kwani kweli pesa anazo lakini kwanini hazihesabiki na wakati idadi ya pesa zinaweza kuhesabika yalinipa hofu!
Yajayo yanafurahisha!


ITAENDELEA
Nitarudi

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​



Sehemu ya 10



Michakato ikawa inaendelea huku duka likizidi kupanuka nami kwa upande wangu nikawa bize sana kiasi cha kunifanya kutoweza dukani kwa muda mwingi kwahiyo nikamchukua mmoja wa wanafamilia na kumuweka kusimamia shughuli za pale dukani akiwa kama muuzaji nami nitakuwa nikipita kutazama mahesabu lakini kaka alimzuia na akasema "kwanini tunauliza maswali yasiyo na majibu,kama wewe ni ndugu yetu kweli na unataka tuwe washirika na vitu vyako kweli kwanini unashindwa kutuambia ukweli?" Ilinipa shida sana hiyo na naamini hata wewe leo hauna pesa na watu wanakuna katika maisha ya kawaida siku ukapata pesa katika mazingira yoyote kwa sababu pesa inaweza kumjia yoyote yule,tizama mimi zimenijia katika mazingira haya sikuwahi kuwaza,sikuota ndoto na zimekuja nyingi katika maisha yangu hata wewe utakapopata pesa watu wakaona mabadiliko yako lazima kuna vitu watazungumza,kama hawatazungumza umejiingiza kwenye mambo mabaya,umejiingiza kwenye ushirikina utawatoa sadaka kuna shuhuda shuhuda za uongo watakwambia kuhusu wewe kumbe sio,mimi hizi pesa sijapata kwa njia zozote watu wanaweza wakanijudge nazo,nimepata katika mazingira ambayo nakueleza lakini siwezi kuzungumza,ni vitu ambavyo havizungumziki,nikamwambia kaka "mtakapokataa sitapoteza hata dakika moja,nina uwezo wa kuajiri mtu na nitamlipa tena nafikiri ntafanya nae kazi kwa mazingira mazuri kwa sababu atafanya vizuri na nitamlipa vizuri pia" lakini huyo ndugu yangu yeye alikuwa na utayari "mi nafanya bwana,kaka yeye ndio anazuia mi nafanya bwana" nikamwambia "tulia hapa fanya kazi,hufanyi kazi kama ndugu tu,unafanya kazi nakupa mshahara,wapi unaweza ukapata laki mbili mwisho wa mwezi na nakupa mahitaji yote laki mbili yaani umebaki nayo,chakula nakupa nauli nakupa utapata wapi kazi kama hiyo na natakaka kuona mwendo wako mwanzo na kama utaenda vizuri biashara inalipa ntakuongeza mshahara,tulia ufanye kazi achana na maneno ya kaka".

Nilizidi kugawa majukumu kwa sababu kuna jukumu kubwa liko mbele yangu,kuna biashara kubwa iko mbele yangu sasa ambayo naenda kuitazama,sikuishia hapo kwani nikaenda tena kwa yule mama ambaye ana watoto wa yule mshkaji kule gerezani,nilienda kama nilivyosema mapokeo ya yule mama yalikuwa yamebadilika sana ,pesa imefanya mapokeo ya mama yabadilike,mama sasa hivi anatabasamu na anaongea na mimi kwa sauti tofauti kabisa na ile ya mwanzo,yaani sasa hivi naipata sauti flani nzuri nzuri kwa huyu mama na nakumbuka sana nilipofika kwa mara ya pili kwani mara ya kwanza nilimwambia ntafika kuchukua majibu na nikawa busy nilipopata nafasi nikaenda tena hadi aliniandalia chakula😂! Unaona? Pesa inakupa heshima,inakupa kibali,pesa inakupa vitu ambavyo hauwezi kuvipata kama huna pesa,ni kweli kabisa,nikapata chakula nikafurahi nikiwa na hawa watoto na nikamwambia "vipi kuhusu mawazo ambayo nilishea na wewe" akanambia "lolote utakalosema mimi nimeona iwe sawa,iwe sawa kwani siwezi kujua uliishi vipi na mzazi mwenzangu,siwezi kujua lakini ninachojua umekuja kwetu kwa mema tu" nikamwambia "ni kweli nimekuja kwa wema tu" nakumbuka tulizungumza mengi na akanipa michakato ambayo anataka kuifanya akasema yeye anapenda mambo ya vinywaji,anapenda mambo ya vinywaji yaani akifungua kama glocery inaweza ikamfaa,mimi nikamwambia "usiwaze kufungua glocery waza kufungua bar kubwa kabisa" akasema "kweli mi nifungue bar? Nimiliki bar ntaweza wapi?"

Nikamwambia "kwani wanaoweza wanawezaje,hata wewe utaweza" akasema "sijui,ntawezaje kupata huo mtaji wakuweza kufungua bar kubwa" nikwamwambia "wala usiwaze kuhusu hilo,kwenye bar uwa kuna namna yake unaweza usichukue bar nzima,unaweza kuwa na wenzako wewe ukachukua eneo la vinzaji wengine wakachukua eneo la chakula inategemea vile nyie wenyewe mnajipanga" akanambia "una mawazo kweli mazuri,umeniwa wazo zuri na umenipa akili nimekuwa sasa hivi nawazawaza vitu vingi lakini nimeona eneo la vinywaji mimi linanitosha kabisa lakini mtaji wake ni mkubwa sijui yani,sijui kama itawezekana" nikamwambia "wewe sema unachotaka,hicho unachotaka mimi kwangu itawezekana" aisee mama alifurahi sana,mama alifurahi sana kwa sababu sasa nimeshamaliza nataka kuondoka mama anatamani nibaki😂! Nabaki nafanya nini? Nabaki nafanya nini kwa huyu mama,nikamuaga na nikamuahidi ntakapokuja awe na majibu na ikiwezekana atafute hilo eneo liwe zuri,asitafute eneo ambalo hakuna biashara,atafute location nzuri nami nikamuahidi "nami nazidi kukutafutia uko kama nitapata eneo zuri nitakujuza mapema" tulizungumza na huyu mama haya manen kwa uzuri kabisa lakini najua huyu mama ana maswali mengi sana lakini alipokea ombi langu nililopeleka kwake.

Nakumbuka nimeondoka na kuendelea na mishe nyingine huyu mama akaanza kunitumia meseji "vipi Rojas uko poa? Wadogo zako huku ni wazima kabisa wanakusalimia sana" hakuishia hapo akawa ananipigia simu niongee nao,"ongea nao basi" nikamwambia "sawa" naongea nao nikawa mwenye furaha napiga nao story lakini akawa ananipigia simu majira hata ya usiku,majira hata ya usiku wa saa 4 ananipigia simu unaona,na hii ni nilipotoka round ya pili hii ambayo nilienda kuzungumza nae kuhusu kutafuta eneo la bar na nini,simu za usiku ananipigia ananiambia nini? Ananisalimia,ananitakia usiku mwema,basi tutaongea asubuhi,uko na nani,ananitumia meseji au tunazungumza kwenye simu na mazungumzo kama hayo😂

Mimi najua huyu mama anapotaka kwenda na kama nilivyosema awali kuwa pesa inaweza kumbadilisha kabisa mtu mawazo na kwa mtu unampa kwa lengo wewe wewe unalolijua na silo analowaza yeye,yeye anawaza vitu vingine kwa sababu huyu mama kwa jinsi nilivyoongea nae anavyowaza labda mimi nimefall in love na yeye,ndivyo akili yake ndivyo inavyomwambia na labda anaona ninavyoonesha nia yakutaka kumpa mtaji basi kabisa kwanini asiwe na mimi,ndivyo nilivyoendelea kuisoma akili ya huyu mama lakini mimi wala siko uko,yaani sijawahi kumtazama kwa huyu mama kwa umakini,sijawahi,yaani namuona ni mama ninayemheshimu,sijawahi ku pay atention kutazama chochote kuona kitanivutia kwenye upeo wa macho yangu kwake hata siku moja,nazungumza hiyo kwa ukweli kabisa,sijaona chochote kwa sababu nimebeba ile heshima ambayo mshkaji alinambia na mimi niko karibu na huyu mama kwa ajili ya hawa watoto ili nitimize ahadi ambayo rafiki yangu alinambia,nikasema ni akili zake tu ataelewa,atanielewa baadae wala sina haraka na hili.

Wakati michakato ikiwa inaendelea nikapata bahati kwa sababu niliwaambia watu wanitafutie eneo ambalo naweza kufungua bar,kuna mtu akanipa hiyo taarifa na nikamwambia huyo mama kuna eneo nimepata naye akanambia kuna eneo amepata akanambia "njoo Rojas ungekuja kwanza kuliona hili" nikamwambia sawa nikafunga safari nikaenda kuliangalia nikamwambia "sawa lakini lile mimi nililoambiwa naliona ni bora zaidi na ukilipenda wewe mwenyewe utakuwa na choice" akanambia "sawa" kweli tulienda pale na uzuri huyu mama ana uelewa sana yaani ameishi kwenye ulevi mpaka akawa na experience kubwa sana kwa sababu huyu mama ni mlevi mlevi sana😂. Tulizungumza mengi hapa na makubaliano tulizungumza nao hapa katika hii bar,walizungumza mambo ya biashara,mwanzo wa kufanya biashara kilibainika nami ikabaki ni kutoa tu pesa sawasawa na uhitaji wa huyu mama aliokuwa nao na nakumbuka tumezungumza sasa tumerudi nimdrop mahali ili mimi niendelee na mishe zangu nakumbuka huyu mama akanambia "sijawahi katika maisha yangu kukutana na mtu akanisuprise kama ulivyonisuprise wewe,yaani mpaka natafuta eneo hadi wenzangu wananiuliza ni nini umekutana nacho,ni muujiza gani nimekutana nao,wananiambia mimi ni muongo,nawaambia ni rafiki wa mzazi mwenzangu wananikatalia wanasema wewe ni mtu wako" nikamwambia "huna hata sababu ya kujieleza kwao kwa sababu hata ukijieleza,hata ukijitetea watakuwa na majibu yao ila wewe baki na unachokijua kuwa ni rafiki wa mzazi mwenzio,mimi ninachokuombea ni ufanikiwe,unajua biashara haitaki uweke mbele urafiki na usipageuze pale marafiki wanakuja wanakunywa wanakopa" akasema "siwezi kufanya hayo makosa,nimeangaika sana kutafuta mtaji,siwezi kufanya hayo makosa yaani siku unanipa pesa na kusema nifanye biashara na ndio mwanzo wa mimi kutoka katika umaskini,sitaishi tena kuwa mwanamke wakuombaomba,sitaishi tena kuwa mwanamke wa kukutana na mtu aniambie kwamba atanipa pesa niende nikampe furaha,sitaishi tena hayo maisha kwani nimekuwa nikiangaika kwa ajili ya watoto wangu ili wale,ili wavae na ndio maana nimekuwa hata na tabia ambazo najua unajua" nikamwambia "hata wala mimi sijakuhukumu kwa chochote kile naamini hata iki unaenda kusimama nacho kitawafaa pia na watoto" akasema "kabisa,nakushukuru sana" nikamwambia "sawa,kesho ntapita benki na nitakuletea pesa zote unazozihitaji" akesema "kweli" nikamwambia "kweli namaanisha" nilizidi kumchanganya akili ya huyu mama kiukweli nikachanga akili yake isivyo kawaida.

Hapo mimi sikuwa na ukaribu na wanawake kwa kiwango hiki nilicho karibu na huyu mama,nikizungumza hivi najua unaelewa yaani ule uclose wa kuzungumza hivi,mishemishe kama hizi tunatafuta,tunawasiliana,tunaongea,kwa maeneo kama haya yaani ulezi wa mtoto,malezi kwa ujumla sijui nini kwa mara yangu ya kwanza yaani nayaishi hayo,akinambia "watoto wananini,wanahitaji sijui nini yaani moja,mbili,tatu" siunajua hayo ni mambo ya watu wa familia nami bado ni kijana sikuwahi kuishi hivyo,niliachana na huyu mama nami nikaendeleatna michakato yangu kama kawaida.

Nazidi kukimbizana na nikamkamilishia ahadi yake ya pesa yule mama,nilienda kumpa taarifa mshkaji wangu kule gerezani nikimjuza hatua jinsi nimepiga,jinsi ambavyo nimefanikiwa nilimweleza yote "vipi na suala la kuwahamisha kutoka pale wanapoishi kwenda kwenye nyumba nyingine?" Nikamwambia "yote yatakamilika" akafurahi sana na akanambia "kuwa mwangalifu sana na yule mwanamke anapenda sana hela na kwenye hela yule mwanamke anaweza fanya chochote,usije ingia tamaa nae kwani ni mwanake ambaye hajawahi kuwa na utulivu,asije kukushawishi kwa sababu ameona umeanza kuwa na pesa ukajikuta siku umedondoka nae,nakutahadhalisha kwa sababu nakupenda kwani mwanamke mwenye kubadilisha wanaume kama nguo hafai,si ni kweli?" Nikasema "ni kweli,hawezi kufanikiwa kwangu na nimeshamjengea mazingira mazuri sana kwenye akili yake naamini mpaka sasa ameelewa siko upande huo" akasema "ameshakutegatega eeh?" Nikamwambia "sio sana" akasema "lazima ulishinde hilo jaribu mtu mzima yule" nikamwambia "ni kweli " mengi nilimueleza na nikamwambia harakati zote zinazoendelea na alizidi kufurahi sana,alinambia lakini nisimsahau yule mwanamke niwe naenda hata kumjulia hali na nimsikilize nini anawaza ambacho tunaweza kumfanyia,nikamwambia "sawa,hivi ni hawa tu katika maisha yako unaowathamini uliwaza ukifanikiwa katika maisha utawafanya wawe bora zaidi na vipi kuhusu shangazi yake kule kijijini?" Akasema "sasa hayo nakuachia wewe" nikasema "unaniachia mimi vipi wakati hao ni ndugu zako?" Akasema "kama uliguswa na shangazi kwa sababu ya mapokezi yake sawa lakini mbona mimi hawaji kunitembelea? Si kwa sababu wanajua sina kitu,si wanajua nitaozea gerezani? Si hata kama mmoja angetokeza ungechukua hata milioni kumi ukampa imfae kwa biashara lakini wameniacha huku wanajua mimi nimeisha sasa mimi naweza ninkfanyaje,eti Rojas nifanye nini sasa,kama kuna siku kuna mtu ataamka kuja kunitembelea nitakwambia umpe pesa" tukacheka sana na akaniuliza "na wewe vipi kuhusu ndugu zako" nikamwambia "nina changamoto kubwa sana lakini sio kubwa kiasi nishindwe,nitasonga tu" akasema "ahadi yangu itunze,usimwambie mtu siri hii" nikamwambia "nakumbuka sana na nitaitunza siku zote za maisha yangu mpaka siku utakapotoka,utakapokuwa huru tena na tukaungana pamoja" akasema "naingoja kwa furaha sana siku hiyo" nikamwambia "lakini vipi kwa hizi pesa tulizopata haziwezi kubadilisha chochote katika hukumu yako?" Akacheka na akasema "natamani iwe hivyo Rojas lakini nimepoteza matumaini sijui kuna muujiza gani mbele yangu,sijui,sitaki hata kuyazungumzia hayo" nikamwambia "sawa,basi tutangea wakati mwingine" akasema "basi usichelewe sana hata kuja kunisalimia tena najua kuna kipindi utakuwa busy hutakuwa huji kabisa" nikamwambia "haiwezekani lazima nitakuja na nikikumbuka mafanikio yangu kuna mtu hiyo sauti tu yatosha kunikumbusha mi kuja" akanambia "Rojas wajua wewe ni mtu mwema sana,moyo wako ni wenye utu ndani yako lakini endapo ukishea na watu mambo yako ya sirini sana watu watageuza moyo wako utakuwa mbaya kuliko kawaida,basi endelea kutunza wema wako na siri zako ili watu ili wasiweze kukuharibu" kiukweli sikuweza kuelewa kwanini mtu huyu amekuwa akinisisitiza sentensi hii mara nyingi,hii sentensi amekuwa akiniambia toka nikiwa ndani gerezani kwamba watu ni wazuri wengine wana mioyo yenye utu ndani yao lakini watu wanawabadilisha kwa maneno,kwa kuchochea vitu vyenye hila ndani yao,watu wale wanabadilika na kuwa wabaya.

Nimekuwa nikikimbizana sana,michakato imekuwa mingi sana na ukiwa na pesa kuna connection ya watu wenye pesa wanakuja kwako,iki ni kitu cha ajabu sana kwani wakati nikiwa sina kitu watu niliokuwa nazungumza nao,watu waliokuwa wananisogelea katika maisha yangu ni watu wa hali ya chini sana yaani ni mtu ambaye hauwezi hata kumuomba hata kiasi flani cha pesa kwa mfano nikiwa hata na simu naweza kumkosa mtu wa kumpigia kumuomba hata elfu kumi,hao ndio watu waliokuwa wamenizunguka lakini wingu la pesa limekuja katika maisha yangu yaani kuna watu wanakuja kwangu wenye pesa,wenye kuzungumza habari ya pesa,wenye kuzungumza fulsa ya biashara flani,nami maombi yangu kila mtu apate pesa,kila mtu apate pesa kwa mazingira yoyote yale pesa ije kwenye maisha yako,vitu vinabadilika sana kwani hauwi kama mwanzo,ongea yako inabadilika,tembea yako inabadilika,akili zako pia zinabadilika,kuwaza kwako kuna badilika,yaani vitu vyako vinabadilika haviwi kama kawaida.

Nikapata mtu alinambia "kama una hela na uzidi kuwa na hela zaidi kuna eneo la kuwekeza pesa" akanishauri niwekeze pesa kwenye eneo la madini,sasa huo ni mwanga mpana sana,ni mambo makubwa sana mengine sitaweza kuyazungumza yote kwa upana lakini alinambia "chungulia huku uone jinsi michakato inavyofanyika na jinsi watu wanapata pesa,ukiwa na pesa unaweka pesa unapata pesa" mengi nilielezwa nami nilivutiwa sana na uko "nikasema basi ntachungulia uko" mimi ni kijana nimekuwa nikiendesha taxi na sina elimu kubwa ni elimu yangu hii yakujipambania katika maisha lakini nina neema ya kujua jua vibiashara biashara hivi,naona kuendesha taxi kulifanya akili yangu kukua kwa haraka kwahiyo akili yangu sasa inatizama wapi nitupe pesa wapi wapi nitupe pesa,tulifanikiwa kupata magari matano kwa pamoja na yote tukayafanya taxi ambayo yote yalikuja kwa pamoja,yalipofika tu jambo la kwanza kulifanya ni kwenda kule gerezani na kwenda kumwambia habari hizi,nikamwambia "hizi gari ni za kwako" akasema "hapana hizi gari ni za kwako Rojas,kwa sababu hauwezi kuandika jina langu,utaandika majina ya watoto wangu" nakumbuka sana hii sentensi, alinambia "Rojas katika vitu ambavyo unafanya sitakwambia vyote uandike kwa majina ya watoto wangu,tutakuwa tunagawana au unasemaje?" Sikupinga katika maneno haya, basi akanambia "basi katika magari haya mawili tu andika majina ya watoto wangu" nikamwambia "unajua bado uko gerezani na michakato ya nje bado haujajua,kuna process za hapa na pale,kuna vitu vya kuandika nitafanya hivyo lakini kama umekuwa ukiniamini mimi mtu mwema sawasawa neno lako ntalibeba na ntalifanyia kazi" tuliongea mengi na akanipa ushauri kuhusiana na biashara na akanambia "wewe ni mimi,wewe ni mimi niko uraiani sasa,ninafurahia kila hatua yako" nikamwambia "ahsante,nashukuru sana" mimi nimekuwa nikija huku gerezani mara kwa mara kuja kumpa feedback ya nini kimekuwa kikiendelea.

Familia yangu ilizidi kushtushwa mpaka nikaitwa na vikao lakini nakumbuka siku moja kaka yangu alinambia "mdogo wangu njoo tuongee" awamu hii kaka alizungumza mpaka alitokwa na machozi "kama ni mafanikio mdogo wangu mimi sikatai,mimi ni kaka yako sdna neno moja nipate amani moyoni mwangu,tunaangaika,tunateseka,unatusaidia ni kweli lakini sitaki mdogo wangu jambo baya likutokee,sitaki shida ikotekee kwani unajua jinsi ambavyo tunavyokupenda na jinsi ambavyo nakupenda,nimejitoa kwa mangapi kwa ajili yako,kuna siri unanificha mimi?" Unajua huyu kaka yangu na mpenda sana,alilia kwa machozi sana na nikaona SIWEZI KUMFICHA KWELI KAKA YANGU,naweza kuwaficha wote lakini kadri siku zinavyoenda naona hapa panazidi kuwa pagumu kwa kaka ndipo niliposukumwa kutamani kusema ili kaka awe na amani katika hili.



ITAENDELEA!
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​



Sehemu ya 11



Moyo wangu unatunza siri na moja kati ya vitu nilimuahidi huyu kaka kule gerezani ni kuhusiana na kutunza siri,niliifanya siri hii kuwa ya sisi wawili peke yetu na yeye akiniambia "nimekupa siri ya maisha yangu sijawahi kumpa mtu yoyote hii siri mahali nimetunza pesa sikuwahi kumwambia mtu na ndio maana kile kijumba watu hupita na pengine wengine uenda kufanya shughuli zao uko na hawajawahi kujua chini ya ardhi ziko pesa nyingi,mimi nikamuahidi ya kwamba nitaitunza siri hii lakini kaka amezungumza nami katika lugha ya urafikiya undugu kabisa,nasikia moyoni mwangu angalau niweze kusema nae jambo,nikamwambia kaka "kuna vitu ni vigumu sana hata kusema,naogopa hata kusema" kaka akanambia "ni kitu gani mdogo wangu kama ni cha hatari niko tayari hata mimi kuingia kukusaidia sitamani kukuona unapata matatizo,unajua" nikamwambia "kaka najua" nikaketi na kaka na nikamwambia "hii ni siri,ni siri ambayo sijawahi kutaka kumwambia mtu yoyote yule" kaka akanambia "hata mimi ntaifanya kuwa siri kwa sababu wewe mdogo wangu umetaka iwe siri,niambie" ndipo nilipoanza kumwambia kaka ila nilimwambia kwa uchache sikumueleza kwa upana kama safari ya huyo mtu na mimi ilipoanzia,nilimwambia "kaka ni kweli nina pesa,unaona nafanya maendeleo haya unaona ninavyoagiza magari,unaona jinsi nimefungua biashara yaani kufungua duka la jumla na nimeweka pale kiasi cha milioni ishirini,ni kweli nina pesa lakini kaka hizo pesa si zangu,ni pesa za mtu na huyo mtu amekuwa anatamani kufanya makubwa sana lakini yeye amekosa hiyo bahati ya kuishi maisha ambayo mimi naishi ya uhuru" kaka anakanambia "una maanisha nini,ni nini ambacho unamaanisha? Ni mtu gani ambaye kakosa uhuru,ni vitu gani unazungumza,nikamwambia "kuna mtu amenipa majukumu ya kumfanyia vitu vyake kwakuwa yeye hawezi kufanya hivyo" akanambia "ni nani huyo na kiasi gani cha pesa akupe hata uweze kuagiza magari mengi kiasi hiki na hizo pesa unaweka wapi mwisho wa siku uweze utahatarisha maisha yako na hizo pesa unazijua amezitoa wapi? Kaka alinihoji kwa kuonesha kunijali sana na ni kweli kaka ananijali sana,nikamwambia "mtu huyu yuko gerezani kaka" kaka akashangaa sana "yupo gerezani? Sasa mtu yupo gerezani anawezaje kukupa wewe pesa? Nikamwambia "kaka ni stori ndefu sana ila elewa niko na pesa ila si za kwangu,mtu huyo yuko gerezani anatumikia kifungo na ameniomba nimsaidie kufanya hivi vitu nikiwa uraiani,kwahiyo nimechukua majukumu yake nafanya vitu ambavyo yeye alitamani kuvifanya ili siku moja akitoka gerezani aone hatua ameshaipiga kuliko pesa kuendelea kukaa sehemu bila kuzalishwa" nakumbuka kaka alinambia "kwahiyo umekaa chini na kunitungia kastori,umenitungia kasimulizi kakusadikika flani hivi,iko kitu kinawezekanaje? Hakuna kitu kama iko unanidanganya" nikamwambia "kaka nilihisi hata nikikwambia hautaweza kuniamini" akanambia "ni nani uko gerezani,ni nani ambaye awe na pesa hizi akupe wewe,hana ndugu? Hana watu wa karibu akupe wewe?

Nikamwambia "kaka huyu ni mtu ambaye yuko gerezani ana muda kidogo lakini ndugu zake walimtelekeza uko gerezani,hakuna watu wamekuwa wakienda kumwangalia hata kumtia moyo,hakumuona mv wa kumpa hilo jukumu,kipindi mimi naenda gerezani na nikaanza kuwa na urafiki naye ndio kipindi aliniamini nakuniona ni mtu mwema na akaniomba kama naweza kuwa mwaminifu kwake,ndicho kaka kilichotokea" kaka akaniuliza "ndio mwenye wale watoto uliokuwa ukijipa stress? Nikamwambia "ndio kaka" kaka akaanza kuamini katika nnachokisema baada ya kuendelea kumwambia lakini kaka aliyashangaa sana haya maelezo ambayo mimi namwambia nakumbuka sikutaka kumuweka kaka kiundani zaidi niliongea hayo tu kwa uchache,aliniuliza "pesa ziko wapi? Nikamwambia "kaka siwezi kukwambia" akasema "mimi ni kaka yako" nikamwambia "kaka naweza kukwambia vyote lakini nilimwambia mtu huyo sitasema kwa sababu ni maelekezo yake aliyonipa,kama nilivyokwambia kaka hizi pesa si za kwangu ila yeye aliniruhusu nifungue duka,lile duka la nafaka ni la kwangu lakini kuhusu magari sio ya kwangu,hivi vitu vingi sio vya kwangu"

Nilimueleza kaka yangu kwa upendo kabisa kwa sababu huyu ni kaka yangu na niko nae karibu sana katika mahangaiko yangu,katika mateso yangu kwa mfano kipindi kile nimekwenda gerezani ni kaka ndio alinipigania mpaka hatua ya mwisho akunyamaza,hakutulia mpaka alipoona mimi mdogo wake nimeachiwa huru kwahiyo yupo na mimi siku zote kwahiyo naamini nimemwambia kaka yangu naamini nimemwambia mtu sahihi,nilishea na kaka hayo na kaka alizidi kuniuliza maswali lakini sikujibu yote kwa sababu sikutaka kuzungumza kila kitu,aliniuliza "sasa ulipataje hizo pesa,alizihifadhi wapi?" Hayo yote aliniuliza lakini sikusema.
Baada ya kumwambia kaka hayo maneno nakumbuka niliporejea nyumbani nilisikia moyo wangu unauma sana,nilisikia moyo wangu unapatwa na uchungu kwanini nimesema,nilijilaumu kwanini kinywa changu kimezungumza siri ambayo nimeitunza kwa ahadi kuwa nitaitunza na sitaisema,mbona naumia hivi nami naona nimemwambia mtu sahihi,mbona nimemueleza kaka yangu kwanini nasikia hivi vibaya? Sikulala mpaka asubuhi,ushawahi kufanya jambo alafu ukawa unajilaumu kwanini unafanya? Mimi nilisikia hatia ndani yangu kwanini nimemwambia kaka,kama ningenyamaza kwani nini kingetokea,angenifanya nini? Niliona nimekosea,sikutakiwj kufanya hivyo.

Lakini unajua neno linapotamkwa linakuwa lishatamkwa unakuwa hauna namna yoyote yakuweza kulifuta tayari linakuwa lishatamkwa,nakumbuka kulipopambazuka na siku mpya kuingia kaka alinitumia meseji ikisema Rojas nataka tuongee,naomba nije nyumbani kwako tuzungumze,nilikuwa na ratiba za mishe zangu za hapa na pale lakini kaka yangu namheshimu sana na kama anasema ana jambo anataka kuja nyumbani litakuwa ni muhimu sana,nikamwambia kaka sawa na kaka alikuja nyumbani akanambia "mdogo wangu sijalala usiku kwa maneno uliyoniambia nimekosa usingizi,sijajua uko katika hatari kwa kiasi gani sijui lakini tu kwa experience yangu ya maisha,kwa maisha mimi nimeishi,mimi ni kaka yako najua vitu vingi,napata mashaka sana,nasikia kukosa amani sana kuhusiana na kile umenieleza jana lakini kuna kitu nimesikia amani nacho ndani ya moyo kwa sababu umesema huyo mtu yuko gerezani na hajawahi kumwambia mtu yoyote kuhusiana na hizo pesa,sasa mdogo wangu mimi najambo nataka kukwambia,mtu yupo gerezani na pesa unazo wewe uraiani unajua anatoka lini? Sikujua kaka kwanini ananiuliza maswali kama haya tena akiwa siriasi kweli amefunga safari tuje tuzungumze kuhusiana na hili na nikamwambia "kaka, sijui labda kuna neema itakuja ya yeye kutoka au pengine hiyo neema isipotokea uenda maisha yake yote akamaliza gerezani" "kwani amefungwa kifungo cha maisha? Nikamwambia "kaka kesi ya huyo mtu ilikuwa ngumu sana kwa maelezo ambayo nimepata,alinambia ni miaka 30 lakini nikaja nikagundua yule mtu amefungwa maisha" akasema "amewezaje kukudanganya wakati ni rahisi tu kujua miaka ya mtu" nikamwambia "unamaanisha nini? Akasema "mimi naweza kuifanya hiyo kazi nikajua miaka yake ambayo anatumikia uko gerezani,yaani tujue miaka yake ni mingapi,ni wa kutoka au siwakutoka kwa sababu hapo tupate uhakika" sasa nikawa najiuliza kwanini kaka azungumze hivyo,nikamwambia "yanini kuyajua hayo kwa sababu mimi nimemshauri kitu kwa sababu anazo pesa nyingi alizitafuta katika nafasi yake akiwa uraiani na pesa inanguvu nami nilimshauri ikiwezekana sehemu ya pesa yake ebu atumie uenda akaupata uhuru kwa nguvu akarudi huku uraiani kama ni rushwa au namna yoyote ile itakavyowezekana" nakumbuka kaka akanambia "wewe umshauri maneno kama hayo kwanini? Nikamwambia "kaka ni mtu mwema tu" akanambia "unajua hizi pesa amezitoa wapi? Nikamwambia "hajawahi kunieleza wapi alipozitoa" akanambia "hawa ndio watakuwa watu ambao ni wahujumu uchumi" nikamwambia "unamaanisha nini? Akanambia "kuna watu ambao walijilimbikizia pesa lakini kuna nyakati kuna msako uwa unapita na watu uhofia kuhusiana na hizo pesa kwa sababu hawaziweki benki wanaogopa,watu wengi kumekuwa na historia walikuwa wakichimbia pesa ardhini,vipi hizi pesa hakukwambia ukazichukue ardhini?

Nikashtuka,nikamwambia "kaka kwanini tunazungumza haya na wakati tulishazungumza jana na tumeshamaliza kwa sababu niliona nikushirikishe kaka yangu" akasema "ah umenishirikisha ila wewe bado mdogo hujui vitu vingi mimi ni kaka yako,sasa mimi ni kaka yako mimi najua maisha na najua vitu vingi,unajua ni kwanini huyu mtu kakutafuta wewe? Kwanini uwe wewe ushawahi kujiuliza? Hana watu ambao ameshawahi kufanya nao dili? Hawapo? Kwanini iwe wewe? Unajua kwanini? Nikamwambia "ndio najua" akaniuliza "unajua nini? Nikamwambia "najua kwakuwa tulikuwa marafiki,tuliishi kwa furaha na akaona mimi ni mtu ambaye sina shida yoyote" akasema "sio kweli,iko sababu nyuma ya huyo mtu kukutafuta wewe" sasa mimi kweli uenda kaka yangu ana upeo mpana na akili nyingi kuliko mimi siwezi kataa,sasa mimi namuuliza kaka "kwa sababu zipi? Anasema "si unaona hujajua kwanini akutafute wewe,ngoja nikwambie mdogo wangu mitego ya pesa ni mikubwa sana,waweza pesa itumia leo pesa isiyo halali inaweza ikakuletea shida hata baada ya miaka 10 baadae inaweza ikakuhukumu,ikawa kitanzi kwako,ikatesa moyo wako na maisha yako na ndugu zako" nikamwambia "unamaanisha nini" akasema "pesa hiyo siyo halali,hiyo pesa ni pesa haramu na amefanya hivyo ili siku hukumu ikija ikukute wewe na yeye akiwa pembeni ametulia" nikamwambia "sasa litampata vipi mtu aliye gerezani" nakumbuka kaka akanambia "ndio maana nakwambia wewe bado mdogo,uelewa wako bado mdogo haujajua kuchanganua mambo,usalama wako Rojas ni kukata kila connection ya wewe na huyo mtu wa gerezani na kukata connection na majukumu yote aliyokupatia na hizi pesa zisiwe chini yake,ziwe ni pesa zako sijui kama unanielewa? Kaka alinambia maneno hayo tena ni siku ya pili tu yaani nimemwambia jana na leo ananiamkia asubuhi kumepambazuka kaka anakuja na ujumbe kama huu,nikamwambia "kaka mimi Rojas siwezi kufanya kitu kama hicho,siwezi kufanya kama hivyo,siwezi kutumia pesa isiyo ya kwangu kuifanya ya kwangu siwezi,siwezi kaka kufanya hivyo,ahadi niliyompa mtu huyu nitaitimiza siku zote siwezi kuikengeuka hata kiku kimoja maana nimetafuta pesa katika nyakati zote sikuwahi kupata kwanini nimsaliti mtu ambaye amekuwa mwaminifu kwangu ambaye ameamua kunitunuku na kunitoa katika umaskini nakunipa maisha mengine,kwanini kaka unazungumza maisha ya ushetani hivyo" nakumbuka kaka akacheka na akasema "ushetani? Mdogo wangu kweli hauyajui maisha? Nazungumza mambo ya maana wewe unasema ushetani mimi nazungumza ushetani?" Kiukweli sikupenda kabisa kauli za kaka kabisa na nikamwambia "ndio maana moyo wangu umekosa amani kabisa kukushirikisha,hukustahili kunambia maneno haya tena ikiwa mapema kama hivi" akanambia "nakwambia mapema kwakuwa wewe hujui,wewe bado mdogo hujui kadri unavyozidi kwenda gerezani,wewe si kila siku uwa unaenda gerezani mwisho wa siku utastukiwa,huyu mtu bado anafatiliwa kule gerezani usihisi watu wametulia kumfatilia nisikilize mimi ninachosema" kaka akanambia "huyu ni mhujumu uchumi hawezi kukwambia na mimi ndio nakwambia sasa kwa sababu najua haya mambo ziko nyakati hata wewe ulikuwa bado mdogo kuna watu walifanya hujuma,walihujumu uchumi hawa watu walifanya namna nyingi hawajaacha kufatilia siku mpaka anapokufa ndio huyo mtu ndio wanaacha hivi ninakwambia we si uwa unaenda si una route za kwenda? Unavyoenda watu wameshachora ramani,kuna mtu ana dot dot alikuwa gerezani ametoka lakini anaendeleza ukaribu na huyu mtu,mdogo wangu sasa hivi unakamatwa,unakamatwa na unaniingiza kwenye matatizo kata hiyo connection haraka sana usiende gerezani unakamatwa na ninavyozungumza hivi na pengine si siku nyingi kutoka leo na umezungumza kwangu kwa sababu Mungu hataki upate matatizo"

Kaka anaendelea kunambia vitu yaani mimi naenda gerezani kila siku sikuwahi kuwaza hata siku moja kuwa hizi route za kwenda gerezani ninazofanya labda zinaweza zikawa na ishara yoyote lakini kaka anasema huyu mtu bado yuko kwenye uangalizi kwani amehukumiwa lakini haimaanishi kwamba ameachiwa,huyu bado anafatiliwa yuko kwenye uangalizi.
Toka kaka amezungumza siku ile alinipa hofu,nilianza kuwa nahofu moyoni mwangu kwa maneno kaka aliyoniambia,nakumbuka kama baada ya siku mbili toka siku zile tumezungumza na nikamkatalia kaka akaja na akanambia kitu cha ajabu sana,mimi nilizungumza na kaka na sikuwa nimemtaja mtu kwa majina yake ambaye ndiye yuko gerezani,ambaye ndiye amenipa hili dili na mimi nafanya hivi katika mazingira na sikumuweka kaka kiuwazi sana,kaka alinijia na jina kamili,jina kamili la yule ndugu kule gerezani😂 na akanambia alikuwa gereza flani na akapelekwa gereza flani,yaani amemjua sasa kuliko hata mimi,kuliko mimi ambaye nafanya nae kazi katika mfumo ambao nimekuambia na akanambia uwa naenda gerezani mara ngapi (akanipa idadi),niliogopa sana na nikamuuliza "kaka umeyajuaje yote haya" akasema "nimejua kwakuwa mimi ni mkubwa kwako,mimi ni kaka yako,najua mambo kuliko wewe,hivi unajua kuna watu pale gerezani kila unapoenda kumtembelea uwa wanarekodi? Unajua wewe mpaka sasa hivi inawezekana umeshaanza kufatiliwa mpaka unavyoondoka asubuhi mpaka jioni shughuli zako unavyofanya na watu unaoongea nao,unajua iko kitu?" Niliogopa sana na kaka akasema "uko unatazamwa mdogo wangu,watu wanakufatilia" nikamuuliza "kaka umejuaje,umeyajuaje haya?" Kwa sababu kaka yangu ni mtu wa kawaida tu,ni mtu wa kawaida kusema amjue hadi mfungwa hivyo mimi nilivyomueleza hadi apate connection na kujua mimi nilienda siku flani na siku flani huyo ni mtu wa namna gani,si unaona unaogopa,unajua hii sentensi ninayokwambia maana yake nini,maana yake yule mtu ni kweli siku zimepita ila bado anaendelea kufatiliwa na amemtafuta mtu mdhaifu mdogo ili isiwe rahisi mtu yoyote kujua lakini mambo yashajulikana,unajua uko katika hatari kwa kiasi gani? Unajua?

Niko hapa kaka yako nataka nikusaidie,nataka nikusaidie,utapata matatizo upigwe kifungo cha maisha,kwanini hajatumia ndugu zake,kwanini akutumie wewe? Maneno ya kaka yalizidi kuniogopesha na labda kutokana na umri wangu sielewi lakini niliogopa,naogopa kwenda gerezani,sitaki kwenda tena uko.



ITAENDELEA!
 
Ndugu zangu jana jioni nilidhani nimeipost sehemu ya 10 kumbe haikukubali na muda huu natizama ndio nagundua hilo,poleni kwa usumbufu na ndio nimetupia vipande viwili,tuenjoy story wandugu!
Ssante cuzo hapo mchanganyo umeanza. Je kaka mkweli au anampoteza maboya...
Naona hela zikienda kuyeyuka, kuna ndugu huwa na wivu mtu akipata pesa. Acha tuone yajayo... barikiwa kwa uandishi cuzo ake.
 
Back
Top Bottom