Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Sasa kama Rojaz hakufirisika,,,mbona dk za mwisho alikuwa anauza mitumba jjini Mwanza
Yawezekana ikawa ni story tofauti ama baabae ikawa na muendelezo mwingine lakini kwa hii niliyoiandika hapa yenyewe imeishia hivyo na kama hiyo ya kuuza mitumba waweza weka link yake hapa ili kama ikituvutia tuiweke hewani kwa faida ya umma wa jamii forum
 
Boutafrica
 
Ebu nitumie link ya hiyo ya kuitafuta kwa madiba na mambo ya makina tuiweke hapa🤣🤣🤣
 
Mkuu,,Me ninavyojua hakuna Rojaz wawili ambao walipitia pale RAF,,,ninamjua Rojaz mmoja tuu,,,na ndiyo huyo alimpeleka Zabron Mzee wa Gamboshi pale RAF,,pia Zabron ndiye alisema Alikutana na Rojaz mtaani anauza mitumba na wakati huo yeye mwenyewe Zabron alikua anauza mitumba ndipo walipoenda mgawahani Rojaz akaanza kumwambia Zabron,,kwamba nimemaliza kipindi ktk kipindi cha sintosahau week iliyopita na nashukuru watu wamenichangia changia ndipo nikaona nianzishe biashara ya kuuza mitumba,,,zabron akamwambi me mwenyewe ninamkasa,,Rojaz akamwambia hebu nisimulie,,Zabron kwa kifupi akamwambia,,ashaishi na jini pia aliwahi kupelekwa ktk Kijiji cha wachawi kimazingara,,,Rojaz akamwabia zabron,,,aisee!!!una bonge la Story hebu twende RAF tukaweke Booking,,ndipo wakaenda na Zabron hadi pale RFA na zabron akaanza kuruka kwa hewa na simulizi yake ya Sitoisahau Gamboshi....

So nimejaribu kukufahamisha Namna gani jamaa alipomaliza Simulizi yake pale RAF na maisha mengine yalivyoendelea,,,Me ni miongoni mwa watu ambao sikubahatika kusikiliza simulizi ya Rojaz Radioni ingawa nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa hicho kipindi,,,,na nimeanza kufuatilia kile kipindi baada ya Fredrick Bundala kushika usukani,,ingawa inasemekana creator wa hicho kipindi ni Roy Maganga....
 
Upo sahihi asilimia mia, Roy maganga ndo alikua nahodha wa hicho kipindi enzi hizo kabla hajampa uskani bundala, binafsi nakumbuka Rojaz ndie alisimulia story nzuri na iliyosisimua watu wengi na alikua Rojaz mmoja tuu, pengine alitokea mwingine lkn mwisho wa Rojaz ulikua ni kuuza mitumba kama ulivyosema
 
Mm nimesikiliza story yake ya rojaz mwanzo hadi mwisho, kipindi anaanza safari ya kwenda sauzi anapaita Jo beg, alienda kwa kuunga unga hadi analishwa panya njiani

Enzi za roi mbaliki manganga & fedrick bundala sitosahau ilikuwa ya moto sana sio kama ya saivi
 
Je ndiyo hii aliyoiandika huyu member
 
Siyo mchezo
 
Chai ya rangi hii ya kutunga, kwanza sio yeye asilimia 100.
Kuna eneo nimesema mimi ndio mhusika? Rejea kusoma majibu niliyokuwa nawapa watoa maoni,story iko youtube nami nilichofanya ni kuitoa ktk sauti na kuiweka ktk maandishi,pole kwa kupanic usiweke negativity kichwani
 
Hapo kaandika au katumia program ya computer ya kubadili audio ya simulizi kwenda kwenye maandishi.
Kama unadhani nimetumia program yoyote kuibadili hii story nakujuza si kweli,nimeandika kwa mkono wangu kipande kwa kipande,sitaki kujisifu ila ninajitahd ktk upande wa kuandika tena natumia simu tu wala si computer,kuna story km 3 nimeshazidownload ila changamoto ni muda tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…