gachacha
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 2,584
- 3,977
Hivi huyu rojaz si ndo alienda sauzi Africa kwa miguu kipindi anasimamia kipindi roy , au ni mwingine tenaSasa kama Rojaz hakufirisika,,,mbona dk za mwisho alikuwa anauza mitumba jjini Mwanza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi huyu rojaz si ndo alienda sauzi Africa kwa miguu kipindi anasimamia kipindi roy , au ni mwingine tenaSasa kama Rojaz hakufirisika,,,mbona dk za mwisho alikuwa anauza mitumba jjini Mwanza
Ndiyo huyo mkuuHivi huyu rojaz si ndo alienda sauzi Africa kwa miguu kipindi anasimamia kipindi roy , au ni mwingine tena
Yawezekana ikawa ni story tofauti ama baabae ikawa na muendelezo mwingine lakini kwa hii niliyoiandika hapa yenyewe imeishia hivyo na kama hiyo ya kuuza mitumba waweza weka link yake hapa ili kama ikituvutia tuiweke hewani kwa faida ya umma wa jamii forumSasa kama Rojaz hakufirisika,,,mbona dk za mwisho alikuwa anauza mitumba jjini Mwanza
BoutafricaMKASA WA KUSISIMUA WA ROJAZ:
katika kipindi cha sitasahau cha radio free Africa
Sehemu ya 4
Kitendo cha kuwa huru kiukweli nilimshukuru Mungu sana na kujisemea peke yangu moyoni kuwa ukimuona mtu anamfanyia hila mwingine na kupelekea huyo mtu kupelekwa jela ujue huyo sio mtu mzuri katika maisha yako,nilishukuru kwa kuwa haki imetendeka na imebainika kuwa kuwa mimi sio mhusika wa lile tukio ingawa haikuwa ndani ya siku moja au mbili lakini ukweli umejulikana,nimerejea sasa uraiani na maisha yanaendelea na nashukuru kwa uhuru nilionao kuweza kujiamulia mambo yangu,ndugu jamaa na marafiki walijitokeza wenye kunipongeza,wenye kunipa pole yote hayo niliyapokea lakini nina ahadi mimi nilimuahidi mtu nikiwa kule gerezani,huyu mtu nimekutana nae gerezani,huyu mtu aliniomba sana niende kuitembelea familia yake alinipa maelekezo tena alizungumza nami mengi kuhusiana na familia yake hasa kuhusu watoto wake kuwa kuna mwanamke ambaye alizaa nae hao watoto lakini kwa wakati huu hawako kwenye mahusiano na pia ana mchumba wake kwahiyo haya maelekezo yote nilikuwa nayakumbuka nyakati hizi wakati nipo uraiani,zilipita kama wiki tatu hivi nikawa nasikia kama mzigo ndani ya moyo wangu kwanini niahidi kitu alafu nishindwe kukitekeleza ni kweli kwamba nimeshindwa kwenda kuwaona hawa watoto?
Nikasema hapana na kwakuwa nilikuwa na vijisenti kidogo kwa sababu nimetoka gerezani familia yangu ipo nashukuru walinishika mkono na nikawa hapa nyumbani,nilitumia kapesa changu kidogo kwa kununua nyama kilo moja nakumbukb na nilinunua sukari nusu kilo nilivibeba nikiwa na dhumuni la kwenda kuitizama familia ya mtu ambaye nimekutana nae gerezani na wala sikuwa namjua kabla ya hapo yaani tumekutana gerezani,nikafata maelekezo hadi nikafika lile eneo ambalo nililoelekezwa,kweli nilifika na kweli ndicho nilichokutana nacho,nilikutana na mwanamke mmoja,mwanamke huyo alikuwa mnene na mweupe sana,alinikaribisha na nikamueleza ujumbe ambao nilikuwa nimepewa na rafiki wa kule gerezani,nakumbuka sentensi ambayo alinambia huyu mama "eeh kwahyo amekuambiaje?" Hii ndio sentensi ya kwanza huyu mama alinambia nami nikamwambia "amenituma nije kuwasalimia watoto" akanambia "eeh ukishawasalimia?" Nikamjibu ndio alivyoniagiza kuja kuwasalimia angalau nizungumze nao na kuwaeleza jinsi baba yao anawapenda sana na siku zote anawaombea baraka,akasema "hayo maneno nimeshayasikia sana je yanasaidia nini kwa watoto wangu,yanasaidia nini?
Kiukweli huyu mama hakunipokea vizuri lakini nilishapewa tahadhari toka kule gerezani kuwa huyu mama ni mkorofi sana,sasa kwa sababu nilishaelezwa hayo ilibidi tu niwe mpole,akaendelea kunichamba "kwahiyo uko gerezani hakuna kitu anachona sisi kinatufaa zaidi ya hiyo nyama na sukari,kwahiyo tunaishi kwa ajili ya nyama na sukari? Hao ndugu zake washenzi wasio na maana kila siku napata ujumbe ntasaidiwa ntasaidiwa je nasaidiwa kitu gani? Ameharibu maisha yangu mbwa yule" akaanza kutamka maneno ya kashfa kumuhusu kaka yule na kiukweli ukiniuliza mimi nafahamu mengi kiasi gani kumuhusu yule kaka kule gerezani kiukweli sijui na hauwezi amini ni machache ambayo yeye amenieleza na upande wa pili wa ubaya wake mimi siuelewi lakini ni mtu aliyenifanyia wema nyakati tukiwa gerezani na alikuwa mtetezi wangu katika mambo mengi sababu gerezani kuna maisha yake uko,kuna watu wababe,wakorofi lakini kama kuna mtu anakukingia kifua unamuona huyu ni kaka,kaka mzuri kwahiyo hajawai kunitendea ubaya wowote na inawezekana kweli ni mtu mbaya kwa sababu alishanieleza kuwa yupo hapo kwa sababu alitakiwa kulipia yale yote aliyoyatenda uraiani,anatumikia kifungo anachoamini alistahili,huyu mama alizungumza mengi nami nikawa nimetulia tu namsikiliza na nikamwambia "tuzungumze tu kwani mimi ni mjumbe tu na mjumbe hauwawi,mimi ni mtu mwema tu ambaye nilifungwa na nikakutana na huyu ndugu baba watoto wako,ni mtu ambaye aliniomba sana nitakapotoka nisiache kuja kuwana watoto wake,sasa ahadi nilimpa na toka nimetoka gerezani ilitakiwa nifanye mapema na nimekuwa nikijisikia hatia kwa sababu nimeshindwa kulitekeleza hilo kwa haraka kwahiyo nimekuja ili kuweza kusikia amani ndani ya moyo wangu" nilimueleza hayo na nikapata nafasi ya kuzungumza na watoto,ana watoto wazuri sana,baba yuko gerezani na kwa mtu mwelevu ukitizama mazingira ulikuwa unapata picha kuwa hawakuwa na maisha mazuri kwahiyo mama anajipigania kwa vile anavyoweza na mama mbabe sana huyu maana hata akiongea tu unajua kama huyu mama ni mbabe,niliwambia watoto bac yao anawasalimia sana na anawapenda na siku moja anaamini atajumuika na nyinyi na nakumbuka mtoto wake mmoja mkubwa alinambia kuwa mama yao aliwaambia hawataweza tena kujumuika na baba yao katika maisha wanayoishi nami nikawaeleza kuwa sio kweli kwani baba siku moja atajumuika nao na wataungana nae na kula nae chakula pamoja na furaha itakuwa katika maisha yao ya kila siku.
Nikawaambia mimi ni anko wao na nitakuja mara kwa mara kuwatembelea na kama kuna uhitaji wa vifaa vyovyote vya shule wataniagiza na ntakaporejea tena ntawaletea hivyo vitu,wakaniandikia vitu vyao ingawa nilikuwa siko poa kivile na ukizingatia nina muda mfupi toka nitoke gerezani lakini mazingira yao yalinisukuma tu kuweza kufanya hilo jambo,mimi ni mwanaume tena mpambanaji nimeguswa sana na hii familia hasa hawa watoto,niliondoka nikiwa najisikia deni ndani yangu tena nakumbuka yule mtoto mdogo aliniuliza "utarudi kweli? Utakuja tena kuja kutuona? Nikamjibu "ntarudi na ntaleta hivi vitu mlivyoniagiza kwa ajili ya shule" nikaondoka zangu kurejea nyumbani na nakumbuka pia nilishea hili jambo na kaka nilipofika nyumbani,nilimueleza kaka jinsi nilivyoikuta familia ya yule ndugu wa kule gerezani,kaka alisikitika sana na kusema "maskini hakuwaza kama siku moja atakuwa mbali na watoto wake tazama sasa future ya watoto inaweza kuharibika kama mama atakosa misingi mizuri ya malezi kwa ajili ya watoto,akijichanganya tu anaharibu watoto lakini kama atasimama anaweza kuwalea watoto wake vyema" nikamueleza jinsi nilivyomuona ni kama mama ambaye ameshajichanganya sana na tukasikitika pamoja na nikamueleza jinsi watoto walivyonipa mahitaji yao ya vifaa vya shule lakini bro mimi navitoa wapi? Kaka akacheka na kunambia "ndio ukapambane sasa mwenzetu umeshapata familia eeh msamaria mwema umejikuta umekuwa na familia ya watoto wawili,mimi sina la kukusaidia nadhani unajua kuhusu hali yangu ya kipesa,wewe pambana bwana ahadi umetoa ipambanie" maisha yakaendelea na kaka kule gerezani nilimuahidi ntakapoenda kwa watoto wake ningekwenda kumjulisha maendeleo yao,kwakuwa mi niko kitaa nikaona sio vyema kukaa tu na ni vyema kusaka dili za kufanya kwakuwa maisha lazima yaendelee,katika kutafuta japo videiwaka na ukitilia maanani nimetoka gerezani kuaminika nako kukawa ni mtihani kwa walio wengi maana wengine akijua ulienda ndani anajua kama ulitenda kumbe uhusiki chochote,kuaminika kulipunguwa maana wanahisi unaweza kumpa gari yako ana mikosi gari ikapata matatizo yaani nikawa nakataliwa kihivyo,maisha yaliendelea kuwa magumu japo kaka alikuwa ananiambia "hivi ndivyo ilivyo kwa wewe kujenga kuaminika inahitaji muda kidogo,wako watakaoona una nuksi,wapo watakaona ulihusika kwa namna moja au nyingine ukweli unaujua wewe na Mungu wako lakini ni muda mfupi tu lakini uvumilivu unahitajika ili mambo haya yapite na tuyaruhusu yale mazuri yaje kwetu"
Familia yangu ilinitia sana moyo,ilinifariji sana,kila ninachojaribu kufanya kwangu kilikuwa hakifanikiwi pamoja na kuwa ni dereva mzuri tu hata deiwaka sipati,kuna siku nikaona ngoja nikamcheki mshkaji kule gerezani nikikumbuka pia nina ujumbe kutoka kwa watoto wake nimpelekee zile salamu watoto wake walinipa ,sijafanikiwa katika ahadi ambazo niliwaahidi,nikaenda na nikapata nafasi ya kuzungumza na mshkaji,mshkaji alinambia "umekuja?umekuja kuniona mimi?"
Alifurahi sana, Nikamwambia "ndio kaka si nilikuahidi" akanambia "nilihisi hautakuja maana siku niliona zinasogea na nikaona ahadi zako zitakuwa kama ahadi za watu wengine walizokuwa wakiniahidi" nikamwambia "hapana lazima ningekuja kwani sijawahi kumuahidi mtu kitu cha uongo sipendi kufanya hayo ya kuahidi alafu nisitekeleze,lakini nimerudi uraiani mambo yamekuwa si rahisi" akasema "najua hayawezi kuwa rahisi lazima ujipe muda" nikamwambia "ni kweli,kweli kabisa nimerelax najipa muda" akanambia "mambo yatakaa vizuri,amini Rojaz mambo yatakaa vizuri,niambie kuhusu watoto wangu" ndipo nilipomueleza mazingira niliyowakuta watoto wake ila wako na afya njema tu asiwe na wasiwasi akasema "wamesemaje? Wamenikumbuka?" Nikamjibu "ndio wanaonesha kukukumbuka sana na wanaonesha kukupenda sana" akasema "mama yao anawafanyia ukatili watoto hataki kabisa hata watoto wanitembelee,naumia sana" niliona jinsi anavyosononeka akizungumza hayo nikamwambia "mambo yatakaa tu sawa,nimewaahidi watoto wako kuwa wewe utatoka siku moja utajumuika nao" akacheka,akasema "mmh eeh wakasemaje" nikamwambia "inaonekana kama walikuwa hawana matumaini lakini nilipowaambia nyuso zao zimeonekana kuwa zenye furaha" akanambia "umewaambia vyema,asante nakushukuru sana,umerejesha furaha yangu na umenifanyia jambo ambalo sikuwahi kulitegemea,kwa hii sentensi naomba uamini ninachokisema,umetenda kwangu jambo kubwa sana,nimekuwa nikitamani nikutane na mtu mwenye utu kama wewe lakini hauwezi amini sijawahi kukutana nae" mimi nikatabasamu na kujiuliza hivi kitu gani cha thamani nimefanya hapa,haya ni maisha yangu ya kila siku kwani nimekuwa nikiguswa na watu wenye changamoto za hapa na pale na mimi ni huyu,mimi ndio Rojaz ninapomuahidi mtu kitu ninachoweza kwa hakika kukitenda lazima nikitekeleze kwahiyo nimefanya haya ndio maisha yangu ya kila siku hakuna wema ambao natakiwa nionekane nimetenda wema,haya ni maisha yangu ya kila siku,akanambia "aisee Rojaz nakushukuru sana umepanda kwangu kitu kikubwa sana,Rojaz unaweza kunisaidia kitu?"
Nikasema "ndio mimi niko hapa" akasema "sawa Rojaz naomba sasa ukamtembelee msichana wangu,najua amevunjika moyo,watu wamemvunja moyo lakini naomba ukanipelekee salamu" nikamwambia "nikamwambie nini? Akasema "najua wewe ni mtu mwema we nenda kazungumze nae tu,ukamwambie jinsi tulivyoishi vyema tukiwa huku gerezani na jinsi ambavyo nilikuwa nikimzungumzia vizuri na jinsi ambavyo nampenda,kitu ambacho kinaniuma ni kukosa uhuru na kuishi na mwanamke ambaye ninampenda" nakumbuka nilitabasamu tu aliponambia hayo,nikamwambia "brother siku utapata chance na utaishi na mwanamke unayempenda" akasema "haiwezekani,hawezi kuningoja mie majira yote hayo,najua na sitamlaumu,sitamlaumu hata siku moja" nikamwambia "sawa" ila alifurahi sana,yaani unafanya kitu kwa mtu yaani unamuona anafurahi mpaka unashangaa alifurahi nini kwa kiwango iki na alisema "umenipa furaha isiyo ya kawaida,baada ya hapo nakumbuka niliondoka nakurudi zangu nyumbani na harakati zangu za kudonoadonoa kama kawaida ziliendelea kama kawaida kwa sababu mambo yalikuwa bado hayajakaa vizuri,kweli siku nilipanga na kama alivyonielekeza nilienda,mimi niliombwa kwahiyo kama niliombwa na nilimuahidi kutenda ndio nilienda sasa,kweli nilikutana na huyo mwanamke na nikafanya nilivyoelekezwa kikubwa nilimpa salamu zake nyingi sana na nikamueleza jinsi huyu kaka anavyompenda na jinsi anavyojisikia vibaya kuishi gerezani na kukosa kuishi na mwanamke anayempenda,mwanamke wa ndoto yake,kiukweli yule dada nilimuona ni mtu aliyekwisha mkatia tamaa mshkaji lakini mimi nilimwambia mapenzi ya kweli uwa hayafi,mapenzi ni kuvumilia na kama kweli unampenda utamvumilia na siku moja atakuwa huru na mtaungana tena uraiani na kuishi yale maisha mliyokuwa mkiishi awali,lakini mtu akiwa gerezani na hasa ambao wana miaka mingi gerezani watu wao wa karibu wanakuwa na ukaribu siku zile za mwanzo lakini kadri siku zinavyosogea watu huchoka na huyu ndio binadamu alivyo,atakuwa na bidii sana mwaka wa kwanza,mwaka wa pili,ukianza mwaka wa tatu anaanza kuchechemea baadae aah anaanza kuchoka,anachoka kweli kweli anaona kwani nini na jamii nayo watu wako tofauti,mtu ameshaenda gerezani miaka thelathini unamngoja wa nini,huyo mtu amefungwa kifungo cha maisha unamngoja wa nini ushindwe kuendelea na maisha yako,watu wana mapokeo tofauti mwingine anaanza maisha mapya,mwingine anavumilia lakini unamuona hizi ni dalili za mwisho hizi kachoka kabisa lakini ujumbe mimi kama mjumbe nilifikisha na nilimwambia ntakuwa nakuja mara kwa mara kukusalimia na kukujulia hali kwa namna moja au nyingine lakini ni mwanamke ambaye maelezo yangu aliyapokea kikawaida tu "nashukuru,asante" yaani hivyo.
Nashukuru baada ya muda nikapata gari lakujishikiza kama deiwaka yaani gari lina dereva wake nami nakuwa kama namsaidia pale anapokuwa amechoka,kaka ndio aliniunganisha kwa huyo jamaa mwenye gari nikawa napigapiga mishe ujue ukitoka jela inakuwa sio rahisi kurudisha uaminifu katika jamii inayokuzunguka,ni watu wenye imani kubwa kwako tu ndio watakaothubutu kuweza kukupata tena nafasi ya kukukabidhi gari wao wanajua ni changamoto tu za kimaisha umekutana nazo tena haukuhusika kiukweli inabidi mtu akujue kwa ukaribu sana kama huyu mtu ananipa gari analerax na naenda na kurudi salama,kweli maisha yakawa yanaenda na Mungu akajaalia nikawa napata vijipesa kidogo nakumbuka nikaenda kununua vifaa kidogo nakumbuka ilikuwa ni peni,rula rula,madaftali na nikaenda kuwacheki wale watoto wa mshkaji,nikaenda kuwatizama wale watoto nakuwapatia yale mahitaji na pia nilibahatika kununua na chakula,nilinunua unga,mchele,mafuta,nilinunua nyama,mafuta kile kidumu kidogo yaani nikaenda safari hii angalau na kifurushi,vifaa vya watoto nilibeba hivyo vichache ingawa waliniandikia vingi,najua mazingira ya pale vyakula ilikuwa ni kitu bora zaidi kukipa kipaumbele katika nilivyochukua,nimefika Mungu mwema nikamkuta na yule mama na akanambia "umekuja tena?" Nikamwambia "ndio bwana nimekuja tena,nimekuja kuwaona hawa ndugu zangu" ilikuwa ni siku nzuri tena ukitilia maanani ilikuwa ni jumamosi wakanambia anko umekuja? Yaani walinikumbuka,nikawaambia "
Si mnakumbuka niliwaambia kuwa ntakuja? Mambo kati hapa hayakuwa rahisi sikupata pesa haraka yakununua vitu ndio maana nikachelewa lakini nimekuja" nikawapatia vitu vyao na chakula,awamu hii yule mama angalau alinipokea vizuri akasema "eeh una ujumbe gani mwenzetu" nikamjibu "sina ujumbe wowote nimekuja tu kwa ajili ya kuwaona hawa ndugu zangu" akasema "haya tunashukuru" nikazungumza na watoto nakuwakabidhi vitu vyao japo sikuwa nimewakamilishia nikawaambia kuwa nitakuja tena na waandike vingine wanavyovihitaji,kwahiyo vile ambavyo sikuvinunua wakaandika na vingine ndio maana kaka anasema mwenzetu umekuwa na familia siku hizi lakini ni mzigo ambao niliubeba ndani yangu kwa kuwaona hawa watoto ambao hawana hatia yoyote,niliondoka hapo nikiwa na furaha kwelikweli na nikiwa na amani sana kwamba leo mimi nimefanikiwa kuwapa chakula watu ambao pengine wangekula mlo mmoja au kesho labda wangekula mlo mmoja au wangeangaika kwenda kuombaomba lakini mimi kwa mchele kidogo,kwa mafuta nimewastili siku mbili tatu watapata chakula kizuri,nilirudi kwa furaha na nikalala usingizi mzuri sana.
Pilikapilika ziliendelea na huku nikiendelea kumuelezea kaka kile kinachoendelea kuhusiana na mimi kwenda kuwatembelea hawa watoto,nilienda tena kuwatembelea hawa watoto,na nikaenda tena,nakumbuka nilienda kama mara tano kwenda kuwatembelea hawa watoto na kila ninapoenda kile nilichobarikiwa naenda kuwapelekea,sasa wameshanizoea na huyu mama alishanizoea hata siku moja alishaniambia "wewe ni rafiki wa baba ...(akitaja jina la mtoto wake) ina maana mmejuliana gerezani,unamjua mtu huyu?" Nikamwambia "sitaki kujua chochote ninachojua ni mtu mwema,tulipokuwa gerezani tumeishi vizuri na hili ni ombi lake kwangu na kwa sababu mimi nipo uraiani hawa wamekuwa kama wadogo zangu"
Muda ukaenda baada ya kuwatembelea hawa watoto na nikaona sasa ni wakati wa kwenda gerezani kumsalimia ndugu yangu,ameshakuwa ndugu yangu angalaunimpashe jinsi mambo yanavyoenda uko uraiani na jinsi watoto wake wanavyoendelea vizuri na maisha yanaendelea,nilipofika gerezani awamu hii na kupata nafasi ya kuzungumza na huyu kaka ambaye mimi nilimkuta gerezani na kumuacha uko viko vitu aliniambia nilishangaa sana!
Itaendelea!
Ebu nitumie link ya hiyo ya kuitafuta kwa madiba na mambo ya makina tuiweke hapa🤣🤣🤣Bro Kama wewe ndo ulikua ukiihadithia hii simulizi radio free na mzee mzima sky Walker hongera Sana, na wewe kwangu umekua kiigizo chema kabisa katika kuwatendea wema watu wasio na hatia, naikumbuka ile beat iliokua inaplay background wakati wa simulizi, nlikua najitahidi Sana Kila jumapili niwe pembeni ya redio. Ni miongoni mwa vipindi Bora kabisa vya redio kuwahi kutokea hapa Tanzania, nasubiri simulizi ya kuitafuta kwa madiba na Mambo ya "makina"
Mkuu,,Me ninavyojua hakuna Rojaz wawili ambao walipitia pale RAF,,,ninamjua Rojaz mmoja tuu,,,na ndiyo huyo alimpeleka Zabron Mzee wa Gamboshi pale RAF,,pia Zabron ndiye alisema Alikutana na Rojaz mtaani anauza mitumba na wakati huo yeye mwenyewe Zabron alikua anauza mitumba ndipo walipoenda mgawahani Rojaz akaanza kumwambia Zabron,,kwamba nimemaliza kipindi ktk kipindi cha sintosahau week iliyopita na nashukuru watu wamenichangia changia ndipo nikaona nianzishe biashara ya kuuza mitumba,,,zabron akamwambi me mwenyewe ninamkasa,,Rojaz akamwambia hebu nisimulie,,Zabron kwa kifupi akamwambia,,ashaishi na jini pia aliwahi kupelekwa ktk Kijiji cha wachawi kimazingara,,,Rojaz akamwabia zabron,,,aisee!!!una bonge la Story hebu twende RAF tukaweke Booking,,ndipo wakaenda na Zabron hadi pale RFA na zabron akaanza kuruka kwa hewa na simulizi yake ya Sitoisahau Gamboshi....Yawezekana ikawa ni story tofauti ama baabae ikawa na muendelezo mwingine lakini kwa hii niliyoiandika hapa yenyewe imeishia hivyo na kama hiyo ya kuuza mitumba waweza weka link yake hapa ili kama ikituvutia tuiweke hewani kwa faida ya umma wa jamii forum
Upo sahihi asilimia mia, Roy maganga ndo alikua nahodha wa hicho kipindi enzi hizo kabla hajampa uskani bundala, binafsi nakumbuka Rojaz ndie alisimulia story nzuri na iliyosisimua watu wengi na alikua Rojaz mmoja tuu, pengine alitokea mwingine lkn mwisho wa Rojaz ulikua ni kuuza mitumba kama ulivyosemaMkuu,,Me ninavyojua hakuna Rojaz wawili ambao walipitia pale RAF,,,ninamjua Rojaz mmoja tuu,,,na ndiyo huyo alimpeleka Zabron Mzee wa Gamboshi pale RAF,,pia Zabron ndiye alisema Alikutana na Rojaz mtaani anauza mitumba na wakati huo yeye mwenyewe Zabron alikua anauza mitumba ndipo walipoenda mgawahani Rojaz akaanza kumwambia Zabron,,kwamba nimemaliza kipindi ktk kipindi cha sintosahau week iliyopita na nashukuru watu wamenichangia changia ndipo nikaona nianzishe biashara ya kuuza mitumba,,,zabron akamwambi me mwenyewe ninamkasa,,Rojaz akamwambia hebu nisimulie,,Zabron kwa kifupi akamwambia,,ashaishi na jini pia aliwahi kupelekwa ktk Kijiji cha wachawi kimazingara,,,Rojaz akamwabia zabron,,,aisee!!!una bonge la Story hebu twende RAF tukaweke Booking,,ndipo wakaenda na Zabron hadi pale RFA na zabron akaanza kuruka kwa hewa na simulizi yake ya Sitoisahau Gamboshi....
So nimejaribu kukufahamisha Namna gani jamaa alipomaliza Simulizi yake pale RAF na maisha mengine yalivyoendelea,,,Me ni miongoni mwa watu ambao sikubahatika kusikiliza simulizi ya Rojaz Radioni ingawa nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa hicho kipindi,,,,na nimeanza kufuatilia kile kipindi baada ya Fredrick Bundala kushika usukani,,ingawa inasemekana creator wa hicho kipindi ni Roy Maganga....
Mm nimesikiliza story yake ya rojaz mwanzo hadi mwisho, kipindi anaanza safari ya kwenda sauzi anapaita Jo beg, alienda kwa kuunga unga hadi analishwa panya njianiMkuu,,Me ninavyojua hakuna Rojaz wawili ambao walipitia pale RAF,,,ninamjua Rojaz mmoja tuu,,,na ndiyo huyo alimpeleka Zabron Mzee wa Gamboshi pale RAF,,pia Zabron ndiye alisema Alikutana na Rojaz mtaani anauza mitumba na wakati huo yeye mwenyewe Zabron alikua anauza mitumba ndipo walipoenda mgawahani Rojaz akaanza kumwambia Zabron,,kwamba nimemaliza kipindi ktk kipindi cha sintosahau week iliyopita na nashukuru watu wamenichangia changia ndipo nikaona nianzishe biashara ya kuuza mitumba,,,zabron akamwambi me mwenyewe ninamkasa,,Rojaz akamwambia hebu nisimulie,,Zabron kwa kifupi akamwambia,,ashaishi na jini pia aliwahi kupelekwa ktk Kijiji cha wachawi kimazingara,,,Rojaz akamwabia zabron,,,aisee!!!una bonge la Story hebu twende RAF tukaweke Booking,,ndipo wakaenda na Zabron hadi pale RFA na zabron akaanza kuruka kwa hewa na simulizi yake ya Sitoisahau Gamboshi....
So nimejaribu kukufahamisha Namna gani jamaa alipomaliza Simulizi yake pale RAF na maisha mengine yalivyoendelea,,,Me ni miongoni mwa watu ambao sikubahatika kusikiliza simulizi ya Rojaz Radioni ingawa nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa hicho kipindi,,,,na nimeanza kufuatilia kile kipindi baada ya Fredrick Bundala kushika usukani,,ingawa inasemekana creator wa hicho kipindi ni Roy Maganga....
Je ndiyo hii aliyoiandika huyu memberMm nimesikiliza story yake ya rojaz mwanzo hadi mwisho, kipindi anaanza safari ya kwenda sauzi anapaita Jo beg, alienda kwa kuunga unga hadi analishwa panya njiani
Enzi za roi mbaliki manganga & fedrick bundala sitosahau ilikuwa ya moto sana sio kama ya saivi
Chai ya rangi hii ya kutunga, kwanza sio yeye asilimia 100.Je ndiyo hii aliyoiandika huyu member
Tuko pamoja....stori ndefu ndio zangu.Tuko pamoja Hadi Tamati kwa sisi wapenda story ndefu tutakuwa hatulali humu
Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Siyo mchezoMkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa
Sehemu ya 6
Kiukweli niliondoka pale magereza akili yangu ikiwa haijakuwa sawa na fikara nyingi zikiwa zimenitinga na kujiuliza sana huyu mtu amesema anataka kunipa utajiri,utajiri huo atanipa katika mazingira gani? Je atatoka? Je kuna mtu atanambia nikamuone? Au nini ni nini katika sakata hili? Kiukweli sikuweza kumuelewa hata kidogo huo utajiri napewa katika njia gani😂
Siku zikakatika nami kama kawaida yangu nikawa naendelea na mishe zangu zakusaka mkate wangu na pia bila kusahau wale watoto wa huyu ndugu sikuwatupa kwani pale ninapopata japo kidogo nilikuwa naenda kuwatembelea nao wakawa wanaifurahikia hali hiyo pamoja na mama yao,kiukweli nilijitahidi kuziba pengo la huyu ndugu yangu ambaye alikuwa katika mikono ya dola na ilikuwa haijulikani ni lini atakuwa huru ili kuweza kujumuika tena na wapendwa wake.
Baada ya masiku kadhaa ya mihangaiko hatimaye nikaenda tena kumtembelea yule ndugu na kubwa kuliko yote ni kuona ni kwa namna gani huyu ndugu ananielezea huo utajiri alioniahidi,nilifika pale magereza na kutimiza masharti kama inavyotakikana kwa yule anayekuja kumtembelea mfungwa na hatimaye nikafika na kukutana na ndugu yule,kiukweli alifurahi sana na kunambia "umekuja ndugu yangu? nimefurahi sana sana sana na je vipi vijana ulifanikiwa kwenda kuwatembelea?"
Nikamjibu "vijana hawajambo wanaendelea salama na masomo yao na wanakusabahi sana na kiukweli wamekumiss mno" baada ya kumwambia maneno hayo alikaa kimya kwa sekunde kadhaa na akatoa pumzi kubwa ya kuonesha kama mtu aliyekuwa kwenye tafakuli nzito na akanambia "ni kweli wanangu wanaumiss uwepo wangu na najua hata mie nimewamiss sana ila ndio hivi hatuwezi kupingana na majaaliwa ila naamini uwepo wako utaziba kwa kiasi kikubwa pengo langu kwani kile ambacho nilikuwa nakipambania kwa ajili ya kesho bora ya wanangu na mchumba wangu wewe utaenda kukitekeleza kwa niaba yangu kasoro vile ambavyo tumeapizana kuwa usije ukavitenda,nimekuamini ndugu yangu na nimeamua kukuelezea siri nzito iliyokuwa ndani ya mkebe wa moyo wangu na hakuna yoyote niliyewahi hata kumpa dondoo,kufungwa kwako kulikuwa umeletwa maalum ili uje unipokee kijiti na uende kutekeleza kile nilichokuwa nakitamani kwenda kukifanya" akasita kuendelea kwa kitambo kidogo na machozi yakawa yanamlenga ila kiukweli sikuwa najua ni machozi ya furaha kwa uwepo wangu au huzuni,kiufupi sikuelewa nami nikawa kimya nikiwa namsikiliza kwa umakini maneno yake.
Akaendelea kunambia ndugu yangu mimi nina utajiri,elewa nina utajiri na ninakusisitizia kuwa nina utajiri ambao utakwenda kubadili dunia yako na kwa muda niliokaa nawe hapa gerezani naamini wewe ndio mtu pekee utakayeweza kutekeleza maagizo nitakayokupa,ninao ndugu wa damu ila kwakuwa nimekwama humu nao wamenisusa na hawataki hata kujua hali yangu je nami natakiwa kujishughulisha kuhusu hali zao? Akalitupa swali kwangu nami nikamjibu "ni kweli usemayo ila hauwezi jua wametingwa na mambo gani" akadakia "je wewe hauna mambo yako? Mbona umekuwa ukija mara kwa mara hapa kuja kunitembelea,je niseme kinachokuleta ni hili jambo? Mbona umekuwa ukija kabla yakukutamkia kuhusu hili? Wewe ni ndugu yangu na nipo tayari kukubadilishia maisha yako na ya watu wangu wa karibu,wakuwazingatia ni watoto,wewe mwenyewe,mchumba wangu na kiasi mama wa watoto ila sikukatazi kuwatizama ndugu zangu lakini kwangu hawana umuhimu wowote ni wewe tu kama itakupendeza" kiukweli maneno yake yalinivuruga sana na nikawa nataka anielezee sasa na aache kuzunguka kwani ile hamasa yakutaka kuelezwa ikawa imenipanda.
Akanambia "najua nakuvuruga ila utaenda kijiji flani (akakitaja) na uko katika iko kijiji ndipo ilipo asili ya ukoo wangu na kuna ndugu zangu wengi tu na utakapofika pale yoyote utakayeonana nae mwambie nataka kwenda kwenye mji wa ukoo flani (akautaja ukoo wake),ni ukoo maarufu sana na pale katika nyumba ya familia kuna shangazi yangu,kaka yangu mkubwa na baba mkubwa" akavuta pumzi kidogo na kuendelea "najua unajiuliza ukifika utajielezaje kwao na wasijue dhumuni lako kuu lililokupeleka uko,wewe ni mtoto wa kiume najua hautashindwa kupata namna yakucheza na akili zao,nenda kijijini nami nitakupa maelezo makuu nawe jukumu lako ni kuyatekeleza maelekezo" nikawa namsikiliza tu huku nikitikisa kichwa kukubaliana nae na ikizidi ni kusema "ndio" yule ndugu aliendelea "utakapofika pale wewe waweza kuwaeleza kuhusu mimi na kutia ufundi wako zaidi na wala usiharakishe ulichokifata,soma mazingira usiwe na pupa ukawastua kwani nimeficha hazina kubwa na hiyo haipo ndani ya hiyo nyumba kuu ya ukoo" alipofika hapo nikawa nawaza na kuwazua,akaendelea kunielekeza " pembeni mwa hiyo nyumba kuna kijumba ambacho hakijamalizwa kimeachwa kama pagale ndipo ulipo mzigo huo ninaotaka uufate,ndani ya iko kijumba kuna kitanda cha kamba na ndipo ninapotaka uende kwani hiyo hazina nimeifukia chini ya kitanda iko,zingatia mzigo huo ni wako wewe na uamuzi wakuwatizama wengine nimeukabidhi kwako" kiukweli nilivuta pumzi ndefu na kujiuliza peke yangu hiyo hazina gani na chanzo chake ni nini na kama aliyeyasoma mawazo yangu akasema "wewe ni mwanaume najua hautashindwa kuipata hiyo mali na utatoka nayo na kwenda kutekeleza yale tuliyoahidiana leo" nikawa najiuliza je ni dhahabu,almasi,pesa au ni nyara gani ambayo ndugu huyu ameniambia na kunisisitiza kuwa ni hazina na natakiwa nitoke nayo na nikishatoka nayo nisiyafungue bali nihakikishe kwa nafanya kila liwezekanalo hazina nifike nayo mjini na nikishafika tu nisichelewe na nihakikishe narudi kule magereza na kunipa maelekezo zaidi ya nini chakufanya,tukafanye maongezi na kumpa vitu ambavyo nilikuja navyo kama sabuni na vinginevyo na tukaagana na akanambia "kila la heri ndugu yangu na nategemea ndani ya muda mfupi ntakuona ukija hapa ukiwa mtu mwingine kabisa,kapambane ndugu yangu" nami nikamjibu na kutabasamu lakini ndani ya ubongo wangu sikuwa hata na chembe ya tabasamu kwani nilikuwa na mawazo lukuki nikitaka kujua hiyo hazina ni hazina gani,chanzo chake,kwanini mimi na mengine mengi yalinizonga.
Kiukweli sikuweza kukaa kwa amani kwani kila nililowaza halikuweza kupata hitimisho na nikizingatia ndugu huyu alinitaka kwenda mwenyewe na nisishirikishe mtu yoyote kwani yeye amenipa madaraka mimi na niyatekeleze mimi tu,siku hii niliingia kulala mapema na hata chakula ni kama niligusa tu na saa 1 nipo ndani ya kitanda na hata usingizi uliponichukua wala sikufahamu nilijistukia ni kumekucha na lindi la mawazo likaniandama upya😂
Nilijizoazoa hapo na kufanya usafi wa mwili huku tafakuli kubwa ikiwa ni kwa namna gani nitaweza kwenda uko kijijini kwenye hiyo "hazina" niliyoambiwa na yule ndugu kule jela,nikiwa na viakiba vyangu vya pesa nikanunua vijizawadi ili nitakapofika kule nisiwe mnyonge katika mapokezi,kwakuwa yule ndugu alinijuza baadhi ya ndugu muhimu nami nikanunua kitenge na fulana mbili na sukari kilo mbili na chumvi na hatimaye nikajikongoja na kuelekea stendi kupanda gari za kwenda uko kijiji husika,kiukweli wakati wote wa shughuli zangu za udereva sikufanikiwa kufika maeneo ya uko,kwangu ulikuwa ni mazingira mageni kabisa na kwakuwa nililazimika kwenda kukawa hakuna budi na kweli nilifanikiwa kufika na nilipofika katika kituo ambacho yule ndugu alinielekeza kushuka nilifanya hivyo,mara baada ya kushuka nikasogea ng'ambo kidogo na kukuta sehemu watu wamechangamana wakifanya shughuli mbalimbali kama ufundi na ukodishaji wa baiskeli,wauza matunda,mazao ya chakula na hata mafundi nguo,kiufupi ilikuwa ni senta flani imechangamka nami nikajongea na kuwakuta kinamama wakiwa na biashara zao za vitafunwa, nikawajulia hali na kuwauliza kama nilivyopewa maelezo na yule ndugu yangu wa jela,kiukweli ukoo wao walikuwa ni watu wanaofahamika sana na haikunipa tabu kuweza kupelekwa hadi katika mji wao,nilipewa vijana wawili wadogo ambao walisisitizwa nipelekwe hadi mlangoni,kiukweli maisha ya vijijini ile heshima kwa mgeni bado ina nguvu sana.
Nilifikishwa tena nikiwa nimebebewa ile mizigo yangu na nikatambulishwa kwa mama mtu mzima ambaye tulimkuta ndio anatua mzigo wake wa kuni na jembe,nilikuja kumjua baadae kuwa ndio yule shangazi niliyehadithiwa na yule ndugu yangu,nikakaribishwa na baada ya salamu kama ilivyo ada nikajitambulisha mimi ni nani na ujio wangu pale,nilimpamba sana yule ndugu na kuwaeleza kuwa tulikutana jela na alinisaidia sana katika kuyakabili mazingira yale kwakuwa sikuwa na nguvu yakuweza kupambana na watemi wa jela ambao wengi wao wametawaliwa na utemi hata kama haujawafanya jambo lolote,kiukweli shangazi alinikaribisha na akawaita na baadhi ya wanandugu na kunitambulisha kwao, wakati wa jioni shangazi akaniandalia maji huku akiingia jikoni na kuandaa chakula na pia kulikuwa na kijana ambaye kiuwajihi alikuwa amenizidi kama miaka miwili au mitatu sema ugumu wa maisha na msoto wa kazi ngumu kijijini yeye alikuwa amejengeka kimwili nami nikionekana kimbaumbau,nilikuja kumjua jina lake kama Kaombwe,Kaombwe alikuwa nami katika kunipa kampani na ni mtoto wa baba yake mkubwa yule ndugu yangu wa kule jela.
Chakula kililetwa kilikuwa ni ugali wa mtama na mboga ya majani na maziwa ya mtindi tukawa tunakula huku michapo ya kimaisha na Kaombwe ikawa namuelezea vitu na wema mbalimbali ambao ndugu yao tumetendeana nia ilikuwa ni kumjibu kimtindo isi ajue nia ya kunileta pale kijijini,nikajifanya kuwa hali yangu ya kiuchumi imekuwa na nafuu sana na kutokana na wema wa yule ndugu nimeonelea kuja kuangalia ni kwa namna gani nami naweza kuacha alama katika mzizi wa ukoo wake ili hata atakapotoka aone ni kwa namna gani nimeuthamini wema wake kwangu,Kaombwe alifurahia na akawa analeta maswali ya udadisi kujua kama ni muda gani watu wanavyolala jela,je kifungo uwa kinahesabiwaje,nyapala anapataje cheo iko na mengine mengi nami nilimjibu kadri nilivyoweza kwani niliamini hawa ndio wenyeji wangu na kufeli au kufanikiwa kwa jambo langu kuna mchango mkubwa kutoka kwao.
Mara baada ya kumaliza michakato ya kuoga na kula nikaelekezwa chumba cha kwenda kupumzika na ni chumba ambacho nilishea na Kaombwe,kwakuwa sikuwa mwenyeji na kuogopa kuwaboa wenyeji nikawaaga na kuingia ndani huku mawazo yangu yote yakiwa katika hazina niliyoambiwa na kwanza kukiona iko kijumba ila nikayakumbuka maneno ya yule ndugu kuwa "usiwe na papara wewe tulia soma mazingira kila linalotakikana ulifanye kwa umakini na usiwape nafasi ya kukuwekea shaka" kweli nikayazingatia,usingizi haukuja kiukweli sauti za wadudu wa vijijini,chafya za ng'ombe na hata mapito ya watu ingawa haikuwa ya kivile yote niliisikia,usingi uligoma kabisa na hata Kaombwe alipoingia ndani kuja kulala nilimsikia kuanzia anabadili nguo hadi usingizi kumchukua na kuanza mikoromo mimi sikuwa na hata lepe la usingizi,mimi kitabia kwanza eneo likiwa jipya kwangu usingizi uwa unachelewa sana kuja sasa ukichanganya na hili sakata yaani ndio kama umenambia leo mkesha umekuhusu.
Nadhani kama nilipata usingizi basi hayakuzidi masaa matatu na kilichonistua usingizi ni wenyeji wangu walikuwa wakichukua zana zao na kutaka kuelekea mashambani kwani wenyewi wa maeneo haya kwa namba kubwa walikuwa ni wakulima hivyo uwa wanajihimu mapema kwenda mashambani kabla jua halijachanganya na pale nilimsikia shangazi akiongea na Kaombwe,nyumba za vijijini hazikuwa na dari hivyo mtu aliyeko kolidoni anapotaka kumpa ujumbe aliye ndani anakuwa hapati tabu na shangazi akawa anamueleza Kaombwe asitoke abaki nami kwani wao wote wakiondoka mgeni haitakuwa vyema kubaki mwenyewe,nikajinyanyua na kutoka nje na kumsabahi shangazi nikamwambia kuna mzigo wako na nikachukua ule mfuko wenye zawadi na kumpa yeye zinazomuhusu na zile flana moja nikampa Kaombwe na nyingine nikaomba apatiwe baba mkubwa atakapoamka,kiukweli shangazi alifurahi sana maana sukari,chumvi na kile kitenge kiufupi nilimloga vibaya na hata wale wenzake walifurahia,nikawagusia kidogo kuwa kama nitajaaliwa nataka kumjengea nyumba rafiki yangu kuuenzi wema wake alionitendea.
Siku ile nilibaki nyumbani na Kaombwe tukipiga soga na tukihadithiana habari mbalimbali kama mambo ya siasa,mpira ingawa sikuwa shabiki kihivyo na hali ya mvua na ukame ambao wakulima wanakabiliana nao,kiufupi stori almradi muda usonge na ilipofika jioni watu waliokuwa wamekwenda mashambani wakawa wanarejea majumbani lakini pamoja na kubaki pale nyumbani sikuacha kuyakagua mandhari ya pale ili kuziona zile alama muhimu kama kile kijumba na kweli nilikiona kwani kilikuwa mita chache nyuma ya nyumba hiyo niliyofikia,ni kijumba ambacho kwa muonekano wake ni kama aliyekijenga hakukikamilisha ila inaonekana pamoja na kutokamilishwa kwake kulikuwa kunakaliwa uko nyuma kwani kulikuwa na matambaa kama kitenge (nadhani walifanya kama pazia)kilikuwa kimechokeana kinaning'inia katika kidirisha kidogo na mabaki ya mtungi uliovunjika na kubaki kama vipande vya vigae,sikuzunguka sana kwakuwa eneo lilipo hazina nilishaliona kilichobakia ilikuwa ni kuangalia namna gani nitaweza kuingia ndani ya pagale lile kuweza kuyaona hayo ya ndani kujua yaliyomo je yamo?
Jioni mara baada ya shangazi kurejea na kuanza kuandaa mazingira ya maakuli baba mkubwa alikuja akiwa amebeba jogoo na kumwambia Kaombwe alifanyie utaratibu,naye akalichinja na shangazi akalifanyia yanayopaswa kufanywa,wakati wa maakuli chungu kilichojaa minofu kiliwekwa mkekani na wote wakawa wananisisitiza mie kula kwani kuku yule haswa alikuwa ni wangu na wao wananisindikiza tu.
Siku ikaisha na mimi na Kaombwe baada ya muda mfupi tukajongea kuingia ndani kuimaliza siku na kuisaka siku mpyaambapo asubuhi na mapema wale wa kwenda mashambani wakaenda uko na Kaombwe akanambia kwakuwa nimemgusia nia yakutaka kumjengea rafiki yangu yeye anao vijana ambao anaweza kuwaandaa kwa ajili ya kunisaidia katika ujenzi nami nikamwambia ngoja tu wala hasiwe na shaka kikubwa natizama mandhari kwanza alafu kuna mambo nayafikiria ndio tutaangalia njia bora zaidi na baada ya muda akanitaka radhi na kuniaga kuwa anaenda kijiji flani kuna harakati zake akaweke sawa na hadi mchana tu angekuwa amesharejea na kunitengenezea yale mazingira kama ya kifungua kinywa na mengineyo,mara tu nilipohakikisha kuwa Kaombwe ameshaenda zake na mji ulikuwa kimya kwakuwa mazingira pia ya mji wao yalikuwa yamejitenga na kuzungukwa na mashamba yao ya familia,nikajongea kuelekea katika lile pagale kuweza kujiridhisha na yale maelekezo ya ndugu yangu na nilipofika nikawa naupambua utando wa tandabui ambao ulikuwa umesambaa katika kijumba kile na kusogeza kimlango kilichokuwa kimeshikiliwa na bawabu moja kwa juu,nikausukuma na kuingia ndani huku nikiyapa nafasi macho yangu kutengeneza nuru ya kuweza kuona vilivyomo ndani.
ITAENDELEA!
Hapo kaandika au katumia program ya computer ya kubadili audio ya simulizi kwenda kwenye maandishi.Hongera umejitahidi kamanda kuiandika na kutumia muda wako
Kuna eneo nimesema mimi ndio mhusika? Rejea kusoma majibu niliyokuwa nawapa watoa maoni,story iko youtube nami nilichofanya ni kuitoa ktk sauti na kuiweka ktk maandishi,pole kwa kupanic usiweke negativity kichwaniChai ya rangi hii ya kutunga, kwanza sio yeye asilimia 100.
Kama unadhani nimetumia program yoyote kuibadili hii story nakujuza si kweli,nimeandika kwa mkono wangu kipande kwa kipande,sitaki kujisifu ila ninajitahd ktk upande wa kuandika tena natumia simu tu wala si computer,kuna story km 3 nimeshazidownload ila changamoto ni muda tuHapo kaandika au katumia program ya computer ya kubadili audio ya simulizi kwenda kwenye maandishi.