Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa
Sehemu ya 13
Baada ya kujiuliza sana je ntaogopa kwenda kule gerezani mpaka lini? Hatimaye niliamua liwalo na liwe sitaweza kujitisha na nafsi yangu nikakata shauri kwenda gerezani kumtembelea yule ndugu na nilipofika baada ya salamu za hapa na pale akanambia "Rojas mdogo wangu nakuomba uache kuja gerezani kuanzia sasa ndugu yangu" nami sikukubali tu uamuzi huo pasi na kufahamu kwanini amenitamkia hii kauli na kabla hajanifafanulia akaniuliza "je kuna yoyote umezungumza nae kuhusu siri yetu? Kiukweli niliogopa kumwambia kuwa kuna mtu nilimuambia na ujue hakuwa mtu tu kama mtu bali alikuwa ni kaka yangu kwa sababu tulishaahidiana kutokuisema siri hii,nilikaa kimya tu wala sikuweza kumjibu yule kaka,akaendelea kunambia "basi kama hakuna mtu uliyemueleza nakuomba kuanzia sasa kwanza usije kunitembelea" nikamuuliza "je ni kwa muda gani? Akanijibu "miezi sita kwanza ndio waweza kuja"
Nina maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu ya moja kwa moja na mtu huyu ameshanambia nisirejee mpaka ipite miezi sita "umemweleza mtu yoyote yale ambayo tuliyokuwa tumezazungumza? Nilimwambia "hapana siwezi kufanya hivyo" lakini ni uongo kuna mtu nilimwambia" nilirudi nyumba nikizidi kuyatafakari haya,kuhusu pesa mahala zilipo sikumshirikisha yoyote na hata mtu aliyenipangisha nyumba hii hajui kama mimi nimechimba ndani ya hii nyumba na kuhifadhi pesa,hajui,hii ni siri naitunza mwenyewe,mishe na mambo mengine yakiendelea naye kaka usumbufu ndio ukawa juu aliniambia "tuzungumze,tuzungumze" na wakati hapo biashara inazidi kusogea mbele na kama nilivyosema awali wingi wa pesa unapokujia lazima utaleta mtafaruku kwenye familia na wale wanaokujua,nishawahi kusikia mtu anajitapa "yaani namfahamu flani kindakiodaki" yaani kunatokea watu wanakujua hata kama utaonesha kuna njia sahihi umeipitia kwenye kupata hizo pesa ili kuwatoa shaka waweze kukuamini kwa sababu pesa hazipatikani kirahisi wengi tunapambana sana kuanzia jua linachomoza hadi linazama na wengine marejeo yetu ni usiku kabisa tukiwa hoi na tunadamka mapema kuisaka siku mpya,sasa mimi nimepata wapi kirahisi na wanajua mienendo yangu.
Niliendelea kupiga kazi kwa sababu sikuwa na ubaya na mtu,sikumfanyia yoyote ubaya lakini kaka hakunyamaza wakati wote na alishea na mshkaji wake wa karibu sana na mshkaji wake alizungumza na mimi kitu ambacho kiliniumiza sana,nilijisikia vibaya sana kwa sababu mimi nilimueleza kaka kwa sababu ni ndugu yangu na iweje naye aanze kurusha kete kwenda kushea na watu wengine,nilighadhibika na nikamwambia "mimi siwezi kushea chochote na wewe ndugu yangu,kaka ulizungumza hayo mambo na kaka yangu mimi siwezi kujua hayo mambo kayatoa wapi" wakati huo mimi nakuja kutambua kama kaka ameshamuhadithia mtu na huyo mtu amethubuv kuja kwangu nikahisi kaka labda anahisi sijamuelewa na donge la uchungu likanikaba sana mpaka kuhisi kububujikwa na machozi,nilijuta sana kwa yote niliyomtamkia kaka na yule mshkaji wa kaka akanambia "tuzungumze wewe najua unajua kama mimi ni mtu najua vitu vingi na lengo kubwa ni kukusaidia kwa sababu bado mdogo na inaonekana unamiliki pesa nyingi zitakuletea shida" nikamwambia "siwezi kuzungumza nawe chochote".
Zaidi na zaidi nilimfata kaka nikiwa na hasira sana nikamuuliza "hivi kaka unataka nini? Akanambia "kwanini" nikarudia "unataka nini,kosa langu mimi ni kukushirikisha? Mbona sasa tunataka kuingia katika vita ambayo sikuiwaza kama itaamka kwangu?" Akasema "kwanini mdogo wangu" nikamuuliza "kwanini siri yetu unaenda kuzungumza na watu wengine?" Kaka akanambia "sijashea hii siri na watu baki nimeshea na watu wanaojua vitu" nikamwambia "kaka utaacha lini kuzungumza vitu kama hivi? Ina maana mimi toka nimekwambia habari ya pesa umekuwa hupati usingizi,unataka nini?" Kaka akasema "unajua ninachotaka" nikamwambie "ebu niambie mimi sijui unataka nini" akasema "nataka mdogo wangu uwe salama" nikamwambia "kaka kwanini unaanza kunitishia maisha yangu" akanambia "mimi nakutishia,Unamaanisha nini?" Nikamwambia "kwenda kuwaambia watu eti mimi nina pesa nyingi,ziko wapi? Umeziona?" Akanijibu "si umenambia" nikamjibu "kaka hizo pesa nilizokwambia uliziona?" Akasema "mdogo wangu pesa unazo na umeziweka mahali" nikamwambia kwa hasira "kwahiyo kaka sasa hivi unakaa kuchunguza mienendo yangu,unachunguza maisha yangu,unachunguza ninakotoka na ninakoingia,unataka kusema unataka hizi pesa zituingize katika vita?" Akasema "mdogo wangu sio zituingize katika vita,nataka nikusaidie,sasa hivi mimi niko bega kwa bega nataka nikusaidie" nikamwambia "acha tamaa,kaka acha tamaa na hizi pesa si za kwako na wala haujui hata kiwango cha hizo pesa,hivi mimi wakiitwa watu wenye pesa hata kama kuna mtu nyuma yangu mimi nina pesa? Kufungua hilo duka na haya magari unaona nina pesa? Haya sina pesa nshatumia zote zishaisha" akanambia "usikasirike ebu ondoa jazba mdogo wangu ondoa jazba hivi vitu si vyakuwa na hasira navyo yule ni unajua ni mshkaji wangu nami nimemwambia anisaidie ili tuzungumze lugha moja,tusaidiane" nikamwambia "kaka unanisaidia nini? Nini unanisaidia zaidi zaidi unaniumiza kama unataka mimi na wewe undugu uendelee ninakutaka uache tabia hiyo mara moja,hautapata hata mia yangu,hautapata hata senti moja kutoka kwangu na hiyo vita unayotaka kuiibua na mimi wewe iibue tutapambana" kaka akasema "sasa hayo maneno yote yanatoka wapi,mimi nataka kukusaidia wewe unasema nataka kuinua vita" nikamwambia "unataka kuinua vita na mimi,kaka chanzo cha pesa kilipoanzia wewe hujui,umeongea vizuri mtu yuko gerezani je unajua nilienda wapi kwenda kuzipata hizo pesa? Sasa kama hujui kaa pembeni,niambie matatizo yako nikusaidie wewe na watoto wako lakini usinipande kichwani na ole wako uniletee mtu mwingine tena eti kuja kuzungumza na mimi eti kuja kunisaidia,sitaki msaada wowote mimi,sihitaji na tena ukome" kaka baada ya maneno haya kiukweli alistuka sana nilipomwambia hiyo sentensi kwakuwa nilikuwa sijawahi kumpandia juu kama nilivyompandia hivi kwa sababu nilikwazika sana.
Nimejikuta nimekuwa mtu mwenye mawazo nikijiuliza kaka ana mpango wa kufanya nini lakini hakuna kitu najuta kama kuzungumza na kaka katika hili,najuta sana,akili yangu ilikuwa inanambia nazungumza na mtu sahihi na vile kaka alikuwa mtu sahihi lakini naona taarifa za pesa kaka nae kama zimemchanganya.
Nilipata muda nikaenda kumtembelea mwanamke ya yule kakana alinipokea,hawa ni watu hivi sasa ni kama majukumu yangu kwa sababu ni vitu niliahidi kuvifanya kwa huyo mtu,nimefika nikamsalimia na kuna wakati tukazungumza kwahiyo sasa hivi ananipokea tu vizuri,wakati tunazungumza akawa ananiuliza "mbona unaonekana una mawazo sana?" Nikamwambia "hapana mimi sina mawazo nimekuja tu kukuona mara moja angalau nijue unavyoendelea" akanambia "naendelea vizuri nashukuru pia kwa sapoti,nashukuru kwa kila kitu hata sina la neno la kusema,nashukuru sana,wakati unakuja sikujua hata kama ni mtu mwema" nikamwambia "wala hata usijali,usiwaze kabisa" nakumbuka nikiwa nae hapa simu yake ya mkononi iliita na akasogea pembeni kuongea na simu lakini alikuwa anazungumza taratibu kiasi nikawa sisikii lakini kadri dakika zilivyokwenda akawa anaongea kwa nguvu,akawa anasema "sitaki nakwambia sitaki" yaani kama mtu anazozana nae hivi,hayanihusu na mara aliporejea nikamshukuru na kumwambia "mimi natoka" akanambia "samahani nimejikuta tu najibishana na mtu" nikamwambia "nini shida? Kama naweza kukusaidia pia unaweza ukaniambia" akasema "wewe acha tu katika maisha unajua unaweza kuwa na mtu unategemea mnaweza mkaanza safari pamoja jama rafiki yako mwisho wa siku ndio ameishia gerezani,vitu vingi aliniongopea lakini basi mwisho wa siku nikaamua kumpenda hivyo hivyo hata kama ni muongo,mdanganyifu,hana utulivu lakini yote juu ya yote yakatokea yaliyotokea siwezi kuishi mwenyewe na nikapata mtu lakini amekuwa ananisumbua sana,nikaona mh mambo ya mapenzi tena" anajeruhika na mambo ya mahusiano,mimi nikampa pole nikamwambia "kwenye mahusiano kuna changamoto nyingi lakini mazungumzo ni kitu ambacho kinawarejesha kwenye mwanzo wa mahusiano yenu,ukikutana nae na mkazungumza naamini mambo watakaa sawa" akasema "ni kweli umenishauri vizuri"
Nikawa nimeondoka lakini akili yangu ikawa imejua huyu msichana na yeye kumbe aliingia kwenye mahusiano na inaonekana hayaendi vizuri yanamuumiza hayo mahusiano,nikaachana nayo nami nikaendelea na harakati zangu kama kawaida za kila siku,siku zikawa zinakatika na kaka nimemfungia vioo ,ninajitahidi kutokuwa karibu nae kwakuwa alinikwaza sana na alijua kama alinikwaza sana,nakumbuka siku moja nikiwa kwenye nyumba ambayo ninaishi,ninaishi peke yangu na mtu pekee anayeingiaga ndani ni mtu anayekuja kwa kufanya usafi na ni lazima niwepo,afanye usafi na aondoke ndio nitoke zangu,usiku nikiwa nimelala nikaota ndoto,nimeota ndogo kuna mtu anagonga mlango,gonga sana mlango kwenye ndoto,nikanyanyuka na kwenda kufungua mlango na nilipofungua nikamuona kaka na akanambia "Rojas nimegonga mlango kwa muda mrefu sana mbona haujafungua hata mlango? Nikamwambia "si unajua tena huku ni mbali huku lakini kuna walinzi" hapa kwenye hii nyumba ninayokaa kuna mlinzi,ni mlinzi kabisa na silaha na nilimchukua kutoka kampuni ya ulinzi ambaye uwa anakuja wakati wa usiku na asubuhi anaondoka,sikutaka kuweka mazingira yoyote ya uspesho kwa kuweka walinzi wengi maana watu wanaweza hofia kwanini afanye hivi,niliamua kuishi maisha ya kawaida lakini nyakati za usiku niliweka ulinzi,kwenye ndoto namuona kaka amekuja moja kwa moja hapa mlangoni nikamwambia "karibu,karibu sana" akanambia "asante" kaka akaingia (kwenye ndoto) wakati naruhusu kaka aingie kumbe kaka hakuwa peke yake (kwenye ndoto hiyo)naota akaingia na watu wengine tena watu walioshiba kweli kweli,kwenye ndoto hiyo nikaota namuuliza "hao ni wakina nani?" Akanijibu "hawa wanataka kujua mahali unapoweka pesa kwa sababu manajua pesa zimo humu humu ndani" kaka yangu namuona amekuwa na macho mekundu,macho ambayo tunayo sisi ni meupe lakini yake yamekuwa mekundu,mekundu kama damu,amenitolea macho na kunitamkia "utabaki na uhai iwapo tu utatuambia wapi zilipo pesa" kwenye ndoto nikamwambia "kaka unaniletea hawa watu hapa nyumbani kwangu unahisi mimi nina pesa hapa? Kama tungekuwa na pesa si tungejenga majengo makubwa kaka tukaishi katika majengo yetu,hizo pesa unazofata ziko wapi?" Kaka akasema "najua mahali hizo pesa ziliko,wewe si unajifanya unanificha siri,nendeni kachukueni zile pesa mahali nilipowaambia" naona wale watu (kwenye ndoto)wakielekea moja kwa moja chumbani nikaanza kupiga kelele,nikapiga sana kelele na kumwambia "kaka unafanya vitu gani,kaka unafanya vitu gani" wale watu wakaingia mpaka chumbani na wakaanza kuchimba palepale nilipofukia pesa,wakamaliza kutoa zile pesa na mmoja anasema "sasa inakuwaje,inakuwaje?" Kaka akasema "tupoteze kabisa ushahidi" yaani waniue mimi,nikastuka na kumuona mmojawao amenishikia bastora na kaka anamwambia "sambaratisha ubongo huyo tuondoke haraka" nikastuka kutoka ndotoni na niliogopa sana,hofu iliamka moyoni mwangu na kwa sababu sina mtu wa kuweza kumshirikisha,sina wa kuzungumza nae kuhusu hizi pesa kwa sababu mtu niliyezungumza nae ambaye ni kaka sasa hivi amegeuka na kuanza kuwaeleza marafiki zake kwamba mimi nina pesa kwahiyo siwezi tena kumwambia.
Nilipata sana msongo wa mawazo kwa siku ile,niliwaza sana,nawaza tu,nawaza sana na nikaanza kuwa na uoga,nakumbuka usiku wa siku iliyofatia baada ya siku ile niliyoota nakumbuka nilidumbukia kule chini ninakohifadhi zile pesa nilikuwa na mashine niliyoinunua ya kuhesabu pesa,niliambiwa nisihesabu hizi pesa na kwa mfano nikiwa nimetoa milioni ishirini,nimetoa nikapeleka,nahesabu kiasi kilichohitajika yaani kwa mfano nilipoagiza hizi gari nilihesabu mlolongo wote wa gharama za hadi hapa ,nilitaka kuhesabu yaani nijue tu ndani nina kiasi gani,nishaelezwa nisizihesabu lakini nikazidi kuwaza na kuingiwa hofu, "pesa gani ambazo kila nikihesabu nakosea,ukwelh usiku wa siku ile nilisema lazima nihesabu pesa na nilisema lazima nizihesabu zote,nilibeba pesa nakuweka kwenye kikapu kikubwa,vikapu hivi wanavyoendea sokoni kina mikono huku na huku nikaweka pesa nyingi na nikatoka nazo kutoka chumbani na nikaweka mashine nikaanza kuhesabu zike pesa,nikahesabu,nikahesabu,nikahesabu,nikaendelea kuhesabu kwakuwa natumia mashine na wakati naendelea kuhesabu nikawa najiona siko sawa,ulishawahi kuhesabu kitu hadi ukawa unajiona unataka kuchanganyikiwa? Basi hiyo hali ndio ilikuwa inanikuta mimi wakati huo yaani hadi hesabu nikawa nimeipoteza,nikawa najiuliza hivi hi ni hali gani? Au ukiwa unahesabu pesa nyingi hali hii uwa inatokea? Nikajiuliza sana na ajabu ninapokuwa nataka kiasi flani labda milioni ishirini ya jambo flani hali hii uwa haitokei.
Yule mtu ameshaniambia nisiende gerezani kwa wakati huu hadi baada ya miezi sita nami nina mtanziko wa hizi pesa katika kuzihesabu,nahitaji kumuuliza kwanini iwe hivyo anipe ufafanuzi kwa sababu niliogopa,niliogopa kwa sababu mara ya mwisho aliniuliza "ni nani ulimwambia kuhusu siri hii? Nilikataa,nahesabu pesa wakati niliambiwa nisihesabu pesa na nimepatwa na hali flani ya kuchanganyikiwa wakati nahesabu pesa,nimeanza kutishwa na hii pesa,niliona siwezi kukaa bila kwenda kumuona huyu mtu kule gerezani,sikuogopa,nilienda kumfata gerezani,ahadi ni mpaka miezi sita lakini nilimfata gerezani,alishangaa sana wakati sio makubaliano yetu na hata aliniuliza "umekuja kufanya nini?" Nikamwambia "ni muhimu nimekuja kukuona" akanambia "haukupaswa kuja hapa" nikamwambia "hapana mpaka nimekuja ni jambo muhimu sana" akanambia "ni hatari haukutakiwa kuja hapa" nikamwambia "siogopi jambo lolote" akanambia "huelewi unaloongea" nikamwambia "nisikilize,kwanini mimi kila nikihesabu pesa nashindwa kupata hesabu kamili ya kiwango cha pesa?" Akaniuliza "kwani umehesabu pesa? Nikamwambia "ngoja nikwambie,usitake niishi maisha yasiyo na amani,maisha yangu yametawaliwa na amani siku zote,ulinipa majukumu na nikayapokea kwa amani je nini maana ya kuhesabu pesa na kuwa napoteza kumbukumbu wakati nazihesabu? Akanambia "Rojas kwanini unaenda kinyume na vile tunavyokubaliana? Nikamwambia "nataka maelezo,naomba ukweli je hizi pesa ulizitoa wapi? Akanambia "unaendelea kuniuliza hilo swali? Unachojali wewe ni nini Rojas? Hatutakiwi kuongea kwa muda mrefu" nilmwambia "naomba uniambie sitaki uniweke katika hali ya mawazo" akanambia "usiwe na mawazo fanya kama nilivyokwambia,hautakiwi kukosea" nikamuuliza "kwani hizi ni pesa za masharti? Akanambia "hautakiwi kukosea,umefanya makosa Rojas,unajua nini kitakuja kukupata ukija kukosea tena? Nikamuuliza "nini kitanipata? Akanambia Rojas hauwezi kukosea na zingatia hautakiwi kuhesabu tena zile pesa na uelewe kuwa hauwezi kuhesabu,elewa hauwezi kuhesabu kiwango cha hizo pesa,fanya mambo unayotakiwa kufanya,hizi ni pesa halali kabisa sio makaratasi wala pesa za udanganyifu fanya vitu vya msingi uje baada ya muda tuliokubaliana" alikataa kuendelea kuongea na mimi,nilipata mawazo sana,ulishawahi kupata mawazo? Mimi nilikuwa na mawazo sana na nakumbuka kuna washkaji zangu nilikuwj nao kitaa na nikawapa waendeshe magari ambayo nimenunua wakaniona sipo ok,ni watu washkaji lakini siwezi kuwashirikisha kuhusu mambo yangu ya sirini,wakanambia "Rojas una pesa,Mungu amekubariki umepata pesa lakini unashindwa kuitumia pesa,wewe unahitaji toto zuri,watoto wazuri wapo ambao wako tayari kutumia pesa na sio unajibanabana,kwanini unajibanabana wakati una duka lako,una magari yako yanaleta pesa kila siku na hata kama unataka nyongeza kwa ajili ya hii biashara ufanye vitu vikubwa ndio unashindwa kustarehe wewe mwenyewe? Maisha ndio haya haya Rojas tafuta kitu kitakachokupa starehe unawaza pesa kwamba naingiza natoa kiasi gani huku hujipi furaha wewe mwenyewe bwana,jifurahishe sisi ndio washkaji wako tuko hapa,tunapambana,kula bata kula maisha bwana"
Unajua mimi sio kijanawa kujichanganya sana na ndio maana kipindi kile nimepatwa na mabalaa ya kwenda gerezani nilijiuliza sana kwanini mimi nimekwenda gerezani kwa sababu sio kijana wa maisha hayo lakini msongo wa mawazo uliokuwa unanisonga nikaona natakiwa nipate tulizo la moyo,nipate kutulia moyo wangu,nikaanza kutumia kilevi moja,mbili,tatu ilimradi kujibusti ninajitafutia furaha ili niruhusu maisha mengine yaendelee.
ITAENDELEA!