DALALI MKUU
JF-Expert Member
- May 7, 2022
- 2,011
- 4,705
EPS 1
Heshima Kwenu Wakuu,
Niliwaahidi Kwamba Nitawaletea Mkasa Kuhusu safari au Hekaheka zangu nilizozipata wakati nafanya Shughuli zangu za Udalali Jiji la Dar es salaam na maeneo ya jirani.
Mwaka 2017 Nilitoka kwenye wilaya Niliyokuwa Ninaishi nikaamua Kuhami Jiji La Dar es salaam kwenda Kufanya Kazi zangu binafsi nikiamini Kwamba nitatoboa Kimaisha, Nilikuja Dar es salaam baada ya kufanya akzi maeneno tofauti tofauti Mkoa wa Kilimanjaro.
Nilipofika Dar maisha Yalikuwa magumu sana kwakweli, kuna sehemu nilipata Kazi nilikuwa nalipwa 40k kwa wiki haikuwa inatosha Chochote, Lakini kazi Pia ilikuwa na mateso sana. Nilikuwa nafanya kazi kwenye Kampuni Fulani Binafsi inajihusisha na Masuala ya Matangazo ilikuwa ni kazi ya mteso sana, nilikuwa naingia kazini Asubuhi saa moja natoka saa 12 Jioni.
Nikitoka nakuwa nimechoka sana kiasi kwamba siwezi hata Kufanya shughuli nyingine na mshahara ndio huo kwa wiki unalipwa elfu arobaini tu ukitoa hapo nauli na hela ya kula kwa wiki unabaki na deni au ukijibana sana useme ule mlo mmoja tu unabaki na elfu Kumi.
Kodi nilikuwa nalipa eldu thelathini kwa mwezi maji elfu kumi umeme elfu Kumi jumla Kodi kwa mwezi ni elfu hamsini na kila wiki nikijibana sana kwa mwezi nakuwa na Akiba ya Elfu arobaini yaani kila iki elfu Kumi.
Hapo nilipokuwa nakaa ilifika wakati kodi ikaisha nikawa sina hata Mia mbovu akiba yote nilikuwa nimeitumia kutokana matatizo yaliyojitokeza, Mwenye nyumbaalikuwa haelewi Kitu zaidi ya kutaka hela yake.Yule mzee alinisumbua sana nikaongea nae Anivumilie akanipa Muda wa wiki nikaanza kupiga Bei vitu vyangu vya ndani ila kupata wateja ndio ikawa shida sana, kila nikinidai Mitandaoni hakuna mteja zaidi watacoment watu wanaulizia Uko wapi na bei gani tu.
Aisee nilichanagnyikiwa sana Wakuu Wiki ikakata nikapata ile hela ya wiki Elfu arobain nikakusanya kusanya kwa wadau nilikuwa naapiga Vizinga nikapata elfu sabini nikampa mwenye nyumba ili inayobaki nitamlipa.
Kuna watu ana Roho mbaya sana Yule Mzee akaniambia hapokei Kodi hata kama Imebaki Buku Hapokei na kama siwezi kumpa hela yake nijiandae kuhama nikatafute Chumba sehemu Nyingine.
Pale pale akaanza Kupiga simu anamtafuta Dalali ili amtafutie mpangaji mwingine, Hela yangu ameikataa nilirudi ndani nikawaza sana mambo mengi mno nilipiga simu kwa wadau lakini kila ninayemkopa ananielezea matatizo yake makubwa zaidi nikaamua kuachana nao.
Nikiwa ndani Yule Mzee nikamsikia anaongea na watu anamuonyesha Chumba Changu na wanakubaliana bei afu anamwambia Kuna mtu ndnai ila nitamwmabia afungue uingie ndani ukiangalie.