EPS 7
Simu za Udalali zikaanza Kuita, ila tataizo nilikuwa sina uzoefu w akumpanga mteja, nikawa namtafuta Masai ila masai kanishauri nikipata mteja nimungnishe nae ili iwe Rahisi, namimi nikafanya hivyo.
Mteja wa kwanza Tulipata dada mmoja yeye alitaka Nyumba nzima maeneo ya Mbezi, jamaa akampanga mbezi hamna ila kimara anaweza kupata kodi ilikuwa laki 250 kw Mwezi Yule dada alikuja kucheki siku ya kwanza akaridhikaila akasema atakuja na mume wake.
Basi akatupa service charge elfu ishirini, Masai akaniambia kwa sababu ndio unaanza chukua yote nipe buku ya bajaji tu.
Baada ya siku mbili hivi Yule dada akasema mume wake anakuja kuiona na kama atakubali watalipia, nikmpa amsai taarifa tukaenda kukutana nae jioni hivi kama saa Moja jioni wakaicheki wakakubali, masai akamvutia waya Bosi akamwambia aende steshenari Fulani hivi akachukue hapo mkataba, yeye yupo njiani anakuja kumkabidhi.
Wakacheki mkataba, wakasainisha wakapewa Account maana walisema wanalipa kwa njia ya CRDB, wakafanya malipo na sisi walituwekea TIGOPESA.
Nikagawana na Masai ila amsai akaniambia nimpe laki moja mimi nichukue laki na nusu , Daah nikaanza kuona Mwanga wa amisha mapya ndani ya wiki tu nimepata laki moja na nusu niaksema sasa haya ndio maisha.
Dili moja tu mzigo mrefu unapatikana,,Nikaenda na Masai tukaenda sehemu tukaagiza mchemsho na bia safari tukapiga na story nyingi ambazo zilikuwa zinanipa uzoefu.
Majira ya saa tano hivi tukaagana yeye akaenda mbezi mimi nikaenda zangu maghetoni, usiku huo nilikuwa na furaha sana nikampigia Judy nikamwambia namna ambavyo dili zimeanza kusoma na mzigo niliopiga.
Judy alinipongeza sana akanitia sana moyo, Judy kwenye kutia moyo utafikiri mnyaki.
Tuliongea mengi sana na kubwa aliniambia atakuja kunitembelea aone makazi mapya, tukapanga weekend aje maghetoni kufanya uzinduzi.
Baada ya hapo ilikuwa kila siku usiku lazima Nipost Kwenye magroup ya whatsap na Facebook, insta bado nilikuwa sina wadau, Ilikuwa ukiniunga kwenye Group tu bila kujali lina husu nini mimi usiku napost na asubuhi na Posti huko huko kwenye magroup ili mradi nipate wateja.
Ikawa ndio utaratibu wangu na kazi yangu kwa wakati huo, nilienda hivyo na baada ya mwezi nilikuwa tayari nimeshaanza kujulikana maana Masai alikuwa annipa sana mashavu na kunikutanisha na mabosi.
Kwa mwezi ule wa kwanza nilipata wateja kama wanne Hivi, lakini nakumbuka niliweka akiba laki tatu kwa mwezi huo mmoja.
Siku moja Yule dada niliyemtafutia Chumba Huyu tumwite Jeni, alinitafuta kwa simu
Jeni: Mambo dalali
Dalali : Niko salama, unaendeleaje mazingira hapo umeyapenda?
Jeni: Mazingira mazuri kwa kweli pana utulivu asante sana.
Dalali: Sawa sawa, asante kwa mrejesho.
Jeni: Asante dalali uje ututembelee maana hapa hawaai watu wengi nakuwa mpweka sana
Dalali: Nitakuja huko napita sana ila sikutaka kukusumbua.
Jeni: Poa.
Tuliongea mambo mengi sana ila kwa ufupi yalikuwa kwa mtiririko huo.
Kazi za Udalali huwa hatufuti namba ya mteja.
Kazi ziliendelea na Judy alikuwa ankuja sana maghetoni kunitembelea hadi akapozoea na vihela vikawa vimeanza kuingia ingia na mabosi wananitafuta wenyewe niwauzie vitu vyao.
Nikabadili ghetto likawa na muonekano tofauti lakini chumba nikaanza kukiona Kidogo na hakina hadhi tena ya Mimi DALALI MKUU kukaa hapo kwanza ni uswahilini sana. Maskini akipata…………
Jeni nilikuwa na wasiliana nae sana na katika Maongezi yetu akaniambia Kwamba yeye hajaolewa Yule jamaa aliyekuja anye ni mchepuko wake maana yeye ameoa. Pia akaniambia anafanya Kazi kwenye Kampuni moja hivi ya Mawakili yeye ni sekretari.
Lakini pia alinisimulia kuhusu changamoto alizokuwa za Mahusiano yake ikiwemo kukosa mtoto kwa muda mrefu japo anatamani sana.
Nilimtia moyo lakini kwenye mambo ya Kiroho niko vizuri kidogo nikamuombea nikaahidi kwamba nitaendelea Kumuweka kwenye maombi na nitaenda kwao niwe namuombea.
Alifurahi sana sasa mazoea yakazidi ikawa kila akiamka lazima anicheki kwa whatsap, au apige usiku video call yaani akanizoea sana na akawa huru kunieleza vitu vingi sana.
Na mimi nikawa najitahidi sana maana nilikuwa mlokole Mlevi, na yeye ilionekana alinizoea zaidi baada ya kumdanganya nimeokoka na ni mwana maombi (Huko nyuma nimekulia kwenye maisha ya dini sana na ni mtu wa maombi licha ya kuwa mlevi)
Jumapili moja niliamua niende kwake nikamtembelee kwake, nilivaa Kaunda suti yangu moja ya Kilokole alinishonea Judy, Niliwaka kama Pastor kabisa.
Nilienda nikamkuta amekaa sndani mwenyewe na akanihakikishia kwamba usalama upo Jamaa yake Jumapili huwa haendi kule maana anatoka na familia yake OUT, mimi dalali kichwani mawazo yangu yalikuwa yakifisi kabisa nikasema nikifika tu naomba Tunda kilokole na alzima nimle.
Nilifika nikamkuta sebuleni kibarazani amekaa anachezea simu yake
Dalali Mkuu: Habari Jeni! Mambo vipi?
Jeni: Poa sana Dalali Mkuu! Karibu sana.
Dalali Mkuu: Asante sana,
Jeni: Ubize san, leo hatimaye umekuja
Dalali Mkuu: Kweli kazi zinanibana sana kazi zetu hizi hazina ratiba uanweza kupanda daladala ukapigiwa simu na mteja umepeleke site
Jeni: Hehe
Baada ya mazungumzo mafupi nikajumuika nae tukaendelea na stori za hapa na pale.
Kisha akaniambia Karibu ukae ndani maana nje huku tukiongea tu majirani wote wanasikia huko.
Akatangulia ndani lakini mawazo yangu yote nilisema leo simwachi, nikimuacha atanione mnyonge sana hapa Nipige mzigo niachane nae mchepuko wa watu huyu.
Ndani tulipoingia sikutaka Kumwachia pumzi nilianza na stori za Uchokozi nikimtania alivyo mzuri, akaishia kusema tu anapenda utani wangu na amneno yangu.
Nikapna time ianenda nikamsogelea alipokaa, alikuwa amekaa kwenye Kisofa hivi, nikamshika Begani alafu nikamwangalia Usoni, nikaona sura yake inabadilika kwa kasi sana.