Mkasa wa kweli, kuhusu visa vya kushangaza nilivyokutana navyo katika kazi za Udalali

Mkasa wa kweli, kuhusu visa vya kushangaza nilivyokutana navyo katika kazi za Udalali

Eps 9

Nikamchana nikamwambia hilo dili siwezi kwa kweli, akanimbia twende tukifika unashuka unamuelekeza kwa gari nilimkatalia kabisa nikamwamabia hiyo ni ngumu sana.

Nikamwambia niache hapa niondoke tu ukiwa na dili nyingine utanipa lakini kwa Hii hapana, akanisogeza hadi mbezi kwa msuguri akaniacha hapo. Nikaeleka home nikiwa na mwazo sana kwanza ni mtu mwenye status Kubwa sana katika jamii, ana familia alafu ni mtu wa ibada sana swala zote tano. HIKI NI KISA CHA KWANZA Cha ajabu nilichokutana nacho baadae huko mbele nitakuja kuelezea nikiona kuna sababu ya kufanya hivyo.



Basi baada ya Kuchana na Idris kama kawaida kabla ya kurudi home lazima nipitie sehemu nipate safari au konyagi ndio ilikuwa ratiba yangu ya kila siku.

Kwa uapnde wa kazi nilikuwa nimeshaaminika sana na connection nikawa sasa sifanyi tena za kupanga nyumba na viwanja tu Nikawa sasa natafuta an Masoko ya bidhaa mbalimbali. Nilikuwa natafutia makampuni tender kwenye taasisi za umma na serikali so nikawa maisha yamebadilika kwa kweli.

Muda huo niliamua kumhamisha Judy kibaha ili niwe karibu nae, sio kumuoa, Nilimtafutia sehemu akaweka ofisi yake ya kushonea Nguo maeneo ya njia ya Kinyerezi, Judy alikuwa na bidii sana katika kazi zake,.

Niliona ni vyema nikamlipa fadhila kwa namna alivyokuwa akinijali sana kipindi nasota.

Judy alikuwa ananipenda sana na siku zote alikuwa ananikumbushia suala la Kwenda kujitambulisha kwao ili nifahamike lakini pia wazazi watupe Baraka za kuanza maisha.

Hilo suala lilikuwa linanikera sana nikaona Sasa anataka kulazimisha ndoa nikawa nampanga sana uzuri nikimpanga alikuwa ananielewa.

Alikuwa anapambana sana kwenye kazi yake kuna wanafunzi pia alikuwa anawafundisha pale na wateja walikuwa wanamkubali sana maana alikuwa anjua kushona nguo za kiume na kike mitindo karibu yote alikuwa anpiga sana hela.

Siku moja aliniambia amekusanya ana akiba ya karibu million tatu ananishauri niongezee nikanunue kiwanja, ila nilimkatalia maana kuna dalili nilikuwa naziona nikasema nisije kumuumiza akaumia zaidi.

WAKUU MIO SIO MWANDISHI MZURI, ILA KWA LEO NAISHIA HAPA KUNA MATUKIO MANNE TU NDIO NITAYAZUNGUMZIA KWA UPANA WAKE JUMATATU.

NITAANDIKA KWA KIFUPI EPS KAMA TANO TU ALAFU TUMALZIE
Kama siku utatolea kitabu hii simulizi, basi kiite DALALI WA KICHAGA, utauza sana kwa hilo jina na simulizi yako. Hongera sana, wewe ni mwandishi mzuri.

Ova
 
Back
Top Bottom