Mkasa wa kweli, kuhusu visa vya kushangaza nilivyokutana navyo katika kazi za Udalali

DALALI MKUU
 
EPS 14

N.B Udalali niliacha kuna sehemu nilipata ajira nafanya hapo tangu mwezi wanne mwaka Huu lakini hata hivyo nilikuwa nimeshaacha. Sasa hivi nafanya mara chache sana inapobidi. Nimeweka sawa ili kupunguza maswali.

Kama wewe ni mpangaji au ulishawahi Kununua nyumba kwa watu au kiwanja bila shaka ulishawahi Kukutana na kisa cha Ushirikina hasa Uchawi kwenye Shughuli zako.

Miongoni mwa visa nilivyokutana navyo katika pilikapilika pilika za Udalali ni kazi hii Kuhusishwa na vitendo vya Ushirikina.

Kabla sijaingia kwenye udalali nilikuwa nafikiri kwamba Wenye nyumba ni washirikina sana kumbe visa Vingine vinafanywa na baadhi ya madalali wasiokuwa na maadili.

Kuna visa vingi sana vya watu kufanya Ushirikina asee.

Kisa kimojawapo siku moja Tupo bar na dalali mmoja anaitwa Rama, wakati huo ndio nilikua Nimeshakaa sana kwenye udalali lakini tukawa tuna share Experience za kazi zetu.

Nlimwambia rama Ilivyo ngumu Kumshawishi mteja hadi akubaliane na kazi yako

Rama akaniambia tatizo lako wewe Ni wale wa “MUNGU NISAIDIE” kutoboa ni ngumu sana lazima utembee kidogo kwa wazee.

Aliniambia kwamba madalali wengi wana wa wini wateja kwa sababu ya ushirikina.

Alinisimulia namna ilivyo kwamba ili uweze kupata mteja na hata kumbadilisha akili aache chaguo lake na akubaliane na chagu lako sio kazi rahisi.

Hivyo kuna Bibi ambaye wanamtumia yupo Kihesa Iringa anatoa dawa ya mvuto ambayo ukiitumia ukimshawishi mteja hata nyumba ambayo ipo bondeni anakubali hata kama nyumba aliyokuwa anahitaji yenye sifa Fulani, unaweza kumbadilisha

Huyo bibi wa Kihesa anakupa dawa ambayo ni kama kimzizi ambacho unatakiwa kukiweka mfuko wa nyuma wa suruali yako kila siku unapoenda kwenye mishe mishe zako au kama una kiofisi kuna kidawa anakupa unakiweka kwenye droo unachanganya anhela nyingine zinaitahela tu na watu.

Sikutaka kumbishia maana lengo langu ilikuwa nimsikilize tu ila mimi huwa simaini hayo mambo japo yapo ila sitaki kuyategemea kabisa madhara yake ni makubwa mkuu wala usiyatamani.

Sasa akaniambia kwamba yeye anacho kizizi akiongea na mteja yeyote lazima atakubali tu hata kama alihitaji nyumba Ubungo atampanga atampa ya Kimara au mbezi na atakubali.

Lakini pia unaweza ukawa unahitaji nyumba au kiwanja na mtu akakupeleka abondeni kabisa, au jirani na dampo au sehemu yenye makelele kama bar au kule wanakouza K, unajikuta uekubaliana nae na kulipia ukishalipia ndio akili zinaanza kukufunguka kumbe dawa yenyewe ndio inakuvuta.

Siku ukimkuta mtu amepanga vingunguti machinjoni na ni mtu mwenye akili timamu au amepanga mabondeni mvua ikinyesha tu anaingia ankutoka akiwa anogelea usije kushangaa ujue ni ushirikina unafanya kazi nah ii ni kazi inayofanywa na madalali njaa.

Rama alinaimbia wengine wanachanjiwa dawa kwenye Uume, wanapeleka majina yao kwa waganga kisha wanafanya wanachojua wanakuchanjia dawa kwenye Uboo au shingoni., huyo akikushawishi huchomoki mzee.

Kisa kingine cha Ushirikina hiki nilisimuliwa na Dalali Tumwite Tall wa Tabata Segerea yeye aliniambia sasa hivi dalali mkuu una connection sana na mabosi mpumbaze mmoja uanze kuzifaidi Kodi usikubali kukaa kizembe.

Iko hivi kuna mzee mmoja wa malamba mawili Mwisho, Alikua ndio mtaalam wa hayo mambo ilikuwa ukimkabidhi funguo tu na hauishi hapo anafanya ushirikina wa kukupeperusha anakufanya unasahau kabisa nyumba yako utakumbuka lakini kila ukipanga kwenda unaahirisha, mzee alikuwa anpanga anakula kodi tu kila mwezi na mwenye nyumba hajui chochote kinachoendelea.

Huyu mzee alikuwa an nyumba yake Malamba mawili Alikuwa anaiuza kwa taarifa za watu wa karibu ni kwamba alishawahi kuiuza kwa watu kadhaa alafu wakishalipia anabaki nayo.

Sasa yeye alikuwa na dawa zake alikuwa akishakuuzia nyumba unafanya malipo na anakuambia umpe wiki moja ahamie kwenye nyumba yake nyingine ila ukishalipia hutarudi tena huko na wala hutakumbuka mzee anaendelea kula hela na nyumba anabaki nayo.

Inasemekana yeye watu walikuja kugundua siri kuna jamaa alitaka kununua nyumba hiyo majirani wakamtonya kuhusu hilo swala mnunuzi akasema sasa huu ndio utakuwa mwisho wake. Jamaa akanunua nyumba wakafuata michakato yote kisha akampa hela yake akaondoka mzee akasemaapew siku tatu ahamishe vitu. Usiku akatengeneza dawa zake kama kawaida akafanya ya kufanya, Kesho yake asubuh mnunuzi akarudi akammabia ulichofanya umeshashindwa hama leo leo na ndio ikawa mwisho wa ufalme wa Yule mzee baada ya kuumbuliwa, Kumbe jamaa alikuwa amejipanga sana kiroho alikuwa na kinga zake za kichawi uwezo ukazidiana.

Kwa ambao wanasema uchawi haupo nawashangaa sana, ndio maana tunaomba Mungu kila siku ili atuepushe na hayo mambo.

Tall akaa ananishauri na mimi niitumie hiyo dawa kupeperusha mabosi angalu na mimi nipate nyumba moja niwe nalia kivulini jasho la mtu hiyo siku nilicheka sana nikaona sasa hii kazi sio. Sikuwahi kujaribu kabisa hilo jambo japo alinipa shuhuda nyingi sana.

Kuna mama nyumba moja ilikuwa kibaha ni Apartment nzuri sana, lakini kila wapangaji walikuwa wakikaa pale miezi sita wanaondoka wengine hata hawamalizi hata hiyo sita wanaondoka.

Kuna Familia moja walipanga hapo ilikuwa ikifika kila siku usiku wanasikia watu wanacheka sebuleni wakichungulia ahwaoni mtu.

Kuna watu walikuwa wakilala kuna mapaka yanalia kweli kweli nje ya nyumba yanatoa sauti za ajabu sana, wakati mwingine wakitoka wakirudi wanaona kama matone ya damu mlangoni lakini walikuwa hawaelwi kabisa ni nini kinafanyika.

Mwanzoni walifikiri kwamba labda ni ugeni mawazo na woga ndio unawafanya wanasikia hivyo.

Na aliyekuwa akisikia mara nyingi ilikuwa ni mke wa jamaa sasa siku wamekaa sebuleni TV ikawa inajiwasha na kujizima alafu inatokea kama sauti ya vicheko hivi vya kukera.

Walikuwa wamekaa sebeleni wote woga uliwaingia sasa la mwanaume alikausha kwamba sio uchawi kuna hitilafu baadae kweli ikatulia na wakasahau.

Vile visa vikazidi sasasiku hadi siku nyumba akawa haikaliki kuna wakati walikuwa wanasikia pia kama watu wanarusha mawe kwneye mabati lakini wakauliza majirani wanasema wao hawakusikia.

Majini yakawa yanawavamia usiku yanawanyonga sana jamaa akaona visa vimezidi wakati mwingine wanalala kitandani wakiamka wanajikuta wamelala chini sebuleni tena wakiwa watupu.

Jamaa ilibidi aanze kutafuta ushauri kwa wadau wake wakamwambia atumie dawa za kienyeji mara maji ya upako lakini wapi mateso yakawa ni makubwa sana usiku ni heka heka hakuna kulala. Mwisho wa siku jamaa ikabidi ashauriane na mke wake ahame na stori zikasambaa mtaani mwneye nyumba ni mshirikina na ndani kwake kuna majini.

Ila mwenye nyumba alikuwa ansikia akafikiri majirani wanamzushia au hawampendi kwa hiyo mambo ya Kiswahili wanasambaza kwa watu ili nyumba yake wapangaji wasidumu.

Taarifa zilisambaa sana hivyo akaaamu na yeye kufanya tafiti zake za tiba huko kwa wataalam ndio wapiga Ramli wakamtaji jina la mtu Fulani hivi kumbe ndio alikuwa dalali wake anayemletea wateja.

Kwanini dalali alifanya vile, kwa sababu ile nyumba ilikuwa ni nzuri na watu wanavutiwa nayo na kodi yake ilikuwa sio ndogo na kila akileta mteja anpewa kamisheni yake.

Hivyo kuna madawa alikuwa amesindika huko ili wapangaji wasiwe wana dumu wahame apelike wengine apige hela tu kirahisi, maana unaambiwa kuna wapangaji wengine walikuwa Wanaka hata wiki tu na kodi wanasamehe wanasema wamepata mchongo mkoani wanahama kumbe wamekimbia mbilinge mbilinge za majini.

Baadae waganga walikuja kutoa hayo mazindiko na nyumba kwa sasa sijui ikoje il naamini iko vizuri.

Hivi ni visa ambavyo kwenye udalali nilikutana navyo, Wenye nyumba na wapangaji umakini unahitaji Kama una Sali Sali sana ombea eneo lako kabla ya kuhamia, Wakristo wanafanya maombi yao ya kuteka na kumiliki sijui maombi ya vita n.k ili uweze kuishi vizuri, washirikina wanaweka pia mamlaka zao.

Kwenye uuzaji wa viwanja dalali akifika kwenye uwanja wako ukimpa kazi lakini akigundua unataka kumzunguka au kumpa mtu mwingine unaweza kuuza hicho kiwanja hata laki na kisipate mteja hadi yeye aamue.

Unaweza kuuza kiwanja hicho kwa mwaka mzima kila mteja akija munakubaliana bei anakubali kulipa akiondoka hata simu hapokei tena.

Hiki ni kisa kingine tena kwenye udalali na ni matukio ya kweli sio ya kusadikika. Nitarudi kuhitimisha kesho muda kama huu.
 
Dooo hicho kisa cha kuliwa kodi kilimkuta jamaa nyumba za mbezi akaliwa laki 9, ila matapeli hawana huruma, jamaa alikua amejichanga anatoka kwenye kastoo alikohifadhiwa alipoanza kazi ameona akapange wakapita na laki 9 yake
 
..
 
EPS 15

Baada ya kumalzia baadhi ya Visa kama nilivyowaambia kwenye Epsd za huko juu nilipewa Kesi ya kutishia Kuua kwa sababu ya Kuwa karibu sana na miongoni mwa wateja wangu wa mwanzo kabisa kwenye Udalali,Jeni.

Kesi nilikuwa naenda lakini wakanishauri nimalizane na mchepuko wa Jeni, ili mambo yasiwe mengi. Nilimtafuta Mchepuko wa Jeni nikaongea nae akakubali ila akaniambia nitafute hela nikafute hiyo kesi polisi. Nilimkubalia lakini sikufanya hivyo ahdi leo.

Jeni baada ya kuona mchepuo anamnganagania sana na anatamani ndoa, walienda kushirikisha marafiki zake wakaongea nae Mwamba ikabidi wakubaliane yaishe ili amruhusu mwenzie aolewe maana yeye hana namna anayoweza kufanya.

Jeni alikuja akapata mimba na alifurahi sana maana kwenye maisha yake hakutegemea kama ingewezekana tena maana kwa maelezo yake alikuwa amehangaika sana bila mafaniko, alinishukuru sana kwa maombi namna ambavyo tulishirikana aliahidi zawadi kubwa sana na kwa wakati huo kuna zawadi alinipa hii haina haja ya kuiandika.

Mwaka alikuja kuolewa akamfuata jamaa yake Huko kilndi Tanga wakaendelea na maisha yao na sasa ana watoto wawili.

Mwaka 2019 mwishoni Nilikuja Kupata pia mtoto nilizaa na Judy lakini hatukuoana, hivyo ilibidi wakati wa ujauzito alipokaribia kujifungua alirudi kwao na hata baada ya kujifungua alikaa sana, mimi nilikuwa naendela kuwasiliana nae kama kawaida na kumpa mahitaji yote Muhimu ya Mtoto.

Na mwaka huo pia niliacha shughuli za udalali kuna Dili ambalo Jeni alinipa kuna Company moja hivi nilikuwa naenda kwa ajili ya Kuandaa Tender Documentes na Ishu nyingine zinazohusiana na Tender mbalimbali lakini pia kwenye masuala ya IT ila jukumu langu kubwa lilikuwa ni IT nilipiga hapo kazi sana kwa Muda mrefu hivi.

Hadi siku niliyokuja kupata matatizo makubwa kwenye hiyo kazi nikaja nikafukuzwa kuna ishu ilitokea ya udanganyifu na mimi nikahusishwa moja kwa moja nikafukuzwa nakumbuka hicho kisa nilikisumilia huku miaka ya nyuma

Siwezi kusahau siku niliyofukuzwa kazi nikiwa baa

baada ya hapo nikajichanganya kwenye Company nyingine nikapata kazi kwenye Taasisi Fulani nikawa mkuu wa Kitengo cha Masoko nilifanya kazi pale na ilikuwa ni kazi ya Kusafiri sana nah ii ndio iliyonibadilisha kabisa, maana ilikuwa na Hel asana ile kazi.

Wakati huo Judy alisharudi dar tukaamua tusihi hivyo bila ndoa rasmi ya kisheria/kidini na mtoto alishakuwa mkubwa kabisa na hapo matukio ya usaliti asee yalikuwa yananitokea sana.

Alikuwa ananifuma sana na matukio ya usaliti, maana ile akzi ilikuwa inanikutanisha na watu wengi sana na wengi wao ni wanawake warembo na mimi ndio ilikuwa ugonjwa wangu

Ulevi ndio ilikuwa moja ya sifa yangu kuu Kuna bara za kimara huko, mbezi, na Goba hadi leo nimeacha vimeo vya madeni lakini pia nimeacha huko umaarufu wa Totozi na kulewa chakari.

Matukio yalipozidiana Judy yalimshinda maana tulikuwa hatuna hata watu wa maana wa kutusuluhisha, nilikuwa najitetea sana lakini mwisho wa siku aliamua Tuachane akaendelee na maisha yake.

Tuliahana na wala sikujali kabisa lakini mara kwa mara nilikuwa nawasiliana nae kwa ajili ya mtoto.

Ile kazi ilikuja kuingiliwa na mambo mengi biashara ikayumba wateja wakapungua maana mkoani watu walikuwa wameshaishtukia wauzaji wakawa wengi sana hivyo nikaachana nayo.

Baada ya kuachana nay o mwaka 2023 mwezi wa kwanza maisha yakabadilika sana akiba nikaanza kutumia kiba kidogo niliyokuwa nayo hadi zikaisha.

Jamaa yangu alikuwa kasulu akanipa mchongo wa biashara ya kulangua mazao, tulikuwa tunanunua nafaka kasulu na maeneo mengine ya Kigoma huko hadi katavi ile biashara ilikuwa ni ngumu sana maana kuna wateja tulikuwa tunawatumia mzigo huko dar lakini wakishapata mzigo wanaanza kuzingua malipo.

Lakini pia kupata hasara za mara kwa mara jamaa yangu kwa sababu alikuwa mwenyeji alikuwa ananipa sana hela hadi mwisho wa siku mtaji ukakata.

Nikaachana nae nikahamia Kigoma mjini kuna hela niliuza kiwanja Dar kama Million tatu hivi nikawekeza kwenye biashara ya vinywaji, nyie Kigoma iskieni tu mtaji ulikata ndani ya muda mfupi sana.



Umasiki ukaanza kuninyeemelea nilipigwa sana Uchumi Mkuu, ulinipiga kweli kweli nikawa mlevi tu nashinda vijiweni na kupiga dili za fasta hasa za ufundi kwenye IT lakini kipato kilikuwa kidogo sana kutokana na hali ya kigoma hakuna mtu anaweza kukupa hela ya maana sana sana elfu kumi au kumi na tano.



Maisha yakanipa kwlei nikaw amlevi tu sasa wa zile Pombe za Bei rahisi kunaambayo ilikuwa inaitwa Shimwa ndio ilikuwa pombe yangu, nikaacha na kwenda ibadani kabisa hata maombi nikawa sifanyi tena maana niliona kama dunia imeshanielemea.

Watu wangu wa dar ndio nilikuwa nawapiga vizinga na Jeni mara kwa maraa alikuwa ananiwezesha kama nimekwama sana japo nilikuwa naogopa sana maisha yakuomba omba tena hela ndogo ndogo

Ilifika wakati iakwa hata nakaa wiki bila Kuoga yaani wala kubadili nguo mimi ni kunywa tu asubuhi hadi jioni.

Usiombe maisha yakupige utakumbuka kila kitu, niliahidi kupambana kwa kila nguvu lakini niliamua kurudi Dar mwaka huu mwezi wa kwanza

Nilitafuta akzi sana hata huku JF niliomba mchongo sana ila watu wana ku PM unampa na namba unajieleza wee kisha anakupotezea.

Mtu anaandika tangazo la kazi ukimcheki anakumbia nakurudia, ilikuwa inaniumiza san asana.

Wakati huo nikiwa dar natafuta Kazi na wakati huo huo nilikuwa nishanza kurudisha majeshi pia kwa Judy kwa ajili ya kuomba tuyamalize ili Turudiane maana sasa hata hela ya kula ilikuwa ishanza kunipa chenga.

Marafiki wengi ukwa na shida ndio utawajua, jamaa zangu nilikuwa nimeshawapiga vizinga hadi nikaogopa.

Tumaini lilikuwa limebaki kwa Judy tu na niliona nitafute suluhu kwanza bila hivyo naweza kukata moto.

Wakati natafuta suluhu na Judy pia nilikuwa natafuta kazi kwa udi na uvumba.

NITARUDI SAA TISA KUMALIZIA WAKUU, NIMEJITAHIDI KUANDIKA KWA KIFUPI ILI NISIWACHOSHE MAANA NILIJARIBU SANA KUSIMULIA KWA MTIRIKO MZURI NIKASHINDWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…