Mkasa wa kweli, kuhusu visa vya kushangaza nilivyokutana navyo katika kazi za Udalali

Je ulishamla Jeni mara ngapi?,Judy umesharudiana nae?
 
Hapa safi sana mkuu
Ewaaa hapa safi sana
 
Dalali, kuna sehemu niliona ume comment kuwa ulipata mteja anatafuta frem. Ila baada ya kucheck picha yake whats app uligundua ni kaka'ako ukamblock. Natamani usimulie kwa undani kama utaweza
Ni kwleli mkuu shida nashindwa kupangilia matukio ila hilo nitalisimulia kwa faida yako na wengine.
 
EPS 16

Baada ya Maisha kunipiga kweli kweli, nilifanya jitihada za kina sana kumtafuta Judy mwanzoni alikuwa hataki kabisa kusikia habari ya Kurudiana na wala hata kuonana tu.

Ila mtoto alikuwa anapiga video Call namuona, mtoto alishakua mkubwa kabisa ana miaka mitano

Nilimtafuta rafiki yake aende akaongee nae ila, nilimwambia anipe Muda niongee nae tu uso kwa uso naamini hata kama hataki turudiane angalau tunaweza kuzungumzia hatma ya mtoto na maisha mengine yaendelee.

Nilijua tu nikikaa nae kwa dakika thelathini tu lazima anielewe maana nilikuwa nimeshajipanga kisawa sawa

Rafiki yake alinirudishia majbu ya kunikatisha tama kweli kweli alisema hataki kabisa Kuongea na mimi kwa jambo lolote kama nina shida na mtoto ampe mtu amlete nimuone nikae nae nikichoka Nimrudishe.

Judy aliwahi kumwambia Huyo rafiki yake niwatafute wale Malaya zangu niendelee nao, na hali ninayoipitia anamuomba Mungu ikibidi hadi nitembee barabarani naongea mwenyewe kabisa.

Siku moja alinitumia sms akaniambia uko nyumbani nikamwmabia ndio leo sijatoka siku nzima, akaniambia hata Malaya zako hawajaja kukutembelea au walishavuna wanasubiri msimu tena msimu mwingine wa mavuno.

Alikuwa ananiumiza sana na muda huo sina kazi, sina hela nawaza hata kodi ikiisha nitalipa vipi.

Nilifikiria niuze kiwanja changu kimoja ambacho kilibaki nijipange kwenye biashara ila nikaona kwa maisha yalivyo sitaweza kununua tena kingine.

Baada ya jitihada nyingi sana kufeli niliamua sasa niende mimi mwenyewe kwa Judy nyumbani niaksema hata akinifukuza Poa ila siwezi kutulia kiboya japo aliniambia siku nikikanyaga kwake au kwneye biashara yake ataniitia mwizi au ataniaibisha sana.

Nilisema liwe liwalo nikaenda kibabe asee alivyoniona nilivyokuwa nimebadilika aliishia kunione Huruma maana hakuamini kama hali ilikuwa mbaya hivyo.

Nilienda sikutaka kupoteza muda wala nilimwambia moja kwa moja ila nilijikaza sana "Judy, naomba msamaha kwa moyo wangu wote kwa maumivu niliyokusababishia. Nimejutia sana na natamani kurekebisha mambo. Tafadhali nipe nafasi ya kuzungumza nawe.nahitaji muda wako mfupi tu unisikilize kisha utafanya maamuzi wewe mwenyewe”

Alinicheki bila kusema kitu kabisa nikarudia tena hayo maneno kwa hisia kali sana zile hisia za ndani kabisa.

Akaniambi haya sema hapa kwani unataka kusemaje nikusikilize nikamjibu

Asante sana kwa kujibu, Judy. Naendelea kukuomba msamaha tena kwa jinsi nilivyokukosea na jinsi hii imetuathiri sisi na mtoto . natamani zaidi tujadili hili pamoja, kwa nia ya kujenga upya na kuhakikisha tunaweka familia yetu mbele. Maana ni jambo sasa la kujenga makosa yameshatokea lakini Mungu ametupa nafasi tena tuongee haya mamb.

Nilijieleza kwa unyenyekevu sana na upole ule wa kumaanisha japo baadae nilikuja Kuona kama nimejidhalilisha sana kujieleza sana mbele ya mwanamke.

Nikamwmabia mimi ni hayo tu nimeona nikueleze naye nikampa muda ili aongee

Alinishangaa sana hakuamini kama ningeweza kujishusha hivyo.

Alianza kuongea alianza kunikumbusha matukio ya nyuma jinsi nilivyokuwa kiburi, dharau vile nilikuwa nafuja hela na watoto wazuri bar alifungua faili moja moja hadi mwisho akaanza kutoa machozi, namimi sikuwa mbali nikamsogelea nikaanza kumfuta machozi huku nambembeleza na vimaneno maneno vya Hapa na pale vitamu.

Akaniambia basi ondoka tu tutaongea kwenye simu, Tuliendelea kuongea kwa simu kama wiki hivi tukajikuta kama tumeshaanza kurudiana tena akanaimbia kama nataka turudiane akanipa mashart mawili.

Moja tukapime afya, na sharti la pili hatarudipale home hadi niende kwao na tumalize mambo ya Harusi.

Ilibidi nikubaliane nae maana yeye ndio aliyekuwa amebaki peke yake.

Tulikuja kurudiana japo hadi sasa hatuishi pamoja maana tunafanya mchakato wa kwenda kwao ila kama nilivyowahi kusema sehemu mimi home nilitoka nasitaki kuonana na ndugu zangu ndio kipengele japo nimepanga niende home nimeamua kuwasamhe ndugu zangu ili Turudishe umoja na masuala ya ndoa yafanyike. Siku nikienda homenitawaletea Mrejesho.

Kuhusu masuala ya kazi Mwezi wanne mwaka Huu nilipata kazi sehemu nipo hapo maisha yameanza tena kuleta mwanga, nashukuru mshahara nao sio haba.

Nimeona nishee haya machache kwenu Uandishi ndio unaniangusha. Sifa kuu ya watu wa IT kuandika hatujui wala kusimulia.
 
Inaonekana huyo judy ndio nyota yako ilipo.
 
Usimsaliti JUDY HATA KWA ISHARA.
MHESHIMU HATA UKIWA UNAOTA OTA KWA KUMHESHIMU SANA,NI MKE SIYO MWANAMKE TU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…