Mkasa wa kweli, kuhusu visa vya kushangaza nilivyokutana navyo katika kazi za Udalali

Mkasa wa kweli, kuhusu visa vya kushangaza nilivyokutana navyo katika kazi za Udalali

Yani mnachekesha nimeshajieleza huko mwanzo sihongi mwanaume sijawahi na haitokaa itokee

Msijachanganye habari za mume(huyu nae inategemeana ana mchango gani kwangu)nazungumzia mahusiano ya uhawara
huyo mume huwa inatokea tu vupu mnakua mme na mke 😄
 
EPS 6.

Nikawa tayari nimeacha kazi Rasmi na nimehama kibaha na nimehamia Rasmi Jiji la Dar es salaam mbezi kwa Msuguri.

Maisha mapya yakaanza na vichenji chenji kwneye ile hela ya Judy zilikuwa zimebaki nilikuwa nina jiko dogo la gesi, hivyo nikaenda kununua mahitaji ya ndani ili nijipange upya nijue namna ya kupambana na maisha.

Nikaendelea kukaa pale lakini story ya Masai ya udalali ilinivutia sana nikasema sasa hii ndio kazi ninayotaka nikafanye. Nilikuwa nampigia mara kwa mara masai na kuonana nae lengo anionyeshe njia maana aliniambia kwa kauznia nikipata wateja nimwambie maana kuna nyumba kadhaa na viwanja amevishikilia.

Baada ya wiki hivi nikaanza kutengeneza Posters nakuziweka mitandaoni ili nipate wateja angalu wa kauznia nipate uzoefu.

Kweli baada ya kupost simu zikawa zinaanza kuita ASEE.

HAPO SASA NDIO SAFARI YANGU RASMI YA UDALALI IKAANZA, sasa kwenye hiki kisa au story nitakuelezea matukio ya kufurahisha, ya kusikitisha, dili haramu, dili za ajabu na mambo ya kushangaza ambayo nilikutana nayo. Lengo langu ni ujifunze Mambo mbalimbli ambayo madalai wankutana nayo, namna ya kupambana na changamoto za maisha bila kukataa tamaa, hela inavyoweza kumbadilishia malaika kwa shetani,na mambo mengine mengi.

Baada ya utangulizi huu nitaanz Rasmi Jumatatu hii kushusha vyuma.
Hiyo jumatatu bado?
 
EPS 14

N.B Udalali niliacha kuna sehemu nilipata ajira nafanya hapo tangu mwezi wanne mwaka Huu lakini hata hivyo nilikuwa nimeshaacha. Sasa hivi nafanya mara chache sana inapobidi. Nimeweka sawa ili kupunguza maswali.

Kama wewe ni mpangaji au ulishawahi Kununua nyumba kwa watu au kiwanja bila shaka ulishawahi Kukutana na kisa cha Ushirikina hasa Uchawi kwenye Shughuli zako.

Miongoni mwa visa nilivyokutana navyo katika pilikapilika pilika za Udalali ni kazi hii Kuhusishwa na vitendo vya Ushirikina.

Kabla sijaingia kwenye udalali nilikuwa nafikiri kwamba Wenye nyumba ni washirikina sana kumbe visa Vingine vinafanywa na baadhi ya madalali wasiokuwa na maadili.

Kuna visa vingi sana vya watu kufanya Ushirikina asee.

Kisa kimojawapo siku moja Tupo bar na dalali mmoja anaitwa Rama, wakati huo ndio nilikua Nimeshakaa sana kwenye udalali lakini tukawa tuna share Experience za kazi zetu.

Nlimwambia rama Ilivyo ngumu Kumshawishi mteja hadi akubaliane na kazi yako

Rama akaniambia tatizo lako wewe Ni wale wa “MUNGU NISAIDIE” kutoboa ni ngumu sana lazima utembee kidogo kwa wazee.

Aliniambia kwamba madalali wengi wana wa wini wateja kwa sababu ya ushirikina.

Alinisimulia namna ilivyo kwamba ili uweze kupata mteja na hata kumbadilisha akili aache chaguo lake na akubaliane na chagu lako sio kazi rahisi.

Hivyo kuna Bibi ambaye wanamtumia yupo Kihesa Iringa anatoa dawa ya mvuto ambayo ukiitumia ukimshawishi mteja hata nyumba ambayo ipo bondeni anakubali hata kama nyumba aliyokuwa anahitaji yenye sifa Fulani, unaweza kumbadilisha

Huyo bibi wa Kihesa anakupa dawa ambayo ni kama kimzizi ambacho unatakiwa kukiweka mfuko wa nyuma wa suruali yako kila siku unapoenda kwenye mishe mishe zako au kama una kiofisi kuna kidawa anakupa unakiweka kwenye droo unachanganya anhela nyingine zinaitahela tu na watu.

Sikutaka kumbishia maana lengo langu ilikuwa nimsikilize tu ila mimi huwa simaini hayo mambo japo yapo ila sitaki kuyategemea kabisa madhara yake ni makubwa mkuu wala usiyatamani.

Sasa akaniambia kwamba yeye anacho kizizi akiongea na mteja yeyote lazima atakubali tu hata kama alihitaji nyumba Ubungo atampanga atampa ya Kimara au mbezi na atakubali.

Lakini pia unaweza ukawa unahitaji nyumba au kiwanja na mtu akakupeleka abondeni kabisa, au jirani na dampo au sehemu yenye makelele kama bar au kule wanakouza K, unajikuta uekubaliana nae na kulipia ukishalipia ndio akili zinaanza kukufunguka kumbe dawa yenyewe ndio inakuvuta.

Siku ukimkuta mtu amepanga vingunguti machinjoni na ni mtu mwenye akili timamu au amepanga mabondeni mvua ikinyesha tu anaingia ankutoka akiwa anogelea usije kushangaa ujue ni ushirikina unafanya kazi nah ii ni kazi inayofanywa na madalali njaa.

Rama alinaimbia wengine wanachanjiwa dawa kwenye Uume, wanapeleka majina yao kwa waganga kisha wanafanya wanachojua wanakuchanjia dawa kwenye Uboo au shingoni., huyo akikushawishi huchomoki mzee.

Kisa kingine cha Ushirikina hiki nilisimuliwa na Dalali Tumwite Tall wa Tabata Segerea yeye aliniambia sasa hivi dalali mkuu una connection sana na mabosi mpumbaze mmoja uanze kuzifaidi Kodi usikubali kukaa kizembe.

Iko hivi kuna mzee mmoja wa malamba mawili Mwisho, Alikua ndio mtaalam wa hayo mambo ilikuwa ukimkabidhi funguo tu na hauishi hapo anafanya ushirikina wa kukupeperusha anakufanya unasahau kabisa nyumba yako utakumbuka lakini kila ukipanga kwenda unaahirisha, mzee alikuwa anpanga anakula kodi tu kila mwezi na mwenye nyumba hajui chochote kinachoendelea.

Huyu mzee alikuwa an nyumba yake Malamba mawili Alikuwa anaiuza kwa taarifa za watu wa karibu ni kwamba alishawahi kuiuza kwa watu kadhaa alafu wakishalipia anabaki nayo.

Sasa yeye alikuwa na dawa zake alikuwa akishakuuzia nyumba unafanya malipo na anakuambia umpe wiki moja ahamie kwenye nyumba yake nyingine ila ukishalipia hutarudi tena huko na wala hutakumbuka mzee anaendelea kula hela na nyumba anabaki nayo.

Inasemekana yeye watu walikuja kugundua siri kuna jamaa alitaka kununua nyumba hiyo majirani wakamtonya kuhusu hilo swala mnunuzi akasema sasa huu ndio utakuwa mwisho wake. Jamaa akanunua nyumba wakafuata michakato yote kisha akampa hela yake akaondoka mzee akasemaapew siku tatu ahamishe vitu. Usiku akatengeneza dawa zake kama kawaida akafanya ya kufanya, Kesho yake asubuh mnunuzi akarudi akammabia ulichofanya umeshashindwa hama leo leo na ndio ikawa mwisho wa ufalme wa Yule mzee baada ya kuumbuliwa, Kumbe jamaa alikuwa amejipanga sana kiroho alikuwa na kinga zake za kichawi uwezo ukazidiana.

Kwa ambao wanasema uchawi haupo nawashangaa sana, ndio maana tunaomba Mungu kila siku ili atuepushe na hayo mambo.

Tall akaa ananishauri na mimi niitumie hiyo dawa kupeperusha mabosi angalu na mimi nipate nyumba moja niwe nalia kivulini jasho la mtu hiyo siku nilicheka sana nikaona sasa hii kazi sio. Sikuwahi kujaribu kabisa hilo jambo japo alinipa shuhuda nyingi sana.

Kuna mama nyumba moja ilikuwa kibaha ni Apartment nzuri sana, lakini kila wapangaji walikuwa wakikaa pale miezi sita wanaondoka wengine hata hawamalizi hata hiyo sita wanaondoka.

Kuna Familia moja walipanga hapo ilikuwa ikifika kila siku usiku wanasikia watu wanacheka sebuleni wakichungulia ahwaoni mtu.

Kuna watu walikuwa wakilala kuna mapaka yanalia kweli kweli nje ya nyumba yanatoa sauti za ajabu sana, wakati mwingine wakitoka wakirudi wanaona kama matone ya damu mlangoni lakini walikuwa hawaelwi kabisa ni nini kinafanyika.

Mwanzoni walifikiri kwamba labda ni ugeni mawazo na woga ndio unawafanya wanasikia hivyo.

Na aliyekuwa akisikia mara nyingi ilikuwa ni mke wa jamaa sasa siku wamekaa sebuleni TV ikawa inajiwasha na kujizima alafu inatokea kama sauti ya vicheko hivi vya kukera.

Walikuwa wamekaa sebeleni wote woga uliwaingia sasa la mwanaume alikausha kwamba sio uchawi kuna hitilafu baadae kweli ikatulia na wakasahau.

Vile visa vikazidi sasasiku hadi siku nyumba akawa haikaliki kuna wakati walikuwa wanasikia pia kama watu wanarusha mawe kwneye mabati lakini wakauliza majirani wanasema wao hawakusikia.

Majini yakawa yanawavamia usiku yanawanyonga sana jamaa akaona visa vimezidi wakati mwingine wanalala kitandani wakiamka wanajikuta wamelala chini sebuleni tena wakiwa watupu.

Jamaa ilibidi aanze kutafuta ushauri kwa wadau wake wakamwambia atumie dawa za kienyeji mara maji ya upako lakini wapi mateso yakawa ni makubwa sana usiku ni heka heka hakuna kulala. Mwisho wa siku jamaa ikabidi ashauriane na mke wake ahame na stori zikasambaa mtaani mwneye nyumba ni mshirikina na ndani kwake kuna majini.

Ila mwenye nyumba alikuwa ansikia akafikiri majirani wanamzushia au hawampendi kwa hiyo mambo ya Kiswahili wanasambaza kwa watu ili nyumba yake wapangaji wasidumu.

Taarifa zilisambaa sana hivyo akaaamu na yeye kufanya tafiti zake za tiba huko kwa wataalam ndio wapiga Ramli wakamtaji jina la mtu Fulani hivi kumbe ndio alikuwa dalali wake anayemletea wateja.

Kwanini dalali alifanya vile, kwa sababu ile nyumba ilikuwa ni nzuri na watu wanavutiwa nayo na kodi yake ilikuwa sio ndogo na kila akileta mteja anpewa kamisheni yake.

Hivyo kuna madawa alikuwa amesindika huko ili wapangaji wasiwe wana dumu wahame apelike wengine apige hela tu kirahisi, maana unaambiwa kuna wapangaji wengine walikuwa Wanaka hata wiki tu na kodi wanasamehe wanasema wamepata mchongo mkoani wanahama kumbe wamekimbia mbilinge mbilinge za majini.

Baadae waganga walikuja kutoa hayo mazindiko na nyumba kwa sasa sijui ikoje il naamini iko vizuri.

Hivi ni visa ambavyo kwenye udalali nilikutana navyo, Wenye nyumba na wapangaji umakini unahitaji Kama una Sali Sali sana ombea eneo lako kabla ya kuhamia, Wakristo wanafanya maombi yao ya kuteka na kumiliki sijui maombi ya vita n.k ili uweze kuishi vizuri, washirikina wanaweka pia mamlaka zao.

Kwenye uuzaji wa viwanja dalali akifika kwenye uwanja wako ukimpa kazi lakini akigundua unataka kumzunguka au kumpa mtu mwingine unaweza kuuza hicho kiwanja hata laki na kisipate mteja hadi yeye aamue.

Unaweza kuuza kiwanja hicho kwa mwaka mzima kila mteja akija munakubaliana bei anakubali kulipa akiondoka hata simu hapokei tena.

Hiki ni kisa kingine tena kwenye udalali na ni matukio ya kweli sio ya kusadikika. Nitarudi kuhitimisha kesho muda kama huu.
Naamini haya! Kuna nyumba nauza nimepunguza bei toka 250M mpaka 190M! Hivi leo kaja mteja anaongea kabisa kwamba hii nyumba nanunua ila kimya mpaka saa hii! Na nilimshirikisha dalali mmoja akatafuta wengine na wengineee! Usikute hawa jamaa zake wanapiga pini aysee! This world🙌🏾
 
Naamini haya! Kuna nyumba nauza nimepunguza bei toka 250M mpaka 190M! Hivi leo kaja mteja anaongea kabisa kwamba hii nyumba nanunua ila kimya mpaka saa hii! Na nilimshirikisha dalali mmoja akatafuta wengine na wengineee! Usikute hawa jamaa zake wanapiga pini aysee! This world🙌🏾
Inawezekana kuna ambaye ulianza kuongea nae alafu ukatafuta wengine
 
hii hadithi imeisha kihuni sana! wewe dalali mstaafu na mlokole mlevi popote ulipo agiza mizinga mikubwa miwili nitakuja kulipa kwa kukataa ushoga hadhalani
 
Back
Top Bottom