EPS 11
Jioni niliwapeleka wale Mafundi kwa Idris nikamkuta Yupo site kwake wakakubalina vile kazi watakavyokuwa wakiifanya, mafundio nao wakampa ushauri wao jinsi ya kuifanya, nilikaa pembeni wakati wanakubaliana sikutaka niwasikilize, huwa sipendi kufuatailia makubaliono ya watu.
Baada ya mazungumzo pale tulipanda kwenye gari akatupeleka mbezi tukawacha jamaa kwa Msuguri, sisi tukaendelea na safari hadi sinza maeneo ya Africa sana pale, Tukapiga vinywaji ila jamaa kutokana na kisa ambacho nimekiongea huko juu nilikuwa simwamini sana, nilikuwa namuona mtu wa Hovyo sana.
Tulipiga story baadae ikabidi nay eye azungumzie lile jambo, akaniambia shida ambayo anayo akaniambia nimtafutie kijana ambaye atakuwa anampelekea moto maana yeye asipofanya hivyo kuna shida anaipata lakini pia akifika home hawezi kumpelekea mke wake moto.
Alinaimbia mambo mengi hapa sitayaandika, akaniambia nikiweza kumtafutia atanipa zawadi Nono. Baadae ikabidi tukubaliane kuondoka ila nikamdanganya kuna mtu namsubiri bamaga hivyo yeye atangulie tu, Akaingia wka gari akatoa hela ya kazi ya kumtafutia vijana hiyo siku alinipa laki mbili kisha akaniongezea laki tatu akaniambia nimtafutie huyo mtu wa kumkula.
Niliwaza sana Ujinga wake, alio nao ila niakwaza kama naweza kupata hela na dhambi wataenda kufanya wenyewe mimi kuna shida gani kwani, mimi ninachotafuta ni hela hakuna haja ya kutafakari sana wakati mrija wa hela ndio huo.
Nilianza kutafuta usafiri wa kwenda Home, wakati huo nilikuwa naendelea kuchati na judy na kumelezea mambo kadhaa yanayoendelea lengo ilikuwa ni kumuaminisha kwamba tupo pamoja.
Nilicheki saa nikaona bado mapema nikaona hela nimeshapata mambo ya kurudi hadi mbezi ni kupoteza muda tu, nikakumbuka kuna demu wangu ana ki grocery kinondoni ngoja niende pale.
Nilienda nikaenda kumaliza usiku wangu pale na amisha mengine yakaendelea.
Niliendelea na mishe mishe za udalali kama kawaida ila udalali wangu nilikuwa nafanya kama nilivyoeleza nilikuwa napiga zaidi bidhaa na vitu vyenye hela nyingi ule wa kutegema service charge za elf kumi nilikuwa nimeshahama na ni ndani ya Muda mfupi sana.
Nilikuwa anendelea kuwasiliana na Jeni kama kawaida na alikuwa akiendelea na Program ya maombi ambayo nilikuwa nimemwambia, Na hili ndio tukio la kwanza acha nielezee kwa urefu nashindwa kupangilia matukio hivyo ni afadhali nianze na moja, moja nimalize kisha nifuate Lingine
Ratiba yetu ilikuwa ikiendelea vizuri japo kuna siku nilikuwa nalewa sana hivyo nashindwa kuendelea na maombi namdanganya niko kikaoni au nipo barabarani hivyo namwambia aendelee mwenyewe.
Alinishirikisha sana kwa habari ya Mchepuko wake alivyokuwa anaendelea kumsumbua Kichwa na akanieleza kwamba kwa wakati huo, wamegombana sana na alitishia kama akiendelea kumfuatilia ataenda kumshataki Polisi na pia atamwmabia mke wake kwamba amwambie Mume wake atulie.
Huyo kijana mwingine Tumwite Brown, Brown na Jeni walikuwa wapenzi wa muda mrefu kidogo ila alikuwa anaishi mkoa mwingine na huyo mchepuko walikutana mjini na story yao ndio ikaendelea.
Nilikuwa nampa Company sana kwenye Mambo yake yote na home kwake nilikua naenda tu kama kawaida nikijisikia naenda napiga ane story kisha anondoka naendelea na safari zangu.
Alikuwa ameshanikubali sana, akawa pia ananipa dili za hapa na pale, baada nilikuja kumwmabia nimesoma IT pia ikawa ananipa Michongo ofisini kwao Computer zikiwa na shida au wakihitaji marekebeisho kwenye jambo lolote alikuwa ananipa Pasi.
Lakini pia wakati mwingine akiwa Mjini alikuwa ananikutanisha na Marafiki zake lengo pia ili wawe wananipa Dili, Nilikuwa najivunga sana lakini baadae ikabidi nije nimwmabie kwamba Mimi natumia Pombe nikamchana kabisa maana nilikuwa Napata shida sana kukaa sehemu naye masaa mawili kunywa Juice au soda.
Jeni kutokana na uaminifu wangu alikuja kunipa Dili ambayo ilinipa hela nyingi sana, Brown alikuwa anaishi mtwara baadae akahamishiwa Tanga Kilindi.
Jeni alinipa dili alikuwa na nyumba yake alitaka Kuijenga kisiri siri bila Brown kujua, hivyo hiyo kazi mimi ndio natakiwa kusimamia kuanzia mwanzo hadi mwisho na hata mafundi wasijue yaani kila kitu ni mimi.
Alipiga mshindo wa hela huko masasi baba yake alikuwa na Guest baada ya ndugu kusumbuana kwenye Mirathi wakauza Gust yote na nyumba nyingine za wapangaji zilikuwa masasi huko huko, na shamba ya Mikorosho yalikuwa sehemu aliniambia Inaitwa namalenga Masasi ( Nilikuja kupajua maana niliwahi kwenda hadi huko masasi kwao, ila si kwenda nyumbani niliishia sehemu inaitwa masasi ya zamani karibu na stand ya masasi na soko linaitwa KAUMU)
Baada ya kupata mgao akanipeleka huko kwenye kiwanja chake, Mapinga bagamoyo kufanya hiyo kazi, binafsi nilikuwa sina uzoefu wowote wa ufundi wa kujenga ila niliona hapo siwezi kuiacha kwa kigezo cha SIJUI.
Nilitafuta dogo mmoja chali angu Huyu alikuwa Muha nikamwambia nataka nifanye ujenzi nikampanga maana yeye ni fundi baada ya kuona Ramani nilimwambia anitengeneze makadirio ya Gharama , akini kwanza akaone eneo. Alinikadiria, nikampeleka Jeni nikamwmabia tayari nimeshaandaa makadirio na gharama yake nikampa, So kama akiwa tayari aniambie ili niwapeleke mafundi site. Lakini nilimambia pia kwanza kwenye Hiyo kazi lazima na mimi aniwekee budget yangu.
Akanihakikishia haku nashida, kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kwenda ujenzi ulianza japo ulikuwa una changamoto nyingi sana mafundi hata kama ni marafiki zako ni wasumbufu sana, Kuongeza bajeti na mambo mengi sana.
Ujenzi ulienda taratibu sana baadae nikamwambia kuna majukumu naenda kufanya inabidi nimtafute mtu wa kusimamia, naye akakubali akaajiri mtu kabisa asimamie, lakini hadi hapo alikuwa ameshanilipa hela nyingi Kidgo japo sio kwa mkupuo nilivuna hapo karibu million 11.
Wakati Kazi ile inaendelea walikuwa na mpango wa Kuoana na Brown na mambo yalikuwa yanaendelea Kimya kimya alitaka wafunge Ndoa ya Bomani, ila kwenye suala la ndoa Jeni alikuwa hataki kabisa maana alikuwa anaogopa Kuhusu uzazi lakini pia Mchepuko wake angesikia anaolewa ingeweza kumtokea jambo baya.
Hapa NDIO mtihani Mkubwa alikuwa nao maana jamaa alikuwa anamngangania sana hadi alikua anamkosesha amani, na Jeni naye alikuwa ni sitaki nataka Leo atakwambia simtaki tena ukikaa muda unawakuta tena wapo pamoja.
Brown mara nyingi wikiendi alikuwa ankuja Dar kutembea alikuwa na Nyumba yake huko msumi na biashara ndogo ndogo so alikuwa anakuja na akija Jeni alikuwa anaenda Kulala huko.
Yule mchepuko wa Jeni akaja kupewa habari za Jeni halali pale mara kwa mara na akapewa taarifa zangu, ila kwa sababu alikuwa ananifahamu Nilishakutanishwa nae na jeni mara kwa mara Yule mwamba akafikiri akaunganisha doti akahisi huenda mimi najua Yule demu anamsaliti na mimi ndiye anshirikaiana nae.
Lakini majirani walivyo wa huko wakamwmabia pia ankuja nakaa hadi usiku sana Ilikuwa msala mkubwa sana, jamaa alikuwa ananipigia simu ananitisha sana, akanitafutia Hadi Polisi nikawekwa pale Mikocheni kituo cha polisi sikumoja ya Ijumaa baadae kesho yake nikahamishiwa staki shari jamaa alisema nimemtishia Kumuua. Idris ndio alikuja kunitoa pale baada ya kukaa siku mbili nyuma ya Nondo na Kipigo cha askari nilikipitia.
Baada ya kudhaminiwa nikaambiwa nireport kesho yake Jumatatu saa nne asubu ili kama wamemaliza kesi iende mahakamani.
Niliporudi pale ilibidi nimtafute Jeni ili nimuulize kinachoendelea na jamaa yake hadi mimi ameniingiza kwenye matatizo makubwa, na jamaa yake baada ya kujua nimetoka akanipiga mkwara sana akaniambia nimwambie Jeni anamsaliti na ani nimtajie wanaume wake, na kama sitamtajia na mimi nitakuwa mhusika atanifanyia kitu mbaya.
Jamaa nikaona sasa ameshaanza kunivuruga nilifika home nikapiga kwanza konyagi zakutosha maana nilitoka usiku saa moja Jioni,baada ya kupia vyombo vya kutosha nikaenda kwa Masai kumuomba ushauri wa Kufaa.
Lakini pia nimuombe anisindikize Polisi kesho yake maana idris alisema yeye anaenda kazini kwa hiyo thatapata muda.
Baada ya kumalizana nae ilibidi pia niende kwa Judy maana tangu jamaa amenipiga Pingu sikuwa nimewasiliana ane na sms zake kibao za lawama, hivyo nilienda ili nikajaribu kuweka mambo sawa.
Nilikuwa naawaza sana namna ya kwenda Kumdanganya, kwamba nilikuwa wapi, kwanini nilikuwa sipatikani, sms sijibu ilikuwa ni msala Juu ya msala, wakati huo Jeni hata simu hashiki.