Mkuu hii house niliyoamkiamo ina mambo mazito mpaka walioijenga waliiuza wakatimua mbio..
Na aliyeinunua akaishi hapa muda kidogo nae akapigwa donda ndugu na hawa viumbe akatimka mpaka wa leo hajarudi..
Sasa mimi kwenye kutafuta nyumba mwaka juzi nilikuwa na rafiki yangu ananitembeza kwa piki piki yake..
Kwakuwa nilikuwa nahitaji nyumba kwa haraka sana kutokana na nilipokuwa
Kuna nyumba niliirekebisha lakini aliyekuwa mke wangu kwa wakati huo alikuwa amehitilafiana na msimamizi wa pale ambae ni mama mmoja hivi.
Nadhani hiyo scenario unaipata ikifikia heating point.
Nikalazimika kutafuta nyumba fasta.
Mwanangu akanishauri,,We ni tajiri acha kukaa kwa masikini ona sasa visa vya kimasikini hivyo mtu anakupandishia kodi na mkataba ndio umeisha na hakukupa taarifa kukuandaa.
Nikamwambia so twende wapi akasema kipande fulani kwa Madon tu.
Nikasema duuh huko nitaweza kweli kupata nyumba ambayo itaifaa familia yangu?
Mwamba kwakuwa yeye ni mzawa kipande hiki akanipakia tukaanza kusaka nyumba ado ado maana huku cha kwanza Madon hawatumii madalali kwa asilimia kubwa hawa wa lege to lege.
Wanatumia kampuni za madalali zilizosajiliwa.
Tulianzia nyumba tatu zote nikapata ni upande mmoja hapo wanataka m4 kwa m5.
Nikamwambia mwamba kuna moja nimeielewa turudi town nikadraw pesa tuje nilipie kabisa.
Tukaondoka tukaeñda town nikavuta mzigo tukawa njiani kurudi sasa tukiwa tumefika mitaa fulani lakini huku huku kwa matajiri,
Jamaa akaniambia nimekumbuka kipande fulani kuna nyumba vipi tupitepo tukaicheki?
Nikamwambia yap twende.
Sasa nashangaa jamaa anachepuka na kanjia kembamba hivi.
Kichwani nikawaza hata nikiikuta ni nzuri namna gani siwezi kuilipia kanjia kenyewe ndio haka ka kunipeleka home mbona hapa kati wanaweza kukaa watu wa kazi wakakupora wakakuua bila mtu yeyote kujua?
Ila kwakuwa jamaa kashashika njia sikutaka kumsumbua mara sijui turudi tu maana hata njia yenyewe hairuhusu boda kugeuza.
TUkaenda hadi hiyo sehemu ambapo ndio humu nimekaa naandika huu mkasa.
Baada ya kufika tulimuona msimamizi maana yeye anakaa nyumba nyingine ya juu kidogo kiwanja tofauti kabisa na hii nyumba.
Yeye alituelekeza tu na kutupatia ufunguo..
Jamaa akamwambia si twende utuonyeshe?
Manzi akagoma kabisa akatupatia mfanyakazi wake wa ndani akampa maelekezo pale kiaina hatukusikia walichozungumza.
Basi tukafungua kigeti kidogo ambacho ndio kinaunganisha hivi viwanja viwili tukashuka mgazi na kuingia kulikagua hili jengo.
Aisee limejengwa kwa mtindo wa kipekee halafu la kitambo sana..
Baada ya kulicheki tu nikaelewa kuwa mwenye jengo hili kama ndie alilijenga basi bila shaka alikuwa kwenye chama cheusi..
Nikawa kimya tu tukazama ndani.
Kitendo cha kuingia tu ndani akili yangu ikabadilika kabisa na kujikuta nishalikubali hili jengo maana niliona upande ambao unapangishwa nikaambiwa bei 2.8m kwa mwaka kwanza nikashangaa inawezekanaje hii?
Jengo lina setup yote hii vyumba vitatu jiko liko full na bonge la sitting room kwa bei hiyo?
Sasa kwakuwa mazingira yangu yalikuwa ni kupata sehemu fasta nikamuambia tusiendelee kukagua sana turudi kwa msimamizi tukaenda akatuunganisha na mwenye nyumba nikajaribu kutikisa bei ikaja kwenye 2.5 nikalipa kabisa yaani sikutaka kupoteza muda na nikampa msimamizi pesa ya kufanya usafi tukasepa.
Jamaa yangu ndio akawa ananiambia pale sasa ndipo penyewe kwanza hapana watu wengi.
Nikasema pia ndio aina ya maisha nayoyapenda sitaki kuchangamana na watu kabisa..
Tukahamia maisha yakaanza lakini nikashangaa nyumba nzima niko peke yangu ule upande mwingine hauna mtu.
Kuja kuchunguza vizuri ndio nagundua kuwa kule niliko ndiko ilikuwa living room ya walioijenga hii nyumba.
Yaani kila kitu ni kama mwenye nyumba karudi tu maana sebule ni vile vile jiko nalo.
Kifupi ni kama nilifanya kufiti.
Siku moja niko kwenye boda narudi nyumbani niko mbali bado nashangaa simu ya wife napokea ananiuliza uko wapi?
Namjibu kuwa niko kwenye boda nakuja nyumbani,, anashangaa kisha anasema sawa wahi haraka..
Nikadhani labda baby mama yuko moto anahitaj spana za kwenda.
Kufika nimekaa nimepoa ananiambia kuna mtu kaja ndani ya uzio hadi kwenye varanda anaongea na kucheka kama mimi.
Nikawaza labda wenge lake..
Nikamchukua nikampiga miti na kuendelea na ratiba zangu.
Siku zikasonga sasa siku moja niko sebuleni mwenyewe nikasikia jikoni kama kuna paka anakwaruza ukuta kwa nguvu.
Nikanyanyuka taratibu na kwenda kufungua mlango ile ghafla kwa haraka. Maana taa ya jikoni ilikuwa inawaka.
Nikashuhudia msitari mwembamba wa kivuli ukiwa unatoka nje. Damu zikasisimka mwilini nikarudi sebuleni kukaa.
Imepita muda kidogo koki ya jikoni ikafunguliwa nikanyanyuka na kwenda kucheki.
Kweli maji yanatoka nikafunga koki nikatikisa kichwa huku machozi yakinilenga lenga hivi.
Kitendo hiki huwa sikifanyi mara nyingi maana hapa nakuwa naamsha ile nguvu yangu ya asili nyeusi iliyomo ndani yangu ili kukabiliana na mazingira ambayo nahisi si salama kwa mwanadamu yeyote yule.
Baada ya kufanya hivyo nilizima taa ya jikoni nikalock na mlango nikachukua pc yangu maana ndio kipindi nilikuwa naandika ile riwaya yangu ya Mabaduni wa Serikali..
Kuingia chumbani hapo ni mida ya saa sita kwenda saa saba namkuta wufe kakaa kitandani ananitumbulia macho tu.
Akaniuliza vipi mbona hauko sawa?
Nikamjibu niko sawa tu lala maana nataka kuwasha mishumaa nifanye ibada.
Nikisemaga hivi tu wife anaelewa kuwa kuna kazi nzito inataka kuanza.
Basi baada ya kufanya ibada inayochukua dakika tatu nikazima vyote nilivyoviwasha na kuviweka mahali pake nikavua na vazi la ibada nikapanda kitandani kulala.
Ngoma zikawa zimetoka vyumbani zikaenda kujishona jikoni.
Sasa mle ndio ikawa makao makuu yaani.
Ukiingia tu jikoni zinaanza mbwembwe.
Mwanamke akafuatilia historia ya pale
Aisee alichokuja kusikia kilinisisimua sana nikamwambia ajitahidi sana watoto wangu wasipate hizi taarifa maana hazitawaacha salama..
Mwanamke akawa ananisisitizia kuhusu kuhama nikawa namuuliza tu kuna mtu kadhurika labda?
Anajibu hapana lakini tuhame.. namwambia hapa nitaondoka kwenda kwangu tu tofauti na hapo sihami.
Wife akawa anashindwa kunielewa,, mpaka ile siku tuliyokuja kutengana. Aliondoka yeye na watoto wakaniacha peke yangu ndani humu mpaka leo hii naishi peke yangu na mbwa wangu tu huko nje.
Kwasasa nawatumia mbwa kujua kama nje pameshazungukwa na hawa viumbe hasa ikifika saa nane au saa tisa..
Mbwa wangu watalalamika sana kama vile wanahitaji msaada wangu.
Na ni majibwa makubwa ya kizungu lakini nikitoka nje muda huo wanakuwa wanaona kama ukombozi umekuja..
Nakaa nao kidogo nawapeti kiaina nazunguka nyumba nzima kukagua mazingira kisha narudi ndani nalala.
Sasa miezi ya hivi karibuni wakaniamshia popo ile mbaya..
Ikifika saa tisa au kumi za usiku unakuta mtu umelala usingizi mzito wanatumia ile sauti ya mke wangu kuniamsha usingizini.
Yaani ni kama mke wangu amesimama mlangoni ananiita anaita hata mara mbili au tatu ukiamka kabisa hivi anagonga mlango kwa nje kisha panakuwa kimya..
Kwakuwa naelewa narudi tena kulala.
Ilitokea mara kama tano hivi wakaacha kisha wakahamia chumba cha pili kutoka hiki nacholala huko ndiko wamekita kambi..
Kuna kabinti nilikapata tukaanza mahusiano hivi karibuni..
Kakadai nikisafiri nikaache hapa kaishi tu nitakakuta nikirudi.
Nikakaambia suwezi kukuacha hapa ni bora nivifungie vitu vyangu vichache nilivyobaki navyo nisafiri mpaka siku nitakayorudi..
Kakakaza fuvu ikabidi nikaambie ukweli wote kuhusu hii nyumba na hapo ilikuwa ni usiku..
Walivyosikia nawazungumzia tu wakamwaga maji mengi sebuleni asubuhi naamka nashangaa maji mengi kishenzi sebuleni.
Sikutaka kujiuliza mara mbili maana nyumba yenyewe naishi peke yangu nikachukua mopa nikaanza kazi..
Kingine ni kuwa kila chumba lazima nikumbuke kufunga vizuri ila siloki milango maana ukiacha mlango loose inakuwa ni mwendo wa kusukuma milango mpaka wanafika wa chumbani inakuwa ni kama unachunguliwa kisha wanafunga fasta..
Wataendelea mpaka uende ukafunge mbona..
Mi nishazoea kabisa
Sasa utajiuliza nimwezaje kuzoea hii hali ya hivi naishi na viumbe ndani ambao siijui hata idadi yao.
Ni kwamba maisha haya sijayaanzia hapa huko kwetu kijijini kuna nyumba tunayo ina viumbe hawa wakorofi vibaya mno.
Kwa hiyo heka heka zote hizi ni kama marudio.