Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AnachanganyaMmetoka harusin saa 6 usk.... Mmeingia hotel ukakutana na mauza uza mkabishana takriban masaa 3.... Inakua saa 9 usk alaf baadae simu inapigwa mida ya saa 8 usk Sam anaenda kuongelea pemben Kisha anakuomba msamaha........ Lkn story n tamu ngoja nisubili uje
Story yako yenye title ya kuvutia iko wapi?Ili uwe mwandishi mzuri jifunze kuchagua tittle itakayowavutia wasomaji
Hiyo tittle yako ingekuwa umechapa kitabu usingeuza unaona hata wasomaji humu hawajavutiwa
Mtu km mm ninayesoma vitabu nilipoona tu tittle tayari nikawa nimeimalizia simulizi yako kwenye fikra
Kwasababu mambo ambayo watu hawasahau zaidi ni yale ya kuumiza sana na kufurahisha zaidi
Kwenye Honeymoon mambo ambayo yanaweza yakakufanya usisahau ni
Mume wako kuacha kutokana na kukutana na kitu tofauti na matajirio yake
Mume wako kufa and so
So young lady,learn to create an interesting tittle
[emoji38][emoji38][emoji38]Story yako yenye title ya kuvutia iko wapi?
Wacha kujipa muhimu Kwa vitu havikuhusu
NAJUTA KWENDA HONEY MOON- NILICHOFANYIWA SITAKUJA KUSAHAU β 07
β Paaaah!β Moyo wangu ulipiga.
β Inmaaana anajua nilikuwa chumbani kwa kaka yake?β Nilijiuliza.
Nilimkodolea macho bila kuongea.
β Mbona unanitazama hivyo?β Aliniuliza. Alinishika mkono na kunitikisa.
β Kwani haukuwa chumba namba saba?β
β Aβ¦.aaaaβ¦..β
β Haina haja ya kuwa na kigugumizi. Ulikuwa chumba namba saba na Mke wa Kaka Gaby.β
βMke wa Gaby?β Niliuliza kwa mshangao.
β Usimwite mke wa Gaby. Yule ni Dada yako. Mke wa kaka yangu ni Dada yako. Wewe na yeye inabidi muitane dada .β .
β A..aaaβ¦aaaβ¦.β
βMbona unashangaa sana. Au haukuwa chumba namba saba. Mimi najua ulikuwa na mke wa kaka Gaby. Alikuwa anakufundisha baadhi ya mambo. Kama hakuna ulilojifunza niambie nikamuulize.β
β Nimejifunza.β Niliropoka kwa haraka.
β Kanifundisha mengi.β Nilimwambia. Nilidanganya kwa makusudi. Maana Kama ningekataa angeenda kumuuliza Mke wa Gaby.Na kama angefanya hivyo, ukweli ungekuwa wazi. Ingefahamika sikuwa na mke wa Gaby mle ndani. Na kwakuwa Sam anajua nilikuwa mle ndani basi moja kwa moja angejua nilikuwa na kaka yake.
βKumbe umejifunza. Hiyo ndio faida ya uwepo wao.β Aliniambia.
Alinishika mkono. Kwa pamoja tukaelekea chumbani kwetu.
β Nimesema uongo. Vipi kama Sam anajua nilikuwa na kaka yake? Huu sio mtego kweli?.β Nilijiuliza.
β Acha nimuambie ukweli.β Nilijiambia. Nilimshika mkono.
β Vipi?β Aliniuliza.
β Kuna swala nataka nikuambie.β
β Utaniambia chumbani.β Aliniambia. Alinishika mkono tukaelekea chumbani.
Tukiwa tunakaribia, tulikutana na Bamdogo akiwa na Mkewe.
β Naomba nipeleke kaunta mara moja.β Mama mdogo alimwambia Sam . Bila kuniambia lolote Sam aliondoka na Mama Mdogo kuelekea kaunta. Waliniacha na Baba mdogo.
β Ulinishutumu kwa vitu visivyokuwepo. Sikufika chumbani kwenu ,wala sikumpiga vibao Sam.β Aliniambia Baba Mdogo.
β Mdanganye Sam. Mimi huwezi kunidanganya. Ulifika na nilikukwaruza na kucha zangu. Alama za kucha hizi hapa. Huu ni ushahidi tosha.β
βKama unaamini hivyo sawa. Sina la kufanya, ila ukweli sikuja chumbani kwenu. Kwanza nije kufanya nini? Na kwanini nimpige kibao Sam?β Aliniuliza.
β Maswali unayoniuliza na mimi najiuliza . Nawaza kwanini ulifanya vile? Sababu yake ni nini?β
β Ulikuwa unaota mwanangu. Sikuja chumbani kwenu wala sikumpiga Sam .β Aliniambia.
Kabla sijamjibu aliondoka. Aliniacha nimesimama.
β Hawa watakuwa wananichezea akili. Bila shaka kuna mtihani wananipa. Ukute haya yote wanayafanya kwa makusudiβ Niliwaza.
Niliusogelea mlango wa chumba chetu na kuufungua. Kabla sijaingia, alitokea mke wa Gaby akiwa anakimbia.Alinifata hadi mlangoni. Alinishika na kuanza kunipiga.
β Eeeehβ¦β Niliduwaaa.
β Paaaβ¦β¦.paaaaβ¦β Alinipiga . Alinivamia na kuniangusha chini. Alikuja kunikalia kwa juu na kuendelea kunipiga.
β Kosa langu nini?β
βUnajifanya haujui eeeh..haujiiiiiβ¦β Aliniuliza. Aliendelea kunipiga. Uvumilivu ulinishida. Niliamua kujibu mapigo. Tulipigana. Kama wake wenza tuliangushana na kugalazana.
β Shenziiii..weweβ¦β¦.β
β Shenzi mwenyewe..β Nilimjibu. Nilimshika na kumlaza chini. Nilizishika nywele zake na kuzivutaaaa.
β aaaa..aaaaaaaaaβ¦β¦.β Alipiga kelele.
Kelele zake ziliwashtua wahudumu.Walikuja kututenganisha.
β mmmhβ¦mmmmmhβ¦.β Nilihema juu juu .
Kwa mbali kwenye ile varanda alitokea Mama Mkwe akiwa na Sam.
β Mnanitia aibu .Mnagombania nini?β Aliuliza.
β Nitaongea yote Mama. Mke wa Sam sio mtu . Nitaongea kila kitu.β Aliongea Mke wa Gaby.
HAPPY NEW YEAR