Requal
JF-Expert Member
- Jun 5, 2020
- 1,025
- 1,917
JamiiForums ni zaidi ya habari, nami nimeona niweke hapa kisa ambacho kinaweza kuwa funzo/somo kwa vijana wengi watafutaji hasa wanaopenda shortcut. Mtanisamehe kwa uandishi wangu mbovu na mpangilio wa visa.
Mwaka huu mwanzoni nilikuwa mkoani Arusha kwa jamaa yangu mmoja tuliyetoka nae Kijiji kimoja huko mkoani kwa baba wa taifa.
Siku moja katika matembezi mjini na huyu jamaa yangu, Ghafla nikasikia naitwa jina langu kwa kilugha changu na mchoma mahindi aliyekuwa pembeni yetu "Requal, Omwanono Ge zisiku ndola ukulili igo" nikashangaa kidogo maana alikuwa mmama wa makamo na sikuweza kumkumbuka kabisa. Ikabidi nimjibu "Mazomu", baadae akahamia kwa jamaa akawa anamuuliza umempata wapi huyu kiumbe maana sijamuona zaidi ya miaka 10, katika maongezi ndio nikaja kugundua ni Sarah, sio jina sahihi (Jirani yangu kabisa kule kijijini) ni kweli hatujaonana miaka 10 na zaidi.
Ule urembo wake umeisha kabisa na sasa anaonekana kama bibi yangu japo amenizidi miaka 4 tu ya kuzaliwa.Kiukweli alikuwa amechoka sana na alionekana mtu aliyekata tamaa na maisha kabisa na hapa ndipo nilipoona Kuna haja ya kuweka hapa huu mkasa ili wengine wajifunze.
STORY YA FAMILIA YA AKINA SARAH
Sarah ametoka familia ya watoto watano pale kijijini kwetu, wa kike wawili na wakiume watatu, mkubwa tumpe jina Joseph, anaefuata wa kiume "nyanza", na wa mwisho wa kiume aitwe "Gedo". Hiki kisa kinamhusu zaidi Sarah, Gedo, mama yao pamoja na mume aliyekuja kumuoa Sarah. Kabla hatujafika huko tutamzungumzia kidogo Joseph ili kupunguza maswali huko mbeleni.
Baba yao Sarah alikuwa na wake wawili na mama yao Sarah hakuwa kipaumbele Cha baba yao, mke mdogo ndiye aliyependwa zaidi na familia ya mke mkubwa ni kama ilitelekezwa vile.
Baba yao Sarah alikuwa na ndugu mmoja tu wa tumbo moja wa kiume na wa kike mmoja pia walipenda sana. Hawa wazee ilikuwa ni mfano kijijini pale kwa jinsi walivyokuwa wanapendana. Huyu wa kiume ambaye ni baba yake mkubwa Sarah alikuwa na wake wawili na mke mkubwa alikuwa anasadikika ni mchawi mkubwa sana pale kijijini; anasadikika kufuga misukule Kule kijijini watu wanamuogopa mno tukikutana nae porini mwenyewe huwa tunajificha ili apite, huwa havai viatu akitembea na haachi unyao anapokanyaga. Naye atahusika kidogo kwenye huu mkasa.
MKASA WA JOSEPH
Joseph ni mtu mzima kidogo amezaliwa miaka ya 70's, huyu jamaa ana asili ya roho nzuri sana, mcheshi na mkarimu mno alikuwa family friend wa ukoo wetu, aalioa mwanamke mrembo sana kutoka Kijiji cha jirani yule mke hata ukikutana nae leo ni vigumu kujua Kama ile ni product ya kijijini.
Nikiwa bado niko elimu ya msingi kipindi hicho, Joseph akapotea pale kijijini kwa vile alikuwa family friend ilikuwa rahisi kujua mahali alikoenda, tukaambiwa ameenda mgodini Arusha Merelani kutafuta maisha kwenye machimbo ya Tanzanite, mkewe alibaki na baada ya mda mkewe alimfuata na huko ndio yakawa makazi yao.
Maisha ya familia hii yalikuwa ya kawaida sana, mama yao alikuwa anaishi nyumba ya suit yaani imejengwa kwa mabati chakavu kuanzia chini mpaka juu..na wao walikuwa na nyumba za nyasi pembeni na zaidi walikuwa wanategemea kilimo Cha jembe la mkono ili kuendesha maisha.
Baada ya Kama miaka miwili Joseph akarudi pale kijijini na kabla yeye kurudi kusalimia taarifa zilikuwa zimeshazagaa kwamba Joseph Sasa amewin maisha, watu pale tukawa na hamu ya kumuona kama mnavojua maisha ya kijijini.
Jamaa alikuja kwa gari lake akiwa anaendesha mwenyewe alikuwa ni gumzo pale kijijini na isitoshe alikuwa anagawa pesa kwa kila mtu anaekutana nae, hili halikuwapa watu maswali kwa sababu ya roho yake nzuri toka mwanzo, aliwawezesha sana ndugu na akaanza ujenzi rasmi wa nyumba mpya na ya kisasa kabisa ya mama yake kuishi.
Baada ya kuanza ujenzi baba yao akahamishia kambi kwa mke mkubwa na akapewa kazi ya kusimamia ule ujenzi wa ile nyumba na Joseph akarudi Arusha kuendelea na kazi zake.
Joseph Ghafla akawa na maisha mazuri mno, na mke wake ule urembo ukang'ara zaidi, alikuwa ni zaidi ya mrembo yule mwanamke, walifungua miradi mingi na kujenga nyumba nyingi huko Arusha na wakawa wanakuja kijijini kusalimia mara kwa mara, miaka ikaenda huku utajiri wao unazidi kukua.
Sasa kuna mwaka kukawa na harusi ya ndugu yao inafanyika pale kijijini, bado niko S/M mpaka kipindi hicho, maandalizi yakaandaliwa na Joseph alitegemewa kama mgeni mahsusi na marafiki zake atakaokuja nao. Basi bhana, siku ya mkesha ilipofika kwa yale madisko ya kijijini kwa mnaoyafahamu tulicheza balaaa kunakucha unajikuta una vumbi kuanzia kwenye ukucha mpaka kwenye kope za uso.
Joseph na rafiki zake waliingia usiku huo wa mkesha; tulikula nyama za kutosha ile harusi, kesho yake ikawa ni siku ya kuzawadia, Joseph huohuo usiku akaanza kugawa pesa kama kawaida yake.
Baada ya Joseph kuzawadia akaaga kuondoka pamoja na marafiki zake na walifanya kufuru ya kutisha kwenye kutoa zawadi kabla hajaondoka akaenda kumuaga mke wa baba yake mkubwa yule mchawi na akampa 50k.
Bwana eeeh Kumbe yule mama alikuwa anaona nongwa huyu Joseph kufanikiwa, alichokifanya akachukua zile 50k akazilowanisha then akazisaga zikawa ungaunga kabla ya kuzichanganya na madawa anayojua yeye ili kuuyeyusha utajiri wa Joseph..huku mbele utafahamu ni namna gani hii siri ya huyu mchawi ilivuja.
Safari ya huyu Joseph na rafiki zake kurudi Arusha ikawa ya misukosuko sana walipotea sana huko njiani iliwachukua siku saba kufika Merelani na alipofika mambo yake yakaanza kuwa mabaya mno.
Baada ya ugumu wa miezi kadhaa akaanza kuuza kitu kimoja baada ya kingine, nyumba zote zikauzwa, gari na miradi yote ikafirisika akawa anaomba hata 500 na wanawake aliowajengea wakawa hawataki tena hata kumuona, mke wake pia akamkimbia..Joseph akarudi kwenye umaskini wa kutupwa.
Kwa mujibu wa wazee pale kijijini, Wanasema huyu Joseph Utajiri wake ulikuwa wa masharti nafuu kulingana na nyota yake na masharti yake ilikuwa ni kugawa pesa na mengine madogomadogo na Kama Ingekuwa sio huyu mama yake mkubwa kumuonea wivu na kumroga basi jamaa angekuwa mbali.
HukuJuu tumemzungumzia Joseph kidogo ili kupunguza maswali huko mbeleni lakini mlengwa wa huu mkasa hasa ni Sarah, Gado, mama yake Sarah na mume atakayekuja kumuoa Sarah.
Tuendelee sasa
Gado naye hakukaa mda pale kijijini kwa mda mrefu akaenda Merelani kutafuta maisha pia
Sasa pale kijijini kwetu Kuna mmama mmoja maarufu anaitwa Wasosi ni jina lake halisi, huyu mama ni mcheshi sana kiasi kwamba vijana wengi waliotaka kuoa hasahasa waliokuwa nje ya pale kiutafutaji walimuomba awatafutie mke mwenye tabia nzuri ili waoe..yaani ilikuwa yeye anatafuta Mali inapelekwa halafu mwanamke anaenda kwa mume wake huko mikoani ili kupunguza gharama na wengi wao wanakuwa hata hawajuani.
Sasa huyu Wasosi alikuwa na kaka zake mkubwa nimemsahau jina lakini mwingine namjua kwa jina moja Kiringo ambaye ni mkuu wa Auxiliary police hapo UDSM. Huyu ni mtu wa dini, mcha Mungu hasaaa na mpenda haki na kwa mara ya kwanza nimeonana nae mwaka huu msibani hapa Dar.
Kaka yake mkubwa huyu Wasosi akatangaza nia ya kuoa, Dada mtu huyu Wasosi akamuambia kaka huku kijijini Kuna msichana mrembo sana na mpole mno anakufaa kuoa, kaka mtu akataka atumiwe picha ili ajiridhishe akatumiwa, kweli Sarah alikuwa mzuri kaka mtu akajikuta amempenda akaruhusu wasosi apeleke ujumbe kwao Sarah na alipopeleka akakubaliwa taratibu za kaka kuja pale kijijini kuonana za sarah na familia yake zikafanyika na hatimae harusi ikafika wakaoana wakawa mke na mume.
Wakahamia Dar kimakazi, baada ya mda Gedo akarudi pale kijijini kusalimia vile na Mimi ndio nikawa namalizia Elimu yangu ya msingi. Kumbe jamaa alikuwa ameanza harakati za kuutafuta Utajiri wa giza.
Niko nyuma ya keyboard wakuu na pombe ishapanda kichwani
Endelea...👇👇👇👇👇