Haka kabinti ni kakubwa kwa
Gily kwa miaka 5 yaani 37 , ananipenda sana ni mshauri mzuri ila ikiwa ni kuchepuka basi ni ubinadamu .
Kichekesho ni kuwa sikumuoa kwa kupanga kuoa ila nimlitongoza ili nipite kama wengine wote ila bahati mbaya nilivaliwa kibwebwe na ndugu zake na wazazi usiku niliolala naye wakinitaka nimuoe [emoji848] yaani itoshe kusema ilikuwa ni ndoa ya mkeka ya lazima kabla ya kuifanya official .
Yaani umumtingoza mtu umemchukua siku anakupa raha , asubuhi unafungua mlango unakuta watu nje wanasema wanashida na wewe [emoji3][emoji3] Vijijini watu wabaya ila nahisi alikuwa malaika maana kuanzia hapo ndipo akili ya kusema wacha nioe ilikuja ni baada ya fumanizi na kuepusha kuchafua sifa zangu hapo kijijini maana nilikuwa mgeni .
Ukichanganya binti aliniongopea hana kazi ila baada ya fumanizi la nduguze nilitaka kuonesha umwamba na jeuri za born town mimi ila aliponikata maini ni pale alipohitaji twende polisi huku akidai makubaliano ni ndoa ila nimebatilisha [emoji24] , huku nikielezwa wajihi wake kuwa ni askari ilinifanya kuwa mnyonge zaidi .
Huyu sio slay queen wa hivi niliruka nao kitambo hiko kwenye sikinde na mnanda ila huyu ni mdada wa haja , heshima imekaa , amefundwa kijadi akafundwa japo namdiscourage kwasababu ya historia yangu na matendo yangu ambayo siwezi kuyabadili siku moja ila taratibu as long as tunatoka family background tofauti mno .
Itoshe kusema nina mke , anayenipenda na kunijali kuhusu heshima ndiyo mahali pake , nampenda sana ila nahisi ni God's plan kunikutanisha naye ili labda nipate wa kunilea uzeeni .