Mkataba kati ya DP world na TPA hauna tatizo lolote ila kuna baadhi ya ibara zinatakiwa zifanyiwe mareboresho mfano ibara ya 23

,
Pascal ebu msome mkuu Bams (post # 19) hapo juu uone nondo zake, then ukiweza jibu basi. Great thinkers kama nyie mnapopambanisha hoja sisi makapuku tunanufaika.
Mkuu UmkhontoweSizwe , asante, ila jf ni home of great minds, we are all equal, hakuna ma GT na makapuku, wote ni sawa, wote humu ni great thinkers kwa viwango vyetu na pia ni makapuku kwa viwango vyetu. Nitamtembelea Mkuu Bams
P
 
 
Mkataba upo sawa tatizo ni English naona.
Mkataba uko very clear kuwa IGA itakufa pale HGA itakufa....
IGA itabaki only kama HGA itakufa kinyume na makubaliano....
Mind you hiyo HGA hatujasaini bado ni miaka mingapi
 
Mkataba hauna tatizo ila kuna vipengele / ibara zinatakiwa kufanyiwa marekebisho.

Wewe kweli punguani ?
Hivyo vipengele vyenye kulalamikiwa na wadau mbalimbali na kutakiwa kufanyiwa marekebisho ndilo hasa tatizo lenyewe ndani ya mkataba. Sifa mbaya na nzuri kuhusu kitu haziwezi kuwekwa pamoja ili kujenga hoja ya jumla ili kuhitimisha kuhusu uzuri wake.

Huwezi kusema mtu fulani ni muadilifu sana bali tu aache tabia yake mbaya iliyokubuhu ya wizi. Hiyo tabia ya wizi ndiyo sifa yenye kuondoa kabisa uadilifu wake.
 
Meneja wa Makampuni, huu mkataba una matatizo makubwa. Hauna mazuri yoyote.
Sii kweli, matatizo kweli yapo na mazuri pia yapo!, moja ya mazuri hayo ni DPW watainject kwenye uchumi wetu FDI ya maana kuboresha utendaji wa bandari yetu upande wa makasha, kwa sasa kupakua makasha na kuyapanga kunafanywa manual, DPW wanaleta mitambo ya robotics hivyo kuwa automated kwa computer kazi ni ku kongoli tuu!.
Mkataba huu unatakiwa kuutazama kwa mlengo wa kisheria, kibiashara, kiuchumi na kiusalama.
Nakubaliana na wewe
Bandari ya Dar haijazuka tu, tuliijenga kwa pesa nyingi, kuanzia kuchimba ili kupata kina kirefu, kuna majengo, kuna mashine mbalimbali. Ni karibuni tu, wakati wa hayati Magufuli zimewekezwa karibia trilioni 2.
Ni kweli, ule uwekezaji wa trilioni, 2 ni eneo la rics, DPW anapewa beth nyingine sio hiyo ya tics!.
Sii kwenye, kwanza mkataba ni HGA, bado!, kwenye kila uwekezaji, serikali inakusanya tuu kodi na mwekezaji anachukua faida yote kwa kipindi fulani tuu cha return of investment, akiisharudisha pesa yake na faida, tunagawana mapato. Mbona ndio hivyo kwa mkataba wa bomba la gesi, ndio hivyo kwa PSA 21 za Gesi Asili!. Angalia tarehe ya bandiko hili Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!
Mimi nasubiria HGA
Jambo jingine ni usalama wa nchi. Mkataba unasema DP wanapewa haki ya kuendesha bandari ya Dar lakini yeye ndiye mwenye haki pekee pia ya kuendesha bandari nyingine zote, na haturuhusiwi kumkubalia mwekezaji mwingine.
Sii kweli, subiria HGA!.
Just be positive !.

P
 
Sasa hayo uliyoyataja ndo Shida yenyewe
 
Huo mkataba si ushaingiwa au?
 
Tatizo lilianza pale Mungu Jiwe alipokuwa anamtuma msiadizi wake Kwa wajomba zake!
 
Nimependa ulivomjibu kwa utulivu
 
Kuwa positive haimanishi kutokuwa na upeo wa kuona mambo yanayoweza kutokea.

Ni sawa na mtu anachukua ardhi, anaanza kulima kwa kutegemea mvua, amefanya projections za mapato, unamwuliza, itakuwaje kukiwa na ukame? Halafu akujibu kuwa uwe positive. Yaani usifikirie kabisa kunaweza kuwa na ukame. Huko itakuwa ni kujitia upofu.

DP wana kesi ngapi zinazohusiana na uwekezaji wao nchi mbalimbali? Ujue kunapokuwa na kesi maana yake kuna mgogoro ulioshindwa kutatuliwa kwa njia ya maelewano.

Djibout tu hapo kwa Waafrika wenzetu, nchi inatakiwa kuwalipa DP dola milioni 700 kama fidia wakati uwekezaji wa DP haukufikia hata dola milioni 300.

Hizi kesi kati ya DP na mataifa mengine, ni wakeup call kwetu. Sisi tusijione ni wazuri sana kwa DP. DP inatafuta faida kubwa kupitia uwekezaji na kupitia migogoro.

Mtu mwerevu hujifunza kutokana na makosa ya wenzake. Djibouti walikuwa na mkataba kama huu wa kwetu, wameuvunja, wameishia kutakiwa kuwalipa DP dola milioni 700. Hiyo ni hukumu iliyotolewa na mahakama ya Uingereza.
 
Na ukipinga Kila kitu unaonekana una asili ya kigoma,
Yaan huoni jema lolote?
Huoni chochote kizuri kinaweza kupatkana?
Ww sio Bure utakua C.E.O wa TICS
 
Na ukipinga Kila kitu unaonekana una asili ya kigoma,
Yaan huoni jema lolote?
Huoni chochote kizuri kinaweza kupatkana?
Ww sio Bure utakua C.E.O wa TICS
Huko ndiko tunaita ni kukosa maarifa. Wewe inaonekana ni mtu mbinafsi sana. Yaani hufanyi lolote jema mpaka uwe mnufaika wa moja kwa moja, ndiyo maana unafikiria kila mtu yupo kama wewe. Kwako huangalii ukweli wa kitu, bali maslahi binafsi.

Ninyi ndio mnaoifanya nchi hii iendelee kuwa duni. Hampo tayari kutetea chochote kilicho sahihi kama hakiwanufaishi moja kwa moja.

Bahati nzuri, sisi wengine, tumeuvuka huo uduni wa utu.
 
Haka ka jamaa kajinga sana hapo ulipo huna hata buku mbili mfukoni na unashabikia nchi kuuzwa.
Kwani Pesa ndio nini boss. Pesa tutakufa tutaziacha bora uzima. Bora uzima. Narudia tena bora uzima. Usiogope kutoa mawazo yako hata kama huna buku mbili mfukoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…