Mkataba kati ya DP world na TPA hauna tatizo lolote ila kuna baadhi ya ibara zinatakiwa zifanyiwe mareboresho mfano ibara ya 23

Mkataba kati ya DP world na TPA hauna tatizo lolote ila kuna baadhi ya ibara zinatakiwa zifanyiwe mareboresho mfano ibara ya 23

Sijauona mkataba baina ya DP World na TPA, kama unao uweke hapa tuuone. Niliouona ni ule wa makubaliano ya maendeleo baina ya Dubai na Tanzania "IGA". Bofya chini hapo uuone:

Lakini Faiza hiyo ibara ya 23 si imo kwenye hayo makubaliano?
 
Kwani nyinyi wenzetu hizi akili mlizopewa na Mungu huwa matumizi yake ni yapi? Watu si wamesema kabisa Kuna vitu ndani ya huo Mkataba ni janga na ni uhuni mkubwa, Sasa nyinyi wanufaia na huo Mkataba mkaamua kusema No problem, Kana kweli mna nia njema ya uwekezaji kwanini kudi kubwa la Wabunge wakiongozwa na Spika tuliyemuamini kuongoza mhimili muhimu vile wakashindwa kurekebisha siku ile au kuonyesha hata kukataa?
Hayo unayoonani mapungufu ndio mtego wenyewe huo, mkataba unaweza kuwa mbovu na katili kwa neno moja tu hata kama umetaja mamilioni ya faida kama mnavyoshupaza shingo kuelezea Ajira, muda mkisahau hayo mliyoandika ambayo ndio muhimu zaidi.
 
Lengo langu ni kuvuta attention ya kuwaonyesha hiyo ibara ya 23 mpate kuisoma

Na nyie ndio mnafanya watu wasielewe, hili swala lilitakiwa kujibiwa na wataalamu, wachumi na wanasheria na sio wanasiasa au kila mtu ambae anahisi anaelewa kitu flan

Why hamuongei swala la Ajira? Why hamuongei kuhusu kesi zao za inchi nyingine?

Hayo ndio mambo watu Wana hofu nayo
 
Ni kweli mkuu, swala la ajira mimi nilisha lizungumzia kwenye uzi mwingine. Kuhusu kesi zao katika nchi zingine kuna watu walishazungumzia pia hapahapa jamii forum. Kila mmoja ameshika upande wake kadri anavyoweza.
 
Sasa haikutakiwa kila mmoja ashike upande wake

Ilitakiwa wataalamu na wahusika wakuu watoke hadharani, wafanye vipindi, watu wapige simu waulize maswali

Sasa kinachofanyika now ni kila mtu kujibu hoja Tu na sio kutoa maelezo ya kutosha

Ww unaongea jf je kwa mtu ambae hayupo if? Anapata wapi haya maelezo?

Swala la wataalamu kutegemea wanasiasa linatufelisha sana
 
Machawa mnatuchanganya!

Acheni wazalendo wasionunulika waongee....

View attachment 2667779
Nimemsikiliza Mh. Tundu Lissu kuhusu mapungufu ya mkataba lakini alichoongelea mbona ni mambo ya kawaida tu ambayo hata mtu wa kawaida tu mwenye uelewa wa sheria za mikataba anapaswa kuyajua. Anachoongelea ni "elements of contract" ambazo hata mimi ambaye si mwanasheria nazijua. Kutokujumuishwa kwa "force majeure clauses" kwenye huo "mkataba" sidhani kama kunastahili shutuma nzito alizozitoa Mh. Tundu Lissu. Kwani hayo aliyosema hayawezi kurekebishwa? Mimi nadhani ni vyema kwa Mh. Tundu Lissu kuwa "more objective" na kuongelea mambo ya msingi. Je uwekezaji ni kitu kizuri au kibaya kwa Taifa? Maadamu wananchi wamepewa fursa ya kutoa maoni basi hayo mapungufu yatasemwa na naamini yatazingatiwa. Lugha kali ambayo hailingani na "gravity of the errors/mistakes committed" sidhani kama ni za busara sana. Sisi sote ni binadamu tu "and nobody is perfect including my learned brother Tundu Lissu". Siyo kila kitu kinahitaji lugha kali. Mimi ni mshabiki sana wa wanasheria na huwa napenda sana kuwasikiliza. Kitu ambacho huwa kinanivutia ni namna ya kujenga hoja na siyo "political rhetorics". "Let us all be fair to our country".
 
Mimi sijui cho chote kuhusu sheria. Labda nikupe namba ya TL mkutane wasafi TV mjibishane hoja kwa hoja kuhusu mkataba huu. TL yeye huwa hapindishi maneno wala kupaka sukari kwenye shubiri. Hate or love him - the man just can't entertain hypocrisy...and he will call spade a spade no matter what the consequences. This is a heroic trait in my book!

Au uko kambi ile nyingine ya miamba ya sheria ya akina Maulid Kitenge, Steve Nyerere, Mrisho Mpoto, Mwijaku, Rostam Aziz na wengineo?

Pambaneni kwa hoja mpaka hata sisi laymen wa sheria tuelewe 👏🏼👏🏼👏🏼
 
Asante kwa majibu yako ingawa sikupenda sana "kunidhania" kuwa niko upande ule mwingine. Mimi siyo mwanasheria kama nilivyoandika ingawa pengine nina uelewa kidogo (nilikaa darasani). Hoja yangu ni kuwa watu tunaowaamini (wanasheria) kama akina Mh. Tundu Lissu wawe "more objective and analytical" ili watusaidie na sisi wengine kuuelewa vizuri huo mkataba. Najua yeye kama mwanasiasa anatumia kila mapungufu "kujijenga kisiasa". Ni vyema akaitendea haki taaluma yake na sisi wengine tupate faida. NB: Nashukuru kwa kutotumia lugha ya matusi kama wengine hapa JF.
 
Kimsingi tunaongea kitu kile kile. Wanasheria wangeweka vipengele vyote vinavyolalamikiwa kimoja baada ya kingine na kutuonyesha kwa nini ni kibaya na lazima ama kirekebishwe ama kiondolewe. Na vipi viongezwe kwa maslahi yetu.

Upande wa akina Maulidi Kitenge nao ungetuonyesha kwa nini vipengele vinavyolalamikiwa ni vizuri na viachwe kama vilivyo badala tu ya kutuwekea picha wakitanua Dubai na kuzidi kukoleza moto wa chuki!

Ubaya sasa kila upande ukitoa hoja (hasa huu wa akina Kitenge na Mwijaku) ni za jumla jumla tu tena wakati mwingine ni ad hominem attacks tu zisizo na faida (mf. Rostam alivyomshambulia Dr. Slaa).

Mpaka sasa tunaingia wiki sijui ya ngapi mjadala huu ukirindima lakini binafsi bado sijajua kama mkataba ni wa milele au una kikomo. Sisi tunapata nini na mwekezaji anapata nini? Ni kweli mkataba una-stipulate kwamba mwekezaji ataendesha bandari zote mpaka za maziwani na mito akiamua? Mwekezaji anamilikishwa ardhi ya bandari? Ni kweli bandari za visiwani ziko excluded? N.k....n.k...

Lakini sasa imegeuka na kuwa ushabiki tu kama wa Yanga na Simba; na hii haisaidii cho chote. Mpaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msemaji mkuu wakisimama hakuna hoja ya maana wanayotoa bali kulalamika tu na kuzodoa upande mwingine. Hovyo tu!

➡️➡️➡️ Nina miaka karibia 9 hapa JF mkuu na huwa sina tabia ya kutukanana humu maana hiyo naamini ni matokeo ya malezi mabovu, ugonjwa wa akili (mf. Narcissistic Personality Disorder na clinical depression), wivu na kujichukia, ukosefu wa hoja, kutokujiamini, misplaced anger, childhood trauma na mengineyo. Sana sana mtu akinitukana namtia kwenye ignore list tu na kuachana naye.

Tuko pamoja mkuu 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Nimeusoma mkataba wa bandari kuna mapungufu machache tu yanayoweza kurekebishika. Watanzania tuondoe wasiwasi tushauri kwa lugha nzuri. Mfano kama ikiwezekana ibara ya 23 ingefanyiwa maboresho ili isituminye sana. Ibara inasema hivi:

ARTICLE 23
DURATION AND TERMINATION
1. Subject to paragraph 2 of this Article 23, this Agreement shall remain in force until occurrence of one of the following: (i) permanent cessation of all Project Activities; or (ii) the expiration of all of the HGAs and all of the Project Agreements (subject to any additions or extensions thereto) and the definite resolution of disputes, if any, thereunder.

2. In the event that a HGA is terminated prior to expiration of its term, this Agreement shall remain in force for the time, and to the extent, required by any State Party or by the Project Company to assert any rights arising from, protect any interests endangered by or bring any proceeding resulting from termination of the HGA. Termination or expiry of a HGA shall not affect any accrued rights, liabilities or remedies of any party under such HGA or the related Project Agreements or this Agreement.

3. The termination of this Agreement shall be subject to the prior consent of the State Parties, such consent is not to be unreasonably withheld.

4. The State Parties shall not be entitled to denounce, withdraw from, suspend or terminate this Agreement in any circumstances, including in the event of material breach, fundamental change of circumstances, severance of diplomatic or consular relations, or any other causes recognised under international law. Notwithstanding the foregoing, any dispute between State Parties in respect of such circumstances shall be dealt with in accordance with the requirements of Article 20 of this Agreement.

Nilichokielewa hapo ni hiki:

The Article 23 of the Agreement lies in the lack of clarity and potential limitations regarding the termination of the agreement.

1. Lack of defined termination criteria; The agreement states that it shall remain in force until the occurrence of specific events, such as the permanent cessation of all project activities or the expiration of all Host Government Agreements (HGAs) and Project Agreements. However, the agreement does not provide clear criteria or guidelines for determining when these events have taken place, which could lead to ambiguity and potential disputes.

2. Reliance on termination of HGAs; According to paragraph 2 of Article 23, if a HGA is terminated before its term expires, the agreement remains in force for a certain period to allow the assertion of rights, protection of interests, or the initiation of legal proceedings resulting from the termination. This provision creates dependency on the termination of HGAs and does not account for other circumstances that may warrant the termination of the agreement.

3. Limited termination consent; The agreement stipulates that the termination of the agreement requires the prior consent of the State Parties, which should not be unreasonably withheld. While this provision seems reasonable, the lack of clarity on what constitutes "unreasonable" withholding of consent could potentially lead to disagreements and delays in the termination process.

4. Restriction on termination rights; Article 23(4) explicitly states that the State Parties are not entitled to denounce, withdraw from, suspend, or terminate the agreement under any circumstances, including material breach, fundamental change of circumstances, or severance of diplomatic or consular relations. This provision severely limits the termination rights of the State Parties and may restrict their ability to address significant issues that arise during the course of the agreement.

If possible, Article 23 should be revised and improved because it may potentially lead to disputes and challenges in the event of termination or expiration of the agreement.
Kama walikuwa na nia njema kwa nini wasiandike mkataba wa haki tangu mwazo utakaowanufaisha wao na Tanzania
 
Kimsingi tunaongea kitu kile kile. Wanasheria wangeweka vipengele vyote vinavyolalamikiwa kimoja baada ya kingine na kutuonyesha kwa nini ni kibaya na lazima ama kirekebishwe ama kiondolewe. Na vipi viongezwe kwa maslahi yetu.

Upande wa akina Maulidi Kitenge nao ungetuonyesha kwa nini vipengele vinavyolalamikiwa ni vizuri na viachwe kama vilivyo badala tu ya kutuwekea picha wakitanua Dubai na kuzidi kukoleza moto wa chuki!

Ubaya sasa kila upande ukitoa hoja (hasa huu wa akina Kitenge na Mwijaku) ni za jumla jumla tu tena wakati mwingine ni ad hominem attacks tu zisizo na faida (mf. Rostam alivyomshambulia Dr. Slaa).

Mpaka sasa tunaingia wiki sijui ya ngapi mjadala huu ukirindima lakini binafsi bado sijajua kama ni wa milele au una kikomo. Sisi tunapata nini na mwekezaji anapata nini? Ni kweli mkataba una-stipulate kwamba mwekezaji ataendesha bandari zote mpaka za maziwani na mito akiamua? Mwekezaji anamilikishwa ardhi ya bandari? Ni kweli bandari za visiwani ziko excluded? N.k....n.k...

Lakini sasa imegeuka na kuwa ushabiki tu kama wa Yanga na Simba; na hii haisaidii cho chote. Mpaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msemaji mkuu wakisimama hakuna hoja ya maana wanayotoa bali kulalamika tu na kuzodoa upande mwingine. Hovyo tu!

➡️➡️➡️ Nina miaka karibia 9 hapa JF mkuu na huwa sina tabia ya kutukanana humu maana hiyo naamini ni matokeo ya malezi mabovu, ugonjwa wa akili (mf. Narcissistic Personality Disorder na clinical depression), wivu na kujichukia, ukosefu wa hoja, kutokujiamini, misplaced anger, childhood trauma na mengineyo. Sana sana mtu akinitukana namtia kwenye ignore list tu na kuachana naye.

Tuko pamoja mkuu 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
Asante sana. Natamani haya uliyoandika yangewafikia walengwa na wayafanyie kazi. Kila la heri.
 
Back
Top Bottom