Mkataba wa IGA Ulitengenezwa Kuwa na Vipengele Hasi kwa Tanzania, na Viongozi Wetu Walijua na Kushiriki Uhujumu Huo

Umekuwa mkweli PASCO big up wenzako ma- class mate wako akina Mpandikizi ndio wanapractice to date
 
Chongolo ndio nani, ndio maana makonda alimwona fala tuu
mtamlaumu kila atakaye kaa pale juu, shida ni hii ccm na mfumo wake. Nakuambia hata Lisu akiingia ccm akakaa lale juu akili yake itakuwa kama Wasira. Daw ni kufulumusha ccm out
 
Mkuu kalamu, you are one of more perceptive, serious, intelligent member of JF. Lakini unanishangaza unaposema Magufuli hakuwa Mzalendo? Alikuwa na mapungufu kama wewe na Mimi, of course alikuwa nayo.

Unafikiri angeweza kusaini mkataba kama huu?

Najua alikuwa Hana uvumilivu na criticism, lakini ukiangalia records yake ilikuwa ya kizalendo.

Elimu bure, umeme, maji, hospitali, mahakama, uwajibikaji serikalini, miundombinu ya uhakika, seriousness kuhusu maslahi ya Tanzania.

To compare SSH na JPM ni kumvunjia heshima JPM.

Mimi pia sina chama nipo kwa maslahi ya Taifa.
 
JPM alijenga SGR kwa trilioni 17 ili isafirishe mzigo huu huu wa DP World. Kumbuka kuwa mwarabu anafanya biashara na Kagame ambapo kajenga dry port ya kuweza kutunza kontena 50,000 kwa wakati mmoja.
Mkuu Steven, hatupingi uwekezaji, maendeleo. Tungependa wawekezaji wengi zaidi ila wenye manufaa kwa Taifa. Mikataba mibovu imeingiwa na serikali zilizopita.

Madhara yake tunayalipia hadi Leo.

Issue kama hii JPM angeizungumzia live bila Chenga.

Safari za siri za SSH Dubai, zilikuwa na malengo gani?

Wabunge, watu maarufu kupelekwa Dubai kwenye holiday kuja kuipigia debe mkataba nini malengo yake?

Kwanini wajibu wote in wetu, haki zote ni zao, unafikiri UAE, UK, USA,EU, SA, wangesaini mkataba kama huu na sisi TZ?

Kwanini tunaingia IGA na DP world/ Dubai sio serikali ya UAE?

Saini kwenye mkataba kwa upande wa Dubai hazieleweki, Nani amesaini kwa mamlaka gani?

Kimsingi tunataka serikali ifuate sheria za tenda, uwazi, transparency, kusikiliza maoni ya wananchi na kuyatumia.
 
Unaifahamu VIEITE wewe ?
 
Hoja kwa sasa iwe ni kuchunguza hawa watu wamepewa nini na sio tena ubovu wa mkataba kwani ni wazi huu mkataba ni mbovu kupindukia.
Kama akina kitenge wamepewa ulivyoviona unadhani hawa wazito wamepewa nini ?
 
JPM alijenga SGR kwa trilioni 17 ili isafirishe mzigo huu huu wa DP World. Kumbuka kuwa mwarabu anafanya biashara na Kagame ambapo kajenga dry port ya kuweza kutunza kontena 50,000 kwa wakati mmoja.
Ni jambo jema, sasa kama ni jambo jema kwanini tusiwe wazi na vipengele vyote.

Hizo Trillioni 17 zinaweza kurudishwa kwa miaka mitatu na mizigo wa DRC.

Tunataka kujua oversight, ukaguzi, kuhakikisha madawa, rasilimali zetu za asili hazitafirishwa kama njugu.

Sasa hivi Loliondo wanaimiliki Mfalme wa UAE, hatujui hata Twiga, Zebra, Simba, Tembo wangapi wanasafirishwa kila siku. Sababu kuna Airport ndani pale.

Hatutaki mikataba kama hii.
 
Mkuu 'Lookmalasin', sijui ni kwa vipi inakuwa vigumu kwako kunielewa, lakini najua tupo pamoja sana katika swala la maslahi ya nchi yetu na raia wake. Hilo linanipa faraja sana, hata kama tusipokubaliana kwa kiasi fulani kumhusu Magufuli.

Ngoja nikueleze baadhi ya; na pia nitagusa machache ninayoyaona yalimharibia sana sifa na heshima na kuweza kutambulika kama kiongozi mzalendo kwa nchi hii.

Niliyompendea Magufuli:

1. Uthubutu wa kufanya mambo makubwa kwa kuamini "tunaweza kufanya" - hili ninaliweka mbele kabisa na ni sifa ambayo inahitajika sana kwa kiongozi kuwa nayo, hasa katika ngazi ya maendeleo tulipofikia sasa. Kuwa na uthubutu hakuna maana kwamba hapawezi kuwepo na makosa katika utekelezaji, la hasha, lakini ni sifa nzuri sana.
Kwa mfano: Bwawa la Umeme la Julius Nyerere tusingekuwa tunalifikiria hadi leo hii. Serikali kuhamia Dodoma ingekuwa bado ni stori za kiswahili tu. Ujenzi wa SGR, Bomba la mafuta Uganda na jinsi alivyowashughukia waKenya juu ya kazi hiyo; n.k., n.k.. Ipo mifano mingi ya uthubutu mzuri kabisa wa kiongozi huyo, hata kama kuna mifano michache pia ya uthubutu wa hovyo, kama uwanja wa ndege.

2. Udikteta - kwa maana ya kutobembelza bembeleza watu na kulembalemba mahali pasipohitaji kubembelezana. Inajulikana sasa wazi kwamba hali tuliyo hapa Tanzania tunahitaji kiongozi mkali, mwenye ngvu, mfuatiliaji wa karibu sana kwa kila jambo linalotakiwa kufanyika. Nchi hii sasa kuikwamua ilipo sasa, tunahitaji kiongozi wa namna hiyo.
Usione hizo zi Malaysia, Korea Kusini, Singapore zilipofikia ukadhani watu walikuwa wakicheana kama tunavyofanya sisi hapa wakati huu. Kulikuwa na maviongozi yenye nguvu huko ambayo hayakuvumilia uozo katika utendaji wa kazi.
Magufuli alikuwa na vimelea vya aina hiyo, angeondoa tu kuonekana kama anafanya uonevu na kukomoa watu kwa sababu ambazo hazikuhusiana na utendaji wa kazi

3. Najua wazi kwamba "Magufuli asingekubaliana na upuuzi huu wa Bandari zetu", na hiyo ni sifa nzuri niliyoipenda.

Kabla sijaandika gazeti jingine hapa, ngoja nimalize kwa kuangalia madhaifu yake ambayo yalimwondolea hadhi aliyoistahili.
1. Kupenda sifa kwa kupitiliza sana. Kuwapambania wanyonge ni jambo zuri sana kwa kiongozi yeyote, lakini asifanye ionekane kama ni kutafuta sifa kutoka kwenye kundi hilo. Sitaeleza zaidi juu ya hili hapa.

2. Kiburi/uonevu na majivuno, na hatawakati mwingine kuonekana kukosa staha na kudhalilisha watu - sitafafanua.

3. Ukatili uliopitiliza - kwenye hili kuna mambo ambayo sitaki hata kuyataja.

Acha niishie hapa.

Lakini, leo hii tunamhitaji sana mtu wa namna hiyo ya Magufuli, bila ya kuwa na mapungufu makubwa kama aliyokuwa nayo Magufuli.
Sijui tutampata vipi mtu huyo. Nina hakika wapo, tatizo tu ni kuwaopoa waliko jificha.
 
Ndugu zetu Kuna kitu wanasema" ukichimama nchale, ukikaa nchale".
Ukiukubali unaliwa, ukikataa unaliwa!!!
Kuna namna nyingi ya kukusanya hela za Uchaguzi ujao
 
Binadamu wote tuna mapungufu. Wale viongozi walioleta maendeleo mwanzoni South Korea, Singapore, Malaysia, USA, UK, France walikuwa pia na mapungufu.

Anyway turudi kwenye mkataba IGA nipo na wewe 100%.

Nakubaliana na hoja yako, heading, kwamba mkataba ulitengenezwa kuwa na vipengele hasi, of course viongozi wetu walijua hivyo ndio maana wakafanya mambo kisirisiri
 
Kwa hiyo mkataba kwa sasa hatuuhoji tumehamia kwenye wanyama wetu?.

Kwanini watanzania tuna akili za kimaskini kiasi hiki?. siku zote tunadhani tunaibiwa sisi tu.

Hayo madini tunayo teknolojia ya kuweza kuyapandisha thamani? hizi akili za kichoyo hazitufikishi popote.
 
UAE ni muungano wa majimbo saba yanayounganishwa pamoja. Dubai likiwa ni jimbo mojawapo lina haki ya kufanya uwekezaji mahali popote duniani bila kuingilia katiba ya UAE.

Hii ni IGA sio BIT tusema wajibu wote ni wetu. Na mikataba inayokwenda kufanya kazi ni ile ya HGA ambayo ni mingi kutokana na mawanda ya uwekezaji wa DP World.

Rais hasafiri kwa siri hata siku moja, wewe au mimi kutojua kuhusu safari hiyo hakuifanyi ikawa ni ya siri.

Malengo ya wabunge kwenda Dubai ungewauliza moja kwa moja wao wenyewe wapo kwenye nafasi ya kukujibu.

Nchi inatazama uwekezaji utakaoongeza tija ya bandari yetu kwa kutuondolea foleni za upakuaji wa meli pale TPA. Pia kutupunguzia gharama zote za mizigo wakati ikiwa katika eneo la bandari.
 
Da, usiongee yote, jifunze kuweka kiporo cha maneno. Watu wana hasira.
Wenye hasira za halali ni wale wanaofanya biashara ya kuingiza bidhaa na kusafirisha nje kupitia bandari yetu, hao ndio wadau halisi wa bandari.

Hasira zao zina maana na sababu za msingi kuliko hawa kina Kalamu na Bams wadau wanaojificha nyuma ya majina ya bandia, hasira yao haina msaada wowote kwa uchumi wa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…