Mkataba wa IGA Ulitengenezwa Kuwa na Vipengele Hasi kwa Tanzania, na Viongozi Wetu Walijua na Kushiriki Uhujumu Huo

Mkataba wa IGA Ulitengenezwa Kuwa na Vipengele Hasi kwa Tanzania, na Viongozi Wetu Walijua na Kushiriki Uhujumu Huo

Kwenye mikataba yote kuna eneo la drown by...

Kwenye hili la elimu ya kuunga unga ni kweli, mimi ni wale wa zamani 60s, enzi zetu LL.B inatolewa UDSM pekee!, chuo kilikuwa kina enrols only 60 students top creams, darasa letu Ilboru, tukachukua nafasi 10 tukiwa ndio top in Tanzania, mimi sikufanikiwa kupenya ndio nikaenda journalism, nikaunga unga mpaka nikapata LL.B

Sithubutu kujiita the best legal brain, kwasababu sijaonyesha popote u best wangu ila....

No sio sijawahi kushinda kesi yoyote high court, bali sijawahi kupanda Mahakama kwa kesi yoyote kwasababu I don't practice!

Asante sana for info, na leo ndio nimejua kumbe Fuma ni verified name na ni wakili!.
Nice to know you.
P
Umekuwa mkweli PASCO big up wenzako ma- class mate wako akina Mpandikizi ndio wanapractice to date
 
Chongolo ndio nani, ndio maana makonda alimwona fala tuu
mtamlaumu kila atakaye kaa pale juu, shida ni hii ccm na mfumo wake. Nakuambia hata Lisu akiingia ccm akakaa lale juu akili yake itakuwa kama Wasira. Daw ni kufulumusha ccm out
 
Mkuu 'Lookmalasin', naomba nijitambulishe kwako, kwa maana naona hunijui mimi.
Kwa wanaonifahamu tokea nijisajili humu JF, na kusoma chochote nilichoandika humu hawawezi kamwe kunipanga kama ulivyonipanga wewe.

Ngoja nikufahamishe kwa kifupi sana ninakosimamia.

Kivyama vya siasa, hakuna chama nilicho mwanachama wala mfuasi wake. Chama pekee nilichonacho ni maslahi ya Tanzania na waTanzania wote, hata hao wanaoshabikia vyama vilivyooza kama CCM.
Kwa viongozi wa kisiasa, nitamuunga mkono kiongozi yeyote anayesimamia kwa dhati kabisa maslahi ya nchi yetu. Sasa naona hapa ndipo unapotaka kunilazimisha niungane nawe katika kumtambua Magufuli kuwa mfano huo wa kiongozi.
Hapana. Ninayatambua sana mazuri aliyojitahidi kuyasimamia Magufuli, kwa manufaa ya nchi hii, hili ninakuomba utambue hivyo.
Magufuli anakosa sifa ya kuwa Mzalendo, kama alivyostahiri kutambuliwa, kwa sababu ya tabia zake nyingi amabazo hazikuonekana kuwa za kizalendo kabisa. Sitaki kuyataja mambo hayo hapa, kwa sababu yanafahamika.

Laiti kama Magufuli angeachana na haya mambo ya ajabuajabu, akabaki na ukali wake, na juhudi zake za kuitumikia Tanzania, nami leo hii ningekuwa upande wako wa kumsifu, na kumtambua kuwa mmoja wa viongozi wazalendo tuliowahi kuwa nao hapa Tanzania.

Inatosha.
Mkuu kalamu, you are one of more perceptive, serious, intelligent member of JF. Lakini unanishangaza unaposema Magufuli hakuwa Mzalendo? Alikuwa na mapungufu kama wewe na Mimi, of course alikuwa nayo.

Unafikiri angeweza kusaini mkataba kama huu?

Najua alikuwa Hana uvumilivu na criticism, lakini ukiangalia records yake ilikuwa ya kizalendo.

Elimu bure, umeme, maji, hospitali, mahakama, uwajibikaji serikalini, miundombinu ya uhakika, seriousness kuhusu maslahi ya Tanzania.

To compare SSH na JPM ni kumvunjia heshima JPM.

Mimi pia sina chama nipo kwa maslahi ya Taifa.
 
JPM alijenga SGR kwa trilioni 17 ili isafirishe mzigo huu huu wa DP World. Kumbuka kuwa mwarabu anafanya biashara na Kagame ambapo kajenga dry port ya kuweza kutunza kontena 50,000 kwa wakati mmoja.
Mkuu Steven, hatupingi uwekezaji, maendeleo. Tungependa wawekezaji wengi zaidi ila wenye manufaa kwa Taifa. Mikataba mibovu imeingiwa na serikali zilizopita.

Madhara yake tunayalipia hadi Leo.

Issue kama hii JPM angeizungumzia live bila Chenga.

Safari za siri za SSH Dubai, zilikuwa na malengo gani?

Wabunge, watu maarufu kupelekwa Dubai kwenye holiday kuja kuipigia debe mkataba nini malengo yake?

Kwanini wajibu wote in wetu, haki zote ni zao, unafikiri UAE, UK, USA,EU, SA, wangesaini mkataba kama huu na sisi TZ?

Kwanini tunaingia IGA na DP world/ Dubai sio serikali ya UAE?

Saini kwenye mkataba kwa upande wa Dubai hazieleweki, Nani amesaini kwa mamlaka gani?

Kimsingi tunataka serikali ifuate sheria za tenda, uwazi, transparency, kusikiliza maoni ya wananchi na kuyatumia.
 
Sote tuanelewa kwamba nchi yetu Rais ni kila kitu kwetu, hahojiwi na mbaya zaidi huwezi kumshtaki mahakama yoyote nchini, akiwa madarakani au baada ya kuachia madaraka.

Wananchi wa nchi hii wamezoea, kwamba hawawezi kumwajibisha kiongozi huyo kwa njia yoyote ile; na Bunge ambalo sheria inaruhusu kumwajibisha jinsi wawakilishi wa Bunge hilo wanavyopatikana kwa fadhira za mtu huyo huyo mmoja (Rais), halina uwezo wa kumwajibisha mtu huyu.

Bila shaka yoyote, Rais wetu Samia yote haya aliyajua, na hasa baada ya kuona ni namna gani mtangulizi wake alivyokanyaga kila kitu kutimiza matakwa yake.
Kwa hiyo Samia hakuwa na hana hofu yoyote juu ya kufanya aliyonuia kuyafanya siku nyingi, kama angepata fursa hiyo ya kuyafanya

Kwa bahati nzuri kwake, na mbaya kwetu wengine fursa hiyo ikamwangukia bila ya mategemeo yoyote

Sasa anatimiza alichonuia toka siku nyingi.
Hapa nataka kuonyesha mambo yaliyofanyika, kwa maksudi, tokea mwanzo alipochukua uongozi wa nchi ili kufanikisha lengo lake la kuiumiza nchi yetu. Nitaorodhesha mambo aliyoyafanya au kutoyafanya ili kufanikisha IGA hii iliyoletwa kwetu ifanikiwe. Kumbuka wakati wote, yeye anajua hakuna lolote wananchi wanaloweza kufanya kumzuia au kumuwajibisha sasa au baadae.

1. Uteuzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika eneo husika, na kuwaondoa viongozi ambao hawakukidhi mahitaji yake. Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara, Wakurugenzi TPA na kwingineko. Sitataja majina, kwani wanafahamika.
Hawa ni watu maalum walioteuliwa kuhakikisha lengo la IGA (mbovu) linafanikiwa.

2. Kufanya viini macho ili kupoteza lengo.
Paliwahi kuwepo mjadala wa kufufua mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, na yeye Rais aliwahi kueleza kuwa kuna timu ya majadiliano na waChina. Hili halikufika mbali, kabla ya kugeukia kwenye ujenzi wa hatua za mwanzo sisi wenyewe.

Wakati haya yakiendelea, imebainika sasa kwamba DPWorld tayari walikuwa kwenye kibarua cha kutengeneza IGA na wataalam wetu hapa ambao haijulikani walipatikana kwa mpango upi kushughulikia kazi hiyo. Bila shaka ni sahihi pia kusema kuwa ni watu walioaminiwa kutengeneza kitu alichokitaka mteuzi wao kwenye nafasi hiyo.

3. TICTS - abaki/asibaki? moja ya viini macho kuzuga watu, bila shaka hata wao TICTS hawakujua hatma yao itakuwa vipi. Wakati wote huu wa sintofahamu, DP World na wataalam wetu wapo kazini wakisuka IGA ya kutukomesha sisi.
4. Mara BUUUUU! DP World anaingia kwa kishindo kikubwa. Sasa ndipo watu wanaanza kuunganisha doti
Bendera yetu na picha ya Rais wetu juu ya jengo refu kabisa duniani; mara fununu za viongozi kwenda kwenye EXPO Dubai kimya kimya na Rais kukaa huko kwa siri kubwa, kumbe anatia saini mkataba wa kutuuza!

5. Mkataba unavujishwa? Juhudi kubwa zinaanza kufukia mahandaki. Hapana, huo siyo Mkataba, hayo ni "Makubaliano tu, ikiambatana na upotoshaji mwingi mwingine, toka kwa waziri na mtu mwingine aliyeaminiwa sana kusimamia kujua kilichomo ndani ya Mkataba/Makubaliano" hayo. Mtaalam wa sheria mbobezi (tunaambiwa), Hamza Johari ndiye mkuu wa timu. Watu wanajiuliza, na Mwanasheria mkuu wa Serikali alishiriki vipi hadi kufika kwenye hatua hii?
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hasemi kitu, bali kukanusha tu kwamba "Bandari haijauzwa". Hakuna anayejua kiwango cha ushiriki wake kwenye mkataba huo, na kama yeye, kwa nafasi yake anakubaliana na yaliyomo kwenye mkataba. Sijasikia akisema lolote juu ya hayo.

6. Taratibu na Hatua sahihi za kuingia mikataba kama huu (IGA) - Je, sisi kama taifa tunao utaratibu wowote tuliojiwekea wa kuingia kwenye mikataba kama hii? Huu siyo mkataba wa kwanza Tanzania iliouingia, je hiyo mingine kulifanyika mambo gani ambayo yamezoeleka kufanywa, lakini safari hii ikawa ni tofauti?

Hili ni swali lililo wazi, kama kuna utaratibu maalum, je ulifuatwa, hata kwa kiasi fulani tu?
jambo la kwanza linaloniingia akilini ni "Vikao vya Baraza la Mawaziri". Kwa mtizamo wangu, jambo kubwa kama hili haliwezi kufanyika bila ya uwepo wa angalao kikao cha Mawaziri kulijadili..
Vikao hivi vya Baraza la Mawaziri siku hizi vimekuwa kama ni siri kubwa sana, hata kule kutaja tu kulikuwepo na kikao siku hizi ni nadra sana, hata bila ya kutaja yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho.
Kwa hiyo hili ni swali tu kuuliza kama kulikuwa na kikao cha kujadili, au kujulishwa tu kwamba kuna mpango wa ujio wa DP World na hatua zilizokuwa zikifanyika kuwakaribisha hapa.
Kama Mawaziri nao hawakuwa na habari, hilo litakuwa jambo la kushangaza sana linaloongeza uzito katika hoja za andiko hili.
7. Ushirikishwaji wa Bunge katika "kuridhia Mkataba" Bila shaka yoyote palikuwepo na mpango kabambe wa kulishirikisha Bunge katika kufanya hujuma hizi, siyo kwa nia njema bali kwa nia ovu..
a) Kundi la wabunge lililopelekwa Dubai, ni utaratibu upi uliotumika kuwachagua hao waliokwenda? Wanazo sifa maalum ambazo zingewawezesha kutambua mambo ambayo hayana manufaa kwetu?
b) Waliandaliwa na kupewa semina wajiandae kuhusu maswala nyeti katika kazi wanayokwenda kuifanya huko walikokwenda? Walipewa Mkataba wausome wajue yaliyomo kabla hawajaondoka hapa?
Hawa wabunge ni akina nani hasa?

Kama maswali yote haya hayana majibu, maana yake ni kwamba hii ilikuwa ni mbinu tu, iliyotegeshwa kuhalalisha maovu juu ya nchi yetu, maovu waliyoyajua walioandaa mkataba huo na washirika wao wote.
c) Bungeni wakati wa kikao cha Bunge, ni wabunge wapi waliopewa nafasi ya kujadili yaliyomo kwenye mkataba, na ni nani aliyetoa nafasi hiyo kwa wabunge hao maalum? Hawa wabunge walijua kilichokuwemo kwenye huo Mkataba? Mbona hta mmoja wao hakujitokeza na anagalao kutaja tu hata kifungu kimoja alichokuwa nacho mashaka? Hawa wote waliandaliwa kwa maksudi kwa ushirikiano na uongozi wa Bunge?
d) Ushirikiwa wananchi, wanapewa masaa 24 kuleta maoni yao. Maana ya hili ni kwamba hapakutakiwa kuwepo na mchango wa wananchi ili lengo la kuhujumu nchi litekelezwe.

DPWorld wanao uzoefu mkubwa sana katika maswala haya ya Mikataba, kwa sababu kila sehemu walikokwenda wamekutana na chngamoto chungu nzima zilizowakabili.
Wamekuja hapa kwetu, wakamkuta mkuu wetu aliye tayari kabisa kuwapokea kwa masharti waliyoyapenda wao. Mkuu wetu hana uzoefu wowote, na isitoshe hana uchungu mkubwa kuhusu nchi anayoiongoza yeye, ila anayo madaraka ya kufanya lolote analotaka bila kuwajibishwa na yeyote.

Hapa ndipo tulipofikia sasa hivi.

Ingekuwa ni nchi nyingine, Mkataba huu usingemwacha huyu mkuu abaki salama, tena akiendelea kwenye madaraka yake kana kwamba hakuna lolote lililofanyika.
Lakini hii ni Tanzania. Yeye kishasema "Ameziba masikio", wenye kupiga kelele wapige kelele hadi wachoke wenyewe; lakini DP World hakuna wa kumzuia kuja hapa.

SAWA.
Sasa tumebaki na moja tu tunaloweza kulitegemea kuondokana na hujuma hii juu ya nchi yetu.
Je, tunaweza kumpata kichaa mwingine (bila ya baadhi ya mambo ya aliyetangulia mbele ya safari) atuondolee uchafu huu ndani ya nchi yetu? (Bila kujali hasara tutakayoingia kwa kuvunja mkataba (kwani kuendelea na mkataba wa aina hii ni hasara kubwa zaidi ya kulipa hiyo fidia tutakayodaiwa).
Na kwa kuwa ni 'kichaa', bila shaka baadhi ya hawa wahujumu watachukuliwa hatua bila ya kuwaonea aibu.

IGA baina ya Tanzania na Dubai ni hujuma iliyo andaliwa maksudi kuihujumu Tanzania.

N.B. Sikutegemea na wala siyo kawaida yangu kuandika gazeti, lakini leo acha iwe hivyo, kwani hakuna namna.

Samahani kwa makosa ya kiuandishi kama yamo kwenye andiko hili..
Unaifahamu VIEITE wewe ?
 
Hoja kwa sasa iwe ni kuchunguza hawa watu wamepewa nini na sio tena ubovu wa mkataba kwani ni wazi huu mkataba ni mbovu kupindukia.
Kama akina kitenge wamepewa ulivyoviona unadhani hawa wazito wamepewa nini ?
 
JPM alijenga SGR kwa trilioni 17 ili isafirishe mzigo huu huu wa DP World. Kumbuka kuwa mwarabu anafanya biashara na Kagame ambapo kajenga dry port ya kuweza kutunza kontena 50,000 kwa wakati mmoja.
Ni jambo jema, sasa kama ni jambo jema kwanini tusiwe wazi na vipengele vyote.

Hizo Trillioni 17 zinaweza kurudishwa kwa miaka mitatu na mizigo wa DRC.

Tunataka kujua oversight, ukaguzi, kuhakikisha madawa, rasilimali zetu za asili hazitafirishwa kama njugu.

Sasa hivi Loliondo wanaimiliki Mfalme wa UAE, hatujui hata Twiga, Zebra, Simba, Tembo wangapi wanasafirishwa kila siku. Sababu kuna Airport ndani pale.

Hatutaki mikataba kama hii.
 
Mkuu kalamu, you are one of more perceptive, serious, intelligent member of JF. Lakini unanishangaza unaposema Magufuli hakuwa Mzalendo? Alikuwa na mapungufu kama wewe na Mimi, of course alikuwa nayo.

Unafikiri angeweza kusaini mkataba kama huu?

Najua alikuwa Hana uvumilivu na criticism, lakini ukiangalia records yake ilikuwa ya kizalendo.

Elimu bure, umeme, maji, hospitali, mahakama, uwajibikaji serikalini, miundombinu ya uhakika, seriousness kuhusu maslahi ya Tanzania.

To compare SSH na JPM ni kumvunjia heshima JPM.

Mimi pia sina chama nipo kwa maslahi ya Taifa.
Mkuu 'Lookmalasin', sijui ni kwa vipi inakuwa vigumu kwako kunielewa, lakini najua tupo pamoja sana katika swala la maslahi ya nchi yetu na raia wake. Hilo linanipa faraja sana, hata kama tusipokubaliana kwa kiasi fulani kumhusu Magufuli.

Ngoja nikueleze baadhi ya; na pia nitagusa machache ninayoyaona yalimharibia sana sifa na heshima na kuweza kutambulika kama kiongozi mzalendo kwa nchi hii.

Niliyompendea Magufuli:

1. Uthubutu wa kufanya mambo makubwa kwa kuamini "tunaweza kufanya" - hili ninaliweka mbele kabisa na ni sifa ambayo inahitajika sana kwa kiongozi kuwa nayo, hasa katika ngazi ya maendeleo tulipofikia sasa. Kuwa na uthubutu hakuna maana kwamba hapawezi kuwepo na makosa katika utekelezaji, la hasha, lakini ni sifa nzuri sana.
Kwa mfano: Bwawa la Umeme la Julius Nyerere tusingekuwa tunalifikiria hadi leo hii. Serikali kuhamia Dodoma ingekuwa bado ni stori za kiswahili tu. Ujenzi wa SGR, Bomba la mafuta Uganda na jinsi alivyowashughukia waKenya juu ya kazi hiyo; n.k., n.k.. Ipo mifano mingi ya uthubutu mzuri kabisa wa kiongozi huyo, hata kama kuna mifano michache pia ya uthubutu wa hovyo, kama uwanja wa ndege.

2. Udikteta - kwa maana ya kutobembelza bembeleza watu na kulembalemba mahali pasipohitaji kubembelezana. Inajulikana sasa wazi kwamba hali tuliyo hapa Tanzania tunahitaji kiongozi mkali, mwenye ngvu, mfuatiliaji wa karibu sana kwa kila jambo linalotakiwa kufanyika. Nchi hii sasa kuikwamua ilipo sasa, tunahitaji kiongozi wa namna hiyo.
Usione hizo zi Malaysia, Korea Kusini, Singapore zilipofikia ukadhani watu walikuwa wakicheana kama tunavyofanya sisi hapa wakati huu. Kulikuwa na maviongozi yenye nguvu huko ambayo hayakuvumilia uozo katika utendaji wa kazi.
Magufuli alikuwa na vimelea vya aina hiyo, angeondoa tu kuonekana kama anafanya uonevu na kukomoa watu kwa sababu ambazo hazikuhusiana na utendaji wa kazi

3. Najua wazi kwamba "Magufuli asingekubaliana na upuuzi huu wa Bandari zetu", na hiyo ni sifa nzuri niliyoipenda.

Kabla sijaandika gazeti jingine hapa, ngoja nimalize kwa kuangalia madhaifu yake ambayo yalimwondolea hadhi aliyoistahili.
1. Kupenda sifa kwa kupitiliza sana. Kuwapambania wanyonge ni jambo zuri sana kwa kiongozi yeyote, lakini asifanye ionekane kama ni kutafuta sifa kutoka kwenye kundi hilo. Sitaeleza zaidi juu ya hili hapa.

2. Kiburi/uonevu na majivuno, na hatawakati mwingine kuonekana kukosa staha na kudhalilisha watu - sitafafanua.

3. Ukatili uliopitiliza - kwenye hili kuna mambo ambayo sitaki hata kuyataja.

Acha niishie hapa.

Lakini, leo hii tunamhitaji sana mtu wa namna hiyo ya Magufuli, bila ya kuwa na mapungufu makubwa kama aliyokuwa nayo Magufuli.
Sijui tutampata vipi mtu huyo. Nina hakika wapo, tatizo tu ni kuwaopoa waliko jificha.
 
Ndugu zetu Kuna kitu wanasema" ukichimama nchale, ukikaa nchale".
Ukiukubali unaliwa, ukikataa unaliwa!!!
Kuna namna nyingi ya kukusanya hela za Uchaguzi ujao
 
Binadamu wote tuna mapungufu. Wale viongozi walioleta maendeleo mwanzoni South Korea, Singapore, Malaysia, USA, UK, France walikuwa pia na mapungufu.

Anyway turudi kwenye mkataba IGA nipo na wewe 100%.

Nakubaliana na hoja yako, heading, kwamba mkataba ulitengenezwa kuwa na vipengele hasi, of course viongozi wetu walijua hivyo ndio maana wakafanya mambo kisirisiri
 
Ni jambo jema, sasa kama ni jambo jema kwanini tusiwe wazi na vipengele vyote.

Hizo Trillioni 17 zinaweza kurudishwa kwa miaka mitatu na mizigo wa DRC.

Tunataka kujua oversight, ukaguzi, kuhakikisha madawa, rasilimali zetu za asili hazitafirishwa kama njugu.

Sasa hivi Loliondo wanaimiliki Mfalme wa UAE, hatujui hata Twiga, Zebra, Simba, Tembo wangapi wanasafirishwa kila siku. Sababu kuna Airport ndani pale.

Hatutaki mikataba kama hii.
Kwa hiyo mkataba kwa sasa hatuuhoji tumehamia kwenye wanyama wetu?.

Kwanini watanzania tuna akili za kimaskini kiasi hiki?. siku zote tunadhani tunaibiwa sisi tu.

Hayo madini tunayo teknolojia ya kuweza kuyapandisha thamani? hizi akili za kichoyo hazitufikishi popote.
 
Mkuu Steven, hatupingi uwekezaji, maendeleo. Tungependa wawekezaji wengi zaidi ila wenye manufaa kwa Taifa. Mikataba mibovu imeingiwa na serikali zilizopita.

Madhara yake tunayalipia hadi Leo.

Issue kama hii JPM angeizungumzia live bila Chenga.

Safari za siri za SSH Dubai, zilikuwa na malengo gani?

Wabunge, watu maarufu kupelekwa Dubai kwenye holiday kuja kuipigia debe mkataba nini malengo yake?

Kwanini wajibu wote in wetu, haki zote ni zao, unafikiri UAE, UK, USA,EU, SA, wangesaini mkataba kama huu na sisi TZ?

Kwanini tunaingia IGA na DP world/ Dubai sio serikali ya UAE?

Saini kwenye mkataba kwa upande wa Dubai hazieleweki, Nani amesaini kwa mamlaka gani?

Kimsingi tunataka serikali ifuate sheria za tenda, uwazi, transparency, kusikiliza maoni ya wananchi na kuyatumia.
UAE ni muungano wa majimbo saba yanayounganishwa pamoja. Dubai likiwa ni jimbo mojawapo lina haki ya kufanya uwekezaji mahali popote duniani bila kuingilia katiba ya UAE.

Hii ni IGA sio BIT tusema wajibu wote ni wetu. Na mikataba inayokwenda kufanya kazi ni ile ya HGA ambayo ni mingi kutokana na mawanda ya uwekezaji wa DP World.

Rais hasafiri kwa siri hata siku moja, wewe au mimi kutojua kuhusu safari hiyo hakuifanyi ikawa ni ya siri.

Malengo ya wabunge kwenda Dubai ungewauliza moja kwa moja wao wenyewe wapo kwenye nafasi ya kukujibu.

Nchi inatazama uwekezaji utakaoongeza tija ya bandari yetu kwa kutuondolea foleni za upakuaji wa meli pale TPA. Pia kutupunguzia gharama zote za mizigo wakati ikiwa katika eneo la bandari.
 
Da, usiongee yote, jifunze kuweka kiporo cha maneno. Watu wana hasira.
Wenye hasira za halali ni wale wanaofanya biashara ya kuingiza bidhaa na kusafirisha nje kupitia bandari yetu, hao ndio wadau halisi wa bandari.

Hasira zao zina maana na sababu za msingi kuliko hawa kina Kalamu na Bams wadau wanaojificha nyuma ya majina ya bandia, hasira yao haina msaada wowote kwa uchumi wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom