Mkataba wa IGA Ulitengenezwa Kuwa na Vipengele Hasi kwa Tanzania, na Viongozi Wetu Walijua na Kushiriki Uhujumu Huo

Ni kweli mnatutumia km condom kwa uongozi wa CCM. Bado haujanishawishi kuukubali huu mkataba.
Mkataba wenyewe wa milele hauna ukomo. Km hauna ukomo kwa maana hiyo bandari ishauzwa hivyo.
1. Hizo gharama za kuendesha bandari, kununua vifaa winchi, camera, kuajiri watu n.k inaweza kuzidi gharama ya kununua ndege 5 za ATCL?
2. Hakuna njia au ubunifu wa kufanya ili kuziendeleza rasilimali zetu tofauti na uwekezaji?
Ubinafsishaji, sioni faida yoyote zaidi ya kuwafanya wananchi waishi maisha magumu. Mfano Gesi ya Mtwara kwa tamaa zenu za ubinafshaji leo mtungi wa kati unajazwa kwa elfu 57. Hakuna unafuu wowote
Leo hii vifurushi vya data vipo juu kulinganisha na vipato vya wananchi. Hata TTCL tulitegemea iwe mkombozi nalo linatunyonya, huduma mbovu, laini hazipatikani, vocha hakuna, vifurushi vipo juu.
Unatetea huo mkataba wa milele kwasababu tayari meshachukua asilimia zenu.
Hii DP world ikipita, kodi zitapanda kwasababu hamna sehemu za kupata kipato cha kuongoza hii nchi, mtarudi kubuni mbinu ya kuwakamua wananchi ili serikali ipate hela.
Dhahabu, almasi, Tanzanite na gesi zote mebinafsisha na matokeo yake hamna sehemu za kupata hela, mkakimbilia kuweka tozo kwenye miamala ya simu.
Mkimaliza kuuza bandari, mtakuja na tozo au kodi mpya kwa ajili kuwakamua wananchi kwasababu hakuna mapato tena.
Viongozi wa Tanzania wanawaza wanufaishe matumbo yao, kubinafsisha na kubuni mbinu za kodi na tozo ili kuchukua visenti vya wananchi hawawazi watumie njia gani ili waendeleze rasilimali za Tanzania. Hamuwezi kuanzisha mradi wowote mkafanikiwa kwasababu ya rushwa na ufisadi wenu.
Ndiyo maana miradi yote iliyoanzishwa na serikali yote inapumulia mashine. ATCL, TTCL n.k hasara tu
Utasema nchi inaongozwa kwa kodi, sikatai hata Nyerere alisema "anatamani kila mwananchi alipe kodi ila utawatoza nini?" Mtu anauza mchicha unataka alipe 20,000 ili apate kibali cha kuuza.
Nyie viongozi, mjitafakari mnavyoongea au kuandika, watu sasa wameelimika.
 
Ujinga ni mzigo mzito sana, mtu anapokuwa nao anadhani kila mtu kabeba mzigo kama alivyoubeba yeye.

Kutokana na jinsi ulivyohangaika na swala hili la Bandari tokea mwanzo, ni wazi kabisa kwamba umewekeza sana kwenye jambo hili.
Matokeo yake sasa, hata unayoendelea kutetea humu kuhusu jambo lenyewe unashindwa kutambua kwamba unazidi kujionyesha ujinga ulionao juu ya swala lenyewe, wakati ukidhani kurudia mara kwa mara ujinga huo huo utawafanya na watu wengine wawe wajinga kama wewe.

Sasa sijui mwishoni utafikia wapi na jambo hili ambalo sasa ni wazi kwamba ni hujuma mahsusi iliyofanyiwa taifa letu.
 
Nikiwa mzalendo niliyeishi nchi hii tangu awamu ya kwanza mpaka ya sita ninayo haki ya kuipigania ili ifaidike na uwekezaji wenye lengo la kuondoa wapigaji wote wa pale TPA.

Huu ni wajibu wa msingi kabisa, nikiwa mtanzania niliyemuona Mwalimu Nyerere live akihutubia katika viwanja vya ikulu miaka ile ya themanini mwanzoni ninao wajibu wa kimaadili wa kuipigania nchi hii iweze kuondoka katika mikono ya mafisadi na madalali wao kina Kalamu.
 
Kuuita mkataba ni wa milele tayari ni kielelezo cha kutoelewa nini kimepitishwa bungeni.

Yote uliyoandika baada ya hapo ni sawa na bure yaani ni sawa na kuupaka rangi upepo.
 
Ukiwa umefuata kilichoandikwa na website ya World Bank tayati umepotoshwa na wewe. Benki ya dunia haikumtaka DP World achukue uendeshaji wa bandari yetu.

Wakaja na taarifa ya kutengeneza ya kwamba pesa imetoka Marekani wakati ni upotoshaji tu kama mwingine wowote ule.
 
Walikuwa wanawaza wanamtengenezea Magufuli huo mkataba
 
Nikiwa mzalendo niliyeishi nchi hii tangu awamu ya kwanza mpaka ya sita ninayo haki ya kuipigania ili ifaidike na uwekezaji wenye lengo la kuondoa wapigaji wote wa pale TPA.
Kwa kukusoma tangia umeingia humu JF kwa jina hili, utakuwa ni tapeli wa hali ya juu sana kujitangazia sifa hiyo uliyojitangazia mwenyewe katika mistari hiyo miwili.
Of course, kila mtu anayo haki ya kujitangazia lolote apendalo mwenyewe, hiyo ni haki yako.

Kuhusu "...swala la wapigaji wote wa pale TPA", sidhani kuwa wewe na hao mnaoshriki katika mkataba huu wa DP World; kuwa hilo ndilo lengo lenu kuu, ila ni kisababu tu kizuri mojawapo cha kukitumia kuhalalisha lengo kubwa nyuma ya mkataba wenyewe.

Na kama huelewi ngoja nikufanyie mhtasari: ukilinganisha hasara inayosababishwa na hao wapigaji wa pale TPA na hujuma hii mnayolifanyia taifa letu, ni mara mia nchi ibaki na visamaki hivyo vya TPA kuliko nyie mapapa wa hujuma.
Hivyo vidagaa vya TPA tunao uwezo sisi wenyewe, hapa hapa kuvishughulikia na kuviondoshea mbali, kuliko huu mkataba wa kitumwa mnaotafuta kutuingiza kwa hujuma zenu tu kwa taifa letu.

Imenilazimu nikujibu, kwa sababu unarudiarudia ujinga huu wa upotoshaji, kana kwamba sisi wengine wote tunafurahia hali hiyo ya hapo TPA.
 
Hoja kwa sasa iwe ni kuchunguza hawa watu wamepewa nini na sio tena ubovu wa mkataba kwani ni wazi huu mkataba ni mbovu kupindukia.
Una akili kubwa sana mkuu, Lissu aliwataja baadhi kama mbunge msukuma kuwa waliipewa rushwa na wengine ambao hawajakanusha tuhuma hizo mahakamani kuwa wamechafuliwa jina, hii ni dharihi kuwa hawa watu wamepokea hongo na sasa ni wakati wa kujua ni kiasi gani walihongwa na kwangu mimi wananchi tunatakiwa tuwaadhibu kama vibaka kwa kuwachoma moto
 
Nchi haiwezi kubaki na visamaki wakati teknolojia za kisasa kabisa zipo. Samia kakataa hujuma za wachache wanaowafanya wengi wajinga, Mtalia na kusaga meno lakini upigaji hapo TPA ndio umefika mwisho.

Mkataba hauna utumwa wowote kama unaielewa vyema mantiki nzima ya IGA na HGA zinazokwenda kujadiliwa na wadau wa bandari.

Tunawadhulumu sana wadau halisi wa bandari kwa kuendekeza siasa zetu za mijadala mingi isiyobadilisha chochote katika mienendo ya biashara zao.
 
Hii fani ya "kuigiza" haifai kabisa kwako. Nakushauri uachane nayo moja kwa moja.
 
Kama ilivyo kawaida yako unajifanya kujisahaulisha kinachozungumziwa kwenye mkataba ni nini.
Peleka hadaa hiyo kwingine siyo kwangu
 
Hao viongozi wana kinga gani ya kutoshitakiwa kwa kuhujumu nchi? Muda ndio huu sio mpaka baadaye ndio waje washitakiwe wakiwa hawapo madarakani kama kina yona na mramba
Hawastahili kushitakiwa mbona wezi wa kuku tunawachoma moto hawa wanatakiwa tuwapige moto mchana kweupe
 
Acha ujinga wewe rubbish
 
Hii fani ya "kuigiza" haifai kabisa kwako. Nakushauri uachane nayo moja kwa moja.
Nimekulia maeneo ya gymkhana, karimjee na ikulu nikiwaona wanasiasa kina Samuel Sitta, Nalaila Kiula na wengi wakubwa serikalini.

Sio muigizaji kama unavyodhani ni mzalendo halisi.
 
Kama ilivyo kawaida yako unajifanya kujisahaulisha kinachozungumziwa kwenye mkataba ni nini.
Peleka hadaa hiyo kwingine siyo kwangu
Kila kilichomo kwenye mkataba uliopita bungeni mnakipotosha halafu mkiambiwa ukweli mnasema eti ni hadaa. Hovyo kabisa.
 
Nimekulia maeneo ya gymkhana, karimjee na ikulu nikiwaona wanasiasa kina Samuel Sitta, Nalaila Kiula na wengi wakubwa serikalini.

Sio muigizaji kama unavyodhani ni mzalendo halisi.
Mkuu, mimi sina uwezo wa kuhoji ulizaliwa na kukulia wapi. Uwezo huo sina.

Ninachojua na kutokuwa na wasiwasi nacho ni maandishi yako mengi humu JF tangia ulipoingia ukitumia jina hili la 'Steve Joel Ntamusana'.
Maandishi yako yanajieleza vizuri kabisa kuweza kutambua wewe ni mtu wa aina gani hata bila ya kujitangazia sifa hiyo unayotaka watu wakutambue nayo.
 
Kila kilichomo kwenye mkataba uliopita bungeni mnakipotosha halafu mkiambiwa ukweli mnasema eti ni hadaa. Hovyo kabisa.
Hapa unatufanya sisi tusiwe na akili timamu na uelewa wa tunachokisoma ndani ya mkataba huo, huoni kwamba utakuwa na upungufu mkubwa akilini mwako?

Halafu hata unadiriki kusema "mkataba uliopita bungeni..."!

Huyu ndiye "mzalendo" tunayepaswa kumtambua ndani ya nchi hii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…