Mkataba wa IGA Ulitengenezwa Kuwa na Vipengele Hasi kwa Tanzania, na Viongozi Wetu Walijua na Kushiriki Uhujumu Huo

Mkataba wa IGA Ulitengenezwa Kuwa na Vipengele Hasi kwa Tanzania, na Viongozi Wetu Walijua na Kushiriki Uhujumu Huo

Hakuna faida ya kuwa mtanzania maana hawa majizi hawachagui cha kuiba na mijitu imekaa kimya tu na kuwasakama madadapoa ambao wanajitafutia ridhiki yao halali kabisa
 
Hapa unatufanya sisi tusiwe na akili timamu na uelewa wa tunachokisoma ndani ya mkataba huo, huoni kwamba utakuwa na upungufu mkubwa akilini mwako?

Halafu hata unadiriki kusema "mkataba uliopita bungeni..."!

Huyu ndiye "mzalendo" tunayepaswa kumtambua ndani ya nchi hii!
Unaelewa kwanini mkataba ulipita bungeni?.

Pia upo ushahidi wa tukio zima la kusaini huo mkataba kurushwa hewani na TBC, tatizo roho mbaya zimetujaa mpaka kumbukumbu tunapoteza.
 
Mkuu, mimi sina uwezo wa kuhoji ulizaliwa na kukulia wapi. Uwezo huo sina.

Ninachojua na kutokuwa na wasiwasi nacho ni maandishi yako mengi humu JF tangia ulipoingia ukitumia jina hili la 'Steve Joel Ntamusana'.
Maandishi yako yanajieleza vizuri kabisa kuweza kutambua wewe ni mtu wa aina gani hata bila ya kujitangazia sifa hiyo unayotaka watu wakutambue nayo.
Napinga huo ujinga mnaoifanyia serikali ya SSH mpaka mnaingiza sera za udini na ubaguzi.

Hana anachokifanya ambacho watangulizi wake hawajawahi kukifanya. Na kwa kifupi anatimiza ilani ile ile aliyotimiza mtangulizi wake.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hasemi kitu, bali kukanusha tu kwamba "Bandari haijauzwa".

Ushirikishwaji wa Bunge katika "kuridhia Mkataba" Bila shaka yoyote palikuwepo na mpango kabambe wa kulishirikisha Bunge katika kufanya hujuma hizi, siyo kwa nia njema bali kwa nia ovu..

Waliandaliwa na kupewa semina wajiandae kuhusu maswala nyet

ni wabunge wapi waliopewa nafasi ya kujadili yaliyomo kwenye mkataba, na ni nani aliyetoa nafasi hiyo

IGA baina ya Tanzania na Dubai ni hujuma iliyo andaliwa maksudi kuihujumu Tanzania
 
Halafu wakiambiwa;
wao ni wezi wanakuja juu!
Wakiitwa makuwadi wa raslimali zetu wanakuja juu na kutishia watu maisha!

Mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu uko HAI na utatenda kazi sawa na OUVU wenu.
 
Sote tuanelewa kwamba nchi yetu Rais ni kila kitu kwetu, hahojiwi na mbaya zaidi huwezi kumshtaki mahakama yoyote nchini, akiwa madarakani au baada ya kuachia madaraka.

Wananchi wa nchi hii wamezoea, kwamba hawawezi kumwajibisha kiongozi huyo kwa njia yoyote ile; na Bunge ambalo sheria inaruhusu kumwajibisha jinsi wawakilishi wa Bunge hilo wanavyopatikana kwa fadhira za mtu huyo huyo mmoja (Rais), halina uwezo wa kumwajibisha mtu huyu.

Bila shaka yoyote, Rais wetu Samia yote haya aliyajua, na hasa baada ya kuona ni namna gani mtangulizi wake alivyokanyaga kila kitu kutimiza matakwa yake.
Kwa hiyo Samia hakuwa na hana hofu yoyote juu ya kufanya aliyonuia kuyafanya siku nyingi, kama angepata fursa hiyo ya kuyafanya

Kwa bahati nzuri kwake, na mbaya kwetu wengine fursa hiyo ikamwangukia bila ya mategemeo yoyote

Sasa anatimiza alichonuia toka siku nyingi.
Hapa nataka kuonyesha mambo yaliyofanyika, kwa maksudi, tokea mwanzo alipochukua uongozi wa nchi ili kufanikisha lengo lake la kuiumiza nchi yetu. Nitaorodhesha mambo aliyoyafanya au kutoyafanya ili kufanikisha IGA hii iliyoletwa kwetu ifanikiwe. Kumbuka wakati wote, yeye anajua hakuna lolote wananchi wanaloweza kufanya kumzuia au kumuwajibisha sasa au baadae.

1. Uteuzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika eneo husika, na kuwaondoa viongozi ambao hawakukidhi mahitaji yake. Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara, Wakurugenzi TPA na kwingineko. Sitataja majina, kwani wanafahamika.
Hawa ni watu maalum walioteuliwa kuhakikisha lengo la IGA (mbovu) linafanikiwa.

2. Kufanya viini macho ili kupoteza lengo.
Paliwahi kuwepo mjadala wa kufufua mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, na yeye Rais aliwahi kueleza kuwa kuna timu ya majadiliano na waChina. Hili halikufika mbali, kabla ya kugeukia kwenye ujenzi wa hatua za mwanzo sisi wenyewe.

Wakati haya yakiendelea, imebainika sasa kwamba DPWorld tayari walikuwa kwenye kibarua cha kutengeneza IGA na wataalam wetu hapa ambao haijulikani walipatikana kwa mpango upi kushughulikia kazi hiyo. Bila shaka ni sahihi pia kusema kuwa ni watu walioaminiwa kutengeneza kitu alichokitaka mteuzi wao kwenye nafasi hiyo.

3. TICTS - abaki/asibaki? moja ya viini macho kuzuga watu, bila shaka hata wao TICTS hawakujua hatma yao itakuwa vipi. Wakati wote huu wa sintofahamu, DP World na wataalam wetu wapo kazini wakisuka IGA ya kutukomesha sisi.
4. Mara BUUUUU! DP World anaingia kwa kishindo kikubwa. Sasa ndipo watu wanaanza kuunganisha doti
Bendera yetu na picha ya Rais wetu juu ya jengo refu kabisa duniani; mara fununu za viongozi kwenda kwenye EXPO Dubai kimya kimya na Rais kukaa huko kwa siri kubwa, kumbe anatia saini mkataba wa kutuuza!

5. Mkataba unavujishwa? Juhudi kubwa zinaanza kufukia mahandaki. Hapana, huo siyo Mkataba, hayo ni "Makubaliano tu, ikiambatana na upotoshaji mwingi mwingine, toka kwa waziri na mtu mwingine aliyeaminiwa sana kusimamia kujua kilichomo ndani ya Mkataba/Makubaliano" hayo. Mtaalam wa sheria mbobezi (tunaambiwa), Hamza Johari ndiye mkuu wa timu. Watu wanajiuliza, na Mwanasheria mkuu wa Serikali alishiriki vipi hadi kufika kwenye hatua hii?
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hasemi kitu, bali kukanusha tu kwamba "Bandari haijauzwa". Hakuna anayejua kiwango cha ushiriki wake kwenye mkataba huo, na kama yeye, kwa nafasi yake anakubaliana na yaliyomo kwenye mkataba. Sijasikia akisema lolote juu ya hayo.

6. Taratibu na Hatua sahihi za kuingia mikataba kama huu (IGA) - Je, sisi kama taifa tunao utaratibu wowote tuliojiwekea wa kuingia kwenye mikataba kama hii? Huu siyo mkataba wa kwanza Tanzania iliouingia, je hiyo mingine kulifanyika mambo gani ambayo yamezoeleka kufanywa, lakini safari hii ikawa ni tofauti?

Hili ni swali lililo wazi, kama kuna utaratibu maalum, je ulifuatwa, hata kwa kiasi fulani tu?
jambo la kwanza linaloniingia akilini ni "Vikao vya Baraza la Mawaziri". Kwa mtizamo wangu, jambo kubwa kama hili haliwezi kufanyika bila ya uwepo wa angalao kikao cha Mawaziri kulijadili..
Vikao hivi vya Baraza la Mawaziri siku hizi vimekuwa kama ni siri kubwa sana, hata kule kutaja tu kulikuwepo na kikao siku hizi ni nadra sana, hata bila ya kutaja yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho.
Kwa hiyo hili ni swali tu kuuliza kama kulikuwa na kikao cha kujadili, au kujulishwa tu kwamba kuna mpango wa ujio wa DP World na hatua zilizokuwa zikifanyika kuwakaribisha hapa.
Kama Mawaziri nao hawakuwa na habari, hilo litakuwa jambo la kushangaza sana linaloongeza uzito katika hoja za andiko hili.
7. Ushirikishwaji wa Bunge katika "kuridhia Mkataba" Bila shaka yoyote palikuwepo na mpango kabambe wa kulishirikisha Bunge katika kufanya hujuma hizi, siyo kwa nia njema bali kwa nia ovu..
a) Kundi la wabunge lililopelekwa Dubai, ni utaratibu upi uliotumika kuwachagua hao waliokwenda? Wanazo sifa maalum ambazo zingewawezesha kutambua mambo ambayo hayana manufaa kwetu?
b) Waliandaliwa na kupewa semina wajiandae kuhusu maswala nyeti katika kazi wanayokwenda kuifanya huko walikokwenda? Walipewa Mkataba wausome wajue yaliyomo kabla hawajaondoka hapa?
Hawa wabunge ni akina nani hasa?

Kama maswali yote haya hayana majibu, maana yake ni kwamba hii ilikuwa ni mbinu tu, iliyotegeshwa kuhalalisha maovu juu ya nchi yetu, maovu waliyoyajua walioandaa mkataba huo na washirika wao wote.
c) Bungeni wakati wa kikao cha Bunge, ni wabunge wapi waliopewa nafasi ya kujadili yaliyomo kwenye mkataba, na ni nani aliyetoa nafasi hiyo kwa wabunge hao maalum? Hawa wabunge walijua kilichokuwemo kwenye huo Mkataba? Mbona hta mmoja wao hakujitokeza na anagalao kutaja tu hata kifungu kimoja alichokuwa nacho mashaka? Hawa wote waliandaliwa kwa maksudi kwa ushirikiano na uongozi wa Bunge?
d) Ushirikiwa wananchi, wanapewa masaa 24 kuleta maoni yao. Maana ya hili ni kwamba hapakutakiwa kuwepo na mchango wa wananchi ili lengo la kuhujumu nchi litekelezwe.

DPWorld wanao uzoefu mkubwa sana katika maswala haya ya Mikataba, kwa sababu kila sehemu walikokwenda wamekutana na chngamoto chungu nzima zilizowakabili.
Wamekuja hapa kwetu, wakamkuta mkuu wetu aliye tayari kabisa kuwapokea kwa masharti waliyoyapenda wao. Mkuu wetu hana uzoefu wowote, na isitoshe hana uchungu mkubwa kuhusu nchi anayoiongoza yeye, ila anayo madaraka ya kufanya lolote analotaka bila kuwajibishwa na yeyote.

Hapa ndipo tulipofikia sasa hivi.

Ingekuwa ni nchi nyingine, Mkataba huu usingemwacha huyu mkuu abaki salama, tena akiendelea kwenye madaraka yake kana kwamba hakuna lolote lililofanyika.
Lakini hii ni Tanzania. Yeye kishasema "Ameziba masikio", wenye kupiga kelele wapige kelele hadi wachoke wenyewe; lakini DP World hakuna wa kumzuia kuja hapa.

SAWA.
Sasa tumebaki na moja tu tunaloweza kulitegemea kuondokana na hujuma hii juu ya nchi yetu.
Je, tunaweza kumpata kichaa mwingine (bila ya baadhi ya mambo ya aliyetangulia mbele ya safari) atuondolee uchafu huu ndani ya nchi yetu? (Bila kujali hasara tutakayoingia kwa kuvunja mkataba (kwani kuendelea na mkataba wa aina hii ni hasara kubwa zaidi ya kulipa hiyo fidia tutakayodaiwa).
Na kwa kuwa ni 'kichaa', bila shaka baadhi ya hawa wahujumu watachukuliwa hatua bila ya kuwaonea aibu.

IGA baina ya Tanzania na Dubai ni hujuma iliyo andaliwa maksudi kuihujumu Tanzania.

N.B. Sikutegemea na wala siyo kawaida yangu kuandika gazeti, lakini leo acha iwe hivyo, kwani hakuna namna.

Samahani kwa makosa ya kiuandishi kama yamo kwenye andiko hili..
Ninaafiki kabisa. Ingefaa viongozi waliyohudika wafunguliwe mashitaka ya uhujumu uchumi.
 
Ninaafiki kabisa. Ingefaa viongozi waliyohudika wafunguliwe mashitaka ya uhujumu uchumi.
Katika hili la DP World, hili genge la Samia hata hawakujisumbua kuondoa wasiwasi kwa wananchi kuhusu ubaya ulionao mkataba huo, hata kwa kufanya juhudi za kupozapoza hapa na pale wananchi wasiwe na shaka.

Walichoamini wao ni kuwa Rais anayo mamlaka yote ya kupitisha jambo lolote na asihojiwe na mtu. Hili hawakuwa na mashaka nalo kabisa.
 
Napinga huo ujinga mnaoifanyia serikali ya SSH mpaka mnaingiza sera za udini na ubaguzi.

Hana anachokifanya ambacho watangulizi wake hawajawahi kukifanya. Na kwa kifupi anatimiza ilani ile ile aliyotimiza mtangulizi wake.
Inajulikana wazi sasa kwamba wewe ni mhusika wa karibu sana katika hujuma hii anayoifanyia Tanzania huyo Samia. Kuja kwako humu jamvini hakukusaidia chochote kuondoa wasiwasi huo, bali kunazidi kuchochea watu wakatae ujinga wenu.
Maswala ya Dini ni nyinyi mliokimbilia huko, sasa unataka kuyageuzia kwa wengine. Samia hana uwezo wa uongozi, nyinyi genge lake mmechukua fursa ya kumtumia kukidhi matakwa yenu.
Sasa mmemweka kwenye hali ngumu kisiasa; huku mkijua hata uwezo wa kutumia mabavu hana.
 
Sote tuanelewa kwamba nchi yetu Rais ni kila kitu kwetu, hahojiwi na mbaya zaidi huwezi kumshtaki mahakama yoyote nchini, akiwa madarakani au baada ya kuachia madaraka.


Kwa bahati nzuri kwake, na mbaya kwetu wengine fursa hiyo ikamwangukia bila ya mategemeo yoyote
Sasa anatimiza alichonuia toka siku nyingi.Hapa nataka kuonyesha mambo yaliyofanyika, kwa maksudi, tokea mwanzo alipochukua uongozi wa nchi ili kufanikisha lengo lake la kuiumiza nchi yetu.
Pitia jinsi alivyomaliza ''kero' za Wazanzibar haraka sana. Tazama solution yake, ilikuwa kuwabebesha Watanganyika mzigo tu. Pitia kero zote utabaini hakuna kero ilikuwa kuto Fadhila kwa Wazanzibar! hata ACT wanamkubali kwa hilo
1. Uteuzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika eneo husika, na kuwaondoa viongozi ambao hawakukidhi mahitaji yake. Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara, Wakurugenzi TPA na kwingineko. Sitataja majina, kwani wanafahamika.
Hawa ni watu maalum walioteuliwa kuhakikisha lengo la IGA (mbovu) linafanikiwa.
Hili lina ka ukweli. Kwanza, kamteua Mbarawa kuwa Waziri katika Wizara isiyo ya Muungano.
Pili, kamtoa Katibu mkuu wa Wizara ya masuala ya Muungano na kumpeleka Wizara ya Ujenzi ili wafanye kazi na Mbara.Waziri Mbarawa na Katibu Mkuu wake waliosaini Mkataba na DP ni Wazanzibar.

Hili si suala la Muungano na Rais anajua malalamiko ya Wazanzibar ni kuongezwa mambo kinyemela.
Kuwaweka Wazanzibar wasaini mikataba ya jambo LISILOWAHUSU kwa mujibu wao ndani ya Vikao vya Bunge inatia shaka sana. Wazanzibar wamekataa Bandari si suala la Muungano, iweje waingie makubailiano na suala lisilo wahusu! Hawawezi kuwa na uchungu na mali isiyowahusu nq wanaweza pia kutumia fursa hiyo vibaya.

Mwanasheria Mkuu hakuonekana mahali popote, kwahiyo Rais SSH akiwa Mzanzibar alimpa madaraka Mbarawa Mzanziar ashirikiane na Katibu Mkuu Mzanzibar kwa jambo lisilowahusu Wazanzibar! smell rat !

Mkataba umevujishwa na Wazalendo walioko jikoni !.


 
Mwanasheria Mkuu hakuonekana mahali popote, kwahiyo Rais SSH akiwa Mzanzibar alimpa madaraka Mbarawa Mzanziar ashirikiane na Katibu Mkuu Mzanzibar kwa jambo lisilowahusu Wazanzibar! smell rat !

Mkataba umevujishwa na Wazalendo walioko jikoni !.
DP World ni 'project' aliyoisimamia Samia toka mwanzo, hadi wakati Bendera yetu na picha zake zinawekwa kwenye jengo refu, tukiambiwa hatulipii chochote kwa vile "sisi ni watoto wazuri."
Wiki nzima kahamishia Ikulu yetu Dubai, kumbe anatengeneza hujuma juu ya nchi anayoiongoza.

Bungeni, kampa rushwa spika kwa uteuzi wa mme kuwa mwenyekiti wa EWURA kwa maksudi mazima ili Spika atimize lengo lililopangwa kuridhia IGA.
Akina Msukuma na watu wa aina hiyo wakaandaliwa kwa maksudi kabisa, kuwa mstari wa mbele kupigia kelele uzuri wa DP Word na mikataba yake ya hujuma.

Kwa hiyo, kila jambo lilikuwa limepangwa kwa uangalifu toka mwanzo, hapa hapakuwepo na bahati mbaya, au kutojua kinachofanyika, kama watu walivyozoea kupotosha wengine.

Huu ulikuwa ni mpango mahsusi wa Samia pamoja na genge lake lilomshikilia kumtumia kuiumiza nchi yetu
 
Back
Top Bottom