Mkataba wa kazi maalumu

Mkataba wa kazi maalumu

Dashdown

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
403
Reaction score
442
Habari za muda huu ndugu wanasheria

Tafadhali naomba kupata ufafanuzi je sheria inaongelea nini kwenye mkataba wa kazi maalumu.
 
Habari za muda huu ndugu wanasheria

Tafadhali naomba kupata ufafanuzi je sheria inaongelea nini kwenye mkataba wa kazi maalumu.
Kazi maalumu ndo kazini gani ? [emoji15][emoji15]
 
Habari za muda huu ndugu wanasheria

Tafadhali naomba kupata ufafanuzi je sheria inaongelea nini kwenye mkataba wa kazi maalumu.

Hapa lazima useme sheria inaongelea nini kwa mkataba wa muda maalumu yani lengo lako ni lipi kujua kati ya haya

1. Termination grounds yani kusitishwa kwakwe kutafatwa sababu zipi
2. Terminal benefits yani kipi unastahili kulipwa baada ya mkataba wa muda maalumu kuisha
3. Je ukivunjwa kimakosa au kikiukwa kimakosa nini kifanyike au kipi cha kufanya

swali lako lipo kiujumla sana ulitakiwa uelezee hali halisi ila kwa msaada zaidi unaweza kupitia hivi 1. employment and labou relation act 2004, code of good practice 2007, contract for service hizi pitia pitia mifano yake uone inakuaje kitu chake chepesi kama vile kampuni ya ujenzi inapotaka huduma ya ulinzi inaweza kuchukua kampuni ya ulinzi ili ipate huduma ya ulinzi aina yake ya kimakubaliano kidogo inakuwa tofauti hivyo hivyo kuna baadhi ya makampuni na taasisi zina huo mtindo wa kutoa contract for service
 
Naomba pia kuuliza
Je, Internship program ina fit kwenye definition of employment au sio employment
 
Naomba pia kuuliza
Je, Internship program ina fit kwenye definition of employment au sio employment

sio employment ila wanaweka kama program maalumu kuelekea kwenye ajira na huwa ina format yake ambayo pande zote mbili huwa wanaweka sahihi ya makubaliano hayo kwamba ni ukifuzu utapatiwa ajira ila sio lazima ngoja nilete format yake nikitulia huwa ina content tofauti kabisa na content za mkataba wa ajira
 
Hapa lazima useme sheria inaongelea nini kwa mkataba wa muda maalumu yani lengo lako ni lipi kujua kati ya haya

1. Termination grounds yani kusitishwa kwakwe kutafatwa sababu zipi
2. Terminal benefits yani kipi unastahili kulipwa baada ya mkataba wa muda maalumu kuisha
3. Je ukivunjwa kimakosa au kikiukwa kimakosa nini kifanyike au kipi cha kufanya

swali lako lipo kiujumla sana ulitakiwa uelezee hali halisi ila kwa msaada zaidi unaweza kupitia hivi 1. employment and labou relation act 2004, code of good practice 2007, contract for service hizi pitia pitia mifano yake uone inakuaje kitu chake chepesi kama vile kampuni ya ujenzi inapotaka huduma ya ulinzi inaweza kuchukua kampuni ya ulinzi ili ipate huduma ya ulinzi aina yake ya kimakubaliano kidogo inakuwa tofauti hivyo hivyo kuna baadhi ya makampuni na taasisi zina huo mtindo wa kutoa contract for service
Ningependa kujua termination benefits baada ya mkataba wa muda maalumu kuisha.
 
Ningependa kujua termination benefits baada ya mkataba wa muda maalumu kuisha.

Sasa hapo napo nashindwa kusema jibu la moja kwa moja kwa sababu mkataba kuisha unaweza kuisha kwa sababu 1. muda wake umeisha 2. Shughuli mliyokuwa mnafanya imekwama kwa sababu mbalimbali za kiuendeshaji hivyo kuna ulazima wa kupunguza nguvu kazi 3. Ukiwa katika huo mkataba kama ukikiuka matwaka ya msingi ya mkataba au mwenendo mbaya pia mkataba huo unaweza kufika mwisho 4 Kwa makubaliano inaweza ikafika muda muajiri wako anakuita mezani bwana huu mkataba wetu ufike mwisho mnamalizana kitaamu wanaita TERMINATION BY AGREEMENT SETTLEMENT OF DISPUTE hii ndo inalipa zaidi maana unakuta unamkataba wa miaka 3 alafu umetumikia mmoja .

sasa basi terminationan benefits hutegemea na hali halisi ila kawaida yanakuwa yafuatayo

1. Mshahara wa siku ulizofanya kazi
2. Notice ya siku 28 hii kama ukipewa taarifa siku 28 kabla inakuwa haulipwi unapewa kitu kinaitwa non renew of the contract notice
lengo la hiki kitu ni hivi code of good practice 2007 yani kanuni za ajira na mahusiano kazini mwaka 2007 inasema kwamba mfanyakazi anaweza kuwa na matumaini ya kupata mkataba mpya tena baada ya ule wa muda maalumu kufika mwisho ikiwa ile kazi inaendelea sasa kukwepa shida za kisheria na kupelekana CMA ndio maana huwa wanatoa hizi mapema maana ukichelewa hata siku moja sheria inatambua ule mkataba umekuwa automatic renew
3. likizo kama unamalimbikizo
4 kiinua mgongo hii ni mshahara wa siku 7 kwa idadi ya miaka uliyotumikia mfano mshahara wako wa siku ni 70,000 maana yake utafanya hivi 70,000*7 =490,000 utazidisha idadi ya miaka uliyokaa mfano miaka miwili utaizidisha kama ilivyo ila
haitakiwi kuvuka miaka 10 na lazima uwe umetumikia angalau mwaka 1
5 posho ya usafiri mfano uliajiriwa dar ukapelekwa branch ya arusha itabidi wagaramie swala la wewe kurudi dar ila muhimu kusoma kitu kinaitwa place of recruitment ipo kwenye mkataba wako

6. cheti cha utumishi yani cerificate of service
 
Asante sana nitakufata PM kwa msaada zaidi
 
Back
Top Bottom