Mkataba wa kishenzi ni marufuku Tanzania, kama wana dhamira njema, mazungumzo yaanze upya

Kwa nini usiende kulalamika kwa Mbunge wenu Kenan (yule Mdada Mfipa wa Sumbawanga) au kwa kina Halima 19? Mpigangumi ukutani huumiza mkonowe. CCM walishinda Uchagizi 2020 bita sinira uwaache nao watekeleze Ilani yao.
 
Kama hawayumbishwi na maneno ya mitandaoni mbona ameshayajibu?

Kama kweli hayumbishwi anyamaze kimya.

Samia katupeleka utumwani.
Sasa Kama mmeshindwa kujisimamia mnataka Samia afanye nini!? Akiwatumbua Kama alivyokua anawatumbua Magufuli,bado na yeye mtamwita Dikteta,bora Mama wa Watu kaamua kuwauza utumwani ili mkasimamiwe na wageni Kama mlivyozowea! Na naomba Mama aendelee na mwendo huu huu, kila taasisi ikishindwa kujisimamia yenyewe ni mwendo wa kumpa Muwekezaji hadi tutie akili ya kujisimamia wenyewe bila ya shuruti!!
 
Kwa kweli SSH sina hamu nae........bandari Hapana Hapana Hapana Hapana tuongee upya
 
Tatizo letu kubwa siyo bandari, siyo ATCL, siyo TANESCO, BALI NI UBOVU NA ULEGEVU WA SERIKALI, AMBAYE NDIYE MSIMAMIZI MKUU. Na ubovu huu wa Serikali haujaanza wakati wa Rais Samia, umekuwepo wakati wote, na unaendelezwa mpaka sasa.
100% 👍
 
Jf ni ya Wapinzani tukaneni mnavyoweza
Wapinzani ni watu gani? Maana hata wewe ni mpinzani. Kila binadamu kwa wakati fulani ni mpinzani.

Kama unamaanisha JF ni ya wapinzani wa ufisadi, wizi, mikataba mibovu na mabaya mengine mengi, basi pongezi nyingi kwa uongozi wa JF na wanaJF.

Binadamu kwa asili yake ni mpinzani wa uovu, lakini kuna wakati hulka, tamaa, ubinafsi na mazingira yake, humbadilisha na kuwa mpinzani wa wema na mwungaji mkono wa uovu.
 
Ujanja wa hawa maponjoro wanajua hadi leo waswahili hatunazo. Dewji alituambia anawekeza simba billioni 20 hadi leo amewekeza kile amepata simba tu🤣😂🤣.
Hatujui kala ngapi.🚶🏻‍♂️🚶🏻‍♂️
 
Walioko bandarini vipi waarabu washafika huko?
 
Naunga mkono hoja. Sauti ziendelee kupazwa na ikiwezekana tufanye migomo baridi nchi nzima kushinikiza hawa wahuni walioshindwa kusimamia bandari yetu wakaona njia rahisi ni kuiuza waachie ngazi
 
Kuna tetesi wafanyakazi Wa bandari(wale waajiriwa) wameambia wachague kubaki kwa mwarabu au wapelekwe serikali kuu daaah!! Tz my country nn kinakupata!!
 
Yeye ndio ameshindwa kuisimamia bandari ilete matokeo chanya yafaa ang'atuke na sio kuuza uza

Nasikitika kusema wanawake sio watu wa kupewa madaraka makubwa .
"Ni bora kumpa mwanaume mlevi madaraka makubwa lakini sio mwanamke" period
 
Mbona uliwekwa hapa jukwaani, hukuuona? Itabidi niupandishe kama mada inayojitegemea. Labda kwa vile unapandishwa, katikati ya habari, wengine wanapitwa.
Ni kweli mkuu, nifanyie wepesi hata Pm
 
Rejea kichwa cha mada chahusika.

Tanzania haitapoa, hadi mikataba ya kishenzi, mikataba ya kipumbavu aidha ifutwe, au ianze upya.

Hatuko tayari kuja kusemwa vibaya na vizazi vyetu kama tunavyowasema kina Mangungo wa Msovero.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…