Kwa unyenyekevu mkubwa sana "ninadhani" uelewa wako (juu ya jambo hili) "unaweza" kuwa ni mdogo mkuu.
Azam TV (kama muonyeshaji wa ligi) anahusika kwenye matangazo au mabango yanayoandaliwa na TFF au bodi ya ligi kuhusiana na mechi za ligi hiyo.
Mfano Press za timu (bodi ya ligi ndio inaziandaa) zinazofanyika siku moja kabla ya michezo husika ya ligi zikihusisha makocha na manahodha.
Ila kwa sababu kwenye hili jambo umeonyesha "kuchanganya madawa" tangu mwanzo, basi mimi najitolea
kukujengea uwezo.
Chini ya hili wasilisho langu nitakuwekea bango la Simba Sc linaloutambulisha mchezo wa
Orlando Pirates vs Simba uliochezwa pale Afrika ya kusini. Kwenye bango hilo, hakika utamuona huyo Azam TV akiwa ameambatana na "wadhamini wenzake" 7 wa Simba.
Wewe kazi yako itakua rahisi tu, unieleze Je, Orlando Pirates na Simba walicheza mechi ambayo ni ya
ligi kuu chini ya TFF (wenye mkataba na Azam TV wa kuonyesha ligi kuu). ???
Halafu kitu kingine ni kwamba, ndugu yangu
CARDLESS , unatakiwa kufahamu kuwa kwenye "context" ya udhamini wa ligi,
Azam TV anatakiwa kuambatana na
TBC Fm pamoja na
NBC (Zamani na GSM alikua anaingia hapa kabla hajajiondoa kudhamini ligi) katika hilo bango. Tazama picha hii hapa chini.
View attachment 2297634
Unatakiwa kufahamu kwamba:
1. Azam TV ana mkataba na bodi ya ligi (kuonyesha ligi).
2. Azam TV ana mkataba na Yanga (kuonyesha maudhui mbalimbali ya klabu)
3. Ana mkataba na Simba (wa kuonyesha maudhui mbalimbali ya klabu hiyo mfano Press conferences, matamasha kama vile Simbaday, events kadhaa za preseason kwa mfano sasa hivi Patrick Nyembela na crew ya Azam TV wapo kule Ismailia Misri, na mengineyo mengi).
Mikataba hiyo mitatu kila mmoja unajitegemea, tafadhali sana usichangaye mambo hapo.
View attachment 2297630
NB: Lengo sio kubishana, ni kuelimishana. Karibu.