Mkataba wa Simba na Sportpesa ulikuwa dhaifu

Hapo kabla ulikuwa umeolewa! Baadaye ukaanza kumlalamikia mumeo hafai! Anakupa fedha kidogo tu ya matumizi!

Hivyo ukaona bora uombe talaka! Ukapewa. Ndani ya muda mfupi tu, ukapata mwanaume mwingine wa ndoto yako! Ukaolewa naye ili maisha yaendelee! Lakini cha kushangaza baada ya kuolewa, kila siku ni kumlalamikia tu yule mume wako wa zamani mbele za watu, huku ukiwa tayari katika ndoa na mwanaume mwingine.

Samahani bosi pwilo, nimeona nitumie mfano huu ili maoni yangu yaeleweke kwa uzuri zaidi. Maneno mwanamke na mwanaume yametumika kufikisha tu ujumbe. Hayahusiani kabisa na wewe
Unamaanisha Yule msemaji wa Taifa yule
TKT maji Mkuu?
 
Tarimba anakubaliana na simba kwamba watapata hela nyingi kuliko yanga halafu akifika jangwani anabadilisha kibao anawapa yanga dau kubwa kuliko simba kwasababu ya ushabiki wakati simba anawakilisha kimataifa simba walikuwa wavunje mkataba ila wakasubiria mpaka uishe ila alichofanya tarimba kwa simba ni ujinga wawape yanga hzo hela tuone watafika wapi CAF champion's league.
Yaani kupata hela nyingi kuliko yanga ndio sababu ya kumshawishi mdhamini. Labda mngesema mdhamini anapata mileage kiasi na faida kiasi gani kuweka logo yake kwa simba . Huwezi weka mikataba kwa kuangalia yanga . Walikua wanafanya negotiations walikua na mapungufu
 
Tanzania yan tunashindwa kubaini mambo madogo kama haya? Hivi miaka ijayo tutakuwa wazee wa namna gani katika jamii inayotuzunguka?
 
Labda wewe ulikuwa ufahamu lakini wengi tulikuwa tunajua kwamba msimu huu ni mwisho wa mkataba
Kwanini klabu imeendelea kutengeneza jezi?Na sisi washabiki tunaendelea kununua jezi za mdhamini ambaye kwa sasa hadaidii chochote...kama mkataba wa Mbet ungesainiwa miaka miwili iliyopita utaratibu wa kusitisha mkataba ungefanyika bila kuleta athari kwa wadau wengine...Sasa hizo jezi alizozalisha Vunja bei mtamlipa?
 
Aisee nimesikitika sana kumbe na wewe huna akili unabweka tu nenda kawaulize Azam kama hawalipii hiyo Liverpool tv
Liverpool TV pale Azam wana mkataba na Azam tv??????????

Yanga wana mkataba na Azam media kwenye haki za matangazo yao yote.

Au huelewi mikataba inayazungumzwa hapo?? Afu mtu anasema angalia chini hapo uone wadhamini aishiiiiiiiiiii hao Azam wana mkataba na TFF kwenye kuonesha ligi kuu, hivyo lazima tangazo lao liwepo kwenye kila page ya timu ya ligi kuu.
 
Kwa unyenyekevu mkubwa sana "ninadhani" uelewa wako (juu ya jambo hili) "unaweza" kuwa ni mdogo mkuu.
Azam TV (kama muonyeshaji wa ligi) anahusika kwenye matangazo au mabango yanayoandaliwa na TFF au bodi ya ligi kuhusiana na mechi za ligi hiyo.
Mfano Press za timu (bodi ya ligi ndio inaziandaa) zinazofanyika siku moja kabla ya michezo husika ya ligi zikihusisha makocha na manahodha.

Ila kwa sababu kwenye hili jambo umeonyesha "kuchanganya madawa" tangu mwanzo, basi mimi najitolea kukujengea uwezo.
Chini ya hili wasilisho langu nitakuwekea bango la Simba Sc linaloutambulisha mchezo wa Orlando Pirates vs Simba uliochezwa pale Afrika ya kusini. Kwenye bango hilo, hakika utamuona huyo Azam TV akiwa ameambatana na "wadhamini wenzake" 7 wa Simba.

Wewe kazi yako itakua rahisi tu, unieleze Je, Orlando Pirates na Simba walicheza mechi ambayo ni ya ligi kuu chini ya TFF (wenye mkataba na Azam TV wa kuonyesha ligi kuu). ???

Halafu kitu kingine ni kwamba, ndugu yangu CARDLESS , unatakiwa kufahamu kuwa kwenye "context" ya udhamini wa ligi, Azam TV anatakiwa kuambatana na TBC Fm pamoja na NBC (Zamani na GSM alikua anaingia hapa kabla hajajiondoa kudhamini ligi) katika hilo bango. Tazama picha hii hapa chini.

Screenshot_20220720-134603_Instagram.jpg

Unatakiwa kufahamu kwamba:
1. Azam TV ana mkataba na bodi ya ligi (kuonyesha ligi).
2. Azam TV ana mkataba na Yanga (kuonyesha maudhui mbalimbali ya klabu)
3. Ana mkataba na Simba (wa kuonyesha maudhui mbalimbali ya klabu hiyo mfano Press conferences, matamasha kama vile Simbaday, events kadhaa za preseason kwa mfano sasa hivi Patrick Nyembela na crew ya Azam TV wapo kule Ismailia Misri, na mengineyo mengi).

Mikataba hiyo mitatu kila mmoja unajitegemea, tafadhali sana usichangaye mambo hapo.

Screenshot_20220720-134049_Instagram.jpg

NB: Lengo sio kubishana, ni kuelimishana. Karibu.
 
Kwenye hatua ya awali na hatua ya kwanza zinavaliwa. Katazo ni kuanzia hatua ya makundi kuendelea mbele.

Hapa chini ni sportpesa "wakiuza sura" kwenye "viuga mbalimbali barani Afrika"

View attachment 2297405View attachment 2297408
Upo sahihi, ila kumbuka hatua zile mbili yaani ya awali na ya pili ni kwamba hata official broadcastiing wa CAF hashughuliki nayo na hata sponsors wa CAF hawahusiki, ni level ya chini sana ya kimashindano
 
Nafahamu, lakini bado ni "kimataifa"
 
Last time I checked Simba wana:
1. VunjaBei
2. Mo29
3. Mo Extra
4. ATCL
5. Emirates Aluminium
6. Africarriers
7. Azam Media
8. M-Bet

Kama hawa wameletwa kwa "chuki za Mo", basi kumbe hizo ni Chuki zenye manufaa
Sasa hao si ni sawa ni viberiti vya njiti tu sekunde 30 kana zima. ATCL mwenyewe ana loss za Billions. Giant hapo ni Azam tu.
 
M-Bet ni kampuni ya kichovu tu, chuki za MO ni kama mwanamke hivi, yaani yeye ugomvi personal anauingiza kwenye Biashara.

YANGA wenzao wana wadhamini
1. TAIFA GAS
2. MAJI YA AFYA
3. GSM
4. AZAM MEDIA
5. SPORTPESA

Afu bado watapata udhamini mpya hivi karibuni.

MO aachane na biashara za chuki kwa wenzake ana ajikite katika maboresho ya bidhaa zake.
M BET kaweka pesa ya maana , ni ukichaa kuikumbatia Sportpesa
 
Sasa hao si ni sawa ni viberiti vya njiti tu sekunde 30 kana zima. ATCL mwenyewe ana loss za Billions. Giant hapo ni Azam tu.
Nadhani udogo au ukubwa (wa mdhamini), hasara au faida anayoingiza (mdhamini) havimhusu sana mdhaminiwa endapo matakwa ya kimkataba katika udhamini yanatimizwa.
Na pia katika biashara hasara ni kitu cha kawaida kabisa.
 
Kwa unyenyekevu mkubwa sana "ninadhani" uelewa wako (juu ya jambo hili) "unaweza" kuwa ni mdogo mkuu.
Azam TV (kama muonyeshaji wa ligi) anahusika kwenye matangazo au mabango yanayoandaliwa na TFF au bodi ya ligi kuhusiana na mechi za ligi hiyo.
Mfano Press za timu (bodi ya ligi ndio inaziandaa) zinazofanyika siku moja kabla ya michezo husika ya ligi zikihusisha makocha na manahodha.

Ila kwa sababu kwenye hili jambo umeonyesha "kuchanganya madawa" tangu mwanzo, basi mimi najitolea kukujengea uwezo.
Chini ya hili wasilisho langu nitakuwekea bango la Simba Sc linaloutambulisha mchezo wa Orlando Pirates vs Simba uliochezwa pale Afrika ya kusini. Kwenye bango hilo, hakika utamuona huyo Azam TV akiwa ameambatana na "wadhamini wenzake" 7 wa Simba.

Wewe kazi yako itakua rahisi tu, unieleze Je, Orlando Pirates na Simba walicheza mechi ambayo ni ya ligi kuu chini ya TFF (wenye mkataba na Azam TV wa kuonyesha ligi kuu). ???

Halafu kitu kingine ni kwamba, ndugu yangu CARDLESS , unatakiwa kufahamu kuwa kwenye "context" ya udhamini wa ligi, Azam TV anatakiwa kuambatana na TBC Fm pamoja na NBC (Zamani na GSM alikua anaingia hapa kabla hajajiondoa kudhamini ligi) katika hilo bango. Tazama picha hii hapa chini.

View attachment 2297634

Unatakiwa kufahamu kwamba:
1. Azam TV ana mkataba na bodi ya ligi (kuonyesha ligi).
2. Azam TV ana mkataba na Yanga (kuonyesha maudhui mbalimbali ya klabu)
3. Ana mkataba na Simba (wa kuonyesha maudhui mbalimbali ya klabu hiyo mfano Press conferences, matamasha kama vile Simbaday, events kadhaa za preseason kwa mfano sasa hivi Patrick Nyembela na crew ya Azam TV wapo kule Ismailia Misri, na mengineyo mengi).

Mikataba hiyo mitatu kila mmoja unajitegemea, tafadhali sana usichangaye mambo hapo.

View attachment 2297630

NB: Lengo sio kubishana, ni kuelimishana. Karibu.
Hiyo chata ya Azam iko hapo ikiwa ndio imepewa haki ya kuonesha hiyo game sio kwamba ni mdhamini wa Simba mzee acha kujitoa ufahamu.
 
Sportpesa 1B kwa mwaka, M bet 3B kwa mwaka, ni kichaa pekee ndio atakumbatia Sportpesa
Billion 3 ni maneno tu. Tangazo la mdhamini la Simbs Sc club halina pesa. Ni siri[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hapo kabla ulikuwa umeolewa! Baadaye ukaanza kumlalamikia mumeo hafai! Anakupa fedha kidogo tu ya matumizi!

Hivyo ukaona bora uombe talaka! Ukapewa. Ndani ya muda mfupi tu, ukapata mwanaume mwingine wa ndoto yako! Ukaolewa naye ili maisha yaendelee! Lakini cha kushangaza baada ya kuolewa, kila siku ni kumlalamikia tu yule mume wako wa zamani mbele za watu, huku ukiwa tayari katika ndoa na mwanaume mwingine.

Samahani bosi pwilo, nimeona nitumie mfano huu ili maoni yangu yaeleweke kwa uzuri zaidi. Maneno mwanamke na mwanaume yametumika kufikisha tu ujumbe. Hayahusiani kabisa na wewe
Mfano huu unamfaa sana Manara!
 
Back
Top Bottom