Ng'wanza Madaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2008
- 2,268
- 335
Hili shirika letu la reli silielewi. Nadhani kuna elements nyingi za ufisadi ndani yake na sasa shirika linaelekea kufa kutokana na utendaji mbovu. Sijui sana kuhusu uendeshaji wa hili shirika letu la reli labda kuna wadau humu wanajua zaidi.
Sikubaliani na Zitto kuwa serikali inashindwa kutekeleza mapendekezo ya kamati za bunge;ukweli ni kwamba serikali inauwezo wa kutekeleza mapendekezo, lakini HAITAKI kufanya hivyo ili kulinda maslahi ya viongozi serikalini!! Mfano mzuri ni huu wa mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya bunge kuhusu Richmond; mengi ya mapendekezo yake hayahitaji fedha bali ni kuchukua hatua za kinidhamu lakiniwapi Muungwana ameamua kuwa haadhibiwi mtu hapa!!Na Eckland Mwaffisi
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Bw. Zitto Kabwe amesema kusuasua kwa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kumechangiwa na idadi ndogo ya wawekezaji waliojitokeza kuomba zabuni kuendesha reli hiyo, hivyo kuifanya Serikali kukosa mbadala na kumua kuipa Kampuni ya RITES kutoka India kwa mtindo wa 'hakuna namna.'
Bw. Zitto aliyasema hayo Dar es Salaam jana, wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na kipindi cha Mambo Leo, kinachorushwa na Kituo cha Times 100.5 fm
Alisema migogoro mbalimbali ya wafanyakazi inayoendelea TRL, inachangiwa na mwekezaji, Kampuni ya RITES kushindwa kuboresha huduma wanazotoa katika kiwango kilichoratajiwa na kuongeza kuwa kampuni imeshindwa hata kuboresha usafiri wa mizigo na abiria hadi sasa.
Alifafanua kuwa, pamoja na Serikali kumiliki asilimia 49 na RITES asilimia 51, Serikali imeendelea kubeba mzigo mzito zaidi kuliko kampuni hiyo ambayo wananchi waliamini ingeleta mabadiliko makubwa kwa kuboresha huduma hizo.
Alieleza kuwa katika mchakato wa kutangaza zabuni ya uuzaji Shirika la Reli Tanzania (TRC), kampuni mbili tu ndizo zilijitokeza ambazo ni RATES ya India na mwekezaji mwingine kutoka Afrika Kusini ambaye hata hivyo alijitoa hatua za mwisho hivyo kuifanya Serikali kukosa namna na kuingia mkataba na mwekezaji aliyebaki(RITES) .
Sababu kubwa ya mlundikano makontena bandarini ni huduma mbovu zinazotolewa na TRL, nchi mbalimbali duniani, hutumia usafiri wa treni kusafirisha mizigo yao tofauti na Tanzania hivi sasa ambayo haina huduma hiyo pamoja na kuwepo mwekezaji aliyepewa shirika hilo, alisema.
Alidai kuwa mwaka 1996, Serikali ilifanya maamuzi mabovu kubinafsisha mashirika ya umma na kwamba yalikuwepo mashirika ambayo hayakupaswa hata kufikiriwa kuingizwa katika mchakato wa kubinafsishwa.
Alitoa mfano wa Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwamba haikupaswa kuingizwa katika mpango huo zaidi ya kufanyika mabadiliko ya uwekezaji kutoka serikalini.
Alisema Tanzania imebahatika kwa kuwa na nishati nyingi ya gesi na mafuta ambayo kama TANESCO itaongezewa nguvu na uwezo wa kuzitumia nishati hizo, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika kutoa huduma ya umeme na kulifanya shirika hilo kujiendesha kwa faida.
"Mwaka 2006 TANESCO ilipata hasara ya sh. bilioni 167 ikiwa chini ya usimamizi wa Net Group Solution, ambayo baada ya kumaliza mkataba wake, uongozi mpya chini ya Serikali uliweza kupunguza hasara hiyo kutoka sh. bilioni 167 hadi sh. bilioni 62. Kufikia Desemba 2008, hasara hiyo imepungua kutoka sh. bilioni 62 mpaka bilioni 30," alisema.
Alisema Serikali haipaswi kuuza shirika hilo zaidi ya kuliboresha kwa kuzingatia mapendekezo ya kamati yake ikiwa ni pamoja na kuuza hisa zake katika soko la hisa.
Bw. Zitto alisema, Kamati yake ilipendekeza kusitishwa zoezi la ubinafsishaji ili kufanya tathimini na kurekebisha makosa yaliyojitokeza, kwani alidai ubinafshaji uliofanywa nchini kuanzia mwaka 1996, umesababisha mali nyingi za umma kupotea na kunufaisha wachache.
Alitoa mfano mwingine kuwa, Shirika la Ndege Tanzania (ATC),lipo mahututi kiasi cha kuzidiwa na kampuni binafsi ya Precision Air,inayotoa huduma zenye ushindani kibiashara katika soko.
Kamati yangu imetoa pendekezo kwa Serikali, kuipa mtaji wa kutosha ATC ili iweze kutoa huduma zake kwa ubora zaidi na kujiendesha kwa faida ikiwa ni pamoja na kuimarisha viwanja vya ndege katika miji mikubwa na midogo na kuingia katika ushindani wa soko la kibiashara, alisema.
Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya marubani wa ndege za Serikali wamezeeka hivyo ni jukumu la Serikali kuwawezesha kielimu marubani wapya ili kuongeza ufanisi wa shirika hilo.
Alisema, pamoja na mapendekezo mengi yanayotolewa na kamati yake, historia inaonesha kuwa, kwa nchi nyingi duniani Serikali imekuwa ikishindwa kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na Kamati za Bunge.
Alisema, mfano mzuri wa mapendekezo hayo ni yale yaliyotolewa na Kamati ya Bunge kuhusu Richmond iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe lakini hadi sasa Serikali imeshindwa kuyafanyia kazi.
Source: Majira
Hili shirika letu la reli silielewi. Nadhani kuna elements nyingi za ufisadi ndani yake na sasa shirika linaelekea kufa kutokana na utendaji mbovu. Sijui sana kuhusu uendeshaji wa hili shirika letu la reli labda kuna wadau humu wanajua zaidi.
Sikubaliani na Zitto kuwa serikali inashindwa kutekeleza mapendekezo ya kamati za bunge;ukweli ni kwamba serikali inauwezo wa kutekeleza mapendekezo, lakini HAITAKI kufanya hivyo ili kulinda maslahi ya viongozi serikalini!! Mfano mzuri ni huu wa mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya bunge kuhusu Richmond; mengi ya mapendekezo yake hayahitaji fedha bali ni kuchukua hatua za kinidhamu lakiniwapi Muungwana ameamua kuwa haadhibiwi mtu hapa!!
Waliotaka kuwekeza walikuwepo pia Rift Valley ya South africa ambao wamechukua Kandrasi hiyo Kenya na Uganda na hatusiki kelele huko kama kwetu. Na pia nilisikia Wajerumani walitaka kuichukua hiyo kandarasi ya kuiendesha hiyo Reli.Na Eckland Mwaffisi
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Bw. Zitto Kabwe amesema kusuasua kwa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kumechangiwa na idadi ndogo ya wawekezaji waliojitokeza kuomba zabuni kuendesha reli hiyo, hivyo kuifanya Serikali kukosa mbadala na kumua kuipa Kampuni ya RITES kutoka India kwa mtindo wa 'hakuna namna.'
Bw. Zitto aliyasema hayo Dar es Salaam jana, wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na kipindi cha Mambo Leo, kinachorushwa na Kituo cha Times 100.5 fm
Alisema migogoro mbalimbali ya wafanyakazi inayoendelea TRL, inachangiwa na mwekezaji, Kampuni ya RITES kushindwa kuboresha huduma wanazotoa katika kiwango kilichoratajiwa na kuongeza kuwa kampuni imeshindwa hata kuboresha usafiri wa mizigo na abiria hadi sasa.
Alifafanua kuwa, pamoja na Serikali kumiliki asilimia 49 na RITES asilimia 51, Serikali imeendelea kubeba mzigo mzito zaidi kuliko kampuni hiyo ambayo wananchi waliamini ingeleta mabadiliko makubwa kwa kuboresha huduma hizo.
Alieleza kuwa katika mchakato wa kutangaza zabuni ya uuzaji Shirika la Reli Tanzania (TRC), kampuni mbili tu ndizo zilijitokeza ambazo ni RATES ya India na mwekezaji mwingine kutoka Afrika Kusini ambaye hata hivyo alijitoa hatua za mwisho hivyo kuifanya Serikali kukosa namna na kuingia mkataba na mwekezaji aliyebaki(RITES) .
Sababu kubwa ya mlundikano makontena bandarini ni huduma mbovu zinazotolewa na TRL, nchi mbalimbali duniani, hutumia usafiri wa treni kusafirisha mizigo yao tofauti na Tanzania hivi sasa ambayo haina huduma hiyo pamoja na kuwepo mwekezaji aliyepewa shirika hilo, alisema.
Alidai kuwa mwaka 1996, Serikali ilifanya maamuzi mabovu kubinafsisha mashirika ya umma na kwamba yalikuwepo mashirika ambayo hayakupaswa hata kufikiriwa kuingizwa katika mchakato wa kubinafsishwa.
Alitoa mfano wa Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwamba haikupaswa kuingizwa katika mpango huo zaidi ya kufanyika mabadiliko ya uwekezaji kutoka serikalini.
Alisema Tanzania imebahatika kwa kuwa na nishati nyingi ya gesi na mafuta ambayo kama TANESCO itaongezewa nguvu na uwezo wa kuzitumia nishati hizo, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika kutoa huduma ya umeme na kulifanya shirika hilo kujiendesha kwa faida.
"Mwaka 2006 TANESCO ilipata hasara ya sh. bilioni 167 ikiwa chini ya usimamizi wa Net Group Solution, ambayo baada ya kumaliza mkataba wake, uongozi mpya chini ya Serikali uliweza kupunguza hasara hiyo kutoka sh. bilioni 167 hadi sh. bilioni 62. Kufikia Desemba 2008, hasara hiyo imepungua kutoka sh. bilioni 62 mpaka bilioni 30," alisema.
Alisema Serikali haipaswi kuuza shirika hilo zaidi ya kuliboresha kwa kuzingatia mapendekezo ya kamati yake ikiwa ni pamoja na kuuza hisa zake katika soko la hisa.
Bw. Zitto alisema, Kamati yake ilipendekeza kusitishwa zoezi la ubinafsishaji ili kufanya tathimini na kurekebisha makosa yaliyojitokeza, kwani alidai ubinafshaji uliofanywa nchini kuanzia mwaka 1996, umesababisha mali nyingi za umma kupotea na kunufaisha wachache.
Alitoa mfano mwingine kuwa, Shirika la Ndege Tanzania (ATC),lipo mahututi kiasi cha kuzidiwa na kampuni binafsi ya Precision Air,inayotoa huduma zenye ushindani kibiashara katika soko.
Kamati yangu imetoa pendekezo kwa Serikali, kuipa mtaji wa kutosha ATC ili iweze kutoa huduma zake kwa ubora zaidi na kujiendesha kwa faida ikiwa ni pamoja na kuimarisha viwanja vya ndege katika miji mikubwa na midogo na kuingia katika ushindani wa soko la kibiashara, alisema.
Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya marubani wa ndege za Serikali wamezeeka hivyo ni jukumu la Serikali kuwawezesha kielimu marubani wapya ili kuongeza ufanisi wa shirika hilo.
Alisema, pamoja na mapendekezo mengi yanayotolewa na kamati yake, historia inaonesha kuwa, kwa nchi nyingi duniani Serikali imekuwa ikishindwa kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na Kamati za Bunge.
Alisema, mfano mzuri wa mapendekezo hayo ni yale yaliyotolewa na Kamati ya Bunge kuhusu Richmond iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe lakini hadi sasa Serikali imeshindwa kuyafanyia kazi.
Source: Majira
Hili shirika letu la reli silielewi. Nadhani kuna elements nyingi za ufisadi ndani yake na sasa shirika linaelekea kufa kutokana na utendaji mbovu. Sijui sana kuhusu uendeshaji wa hili shirika letu la reli labda kuna wadau humu wanajua zaidi.
Jamani naomba kueleweshwa hili Kwanini nchi kama Ethiopia ina shirika la ndege(Ethiopia airline) ambalo linatesa sambamba na mashirika makubwa ya ndege na wakati nchi kama hiyo haina any source of income zaidi ya vita. Lakini hilo shirika bado halijadorora mpaka sasa je sisi tulio na amani na utajiri wote huu tunashinda na nchi kama Ethiopia.Je tatizo nini?

Kwa sababu 90% ya budget yao ni misaada.
Waliotaka kuwekeza walikuwepo pia Rift Valley ya South africa ambao wamechukua Kandrasi hiyo Kenya na Uganda na hatusiki kelele huko kama kwetu. Na pia nilisikia Wajerumani walitaka kuichukua hiyo kandarasi ya kuiendesha hiyo Reli.
Tatizo huo mkataba ulifungwa kwa maslahi ya baadhi ya viongozi, hiyo Rites ya India ni conduit pipe tu. Utakuta Wawekezaji wenyewe tunao hapa hapa tanzania, kama ilivyo kuwa kiwira Coal Mine na uzalishaji wa Umeme Tanzania
Kesho kutwa Wizara ya Miundombinu inasoma bajeti yake. Kuna taarifa kwamba mashirika yanayochechemea, kama vile Tanzania Railway Limited (TRL), ATCL yatatengewa pesa nono....
Waheshimiwa wabunge, vipi kuhusu kampuni ya TICTS, kwa sababu mkataba wao ulipangwa kusitishwa tangu mwaka jana.
Mkuu heshima mbele, Lakini mwalimu aliahidi kuwaita waingereza baada ya miaka 10 na alifanya hivyo mission accomplished sasa baada ya hapo ndio vurugu mechi bora tuwarudishie tu Wazungu baada ya 90% yao 10% yetu sasa iwe 50% kwa 50%Mutu,
Angalia usishangae sana ukashangaa feri. Watanzania sasa hivi kuharibika kwa kila kitu tunageukia uumbaji wa Tanzania, tunamlaumu Adamu wetu kwa kula pera la Uhuru kujua mema na mabaya. Kwani hujaona kwenye hizo mada mbili kuhusu Mwalimu Nyerere, kila kitu kinasemekana Mwalimu ndio Olduvai Gorge, Zinjanthropus bosei, Alpha na Omega wa msoto Tanzania!