Mkataba wa TRL (TRC)

Mkataba wa TRL (TRC)

Jamani naomba kueleweshwa hili Kwanini nchi kama Ethiopia ina shirika la ndege(Ethiopia airline) ambalo linatesa sambamba na mashirika makubwa ya ndege na wakati nchi kama hiyo haina any source of income zaidi ya vita. Lakini hilo shirika bado halijadorora mpaka sasa je sisi tulio na amani na utajiri wote huu tunashinda na nchi kama Ethiopia.Je tatizo nini?
 
Nilisema zamani sana. SWALA LA ENERGY NI SWALA LA TAIFA.

Makampuni yote yanayo-deal na UMEME, MAFUTA na MAJI lazima yawe ya SERIKALI tu na watu binafsi mikono iwe mbali kabisaaaa.

Pia swala la usafiri hasa RELI lazima lisaidiwe na serikali kwani ni muhimu kwa ajira na usafiri wa Makontena ya mizigo. Hivyo, bila kujali kama kuna hasara au lahh, serikali lazima ilishike mkono na kuangalia jinsi ya kulifanya lifanye kazi kwa faida.

Tatizo linakuja pale mashirika ya umma wanapewa WASHIKAJI. Kuna haja siku moja hawa WASHIKAJI na waliowaweka waje washitakiwe kwa kosa la KUHUJUMU UCHUMI.

ATCL ingelisaidiwa na kuanza kusafiri nje ya Tanzania na huko tukaanza KUUZA parkage za utalii yaani mtu akinunua ticket kama Msafiri, basi anunue tour nzima ya utalii. Faida kubwa inakuwa kwamba, bei inapunguzwa kwa asilimia fulani tofauti na kama akipanda KLM, swiss air nk. Tungelivutia watalii wale wa kiwango cha kati ambao nafikiri kwa maisha ya West, wako wengi sana sana. Nafikiri mashirika ya kitalii kama NEKERMAN wana ndege zao na wanasafirisha watalii kwa faida kubwa tu maana hadi leo hii wapo.
Faida kubwa ya kuwa na ATCL si tu kubeba abiria. Kuna kutangaza utalii/nchi, kupeleka bidhaa za Tanzania nje ya nchi, kuongeza ajira nk. Mie nashindwa kuelwa mtu kama Mataka unashindwa kabisa kupanga mikakati ya kuokoa shirika. Haihitaji kuwa mkali sana wa biashara kujua vitu vya msingi vya kufanya kwa kuanzia kwa shirika lenye ndege 3 na wafanyakazi sijui 300?
 
Hili shirika letu la reli silielewi. Nadhani kuna elements nyingi za ufisadi ndani yake na sasa shirika linaelekea kufa kutokana na utendaji mbovu. Sijui sana kuhusu uendeshaji wa hili shirika letu la reli labda kuna wadau humu wanajua zaidi.

Mkubwa, hakuna siri yoyote kutoka kwa zitto, mambo yalikuwa wazi na matokeo yalitegemewa!!!

Biashara ya reli inanyauka hasa kwa nchi masikini kutokana na kukua alternative means; that doesnt mean we should be ok, hapana!!

They say "Garbage in - Garbage out" we would have saved some by just redoing the whole task au tulie tu!!! TAZARA NAYO IKO NA KAMTUNGI KAKE KA OXYGEN NEXT BED!!! ATC ANPATA PHYSIO NA KWENYE MELI SIJUI HALI MAANA FAILI LA MGONJWA HALIONEKANI

....Dad😕
 
tatizo sio uelewa wa mikataba, tatizo wanaopitia hiyo mikataba wanataka maslahi ndani ya mikataba japo wakijua kabisa in the long run ina side effect kubwa kwa taifa, ila kwa sababu kila mtu amekaa kimaslahi zaidi, wanaingia contract japo ina weakness nyingi tu, kisa kuna percent kaahidiwa. wazalendo wameshakwisha taifa hili.

............................
VIONGOZI WA BORA UTAWALA NA AKILI ZILIZO LALA MWISHO WA SIKU TAIFA WATALIGEUZA JALALA...
 
Na Eckland Mwaffisi

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Bw. Zitto Kabwe amesema kusuasua kwa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kumechangiwa na idadi ndogo ya wawekezaji waliojitokeza kuomba zabuni kuendesha reli hiyo, hivyo kuifanya Serikali kukosa mbadala na kumua kuipa Kampuni ya RITES kutoka India kwa mtindo wa 'hakuna namna.'

Bw. Zitto aliyasema hayo Dar es Salaam jana, wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na kipindi cha Mambo Leo, kinachorushwa na Kituo cha Times 100.5 fm

Alisema migogoro mbalimbali ya wafanyakazi inayoendelea TRL, inachangiwa na mwekezaji, Kampuni ya RITES kushindwa kuboresha huduma wanazotoa katika kiwango kilichoratajiwa na kuongeza kuwa kampuni imeshindwa hata kuboresha usafiri wa mizigo na abiria hadi sasa.

Alifafanua kuwa, pamoja na Serikali kumiliki asilimia 49 na RITES asilimia 51, Serikali imeendelea kubeba mzigo mzito zaidi kuliko kampuni hiyo ambayo wananchi waliamini ingeleta mabadiliko makubwa kwa kuboresha huduma hizo.

Alieleza kuwa katika mchakato wa kutangaza zabuni ya uuzaji Shirika la Reli Tanzania (TRC), kampuni mbili tu ndizo zilijitokeza ambazo ni RATES ya India na mwekezaji mwingine kutoka Afrika Kusini ambaye hata hivyo alijitoa hatua za mwisho hivyo kuifanya Serikali kukosa namna na kuingia mkataba na mwekezaji aliyebaki(RITES) .

“Sababu kubwa ya mlundikano makontena bandarini ni huduma mbovu zinazotolewa na TRL, nchi mbalimbali duniani, hutumia usafiri wa treni kusafirisha mizigo yao tofauti na Tanzania hivi sasa ambayo haina huduma hiyo pamoja na kuwepo mwekezaji aliyepewa shirika hilo,” alisema.

Alidai kuwa mwaka 1996, Serikali ilifanya maamuzi mabovu kubinafsisha mashirika ya umma na kwamba yalikuwepo mashirika ambayo hayakupaswa hata kufikiriwa kuingizwa katika mchakato wa kubinafsishwa.

Alitoa mfano wa Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwamba haikupaswa kuingizwa katika mpango huo zaidi ya kufanyika mabadiliko ya uwekezaji kutoka serikalini.

Alisema Tanzania imebahatika kwa kuwa na nishati nyingi ya gesi na mafuta ambayo kama TANESCO itaongezewa nguvu na uwezo wa kuzitumia nishati hizo, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika kutoa huduma ya umeme na kulifanya shirika hilo kujiendesha kwa faida.

"Mwaka 2006 TANESCO ilipata hasara ya sh. bilioni 167 ikiwa chini ya usimamizi wa Net Group Solution, ambayo baada ya kumaliza mkataba wake, uongozi mpya chini ya Serikali uliweza kupunguza hasara hiyo kutoka sh. bilioni 167 hadi sh. bilioni 62. Kufikia Desemba 2008, hasara hiyo imepungua kutoka sh. bilioni 62 mpaka bilioni 30," alisema.

Alisema Serikali haipaswi kuuza shirika hilo zaidi ya kuliboresha kwa kuzingatia mapendekezo ya kamati yake ikiwa ni pamoja na kuuza hisa zake katika soko la hisa.

Bw. Zitto alisema, Kamati yake ilipendekeza kusitishwa zoezi la ubinafsishaji ili kufanya tathimini na kurekebisha makosa yaliyojitokeza, kwani alidai ubinafshaji uliofanywa nchini kuanzia mwaka 1996, umesababisha mali nyingi za umma kupotea na kunufaisha wachache.

Alitoa mfano mwingine kuwa, Shirika la Ndege Tanzania (ATC),lipo mahututi kiasi cha kuzidiwa na kampuni binafsi ya Precision Air,inayotoa huduma zenye ushindani kibiashara katika soko.

“Kamati yangu imetoa pendekezo kwa Serikali, kuipa mtaji wa kutosha ATC ili iweze kutoa huduma zake kwa ubora zaidi na kujiendesha kwa faida ikiwa ni pamoja na kuimarisha viwanja vya ndege katika miji mikubwa na midogo na kuingia katika ushindani wa soko la kibiashara,” alisema.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya marubani wa ndege za Serikali wamezeeka hivyo ni jukumu la Serikali kuwawezesha kielimu marubani wapya ili kuongeza ufanisi wa shirika hilo.

Alisema, pamoja na mapendekezo mengi yanayotolewa na kamati yake, historia inaonesha kuwa, kwa nchi nyingi duniani Serikali imekuwa ikishindwa kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na Kamati za Bunge.

Alisema, mfano mzuri wa mapendekezo hayo ni yale yaliyotolewa na Kamati ya Bunge kuhusu Richmond iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe lakini hadi sasa Serikali imeshindwa kuyafanyia kazi.

Source: Majira

Hili shirika letu la reli silielewi. Nadhani kuna elements nyingi za ufisadi ndani yake na sasa shirika linaelekea kufa kutokana na utendaji mbovu. Sijui sana kuhusu uendeshaji wa hili shirika letu la reli labda kuna wadau humu wanajua zaidi.
Sikubaliani na Zitto kuwa serikali inashindwa kutekeleza mapendekezo ya kamati za bunge;ukweli ni kwamba serikali inauwezo wa kutekeleza mapendekezo, lakini HAITAKI kufanya hivyo ili kulinda maslahi ya viongozi serikalini!! Mfano mzuri ni huu wa mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya bunge kuhusu Richmond; mengi ya mapendekezo yake hayahitaji fedha bali ni kuchukua hatua za kinidhamu lakiniwapi Muungwana ameamua kuwa haadhibiwi mtu hapa!!
 
tatizo kubwa viongozi wetu wanataka majibu tu 'kusuka au kunyoa', bila kutaka kujua sababu. of all the companies why was this company given the tender, those are the reason u haven't told us, i mean in terms of improving the service and their time scale for the service to be sorted. kwanini nauliza kwa sababu lazima serikali ingejua the realistic targert na wana expect kitu gani from this company and measure their progress as they going, instead of coming out and telling us wanaleta hasara and as majority shareholders they're still depending on the government it shouldn't come to this if you had a close eye on them and watching they're progress rather than let them behave as they want. so why be suprised; your moaning today of the losses, as i said earlier you only wanted or expected two results. remember if you want things done ur responsible for that and not the empoyees.

ametoa hoja (mh.) kwamba kuna baadhi ya secta serikali aikuwa tayari kudhibinafsisha na hii ni sehemu moja wapo. ni vitu ambavyo napiga kelele kila siku sehemu muhimu kwenye maisha ya watanzania bado mapema mno kuziachia kwenye mikono ya makampuni mengine hasa ya kigeni its time serikali ielewe 'engineer' ulaya anafundishwa naa biashara kwa sababu ya sehemu hizi. mi nadhani ni wakati wa serikali kupeleka watu nje kujifunza jinsi vitu vinavyooendeshwa succesfully. im talking about the thousands of the educated without occupations positions in our country we need to create opportunities rather wait for others to do things for us. the government needs to hold these sectors and fill the positions with people qaulified to run them as those Indian managers there.

usiwe mpumbavu, jambo usilolijua ni kama usiku wa giza

kuwa mwelevu, tegemea matokeo fulani kwa kupanga mipango fulani

Mungu Ibariki Tanzania
 
Sikubaliani na Zitto kuwa serikali inashindwa kutekeleza mapendekezo ya kamati za bunge;ukweli ni kwamba serikali inauwezo wa kutekeleza mapendekezo, lakini HAITAKI kufanya hivyo ili kulinda maslahi ya viongozi serikalini!! Mfano mzuri ni huu wa mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya bunge kuhusu Richmond; mengi ya mapendekezo yake hayahitaji fedha bali ni kuchukua hatua za kinidhamu lakiniwapi Muungwana ameamua kuwa haadhibiwi mtu hapa!!

Ukiwa na uwezo halafu usitake kufanya jambo, au ukiwa huna uwezo wa kulifanya jambo hilo hilo, mwishoni usilifanye, watu wakiulizwa umeweza kulifanya au umeshindwa utakuwa umeshindwa.

Kushindwa hapa kunakwenda moja kwa moja na serikali kutofanya, bila kujali kwamba ina uwezo au haina uwezo.Kuna maana moja ya kushindwa inayoambatana na fikra kwamba kulikuwa na juhudi zilifanyika lakini hazikufanikiwa, hii maana ni sahihi, lakini kuna maana nyingine ya kushindwa inayoambatana na fikra kwamba hakukuwa na juhudi, serikali kwa namna moja au nyingine haikutekeleza ilichotegemewa kutekeleza, hivyo imeshindwa kutekeleza.
 
Na Eckland Mwaffisi

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Bw. Zitto Kabwe amesema kusuasua kwa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kumechangiwa na idadi ndogo ya wawekezaji waliojitokeza kuomba zabuni kuendesha reli hiyo, hivyo kuifanya Serikali kukosa mbadala na kumua kuipa Kampuni ya RITES kutoka India kwa mtindo wa 'hakuna namna.'

Bw. Zitto aliyasema hayo Dar es Salaam jana, wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na kipindi cha Mambo Leo, kinachorushwa na Kituo cha Times 100.5 fm

Alisema migogoro mbalimbali ya wafanyakazi inayoendelea TRL, inachangiwa na mwekezaji, Kampuni ya RITES kushindwa kuboresha huduma wanazotoa katika kiwango kilichoratajiwa na kuongeza kuwa kampuni imeshindwa hata kuboresha usafiri wa mizigo na abiria hadi sasa.

Alifafanua kuwa, pamoja na Serikali kumiliki asilimia 49 na RITES asilimia 51, Serikali imeendelea kubeba mzigo mzito zaidi kuliko kampuni hiyo ambayo wananchi waliamini ingeleta mabadiliko makubwa kwa kuboresha huduma hizo.

Alieleza kuwa katika mchakato wa kutangaza zabuni ya uuzaji Shirika la Reli Tanzania (TRC), kampuni mbili tu ndizo zilijitokeza ambazo ni RATES ya India na mwekezaji mwingine kutoka Afrika Kusini ambaye hata hivyo alijitoa hatua za mwisho hivyo kuifanya Serikali kukosa namna na kuingia mkataba na mwekezaji aliyebaki(RITES) .

“Sababu kubwa ya mlundikano makontena bandarini ni huduma mbovu zinazotolewa na TRL, nchi mbalimbali duniani, hutumia usafiri wa treni kusafirisha mizigo yao tofauti na Tanzania hivi sasa ambayo haina huduma hiyo pamoja na kuwepo mwekezaji aliyepewa shirika hilo,” alisema.

Alidai kuwa mwaka 1996, Serikali ilifanya maamuzi mabovu kubinafsisha mashirika ya umma na kwamba yalikuwepo mashirika ambayo hayakupaswa hata kufikiriwa kuingizwa katika mchakato wa kubinafsishwa.

Alitoa mfano wa Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwamba haikupaswa kuingizwa katika mpango huo zaidi ya kufanyika mabadiliko ya uwekezaji kutoka serikalini.

Alisema Tanzania imebahatika kwa kuwa na nishati nyingi ya gesi na mafuta ambayo kama TANESCO itaongezewa nguvu na uwezo wa kuzitumia nishati hizo, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika kutoa huduma ya umeme na kulifanya shirika hilo kujiendesha kwa faida.

"Mwaka 2006 TANESCO ilipata hasara ya sh. bilioni 167 ikiwa chini ya usimamizi wa Net Group Solution, ambayo baada ya kumaliza mkataba wake, uongozi mpya chini ya Serikali uliweza kupunguza hasara hiyo kutoka sh. bilioni 167 hadi sh. bilioni 62. Kufikia Desemba 2008, hasara hiyo imepungua kutoka sh. bilioni 62 mpaka bilioni 30," alisema.

Alisema Serikali haipaswi kuuza shirika hilo zaidi ya kuliboresha kwa kuzingatia mapendekezo ya kamati yake ikiwa ni pamoja na kuuza hisa zake katika soko la hisa.

Bw. Zitto alisema, Kamati yake ilipendekeza kusitishwa zoezi la ubinafsishaji ili kufanya tathimini na kurekebisha makosa yaliyojitokeza, kwani alidai ubinafshaji uliofanywa nchini kuanzia mwaka 1996, umesababisha mali nyingi za umma kupotea na kunufaisha wachache.

Alitoa mfano mwingine kuwa, Shirika la Ndege Tanzania (ATC),lipo mahututi kiasi cha kuzidiwa na kampuni binafsi ya Precision Air,inayotoa huduma zenye ushindani kibiashara katika soko.

“Kamati yangu imetoa pendekezo kwa Serikali, kuipa mtaji wa kutosha ATC ili iweze kutoa huduma zake kwa ubora zaidi na kujiendesha kwa faida ikiwa ni pamoja na kuimarisha viwanja vya ndege katika miji mikubwa na midogo na kuingia katika ushindani wa soko la kibiashara,” alisema.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya marubani wa ndege za Serikali wamezeeka hivyo ni jukumu la Serikali kuwawezesha kielimu marubani wapya ili kuongeza ufanisi wa shirika hilo.

Alisema, pamoja na mapendekezo mengi yanayotolewa na kamati yake, historia inaonesha kuwa, kwa nchi nyingi duniani Serikali imekuwa ikishindwa kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na Kamati za Bunge.

Alisema, mfano mzuri wa mapendekezo hayo ni yale yaliyotolewa na Kamati ya Bunge kuhusu Richmond iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe lakini hadi sasa Serikali imeshindwa kuyafanyia kazi.

Source: Majira

Hili shirika letu la reli silielewi. Nadhani kuna elements nyingi za ufisadi ndani yake na sasa shirika linaelekea kufa kutokana na utendaji mbovu. Sijui sana kuhusu uendeshaji wa hili shirika letu la reli labda kuna wadau humu wanajua zaidi.
Waliotaka kuwekeza walikuwepo pia Rift Valley ya South africa ambao wamechukua Kandrasi hiyo Kenya na Uganda na hatusiki kelele huko kama kwetu. Na pia nilisikia Wajerumani walitaka kuichukua hiyo kandarasi ya kuiendesha hiyo Reli.
Tatizo huo mkataba ulifungwa kwa maslahi ya baadhi ya viongozi, hiyo Rites ya India ni conduit pipe tu. Utakuta Wawekezaji wenyewe tunao hapa hapa tanzania, kama ilivyo kuwa kiwira Coal Mine na uzalishaji wa Umeme Tanzania
 
Jamani naomba kueleweshwa hili Kwanini nchi kama Ethiopia ina shirika la ndege(Ethiopia airline) ambalo linatesa sambamba na mashirika makubwa ya ndege na wakati nchi kama hiyo haina any source of income zaidi ya vita. Lakini hilo shirika bado halijadorora mpaka sasa je sisi tulio na amani na utajiri wote huu tunashinda na nchi kama Ethiopia.Je tatizo nini?

Kwa sababu 90% ya budget yao ni misaada.
 
Nchi ya Ethiopia inayo source of income, trust me I have lived there until just recently. Ethiopian Airlines is a successful venture between the government of Ethiopia and investors from U.S.A. What they do in Ethiopia ni kwamba any sector ambayo mzalendo/wazalendo wanaweza kuwekeza basi hawata kubali foreign investors kwenye hiyo sector unless huyo foreign investor ana ubia na muethiopia. Hizi sector ni pamoja na construction, hotel, tourism, etc. Pia wana diaspora kubwa ambao huja kuinvest nchini mwao kwenye vitu kama business buildings etc. Sector kama electricy. telecommunications and water hizi ni stricly government owned hata muethiopia hawekezi kwenye hizi sector. That is why mpaka leo Ethiopia ina kampuni moja tu ya simu Ethiopian Telecommunications Ltd(ETC). In short hawa wenzetu wametu zidi katika mambo mengi, mji mkuu wao kama Addis Ababa ina barabara nzui kweli na fly overs na two way traffic ni kitu cha kawaida. The good thing about the Ethiopian government is that they don't just talk but they impliment every thing they put on paper. Sasa hivi uchumi wao una kwikwi kidogo kutokana na vita zao zisizo isha pamoja na makali ya hali ya kiuchumi duniani.
 
Kwa sababu 90% ya budget yao ni misaada.

Lakini wana tumia misaada yao vizuri kuliko sisi na ufisadi siyo kama nyumbani ndiyo maana mashirika kama shirika lao la ndege hazi jafa. Ingekua Tanzania inge kua yale yale ya ATCL.
 
Waliotaka kuwekeza walikuwepo pia Rift Valley ya South africa ambao wamechukua Kandrasi hiyo Kenya na Uganda na hatusiki kelele huko kama kwetu. Na pia nilisikia Wajerumani walitaka kuichukua hiyo kandarasi ya kuiendesha hiyo Reli.
Tatizo huo mkataba ulifungwa kwa maslahi ya baadhi ya viongozi, hiyo Rites ya India ni conduit pipe tu. Utakuta Wawekezaji wenyewe tunao hapa hapa tanzania, kama ilivyo kuwa kiwira Coal Mine na uzalishaji wa Umeme Tanzania

Nakushukuru mara mia moja!

Ukweli ndio huo makampuni yote hayakubinafsishwa bali waligawana viongozi walafi wa CCM.
Na hilo limefanikiwa baada ya Rais wa ajabu kuliko wote Duniani maarufu kama Ruksa ambaye ana IQ NDOGO kuliko ya kuku kuingia mkenge na kufuta Azimio la Arusha na kuzaliwa kwa AZIMIO LA ZANZIBAR amabalo limeruhusu viongozi wa chama kuwa na mali !!!

That was when watanzania masikini walivishwa kokwa la utumwa for life!

Marehemu Nyerere alifikia kumsema kwamba alikuwa anashauriwa na mkewe!!!
But because alimwachia mbwa na kamba yake he was absolutely power less alikosea kungatuka uwenyekiti wa Chukua Chako Mapema and he died a pauper!!

The selfproclaimed Reverend Mtikila alizusha vagi la kuwaondoa MAGABACHORI lakini as usual kwa sababu waTZ ni aina fulani ya mbuzi /kondoo tena wa alibadili hilo hawakuliona tunajua masahibu yaliyompata he ended being a jail bird na mwisho Rostam Aziz akampatia makombo yaliyomtoa kwenye picha kubwa sijui kama amemlipa zile 3m/=

Kwa hiyo tusimtafute mchawi haya makampuni hata ya madini ni ya wamatumbi tena wajiita ccm wasafi ila kwa sababu hawajui ABC ya biashara ndio maana tumeliwa!! I hate the green attire kila nikona kiajani nachefuka!!

Je mnajua Ngombe wanaona kila kitu ni kijani ndio maana hata rambo wanakula!! kama watanzania wanavyoiona ccm kingine hawaoni!

Jakaya Mrisho Kikwete pia ni chui kwenye ngozi ya kondoo he was bought cheaply by the sUBASH PATELS;rOATAM aZIZI AND THE REST. hAKUNA WA KUCHEKA MWINGINE: LOWASA;Mramaba wala Yona and Mkapa. hata Kingunge

Hawa wapuuzi ni wasanii na wanachokifanya ni mchezo wa kuigiza!! Can somebody sober from CCM and the GVT machinery come in the open and reconcile showing the break down of all income from MAKAMPUNI WALIYOJIUZIA!!
RITES ni kivuli tu hata Pinda anajua ndio maana anatoa pesa za walipa kodi kupeleka TRL!! sHAME ON THESE black people!!! Tujue imekula kwetu kama tusipochukua hatua kali dhidi yao nyie endeleeni na hiyo chorous ya amani and you will be left in the cold for your lifetime!!!
 
jamanieee, hivi naomba kujiuliza, wahindi wa reli ya kati wanakopesheka na mabenk? are these people trusted by bank kwamba wanaweza wakakopa wakapewa mkopo wa kuendesha shirika hilo. je, wana uwezo kuendesha kampuni hiii, je wanaingiza hela kuliko reli ile ilivyokuwa chini ya tz govt? je wana muonekano wowote wa kufanikiwa in the near future? je tumewapa ile reli ili wajifunzie kufanya biashara? je tumewawa/tumeingia nao ubia ili kuwanufaisha wao,tunajikomba kwao, au tunawaogopa? mbona they are not productive, hawana hela, matatizo chungu mzima.

hivyo tenda ilitangazwaje, mbona nilisikia kuna makampuni mengine yalitoka Ujerumani(western europe) huko lakini yalipigwa chini ili kuwapa hawa wahindi. wanayo experience kasi gani kufanya biashara kama hii, au tutafaidika nao kivipi? tutafaidika au zitakuwa kama reli zile za india? tutawatimua au hatutawatimua.

wanasheria waangalia kama kuna vifungu kwenye mkataba haraka sana ili kama wamekiuka hata kimoja tu, tuwatimue tuingie mkataba na watu wengine. nina uchungu na nchi yangu jamani. mnasemaje?
 
Kesho kutwa Wizara ya Miundombinu inasoma bajeti yake. Kuna taarifa kwamba mashirika yanayochechemea, kama vile Tanzania Railway Limited (TRL), ATCL yatatengewa pesa nono....

Waheshimiwa wabunge, vipi kuhusu kampuni ya TICTS, kwa sababu mkataba wao ulipangwa kusitishwa tangu mwaka jana.
 
Sasa kulikuwa kuna haja gani ya kumpa mwekezaji wa India hiyo TRL kama serikali inatgemea kutoa pesa nyingi kwa ajili ya uendeshaji???
 
Pinda full mzugaji nowadays...anajua hana uwezo wa kuwazidi nguvu mafisadi,tumuombee..
 
images
images

Usafiri wa train India - mmmh, ndio wawekezaji wetu hawa !! Tusubiri budget hiyo.
 
Mutu,

Angalia usishangae sana ukashangaa feri. Watanzania sasa hivi kuharibika kwa kila kitu tunageukia uumbaji wa Tanzania, tunamlaumu Adamu wetu kwa kula pera la Uhuru kujua mema na mabaya. Kwani hujaona kwenye hizo mada mbili kuhusu Mwalimu Nyerere, kila kitu kinasemekana Mwalimu ndio Olduvai Gorge, Zinjanthropus bosei, Alpha na Omega wa msoto Tanzania!
Mkuu heshima mbele, Lakini mwalimu aliahidi kuwaita waingereza baada ya miaka 10 na alifanya hivyo mission accomplished sasa baada ya hapo ndio vurugu mechi bora tuwarudishie tu Wazungu baada ya 90% yao 10% yetu sasa iwe 50% kwa 50%
 
Back
Top Bottom