Mkataba wa TRL (TRC)

Mkataba wa TRL (TRC)

Tuandamane,

Tunashukuru mkuu kwa haya mambo mazuri hivi.....

Nishalishusha kutoka kwenye neti, saivi ni mkao wa kula tu hapa......

Ubarikiwe muzee
 
Leo nimesikia huyu fisadi Marmo nimemsikia huko bungeni akikemea kwamba, kuwa na waraka ulio na mihuri yao "Wizi mkubwa" hapana "siri kubwa" "confidential" ni kosa kubwa sana. Hasa ukikutwa nao. Sijui hawaelewi kuwa kuwaibia wananchi ni kosa kubwa zaidi? Mi sijui wamejisahau kwamba nyaraka hizi ziko hapa jf na kwenye mitandao mingine mingi? Si tutaisomea humu na kuiacha humu huku tukiendelea kuwafunga kwa wizi wao dhidi ya watanzania?
 
Leo nimesikia huyu fisadi Marmo nimemsikia huko bungeni akikemea kwamba, kuwa na waraka ulio na mihuri yao "Wizi mkubwa" hapana "siri kubwa" "confidential" ni kosa kubwa sana. Hasa ukikutwa nao. Sijui hawaelewi kuwa kuwaibia wananchi ni kosa kubwa zaidi? Mi sijui wamejisahau kwamba nyaraka hizi ziko hapa jf na kwenye mitandao mingine mingi? Si tutaisomea humu na kuiacha humu huku tukiendelea kuwafunga kwa wizi wao dhidi ya watanzania?

Kinachonisikitisha ni kwamba hawa mafisadi wakiongozwa na JK hawajawahi kujiuliza wana hawajisumbui kujua tunazipata wapi na vipi hizi mali zao, hawatumii hata akili ndogo tuu kwa kusoma alama za nyakati???????
 
na kama wanasema kuwa tumewaibia mali mzao sasa kwanza kabla hatujakaa mezani kujadili, tunataka kujua kuwa zile malizetu za EPA na RICHMOND wamezitoa wapi na ni nani kawapa, ndo tuanze ustaarabu wa kuweka ngoma katikati kipenga kipigwe, boli lianze na mshindi apatikane
 
Leo nimesikia huyu fisadi Marmo nimemsikia huko bungeni akikemea kwamba, kuwa na waraka ulio na mihuri yao "Wizi mkubwa" hapana "siri kubwa" "confidential" ni kosa kubwa sana. Hasa ukikutwa nao. Sijui hawaelewi kuwa kuwaibia wananchi ni kosa kubwa zaidi? Mi sijui wamejisahau kwamba nyaraka hizi ziko hapa jf na kwenye mitandao mingine mingi? Si tutaisomea humu na kuiacha humu huku tukiendelea kuwafunga kwa wizi wao dhidi ya watanzania?


Bado anfikiri watanzania wamelala kiasi kwamba kuwatisha kutasidia kitu cha msingi ni kuacha kuiba tu na sio kutisha watu kwa sababu kuna watu wanaweza kuamua kujitolea mhaanga ili kuiokoa tanzania kutoka mikononi mwao.
 
Leo nimesikia huyu fisadi Marmo nimemsikia huko bungeni akikemea kwamba, kuwa na waraka ulio na mihuri yao "Wizi mkubwa" hapana "siri kubwa" "confidential" ni kosa kubwa sana. Hasa ukikutwa nao. Sijui hawaelewi kuwa kuwaibia wananchi ni kosa kubwa zaidi? Mi sijui wamejisahau kwamba nyaraka hizi ziko hapa jf na kwenye mitandao mingine mingi? Si tutaisomea humu na kuiacha humu huku tukiendelea kuwafunga kwa wizi wao dhidi ya watanzania?

Haswaa! Waache tu washindwe kutoelewa nguvu za mawasiliano ya kisasa. Wanaifanya Serikali ni mradi wao binafsi wa siri?. Very stupid people.

The table is turning, and we will get them...
 
Shukrani sana mkuu kwa kazi nzuri sana.
Sasa wachambuzi tunaingia mzigoni kujua kunani.
 
Hili swala Mizengo Pinda ameliongelea leo bungeni na kusema matatizo mengi yanayotokea TRL sisi wenywe ndio wakujilaumu. Watu wa wizara hawana njia nzuri za mawasiliano na TRL. Hii inafanya TRL wapate tabu wao kuweza kufanya shughuli zao za kila siku. Watu wa TRL walikwenda juzi kumueleza pm. PM kasema atalishulikia hiki kitu. Kasema kwamba anataka kila barua inayokwenda wizarani (yani wizara ya miundombinu) na copy iende kwake. Labda itasaidia kwa kiwango fulani
 
Big Up Tuandamane, Nimeamini Kweli Kwa Mwendo Huu Mafisadi Watakoma Mwaka Huu. Ila Naomba Kuuliza Hivi Yale Maandamano Yetu Wana Jf Yaliishia Wapi? Kwangu Mimi Naona Huu Ndo Muda Mwafaka!
 
Big Up Tuandamane, Nimeamini Kweli Kwa Mwendo Huu Mafisadi Watakoma Mwaka Huu. Ila Naomba Kuuliza Hivi Yale Maandamano Yetu Wana Jf Yaliishia Wapi? Kwangu Mimi Naona Huu Ndo Muda Mwafaka!
Na ni siku hiyo ya hilo tangazo la maandamano ndio lilinifanya nijiunge na kutumia hili jina, lkn mpaka leo sijaona kitu..... nilifurahia sana jambo la kuandamana kwa kweli
 
Hili swala Mizengo Pinda ameliongelea leo bungeni na kusema matatizo mengi yanayotokea TRL sisi wenywe ndio wakujilaumu. Watu wa wizara hawana njia nzuri za mawasiliano na TRL. Hii inafanya TRL wapate tabu wao kuweza kufanya shughuli zao za kila siku. Watu wa TRL walikwenda juzi kumueleza pm. PM kasema atalishulikia hiki kitu. Kasema kwamba anataka kila barua inayokwenda wizarani (yani wizara ya miundombinu) na copy iende kwake. Labda itasaidia kwa kiwango fulani
Mega hivi hujag'amua kwamba na huyu Pinda ni msanii mzuri? Huku anasema matatizo ya TRL yanaanzia wizarani sijui na huku hizo wizara wanaziongoza wao na hakuna hatua kwa hao wakosaji sio, na huku anasema hivi na hivi. Ni msanii mzuri tu huyu.
kwake kitu kilikuwa kigumu kukieleza na kutolea ufafanuzi ni Meremeta tu. Lakini kila jibu analotoa ni la kutoa matumaini tu. Si hapo unaweza kujua na hakuna analofanya kwa kweli.
Angalia hii Richmonduli. Kila kikao cha bunge huwa anatoa promise kulizungumzia lakini hadi sasa kimya eti anasubiri ruhusa ya spika. Si aombe kwa spika? kwani atakataliwa? Hayyyyyyyyyyyaaaaaaaaaa????????
 
Asante Mwanakijiji.

hii habari ya TRL iunganishwe tafadhali. Chenge hasikiki siku hizi, uko wapi mzaa wa vijisenti!
 
Wednesday May 27, 2009

Govt blocks TRL bank loan

PIUS RUGONZIBWA, 27th May 2009 @ 00:00,

The government has finally owned up that it is worried over the performance of the Tanzania Railways Ltd (TRL), and has since blocked the release of a World Bank loan amounting to $44bn initially aimed at beefing up the firm’s capital. Minister for Finance and Economic Affair Mr Mustafa Mkulo revealed this when submitting a performance report of his Ministry for 2008/2009 financial year to the Parliamentary Committee of Finance and Economy yesterday.

Mr Mkulo told the Committee that the government was not happy “at all” with the investment performance of the Indian investor (RITES) which won a tender to develop the central railway line – hence the move to block the multi-billion loan facility from the World Bank. Instead, the government now wants full explanation on the various and critical matters regarding the capacity of the company in carrying out the investment -- but the company always failed to rise up to the demands.

“We came to realize there was something fishy with the company … it is not open on how it has prepared itself to run the railway according to the contract. “We are hesitant to give out the money fearing at the end of the day it would be a burden to the government… We were worried whether the company will manage to repay it,” he said. The minister added that the government was still paying TRL staff salaries, but expressed optimism that the company would soon start paying the salaries after sorting out some of its problems.

Earlier, committee members Ms Moulidah Anna Komu (Special Seats-CHADEMA) and Dr Omari Mzeru (Morogoro Urban-CCM) asked the minister to give reasons why the government was still dishing out money in salaries to TRL staff to date. The MPs also advised the government to make sure it scrutinizes the financial viability of other foreign companies wishing to invest in the country before awarding them investment deals. “What is our monetary policy governing such investors? The policy -- if any -- must ensure these companies are financially sound before handing our companies to them,” said Dr Mzeru.

On the banking sector, the MPs were concerned over rising interest rates charged by foreign commercial banks and cautioned that if left uncontrolled, people might resort to keeping their money in pyramid financial schemes such as DECI. Dr Mzeru said people in his constituency were now asking the government to introduce alternative systems to soft loans. “Even I, an MP … don’t see the reason of keeping my money in the banks because of their unbearable high interests … what about the rest?” he asked. However, they called on the government to track down all the financial schemes operating illegally.

However, the minister said the government would finally revisit all bank interest rates, and that the Governor of Bank of Tanzania, Professor Benno Ndullu, would soon announce measures to mitigate the impact of the current global financial crisis. On pyramid schemes, he said the office of the Director of Criminal Investigations (DCI) was closely investigating the conduct of at least 20 of them. “About 20 of them are under probe as we talk now. The DCI and his special team are investigating … and they are in for it now,” he said.
 
Na Eckland Mwaffisi

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Bw. Zitto Kabwe amesema kusuasua kwa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kumechangiwa na idadi ndogo ya wawekezaji waliojitokeza kuomba zabuni kuendesha reli hiyo, hivyo kuifanya Serikali kukosa mbadala na kumua kuipa Kampuni ya RITES kutoka India kwa mtindo wa 'hakuna namna.'

Bw. Zitto aliyasema hayo Dar es Salaam jana, wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na kipindi cha Mambo Leo, kinachorushwa na Kituo cha Times 100.5 fm

Alisema migogoro mbalimbali ya wafanyakazi inayoendelea TRL, inachangiwa na mwekezaji, Kampuni ya RITES kushindwa kuboresha huduma wanazotoa katika kiwango kilichoratajiwa na kuongeza kuwa kampuni imeshindwa hata kuboresha usafiri wa mizigo na abiria hadi sasa.

Alifafanua kuwa, pamoja na Serikali kumiliki asilimia 49 na RITES asilimia 51, Serikali imeendelea kubeba mzigo mzito zaidi kuliko kampuni hiyo ambayo wananchi waliamini ingeleta mabadiliko makubwa kwa kuboresha huduma hizo.

Alieleza kuwa katika mchakato wa kutangaza zabuni ya uuzaji Shirika la Reli Tanzania (TRC), kampuni mbili tu ndizo zilijitokeza ambazo ni RATES ya India na mwekezaji mwingine kutoka Afrika Kusini ambaye hata hivyo alijitoa hatua za mwisho hivyo kuifanya Serikali kukosa namna na kuingia mkataba na mwekezaji aliyebaki(RITES) .

“Sababu kubwa ya mlundikano makontena bandarini ni huduma mbovu zinazotolewa na TRL, nchi mbalimbali duniani, hutumia usafiri wa treni kusafirisha mizigo yao tofauti na Tanzania hivi sasa ambayo haina huduma hiyo pamoja na kuwepo mwekezaji aliyepewa shirika hilo,” alisema.

Alidai kuwa mwaka 1996, Serikali ilifanya maamuzi mabovu kubinafsisha mashirika ya umma na kwamba yalikuwepo mashirika ambayo hayakupaswa hata kufikiriwa kuingizwa katika mchakato wa kubinafsishwa.

Alitoa mfano wa Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwamba haikupaswa kuingizwa katika mpango huo zaidi ya kufanyika mabadiliko ya uwekezaji kutoka serikalini.

Alisema Tanzania imebahatika kwa kuwa na nishati nyingi ya gesi na mafuta ambayo kama TANESCO itaongezewa nguvu na uwezo wa kuzitumia nishati hizo, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika kutoa huduma ya umeme na kulifanya shirika hilo kujiendesha kwa faida.

"Mwaka 2006 TANESCO ilipata hasara ya sh. bilioni 167 ikiwa chini ya usimamizi wa Net Group Solution, ambayo baada ya kumaliza mkataba wake, uongozi mpya chini ya Serikali uliweza kupunguza hasara hiyo kutoka sh. bilioni 167 hadi sh. bilioni 62. Kufikia Desemba 2008, hasara hiyo imepungua kutoka sh. bilioni 62 mpaka bilioni 30," alisema.

Alisema Serikali haipaswi kuuza shirika hilo zaidi ya kuliboresha kwa kuzingatia mapendekezo ya kamati yake ikiwa ni pamoja na kuuza hisa zake katika soko la hisa.

Bw. Zitto alisema, Kamati yake ilipendekeza kusitishwa zoezi la ubinafsishaji ili kufanya tathimini na kurekebisha makosa yaliyojitokeza, kwani alidai ubinafshaji uliofanywa nchini kuanzia mwaka 1996, umesababisha mali nyingi za umma kupotea na kunufaisha wachache.

Alitoa mfano mwingine kuwa, Shirika la Ndege Tanzania (ATC),lipo mahututi kiasi cha kuzidiwa na kampuni binafsi ya Precision Air,inayotoa huduma zenye ushindani kibiashara katika soko.

“Kamati yangu imetoa pendekezo kwa Serikali, kuipa mtaji wa kutosha ATC ili iweze kutoa huduma zake kwa ubora zaidi na kujiendesha kwa faida ikiwa ni pamoja na kuimarisha viwanja vya ndege katika miji mikubwa na midogo na kuingia katika ushindani wa soko la kibiashara,” alisema.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya marubani wa ndege za Serikali wamezeeka hivyo ni jukumu la Serikali kuwawezesha kielimu marubani wapya ili kuongeza ufanisi wa shirika hilo.

Alisema, pamoja na mapendekezo mengi yanayotolewa na kamati yake, historia inaonesha kuwa, kwa nchi nyingi duniani Serikali imekuwa ikishindwa kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na Kamati za Bunge.

Alisema, mfano mzuri wa mapendekezo hayo ni yale yaliyotolewa na Kamati ya Bunge kuhusu Richmond iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe lakini hadi sasa Serikali imeshindwa kuyafanyia kazi.


Source: Majira


Hili shirika letu la reli silielewi. Nadhani kuna elements nyingi za ufisadi ndani yake na sasa shirika linaelekea kufa kutokana na utendaji mbovu. Sijui sana kuhusu uendeshaji wa hili shirika letu la reli labda kuna wadau humu wanajua zaidi.
 
Pamoja na maelezo aliyoyatoa Mh Zitto kama ambavyo tumeyasoma katika hiyo post ya hapo, pia tunakosa utaalam mzima wa usimamizi wa wawekezaji wanaokuja hapa nchini.

Kwa mfano mwekezaji akishakabidhiwa shirika basi haijulikani hasa mwenye kutoa maelekezo na ufuatiliaji wa karibu hasa ni nani. Wawekezaji hutumia weakness hii kuweza kwenda huku na kule kama TIC, Wizara mama na hata Ikulu nk katika kupata kile ambacho wanadhani kitawanufaisha. Majukumu yote makubwa ya maamuzi na maelekezi mara nyingi tunayasikia kutoka kwa bungeni kana kwamba hakuna machinery nyingine. Hii inaifanya pia kamati hiyo kuwa na kazi nyingi ambapo nyingine zingefanya vizuri na mamlaka husika yenye dhamana, yaani bodi.


Kwa mfano matatizo ya Reli, unaweza ukajiuliza Bodi ya Reli iko wapi au inafanya kazi gani hadi hilo shirika linakuwa katika hali mbaya? Je, bodi inasubiri kamati ya Bunge iwaelekeze nini cha kufanya?

Tatizo lingine ambalo huwa wakati wote ninalihusisha na usimamizi, ni namna gani serikali kupitia bodi ya TRL wanaweza kufuatila utekelezaji wa makubaliano mama ambayo ndiyo mkataba ulipofikiwa. Mara nyingi huwa kunakuwa deviations nyingi ambazo huletwa na wawekezaji wakati tayari mkataba upo katika hatua za utekelezaji na hili huwa linafanyika pale ambapo mwekezaji anakuwa anataka kufaidika nje ya mkataba wa awali. Mambo haya yamekuwa yakitokea katika mikataba mingi. Kwa hiyo iko haja kabisa kwa serikali kuhakikisha kuwa mikataba inayofungwa wakati wote mwekezaji aitimize kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo. Hatupashwi kuonesha nia ya ku-compromise dhidi ya yule ambaye alijua ni nini maana ya makubaliano.

Tusisahau kwamba kwa wale wanaokuja kuwekeza wanachojali kwanza ni namna gani watatengeneza au kurudisha pesa yao, na njia moja ni kucheza na mkataba, endapo njia hii ya kucheza na mkataba inawalipa haraka haraka habari ya kuboresha huduma obvious itaathirika kwa kiwango kikubwa. Aidha, wakifanikiwa kwa kiasi fulani kutengeneza pesa yao wanayoihitaji huishi kujenga mazingira ya kuvunja mkataba kama vile walivyofanya SAA kwa ATCL.


Ushauri: Serikali ihakikishe kuwa mikataba yote kabla ya kusainiwa ipo katika hali ya kutekelezeka hasa katika upande wa Buisness Plan, kwani hapa unaweza ukaletewa Business Plan inayovutia lakini kama hujui mitego yake utekelezaji wake unakuwa ni sawasawa na sifuri.
 
Back
Top Bottom