Mkazi wa Ngudu, Kwimba afungwa jela miaka 30 kwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi

Mkazi wa Ngudu, Kwimba afungwa jela miaka 30 kwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Mahakama ya wilaya ya Maswa,mkoani Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkazi wa Ngudu wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza,Jumanne Clement(23)kwa kosa la kubaka,kumpa ujauzito na kupoka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 wa kidato cha kwanza.

Hukumu hiyo imetolewa leo jumatano,Aprili 30,2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo,Enos Misana ambaye amesema mtuhumiwa atahukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kwanza na la pili na kwa kosa la tatu atahukumiwa kifungo cha miaka mitano na adhabu hizo zinakwenda kwa pamoja,hivyo atatumikia kifungo cha jumla cha miaka 30 jela.

Pia mshtakiwa ameamriwa kumlipa mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari Jija wilaya ya Maswa, fidia ya Sh 500,000.

Hakimu Misana ametoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Mshtakiwa alishtakiwa kwa alishtakiwa kwa makosa matatu ambayo ni kubaka,kinyume na kifungu cha 130(1)(2)(e) na 131 (1)cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2022.

Kosa la pili ni kumpa mimba mwanafunzi kinyume na kifungu cha 60A (3) cha sheria ya Elimu sura ya 353 marejeo ya mwaka 2002 na kama ilivyofanyiwa mabadiliko madogo katika kifungu cha 22 cha sheria ya mabadiliko madogo namba 2 ya mwaka 2016 na kosa la tatu ni kupoka, kinyume na kifungu cha 134 na 35 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 majerejeo ya mwaka 2022.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 23752/2024, kwa mujibu wa hati ya mashtaka na ushahidi uliowasilishwa mahakamani, mshtakiwa alitenda kosa hilo usiku,Aprili 20, 2024 katika kijiji cha Jijabilishi wilayani humo.
Alidaiwa kutenda makosa hayo na baaaye alimchukua mwanafunzi huyo na kwenda kuishi nae nyumbani kwake mjini Ngudu kwa lengo la kumuoa kinyume na matakwa ya wazazi wake mwanafunzi.

Katika kuthibitisha mashtaka, upande wa Jamhuri uliwaita mahakamani mashahidi watano akiwamo mwathirika (binti aliyetendewa kitendo hicho) na uliwasilisha vielelezo vinne.
 
Hatari,miaka 23 akija kutoka ana miaka 53,sasa akitoka atakuja kufanya nini uraiani? Na hiyo fidia ya laki tano inapatikanaje wakati tiyari amefungwa? Wataalam wa sheria naombeni ufafanuzi
 
Mbususu za buku tano tano zipo kitaa ukabake denti, uozee jela.
Kitaani kwetu ngono ni cheap kuliko chipsi yai, unampa mtu buku tano/mkono unajikojoza kiroho safi. Fala huyo ngoja akaliwe tako na nyampala.
 
Huyujabaka Bali kala Zigo Kwa makubaliano

Ndo ale "denti" alichukua risk ya kifala. Madenti hawaaminiki mzee! Kesi nyingi za kubaka zipo hivyo, denti anajaa kwenye mfumo, unapiga badae akienda kwao anasema, umepiga. Basi linakuwa bango, ubaoni wakienda hawakuachi. Una kula mvua 30, hiyo ya tulikubaliana Hakimu anashusha miwani. Haioni.
 
Huyujabaka Bali kala Zigo Kwa makubaliano
Tafsiri ya ubakaji kwa sheria za tanzania imekaa kipumbavu sana, yaani waliyoiweka walitumia zaidi mihemko kuliko akili.

Hapo kuna uwezekano mkubwa sana huyo binti walikuwa kwenye mahusiano na huyo jamaa, na walifanya ngono kwa makubaliano mpaka binti akashika ujauzito.

Ila kwa sababu tu binti bado hajafikisha umri wao wanaoutumbua hao watunga sheria ndio maana wanatafsiri kuwa ni ubakaji.

Upuuzi mtupu, mnafunga watu waliofanya ngono kwa makubaliano yao na kuyaacha mafisadi yakiendelea kutamba tu mitaani
 
Ilikua ni hekima kubwa zamani kuanza maisha ya ndoa watu wakiwa na umri mdogo. Sababu huo umri wa Hawa wahusika hapa ndio damu na ashiki vipo kwa kiwango Cha juu kabisa.
Kama si ndoa basi zinaa na uchepuko hauwezi kuepukika.
 
Kuna kitu najiuliza, mtoto wa kiume wa miaka 17 au 18 hivi amebalehe tangu akiwa miaka 13, atapata demu wa umri gani? Maana hawezi tongoza wa miaka 18 mwenzake huyo atakuwa mkubwa kwake, akipiga wa 15 anaambiwa amebaka hata kama binti ameridhia!
 
Back
Top Bottom