Mke ajiua kwa sumu ya Wadudu baada ya kupekua na kusoma SMS kwenye simu ya mumewe

Mke ajiua kwa sumu ya Wadudu baada ya kupekua na kusoma SMS kwenye simu ya mumewe

Lakini… kwanini tusipendane, tukatunzana, tukafanya project, tukalea watoto na kutoka out pamoja?

Kwanini tufanye maisha kuwa magumu kwa kufanya mambo pekepeke ilhali tuko wawili na tunapendana?

Mtoto wa mama mkwe nampenda sana nae ananipenda, kwa kutambua hilo hatuwezi kufanyiana mabaya ya kupelekea kuuana/kujiua.
Na tunamtanguliza Mungu atusimamie.

Unaweza kubadilika na kuibadili nyumba yako kuwa sehemu ya furaha. Wenza wa kando hawajawahi kuleta amani ndani ya nyumba.
Mwambie huyo Malay..
 
View attachment 2809543
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma (ACP) Marco G. Chilya akielezea kuhusu tukio hilo

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Marietha Bosco Sagana (32) Mkazi wa Kitongoji cha Matarawe, Kijiji cha Marungu Kata ya Tingi Tarafa ya Mpepo, Wilaya ya Nyasa amefariki Dunia wakati anapatiwa matibabu baada ya kwa kunywa sumu ya kuulia Wadudu chanzo kikiwa ni wivu wa Mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Marco G. Chilya amesema tukio hilo limetokea Novemba 8, 2023 Saa mbili usiku, ambapo mume wa marehemu alikuwa ameenda Shamba lakini alisahau simu yake nyumbani ndipo Marietha (marehemu) alivyoiona simu hiyo akaanza kuipekuwa.
View attachment 2809557
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma (ACP) Marco G. Chilya
Marietha alisoma meseji zote ikiwemo za WhatsApp na akafanikiwa kukuta jumbe za mume wake akiwasiliana na mwanamke Mwingine ndipo Marehemu alishindwa kuvumilia, hivyo akachukua Dawa ya Kuulia Wadudu ya Mahindi (ACTERIC) ambayo iliandaliwa kwa matumizi ya Shamba na kuinywa.

Baada ya kutenda tukio hilo majirani wanaoishi nae waligundua kitendo alichokifanya marehemu baada ya kuwaambia kuwa amekunywa dawa ya wadudu ambapo wakachukua uamuzi wa kumkimbiza Hospitali ya Mission Maguu ndipo akafariki Dunia wakati akipatiwa matibabu.
...R.I.P Marietha. Wivu umekuponza...
[emoji120]
 
Mwanaume mwingine anafanya kwa heshima anaenda kupatia utulivu mbali kwa mchepuko huko lakini bado kuna mwanamke maana mpumbavu Eti anaenda kumfuatilia Mwanaume hadi huko mbali mkoa mwingine.

Unapita vijiwe vya bodaboda kuuliza huwa analala loji gani?

Huwa anakuwa na mwanamke?

Unaenda kwenye loji kutafuta uthibitisho unaupata.

Sijui ni kwa nini Imeandikwa Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.
Mi wakwangu alikuja kunitembelea. Wakati anachoma taka jalalani akakuta kikaratasi cha ndom katika takataka za take kimechomwa ila hakikuungua vizuri.

Akakiokota na kuja nacho ndani huku anahema na jasho linamtoka,"Hii nini"! Ugomvi ukawa mkubwa kweli.
 
Twiiiiiiin; nipo hapa. Kumbe kuna definition mpya tena ya "heshima[emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji44]. Ya kwanza ilikuwa mume achepuke kwa heshima; sasa hivi mume anayekuheshimu; anaweka simu yake password. Mimi huyu mnyaki; mtoto wa mama mkwe aniwekee password hehehehehehehehehehe
Moto utawaka[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] wanyaki tuna nini lakini

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Sure, marehemu alikuwa hajipendi, mtu anayejipenda na kujithamini hawezi kujiua kisa mtu mwingine kagawa kikojoleo chake.

Kwanza ukiwa unajipenda rohoni utajipenda mwilini, unakuwa hot cake, Ile ukiachwa asubuhi unaolewa jioni.....!
Lazima ujipende kwanza wengine wafate.
 
Nkamu hata sielewi hii damu ina nini jamani. Ni [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Leka itolo[emoji1787] yani hii damu ni [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Inaweza kueleweka mtu au watu kukukataa lakini kujikataa mwenyewe nafsi yako hapana aisee!

Dhamana ya maisha yako Mwenyezi Mungu kaiweka mikononi mwako wewe binafsi.

You are 100% responsible of your life, no one can help you.

Ukiwa na mindset ya namna hiyo huwezi kuwa mtu wa kujilizaliza na kutafuta sympathies.
 
Wanapekua simu, wadai talaka Mwanaume anaona isiwe tabu mna achana.

Lakini atakaenda kwa waganga na kwa wachungaji kutafuta kurudiana ni mwanamke.

Victims ni wanawake always.

Mwamposa anawafundisha vizuri sana wanawake.

Mwanamke hata mpambe akija mwende kumfumania mumeo kataa , itakula kwako eventually ukienda kufumania.

Labda iwapo uko tayari kwa gharama zote.

Utaenda kumfania atakupa kipigo atakwambia ummdhalilisha akiwa kwenye utulivu wake ambapo ameukosa kwako ,
Na mwisho ukimtishia talaka anaitoa bila kusita atakwambia mapenzi Hayalasimishwi ila kama kuna mali wanaume wengi hawakubali kuibiwa mali zao na mwanamke ambae hajachangia hata shilingi 100 ktk kupata hizo mali .

Mwamba ni Dokta Juma Mwaka na Davis. [emoji123]
Hapo Mwamposa ametoa "opinions" zake, kadri anavyojisikia au kuona inamfaa yeye. Alichokiongea sio sheria, tena sio neno la Mungu; na sio SI UNIT ya ndoa zote ulimwenguni. Whatever suits him...

Nilitegemea Watumishi wa Mungu wawakumbushe waumini wao juu ya umuhimu wa kutunza viapo vyao vya ndoa na kuwa waaminifu kwa wenzi wao; na sio kukimbilia kuwaambia wanawake wasishike simu za waume wao. Hivi kati ya simu na sehemu za siri ni kipi kinatakiwa kitunzwe na kufichwa zaidi? Sehemu zako za siri unaziweka wazi kama public pizza afu simu ndiyo unajifanya Ina umuhimuuuu.

Tunalea kizazi cha hovyo kwelikweli cha watoto wa kiume ambao definitely watakuja kuwatreat wake zao kama options. Waume wafanye tu wanavyojisikia, na wake hawana options nyingine zaidi ya kuvumilia. Ndiyo maana uzeeni wanaume wengi wana -suffer kwelikweli ilihali wake zao wananawiri tu. What you sow in your wife in your youth; you shall reap it in your old age.

Afu sielewi kwa nini mnataka mwanamke aliyeachwa (divorcee) aone aibu kwa kuachwa/kuacha. Yes ni aibu kama ulifanya ujinga ukaachwa au ulitafuta sababu ya kijinga ili kuvunja ndoa yako; ila kwa mwanamke mwenye akili zake timamu; aliyekaa chini akatafakari na kuona kuwa hiyo ndoa ni threat kwa afya yake ya kiroho, kimwili, kihisia na hata kiuchumi; basi divorce ni uamuzi sahihi kwake.

Afu tusitake ionekane as if kila divorce ikitokea mwanamke ndiye ana-lose; wanaume kibao wameishia kupata depression pia kwa sababu ya kuachwa. Ingawa mbele za watu wanajifanya kujitutumua kuwa hawaumii na wamemove wamevuta vifaa vipya; deep down wanateketea. Tafuta wanawake walioolewa na divorcees afu wakusimulie maisha wanayoishi nao; majority are very very bitter; utalipia uchungu wake wa kuachwa as if wewe ndiyo ulimuacha.

Zamaradi Mketema alipambana weeh na wake wenzie kwa Marehemu Ruge; mwisho akanyoosha mikono juu. Leo yupo zake na Mzee wa "ulisi" na ndoa yao, wanalea watoto wao kwa amani. Kaheshimika from baby momma of father Abraham to a married woman.

Queen Masanja huyo kalilia talaka yake, sasa hivi maisha yake yanamuendea kwa amani. Anafanya vitu, anaishi maono na ndoto zake ambazo asingeweza kuziishi kama angeendelea na ndoa yake na Dr Mwaka. So inategemea na utashi wa mwanamke husika; sio kila mtu anapoteza akidivorce. Wengine wanang'ang'ana kwelikweli wanaishia kufia ndoa; hasara kwa watoto na wazazi wao.

Halafu mlivyo na uchungu mnaonaga kumnyima mwanamke mali ndiyo kumkomesha. Kuna wanawake ambao wapo willing kuacha kila kitu; anasonga mbele kwa ajili ya amani yake ya moyo; baki hapo na mali zako. Peace of mind is all that matters.. .Msiishi na wake zenu kiubabe ubabe as if their lives revolve around marriage.
 
Inashangaza sana imagine mwanamke kama hivyo anajiua just kwa kukuta sms tu. [emoji848][emoji848]

Na Kuna wanawake wengine wengi tu huvunja ndoa zao kwa kukuta sms kwenye Simu za wanaume wao, is this serious? [emoji848][emoji848]

Halafu unakuta tabia hizi za kiburi wanawaambukiza mabinti zao wakija kuolewa nao wata react hivyo hivyo wakizani ndivyo ipasavyo kumbe sio . Hiyo ndio huitwa “mapokeo “
Yaani umalaya wa mwanaume huuoni; ila mke akichoka akaondoka ndiyo aonekane ana kosa????
 
Back
Top Bottom