Mke akiondoka nyumbani kwa ugomvi je? Anafuatwa au atarudi tu. Mwenyewe

Mke akiondoka nyumbani kwa ugomvi je? Anafuatwa au atarudi tu. Mwenyewe

Wiki imeisha yupo kwa dada yake je? Nimfuate au niendelee kumsubiria

Maana mm nimesema siwezi mfuata hata kwa dawa huyu mama watoto wangu ambaye ni jeuri.

Ugomvi ni baada ya kujibishana halafu yeye akanijibu simtishi kwa lolote. Hivo nikamwambia sitamwachia hela ya kula tuone akajibu sawa nisubirie kama atatetereka.

Siku tatu tu akakimbia kwa dada yake anataka nimfuate.
Achana naye atarudi. Ukimfuata atajiona keki. Mwache aonje machungu. Kwa kuwa kaondoka yeye mwenyewe hujamfukuza na ugomvi kaanzisha yeye. Huna kosa mwache. Tena ukiona kimya anza kutafuta na mchepuko akisikia tu atarudi Au kama alivyo shauri hapo juu tafuta chupi, tight Anika Kwenye kamba Afu wewe ondoka jioni utaona huyu hapa 😂 😂 😂
 
Kwa mila zetu za kiafrika, mwanamke hatakiwi kutoka nje ya nyumba na kujiamulia pa kulala kwa hiyari yake bila ridhaa ya mume wake.

Mwanamke anapopishana na mume wake anatakiwa kwenda kwa wazazi wa mume wake au kwa wifi yake huko ndipo itapigwa simu aende kumfuata. Ila mwanamke anapoamua kurudi kwao kwa wazazi wake,au kwa dada au kaka yake au kwenda kwa rafiki yake huo ni utomvu wa nidhamu na kumkosea heshima mume wake.

Mwanaume hatakiwi kumfuata huko alipo. Na akipotea kwa zaidi ya siku 30, then mwanaume anatakiwa kuchukua mke mwingine huyo hatorejea hapo,amejitalikisha mwenyewe.
 
Mdogo wangu, mke anakujaribu kwa vitu vidogo vidogo, ukishindwa kuwa na msimamo nguvu inaongezeka.

Hata kufikia kukuambia umtishi ni matokeo ya baadhi ya mambo aliyokujaribu nayo akajua umtishi.

Sijasema mke anapigwa ili awe na adabu, mwanaume unatakiwa uwe na Msimama wa Israel kama kule Gaza.

Sasa we mfuate, kitakaxlchicuata ni hiki, utasikia analiwa na utaenda pia kumsamehe na kumradisha

Ushauri;

Mwache akae hata kama maana yake ni ndoa kuvunjika, siku anakuja atakuja kwa adabu na atakuja kwa terms zako, na kama haji, ujue umekwepq kifo!

Hawa wanawake mdogo wangu wanakuchimbia kaburi ukiwa hai ili uingie taratibu taratibu.
 
Hata mambo madogo mpaka muyalete humu?
Kanunue chupi moja ya mtumba ya kike, skin tight moja ya kike na khanga moja zote za mtumba. Zifue na nguo zako, zianike nje alfajiri kisha nenda kwenye shughuli zako.
Mashoga zake wakiona hiyo chupi ya kike imeanikwa watamfikishia habari na majibu utakutana nayo jioni ukirudi kazini.
bonge la technic
 
Watu wanakushauri usimfuate lakini jaribi kuangalia chanzo hadi kuondoka,Umesema uliamua kumpa adhabu ya kumnyima chakula,Hilo ni kosa lako la kwanza,Unadhani ukimnyima chakula yeye atavumilia njaa? Unadhani hadi leo Hali uko alipo?
 
Wiki imeisha yupo kwa dada yake je? Nimfuate au niendelee kumsubiria

Maana mm nimesema siwezi mfuata hata kwa dawa huyu mama watoto wangu ambaye ni jeuri.

Ugomvi ni baada ya kujibishana halafu yeye akanijibu simtishi kwa lolote. Hivo nikamwambia sitamwachia hela ya kula tuone akajibu sawa nisubirie kama atatetereka.

Siku tatu tu akakimbia kwa dada yake anataka nimfuate.
Hapo wote mnamakosa,

Mosi, Wewe mwanaume kosa lako la kumnyima chakula.

Hata ugombane vipi suala la chakula na matumizi ya nyumbani ni ya lazima kwa mwanaume kuacha nyumbani.

Kumbuka huyo siyo hawala wako. Huyo ni mke halali wa ndoa.

Kutokumhudumia unataka nani amhudumie Bure bila kumla? Kutokumhudumia unapata wapi uhalali wa kumuita mke?

Kosa la mkeo ,

Mosi, Ni kuondoka nyumbani kwenda kwa dada yake.

Alipaswa akiondoka nyumbani aende kwa wakwe zake.

Yaani ndugu wa mumewe . Kwao hakupaswa kwenda maana huko hayupo tena.

Huko anaenda kwa KIBALI Cha mumewe.

Sasa Kwa kuwa wote mnamakosa ,Basi sameheaneni muanze upya.

Siku nyingine msirudie hayo makosa .
 
Kama huna mchepuko..
Tafuta mwanamke wa Kuzugia,,awe anakuja geto kwako,,,akipritend kama MKE,,ili Majirani wamfikishie taarifa,,atarudi
 
Back
Top Bottom