Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Habar wakuu,

Kwanza niseme TU kisa hiki ni Cha miaka mingi ya nyuma sn ilopita ya ndoa yangu na MKE wangu MAMA G.
Kiukweli miongoni mwa ndoa zilizopita misukosuko mingi miaka 5 ya kwanza ya kwangu naweza kusema ilikua mojawapo.

Misukosuko hii nashkuru iliweza kutujenga imara mpk Sasa naweza kusema sijutii kuoa na naweza kusema nmebahatika kupata MKE Bora kabisa maishani, yaliyopita Si ndwele. Tugange yaliyopo na yajayo.

Anyway,
Nawaletea kisa Cha misukosuko ya ndoa yangu ambapo MKE wangu baada ya ugomvi mkubwa alidai talaka na kutaka tufuate sheria ili tugawane Mali, sema nilichomfanyia nilimnyoosha alijuta na hatosahau maishani mwake na mpk leo Hata tugombane vipi.

Kauli ya "TUGAWANE MALI" ilikoma na hawezi Tena kurudia kuitamka Tena.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
TWENDE PAMOJA SASA
Miaka hiyo baada ya masomo,
Mzee wangu aliniamini Sana akanipa biashara yake flani niisimamie na kweli niliisimamia vizuri na ikafanikiwa kuzaa biashara nyingine mpya.

Mzee wangu huwa sio mchoyo wa fadhila, alininunulia gari Kama zawadi na pia Kama usafiri kurahisisha mizunguko kwenye hizo biashara zake nilizokuwa nasimamia. Nikawa nasimamia biashara za mzee huku nikiwa naishi nyumbani.

Changamoto za biashara ya mzee, ilikuwa inanikutanisha na warembo sana, wahuni na wapenda starehe wa kila aina hapa mjini. Kwahiyo kama kijana nikaanza vijitabia flani hivi vya wanawake. Maana MDA mwingi nilikuwa natembea na pesa mfukoni halafu kipindi kile ukiwa na usafiri plus umaarufu walikuwa wanakuja wenyewe.
Biashara yetu Kuna MDA ilikua inadhamini fashion show na mashindano ya warembo n.k yote ilkua ktk kujitangaza,sometimes kupush uuzaji wa vinywaji.

Kwahiyo jina la biashara ya mzee ilikuwa kubwa, pia langu lilikuwa kubwa eneo lile maana ndo nilikuwa msimamizi mkuu. Kwahiyo suala la kutembea na mrembo nnaemtaka Hata halikuwa issue maana sikuhitaji kujitambulisha Sana, nilikua nafahamika sana.

Sasa kuna kipind nilipita Kwani mdada flani maarufu sana alikua anagombea umiss ktk wilaya Moja Hapa dar na ile show,mazoezi na maandaliz yote yalilikua yanafanyika kwny ukumbi wetu. Nilivomuona nikampenda Basi tukaanza mahusiano. Mashindano yalivoisha Akawa nafas ya 3 na kwenda kushiriki mbele zaidi na kua maarufu sn hivyo kutokana na umaarufu wa yule dada mahusiano yetu yakajulikana sana town na mzee taarifa zile zikamfikia.

Mzee wangu sio mtu wa kukurupuka,
Aliniita na kuniweka chini kunishauri mambo kadhaa wa kadhaa na kunionya khs tabia niliyoianzisha na hatari niliyomo na pia kipind icho ukiskia ukimwi Ni ukimwi haswa akanipa mifano ya Watu walioangamia kwa Njia niliyoingia Mimi. Kisha akanishauri Kama nmeshindwa Ni Bora nitafute mwanamke nioe atagharamia mahali na kila kitu mwenyewe. Mahusiano Yale yafe haraka sn na hii tabia ya umalaya ife Mara Moja.

Always sipendi kumwangusha mzee wangu,nikamuahidi nitalifanyia kazi nipe MDA kidg. Mzee akasema sawa. Baada ya kukaa Nikachambua ktk list ya wanawake wengi nilokua nao,nikaibuka na binti mmoja mrembo sana, ila maisha yake ya kawaida Sana sio mtu wa Bata na umri wake miaka 19 na very submissive kwangu, ana heshima, adabu na utii Sana japo huwa namzingua sometimes ila nikiangalia moyoni mwake ananipenda Sana na kweli naona naweza kummudu na sio wale wa kwenye umiss,fashen show n.k

Basi nikaanza kumuweka karibu binti,
Nilipompa wazo binti kutaka kumuoa akakubali na kwenda kumtambulisha rasmi kwa wazee. Baada ya utambulisho Mzee na bi mkubwa walisita Sana maana binti hakua amesoma sana na alitoka mazingira flan ya kiswahili sana uko magomeni.

Bi mkubwa alimkataa Moja kwa Moja, ila mzee nikivomfafanulia akanielewa maana mzee wangu ananiamini Sana.
Bi mkubwa alimkubali binti tu kwa shinikizo la mzee, maana mzee akishasema ndio final say ya familia nzima na kweli mzee kalipa mahali, harusi na ndoa kubwa ikafungwa tukaanza kuishi pamoja na wife pale pale nyumbani.
 
HAUKUPITA MDA SANA,
Baada ya kuishi pale nyumban, misuguano ikaanza Kati ya wife na bi.mkubwa kila siku kesi wanazinguana mpk kurushiana Maneno makali. Migogoro ile ikawasiingilii inasuluhishwa kila mara na mzee. Mzee asipokuepo Basi najitahidi Kias chake kusuluhisha japo Kuna MDA naona kabisa bi.mkubwa ndo kazingua ila Sasa kumwambia live kua yeye ndo kakosea ikawa ni changamoto.

Ikawa napotezea ila bi.mkubwa akionesha ukali Sana na kupanic ili ionekane wife ndo kakosea,basi zigo lile naliangushia Kwa wife aonekane mkosaji yaishe. ila tukirud chumban wawili namfafanulia wife kwann nilifanya vile kwa bi.mkubwa ili kuweka mambo sawa, Basi ananielewa. YANAISHA.

Migogoro imeenda mpk mzee aliporudi nikamfafanulia magumu nnayopitia kuamua kesi zile za bi.mkubwa na wife, nashindwa nikae upande upi na kumuomba mzee Kama inawezekana nihame TU pale nyumbani tupunguze Hizi changamoto.

Kweli mzee kanielewa na kunambia kwny nyumba Yake kupangisha sehem flan ya wapangaji 6 apartment za chumba na sebule. Basi Kuna apartment moja mpangaji keshatoa taarifa atahama miez mitatu ijayo Kodi yake ikiisha kwaiyo nijiandae akitoka tu nitahamia uko na wife. Basi nikashkuru na kweli MDA ulipofika tukahama pale nyumban na kwenda kuishi mtaani kwenye iyo nyumba ya mzee.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
BAADA YA KUHAMIA NYUMBA YA KUPANGA
Wife alikuwa mama wa nyumbani na nyumba ile jumla tulikuwa wapangaji 6 na almost wengi walikua Wameoa ila wake zao wengi walikua mama wa nyumbani. Kwahiyo mizozo ya Hapa na pale kinamama ilikuwa haiishi.

Sasa pale home,
Wife wangu kwa heshima yangu alitambulika Kama mama mwenye nyumba, maana mzee wangu Ndo mmiliki wa ile nyumba. Na kila kitu pale mimi ndo nilikuwa nasimamia.

Changamoto ikawa kila wakigombana na wanawake wenzie kwenye mambo Yao ya umbea umbea huyu kamsema yule vile, yule kamsema yule kwa flani.

Basi wife anakivaa rasmi cheo Cha umama mwenye nyumba na kuanza kuwabughudhi wapangaji na kuwatishia watahama. Walioshindwa uzalendo kweli wakawa wanahama.

Wengine nikawa natumia ubabe kuwabakisha na kumkaripia sana wife aache tabia za kiswahili pale nyumbani. Mambo yakawa bado Ni changamoto, ugomvi na wapangaji kila siku hauishi.

Nilivyomshirikisha mzee akasema MKE wangu kiumri nmemuoa akiwa bado ni mdogo sana, nimvumilie akikua ataacha, nmempenda mwenyewe kwaiyo hili suala Ni la kuongea na upande wa ukweni, hasa upande wa kike (shangazi zake) niwaelezee hizo changamoto wamfunde vema binti Yao. Yeye Hawezi kuingilia kuja kujadili hizo ishu za kinamama maana Madaraka yote ya pale nyumbani na wapangaji keshanikabidhi Mimi. Nikasema sawa mzee.

Ikabidi kwenda Magomeni alikokulia wife, nikakutana na shangazi zake na kuwaeleza kila kitu, wakamuita na kumsema binti yao. Aliporudi ikawa kama vile kuna utulivu flani kisha akarudia Yale Yale, Ikabidi kurudi kwa mzee kuomba tena ushaur nafanyaje Alichonambia nmeshatekeleza, Ila hamna mabadliko.

Mzee kanishauri kwann Kama habadiliki nisimtafutie shughuli ya kufanya kumuweka bize, nimtoe pale nyumbani kushinda na wanawake wenzake maana ishakua kero Sana. Akanishauri nimfungulie duka awe anashinda uko siku nzima atakuwa anarudi jioni tu. Nikaafiki wazo Lile.

NIKAMFUNGULIA DUKA WIFE

Akawa anashinda dukani anarudi nyumbani jioni, ile plan ya mzee ikawa nzuri sana imefanya kazi. Ule uswahili uswahili na ugomvi kila Mara nyumbani ukawa umekufa.

Sasa duka Lile Akawa anauza yeye ila nalisimamia mimi pia, namuongoza na pia kumkagua mahesabu mara kwa Mara maana Mimi kushinda pale dukani ilkuwa ngumu maana muda mwingi nilikua kwny kusimamia biashara za mzee.

Wife aliifanya biashara ile vizuri sana,
Ikafikia kipindi wateja wakazidi uwezo wa duka, wife akanambia Hapa tuongeze mtaji. Kweli nikaenda kumpa taarifa zile mzee. Mzee alipotutembelea kafurahia na kutuongezea mtaji. Basi Tukatoka kwenye kuuza reja reja na kuanza kuuza jumla na rejareja.

Wife aliposhika ujauzito pilikapilika zile dukani zikawa changamoto, Akanambia anaomba awalete ndugu zake niwaajiri wamsaidie kazi pale dukani. Nikasema hapana, ndugu zake kwenye biashara yangu hata bure sitaki.

Ndugu zako siwajui uwezo wao halafu wanaweza kuleta ushemeji mwingi wakanitia hasara halafu kuwachukulia hatua siwezi maana Ni ndugu zako. Ni Bora tu kuajiri Watu baki ambao nawajua uwezo wao, ili wakizingua tu tunazinguana bila kuoneana aibu Wala kupepesa macho. Akawa kanung'unika ila Kama baba wa familia tayari nishaamua. Imepita na haipingwi.

Basi Ikabidi kuajiri vijana wawili wa kumsaidia nnaowafahamu uwezo wao kutoka kwenye biashara za mzee, mmoja wa stoo na kutoa mizigo ya wateja, mwingine wa kuandika Oda za wateja. Huku wife akisimamia mauzo yote na ndo muhasibu na meneja mkuu pale.

Sasa ikafika kipind wife miez 2 kabla ya wife kujifungua, ikabidi nimpumzishe kuja dukani.
Ikabidi duka tumuachie yule kijana wa kuandika Oda alisimamie na kuandika Oda na kufunga hesabu. Baada ya MDA kijana yule kaniomba nimuongezee Nguvu maana anaelemewa. Nilivyompa wazo Lile wife, akang'ang'ania Kaka yake mmoja Hana kazi aje akasaidie. Nikakubali, Ila Tukakubaliana kuwa akizingua ajue sitoleta ushemeji, nitamzingua live Kama nnavowazingua vijana wengine Watu baki. Sina masihara kabisa kwenye maswala ya pesa. Wife kasema ndio. Kweli yule Kaka wife kaajiriwa na kuanza kazi rasmi.
 
BAADA YA WIFE KUTOKA MATERNITY
Ikiwa Ni miez 5 tangu wife hayupo dukani, kakuta duka linaenda vizuri sana na kumsifia kijana yule tuliemkabidhi duka kuwa kweli tumepata kijana Safi.
Japo alikua wasiwasi nae mwanzoni.
Kijana kafanya Kazi nzuri kulisimamia duka na kuwasimamia wenzie.

Sasa utamu wa ile biashara ukakolea, faida nikawa Naiona na nashkuru Mungu, Nikanunua kiwanja na kuanza ujenzi wa nyumba ya familia mdogo mdogo, pia nikashawishika kufungua tawi jingine, sehemu nyingine ili kuongeza faida. Ikabidi pale abaki wife na kule tawi jipya na changa nikampatia yule kijana wa oda aliesimamia hili duka kubwa vizuri akasimamie na Lile jipya tusongeshe gurudumu. Na maduka yakawa rasmi mawili.

Sasa baada ya Yule kijana wa oda kuelekwa duka changa, na wife kubaki duka kubwa Kama msimamizi mkuu.
Nikaanza kuona shoti za ajabu kwenye mauzo. Hela haionekani na mzigo stoo unapungua sana. Nilipomhoji wife nini kinaendelea nikaona majibu yake hayaeleweki. Ikabidi kufanya uchunguzi, nikagundua kuna mchezo mchafu unafanyika pale dukani Ikabidi kuweka mtego.

Sasa Kuna siku mteja mmoja tulimkamata na mzgo ya wizi haikulipiwa,
Yaan Mteja alinunua friza ila ndani ya friza Kapachika redio kubwa moja ya CD ambayo haikulipiwa Wala Kwenye Oda Yake haikuepo. Alipohojiwa akasema hajui imefikaje ndani ya friza. Alipofikishwa polisi na kufinywa kidogo. Akasema aliambiwa na kijana wa stoo (kaka yake wife) ajazie elfu 50 apewe na redio free ila itafichwa kwny friji atoke nayo kijanja isionekane.

Halafu pesa atampea uko mtaani. Basi Baada ya kupata zile taarifa kaka yake wife tukamkamata na kumpeleka polisi. Na nikawapa tip maaskali wasimtoe wamfinye zaidi aseme michezo mingine michafu aliyowahi kufanya pale dukan.

Kule ukweni pakawaka moto kwanini nimemuweka shemej yangu ndani hata kama kweli kaiba, Ina maana nilimleta mjini kumtesa. Lawama zikaenda kwa wife. Wife akaniomba nimtoe ndani. Nikamkumbusha wife ahadi yetu kuwa kwenye kumchukulia hatua mhalifu nilishaahidi kua sitoangalia ushemeji. Kwahiyo ataendelea kukaa ndani mpaka pale maaskari watakapomaliza uchunguzi wao kumhoji Kaka Yake.

Wife alinung'unika sana Ila sikujali. Nilikuja kumtoa dogo baada kukiri kuhusika kunipiga mizigo mingine ya thaman ya mil 1.3 na nikawaambia nduguze kuwa wazilipe hizo pesa ndo ndugu yao atolewe ndani.

Wakajua masihara ntaleta ushemeji,
Kweli nikawakazia na nilikuja kumtoa siku ya 7 pale ndugu zao walipojichanga na kunilipa laki 9.5 Kati ya mil 1.3 nyingine wakasema niwape MUDA, moyoni nikasamehe na Kaka wife akaachiwa na nikamtimua rasmi dukani kwangu. Na kule nilikokuwa nmewapangishia anaishi na vijana wa dukan kwangu, nikamwambia akasombe kila kilicho chake aondoke, simtaki tena kwenye mazingira yangu. Ikaisha hivyo.
 
BAADA YA SHEMEJI KUONDOKA,
Wife akaendelea kusimamia duka kubwa Ila Sasa duka kubwa likawa kila siku linashuka, ikawa nachukua pesa kwenye biashara za mzee najazia kupunguza mapengo na kukamilisha Oda za wateja. Duka likawa linashindwa kujiendesha lenyewe.

Hali ilipozidi Ikabidi kufanya maamuzi magumu ya kubadilisha wasimamizi wakuu. Wife nikampeleka duka dogo, duka kubwa nikamrudisha kijana wa oda alisimamie. Nione ltakuaje. Cha kushangaza aliporudi kijana wa Oda duka kubwa likatengamaa, Ikabidi nimuache hapo hapo kwa muda. Wife kila akiomba kurudi duka kubwa kwa visingizio lukuki nikawa namwambia subiri, nakufahamisha.

Wife alizidiwa akaanza kutengeneza majungu kuwa kijana wa oda ananipiga dukani, Kuna baadhi ya accessories za dukani kapeleka kwake kule nilikowapangishia anatumia nje ya utaratibu. Ikabidi kwenda mwenyewe kuwakagua kujiridhisha maana funguo za akiba nikikowapangishia ninazo, Kweli nikakuta baadhi ya vitu vya dukani vipo kule ila Ni vitu vidogo TU vya kawaida kama redio ndogo ya kaseti, ndogo tv 18" chogo na kifriji kidogo Cha mlango mmoja.

Kimoyo Moyo nikasema nikimgombeza sana huyu kijana kwa vitu vidogo Kama hivi nitakua namuonea sana Maana ananiingizia pesa ndefu Sana kuliko hata hivi vitu vidogo. Kwaiyo nikamuita akiwepo wife nikamuonya kuwa alichofanya sijapenda akitaka chochote aniombe sio kujichotea tu, akakiri kosa, Kisha nikamsamehe.

Wife kaanza kulaumu kuwa nna ubaguzi, ndugu yake nilimfunga selo ila huyu kijana wa Oda nambeba Sana na Nampa umuhimu kuliko yeye ndo Maana nmemtoa yeye duka kubwa na kumpeleka duka dogo. Nikamwambia wife huyu kijana kateleza kwenye kutoa taarifa tu ila sio mwizi. Akifanya biashara juhudi zake tunaziona ila Yule mdg wake aliyemleta alikuwa ni mwizi kabisa halafu kukiri kosa alishindwa ndio maana nilipeleka polisi akafinywe aseme ukweli. Basi wife kanungunika Sana. Ila sikubadili maamuzi yangu. Kijana akaendelea na kazi

Wife alipoona siku zimeenda duka kubwa harudishwi, Ikabidi aende kuniselemea kwa mzee nilichomfanyia. Mzee kaniita nikamsimulia kila kitu. Mzee akatuita wawili mezani na kutusuluhisha huku akisema nimrudishe wife Mara ya mwisho duka kubwa kwa heshima yake. Ila akishindwa kulisimamia Mara hii, ndo Basi atarudishwa Tena kule duka dogo. Basi nikakubaliana na alichosema mzee na wife akarudi duka kubwa tena.

Baada ya wife kurudi duka kubwa,
Kuna kipindi flan mzee wangu akaugua Sana, kwahiyo nikawa kwenye pilika pilika za kumuuguza huku nikisimamia biashara alizonikabidhi pamoja na za kwake mwenyewe mzee kabla ya kuumwa, bila kusahau kuwapitia wife na kijana wa Oda kuwakagua kila Mara. Kwahiyo Mizigo ukawa mkubwa sana. Naelemewa.

Ikabidi niwaite wife na kijana wa Oda mezani na kuwafundisha nnavyoagiza mizigo, TRA, na upigaji mahesabu, madeni yangu na marejesho yote benki nnayodaiwa, nnavyolipa hadi nnapoagiza mizigo na mbinu zote za kuzungusha pesa ili wajisimamie wenyewe, mimi nmetingwa sana. Kweli wakasema wameelewa somo.

Kisha password za account zangu za biashara zote mbili nikawakabidhi waweze kuwa wanafanya miamala wenyewe kuagiza na kuuza wenyewe. Kila mmoja asimamie duka lake Moja kwa moja kwa Uhuru.

Sasa nikawa Kama nmejitoa,
Nikawa napita TU Mara Moja moja kuangalia maendeleo ila siwafatilii Sana, changamoto Ikawa kwa wife, duka lake halikui na mwendo Ni ule ule wa Kobe. Kule duka dogo kijana wa oda akawa anafanya vizur sana, duka likakua kwa kasi Sana kiasi kwamba baadhi ya Oda zikawa zinatokea kule duka dogo la kijana na kulihudumia duka kubwa. Ikanishangaza Sana.

Nilipoenda kumtembelea kijana,
Nikagundua kuwa dogo keshajiongeza, deni la benki kesharejesha lote kamaliza na hadaiwi, nikamwambia tukachukue mkopo mwingine tuboost akasema hapana mzigo anao mwingi stoo akaenda nionyesha tukikwama ndo tutakopa. Kwasasa tukomae maana kajenga maelewano sana na wale supplier wangu na kapata wengine wapya na wengine wamemuamini sana wanampa Hadi mizigo ya Mali kauli na mzunguko upo anarejesha vizuri pesa zao bila tatizo. Kiukweli Nilifurahi Sana.

Ikabidi kukaa na wife mezani na kumuelekeza anapaswa awe Kama kijana, yeye kwake anasua sua Sana na akizubaa duka la dogo litakuwa ndio duka kubwa sasa na yeye atapitwa. Wife akawa anasema hapendi kulinganishwa. Anafanya kilicho ndani ya uwezo wake, hafanyi mashindano.
Nikambwambia sio mashindano, kijana yule Ni mfano Bora, mpambanaji sana. Kanikosha mno.

Sasa Kuna kipindi duka kubwa likayumba sana, mpaka nikasikia benki wananipigia Simu kila mara marejesho yanachelewa sana. Ikabidi nimuulize wife tatizo nini, akasema biashara ngumu, nikamuacha.

Baada kuona mambo yanakwenda ndivyo sivyo kwa wife duka kubwa linayumba, Kuna mfanyabiashara hapo pembeni jirani yangu Na rafiki yangu nikabidi nimuite nimuombe ushauri nafanyaje simuelewi wife. Hivi na kwenu kunayumba Kama kwangu.

Alichonambia Ni kwamba kuyumba kwa duka kubwa lazima kuwepo maana wife kamfungulia duka, yule kaka wake niliemfukuza Hapa, tena biashara Aina Hii hii na mizigo mingine akishaagiza wife huwa inatoka Hapa Hapa, inakwenda kwenye duka la Kaka ake. Kama nabisha Kuna siku ile gari inayokuja kuchukua mizigo ya dogo ikifika ntakwambia uifatilie uone mizigo itaenda wapi. Itakapofika ndo hapo hapo yule Kaka wife kafungua duka. Dah! Nikabaki na mshangao, ila nikajipa Muda nilichunguze Hilo. Gari ikifika nistue jiran yangu. Kasema ndio.
 
SIKU YA SIKU IKAFIKA
Jirani na rafiki yangu akanipigia Simu kuwa mzigo duka kubwa ndo umeingia, na ile gari ndo imefika dukani inasubiri kufaulisha mzigo mwingine. Wee ukifika usifike dukani bana njia wanayotokea Kisha wakishatoka wafatilie uone mpk watakapofikisha mzigo husika.

Ikabd kuwatonya maaskari wawiki kupata backup na tuifatilie gari wanisaidie kuikamata pamoja na kaka wife Kama wezi wa dukani kwangu maana mizigo Yao ile itakuwa Haina risiti. Kweli wakakubali ile gari tumeiona na kuisubiri.

Ile gari imefaulisha mzigo Kisha kuondoka pale, tumewafatilia mpaka tukaona walipoifikisha.
Kaka wife kaja kuipokea, nikawatuma maaskari wakakague vitashuka vitu gani, kweli wakanitext kuwa njoo uone nikafika na kukuta mzgo wa pesa ndefu mno ulijazwa ile Gari.

Kaka wife akaanza kurusha Maneno mabovu nikawambia maaskari ile gari na mzigo wote na hao jamaa akiwemo Kaka wife waende polisi, maelezo mbele ya safari, Tutajua mbivu na mbichi kule kule kituoni. Kweli wote wamesombwa tumeelekea kituoni.

Tumefika polisi hata hatujaanza kutoa maelezo namuona wife kafika. Ghafla nawaona ndugu wa ukweni nao wamefika. Sikumsemesha yeyote pale. Kaka wife akatoa maelezo anasema ule mzigo Ni wa kwake kanunua duka Letu, Akaulizwa risiti iko wapi, akasema huwa wanapeana TU kwasababu wanaaminiana, kaulizwa khs ushahidi wa malipo akasema pesa wanatumiana kwny account ya benki ya duka. Anamuangizia pesa na sio kwamba kabeba TU vitu kiwizi wizi kutoka dukani kwetu kupeleka kwake.

Ikabidi maaskali wanambie nikafate bank statement wajiridhishe asemayo, nikawambia Kadi ya Hilo duka anayo wife nje, ngoja nimfate anipatie. Nikamfata wife nje anipe Kadi ya benki, nikafate statement akagoma. Nikarudi kuwaambia maaskari, wakamshurutisha Kadi ya benki akanipatia nikaenda benki kuchukua bank statement ya Miezi 6 page za kutosha nikaone hiyo miamala anayosema Kaka wife huwa anampa pesa amuagizie mizigo iko wapi.

BAADA ya kuichukua bank statement, na kuikagua Nikagundua hamna muamala wa maana Zaid ya fedha nyingi kuonekana wife ndo hutuma kwenye account ya Kaka yake kutoka kwenye account ya duka Na kibaya zaidi miamala mingine imefanyika kipindi ambacho marejesho ya benki yanakaribia hivyo kusababisha benki wakitaka kukata Deni lao la mkopo inashindikana wanakuta account Haina fedha za kutosha. Na wakiona siku zimepita pesa haziingii ndo wananipigia Simu Mimi.

Kwani akili ya haraka haraka maaskari na Mimi tukajua kumbe wife ananihujumu maksudi kabisa. Analalamika biashara hamna, marejesho yamegoma kumbe pesa zote anatuma kwa Kaka Yake afanye biashara. Huu Ni uhuni Hadi maaskari wakanishangaa nina MKE wa Aina gani, ndoa gani hii, hamna ndoa Hapa. Nnapoteza Muda, This is inside job.

Sijakaa sawa baba mkwe kafika pale na kuomba kesi ile akaimalize mwny kifamilia. Maaskari wakaniuliza Kama naridhia maana pale hamna kesi tunapoteza muda, mwenye tatizo Ni mkeo anaemtumia pesa sio Kaka yake. Ikabidi nikubali tuondoke pale tukayazungumze nyumbani kifamilia.

Tumetoka pale,
Baba mkwe akanambia nitangulie Magomeni yeye atakuja, alikuja gafla TU pale polisi, kaacha KAZI ya Watu, nikasema Haina shida ba mkwe.
Nmefika ukweni ikabd niwasimulie shangaz zake na wife nilowakuta khs yaliyojiri, wife na akasema yake, Kaka Yake nae akajieleza yake.

Cha kushangaza shangazi zake hao wakawa hawashtuki kilichotokea.
Wakadai yule ni mwanafamilia Kama alivyo MKE wangu, huo sio wizi Wala hujuma, bali pesa inarudishwa kwny familia, nikifariki wanangu watalelewa na hao hao wajomba zake ninaohangaika kuwapeleka polisi ili kuwafunga jela.
 
ZAIDI ZAIDI
wakaanza kunishambulia mimi kwa kitendo Cha kipind kile kumuweka ndani Kaka Yake wife alivoniibia redio na kutia hasara ya mil. 1.3 dukani. wakadai siwezi kusema chochote wakanielewa Mimi Ni mnyanyasaji na katili sana. Kwanza wanamshangaa sana binti yao kwañn Yuko na Mimi mpk sahv, anawezaje kuishi na Mume katili aliewai kumuweka ndugu yake selo. Anaitia familia Yao mikosi.

Nikawaambia kumbe Hapa hamna usuluhishi,Naona tayari Watu mna majibu Yenu. Wakasema "utajua mwnyw bhana, wee Kama umemchoka binti yetu, tuachie tu sio kumnyanyasa na kutudharaulisha kisa hivyo vi pesa vyako"
Nikawauliza, "kwaiyo Maneno yote mnataka hayo nimuache binti yenu?"

Wakasema
"muache hata sahv, unadhan atakosa Mume huyu? Umenoa sasa, binti yetu bado mdogo na mrembo Sana, unamuacha leo na KESHO wenzio wanaoa vizur TU, wanaume wengi Sana hapa mjini. Upo apo? "
Duh! Nikabaki na mshangao.

Nikawauliza,
"Kwaiyo Inamaana mmeniita Hapa kunichamba na sio kusuluhisha?"

Wakasema,
"Kwani alilokuita hapa Nani?
Umekuja TU na kiherehere chako kusemelea kwa baba mkwe wako Kama ulivozoea, mwanaume gani unashindwa kua na misimamo kila kitu unakuja kusemelea ukweni, kua na maamuz bhana, umemshindwa binti yetu turudishie TU."

Nikawaambia,
"Kwaiyo nyie lengo lenu niwarudishie binti yenu sio? Haina shida. Basi huyu Hapa leo namuacha Hapa Hapa. Naondoka"

Nikamwambia wife
" MamaG nadhan umeskia yote waliyosema ndugu zako, haya sasa kuanzia leo Mimi na Wewe bhasi, naondoka na usinifate na hamtoniona Tena nmetia mguu wangu hapa"
kweli nmeinuka pale na kuelekea kwny gari, kuwasha na kuondoka zangu.

Nmeshafika nyumban,
Nna hasira zangu Baba mkwe akawa ananipigia nirud kule tuyazungumze Tena,yeye hakuepo,anaomba radhi wale dada zake wamenikosea Sana heshima kunitukana, Nikamwambia
"Baba mkwe nakuheshimu Sana, sijawai kua na ugomvi na wewe ila kwa matusi nilotukanwa kule ukweni na shangazi zake MKE wangu, kiukweli siwezi kuja uko tena daima na maamuz nilochukua ni kwamba nmemuacha binti yako rasmi. Kuanzia Leo Mimi na yeye Basi. Usinitambue Kama mkwe wako tena" nikakata simu.

Nikapanda kitandani na kulala,
Kulipokucha nikaamkia duka kubwa kukaa mwenyewe kulisimamia,
ilipofika mida ya saa 4 asbh wife kaja dukan anataka naye aendelee kuuza.
Nikamwambia arudi uko uko alikotoka kwa ndugu zake, Mimi na yeye bhasi.
Wife akasema,
"Siwezi kurudi kwetu kienyeji Mimi,hujaniokota barabarani umenichukulia kwa wazazi wangu kwaiyo utanirudisha kwa wazazi wangu"

Nikamwambia,
"Jana tulikua kwa wazazi wako nilikokutoa, wamenitukana Vya kutosha, kwaiyo kule kule nilishakwambia rasmi nmekuacha na wameridhia, kwaiyo ieleweke kuanzia leo Wewe sio MKE wangu. Ondoka Hapa kabla sijatumia nguvu kubwa kukutoa na ukikaidi ntakupiga ntakudhalilisha. Mliyonitukana Jana nyumbani kwenu yanatosha"

Wife akasema,
"Wee Kama unadhan utaniacha kizembe hivyo sahau, uwezi kunifanya chochote kile labda uniue. Nakwambia hivi hili duka pia Mali yangu na Mali nyngn ulizonazo tumetafuta wote nazo tunagawana nusu nusu. Mi sio mjinga Kama unavofikiria. Haki yangu lazima ipatikane"

Nikamuuliza,
"Unasemaje wewe? Haki ipi unazungumzia? Unataka kugawana nusu nusu na nani labda? NaKwa Mali zipi labda za kugawana nusu nusu?"

Akasema,
"Utajua mwenyewe bhana, ila Hilo Duka letu na Lile pagale lako jua lazima tutagawana nusu nusu. Siondoki Hapa labda uniue."

Nikamjibu,
"Sasa kwa taarifa yako, mimi siogopi kugawana mali, na Kwan sababu umeng'ang'ania kugawana, Mimi nakuachia kila kitu uchukue mwny ntaanza upya. Wee Ni mwanamke mpumbavu Sana, miaka 4 TU ya ndoa tayar ushaingia tamaa ya Mali. Na tunakoelekea tukiendelea hivi kutafuta pamoja Kuna siku zikiwa nyingi zaidi utaniua ubaki na mali. Sasa ngoja nitafute usafiri nikupe kila kitu."

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
PALE PALE
nikapiga Simu fuso likaja dukani likapaki nje, nikatoka nje nikaenda kwnyw kijiwe Cha Draft na kahawa nikaomba nipate vijana 15 Kuna kazi ya haraka nusu saa tu kila mtu ntampa elfu 5. Vijana wakaja 10 na kusimama nje dukani.

Mbele ya wife nikawambia,
"Mmemuona uyu shemej yenu hapa, kasema anaomba tugawane hii Mali mnayoiona ndani ya duka.
Hii ndio kazi nilowaitia Hapa,Kwaiyo nnachowaomba sasa, kazi yenu sio mgawanishe hizi Mali nusu nusu.
Bali Nawaomba msombe kila kitu humu ndani mpakie humu kwenye hii fuso Kisha mtanipelekea ukweni pale magomeni sio mbali, MKE wangu na wazazi wake wakafungue duka lao wauze." Vijana Wakabaki na mshangao.

Wengine wakaanza kumshangaa wife imekuaje katoa kauli zile,Nini kimetokea, Tamaa ya namna gani ile, Hapa mnadhalilishana tu na kuwapa Watu faida. wife akaanza kujitetea kua chanzo kimeanzia mbali. Nikasema mimi sijali tulikoanzia.

Najali kauli yake na naifanyia kazi hivi Sasa,na Nampa anachokitaka.
Baadhi ya vijana 3 wakasema wanajitoa hawawez kushiriki, wakabaki vijana 7. Nikawaambia nyie fanyeni kazi ntawalipa peas yenu.

Wakadai kazi ni kubwa sn. Nikawambia ntawaongezea pesa, nnachoomba duka lote hili lisafishwe toeni kila kitu na mfagie kabisa. Wakasema POA na kuanza kutoa vitu kdg kdg kupakia kwny fuso.

Ghafla wife akaanza fujo ili kuwazuia vijana wasitoe vitu dukani, umati ukajaa pale na wenye maduka ya jiran nao wakasogea baada ya kusikia Hilo zogo. Umati Wote ule pale nikawaambia kua
"Mnamuona Uyu shemej yenu Hapa, ana tamaa sana ya Mali huyu mwanamke, tumegombana kasema Anataka tugawane mali, kwaiyo zoezi linaloendelea Hapa msishangae, Mimi Nampa Mali zote Hapa hapa, ntaanza upya mwnyw, na vijana wakitoka Hapa wanaenda kusomba na kule nyumbani tunakoishi Hadi kijiko sitaki kukiona ndani, wampe akaanze maisha yake mapya mwenyewe. Tunakoelekea ataniua"

Baadhi ya Watu wakaanza kumshangaa wife, baadhi wakawambia kakosea aombe radhi, baadhi wakanilaumu kua hata kugawana hakuko hivyo nimpe talaka kisheria twende mahakamani tukagawane.Nikawaambia,
"Sina Muda wa kupotezea kutenga vikao na kwenda mahakamani, Kama Ni talaka naweza kuandika hata Hapa Hapa nipeni karatasi niandike.
Ila mimi kwenda mahakamani kupotezea Muda ili kugawana mali hapana. Tunamalizana Hapa Hapa leo leo kila mtu akaanze maisha yake mapya kivyake. Huyu mwanamke namuachia kila kitu. Hata akitaka boksa zangu namuachia ntatembea mapumb wazi kengele zinagongana. NAANZA UPYA KABISA KUANZIA LEO"

Hakukawia Sana, vijana wakaijaza fuso mzigo. Nikawaambia pesa yenu ntawalipa msiwe na wasi, nawapa kazi ya pili. Nikamwomba yule dreva fuso aniitie CANTER ije Hapa kama kuna mtu wa haraka haraka anamjua. Akasema POA anampigia. Kisha Nikamwambia kijana wa dukani kua iongoze hiyo fuso iliyojaa mzigo mpk ukweni magomeni anapajua na ahakikishe huo mzigo wote unaingizwa ukweni na unamwagwa wote pale kiwanjani kwao hiyo fuso inarudi tupu. Kijana akasema sawa kanielewa. Fuso ikaondoka.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
MZOZO UKAENDELEA,
Watu wakinisihi tuyamalize pembeni Hapa mjini tunawafaidisha Watu, nikawambia Sina MDA wa kupoteza kwenda mahakamani. Na Hilo pagale analodai tugawane Kama Kuna mtu anapesa Hapa aseme naliuza cash pesa yote mpeni huyu Mwanamke akaanze maisha yake. Kama hamna Basi niitieni dalali liuzwe leo leo silazi damu Mimi. Watu wakamsihi wife ashuke pale aombe radhi anadhalilika yeye. Wife akaanza kujishusha nimsamehe Lile neno lilimponyoka TU bahati mbaya. Nikasema maamuzi yangu Ni hayo hayo. Sirudi nyuma. Kazi iendelee.

Hatujakaa Sana,
CANTER tupu ikaingia, nikawaambia vijana wapande twende nyumbani nako tukapakie kila kitu vitu vya ndani navyo vipelekwe Magomeni. Vijana wakasema utatuongezea hela, nkwambia hamna shida ntawaongezea. Vijana wakapanda, CANTER ikang'oa tukaelekea nyumbani. Tulipofika hatukua na muda wa kupoteza vijana wakaingia ndani haraka na kuanza kusomba vitu kuingiza kwny Gari.

Ghafla wife na baadhi ya wafanyabiashara wenzangu wakafika pale nyumbani kunisihi niache vile nilikuWa nakifanya, namdhalilisha wife.

Wife akawa analia na kuwazuia vijana wasitoe vitu kwenye Gari. Vijana wanaingiza, kwenye Gari wife anatoa anarudisha ndani. Vijana wanamsukuma pembeni kuwa wao wako kazini asiwaingilie.

Mzozo ukawa mzozo majirani mtaani pale wakajaa, nikawaambia pale,
"Wote Mmemuona huyu shemej yenu, tumegombana tu anasema tugawane mali. Sasa Mimi Sina MDA mchafu wa kwenda kukaa mahakamani kupotezea ili kugawana mali,Nampa kila kitu Hadi kijiko nisikione ndani kwangu, Leo rasmi naanza upya. Kule dukan, fuso tayar lishapakia mzigo wote wa Dukani linaelekea kwao magomeni Kwenda Kufungua duka ukweni.Na Hapa Hii canter mnayoiona itasomba mzigo wote wa vitu vya ndani na kuelekea kwao kule kule magomeni. Kwaiyo Nataka Akafungua duka lake magomeni na akaanze yake maisha mapya magomeni. Sina Muda mchafu wa kugawana Mali na mwanamke Mimi" wote wakabaki na mshangao.

Hatukukawia Sana mwenyekiti wa mtaa akafika na kunisihi tukayaongee ofisini ya mtaa, nikamwambia mzee nakuheshimu Sana Ila tutayaongea tayari nishampatia huyu mwanamke anachokitaka. Hapa niache tu nimalizie hili zoezi langu afu ntakuja uko ofsini tuyaongee.

Mwenyekiti akaanza kuniletea habar za kuniitia polisi nakaidi agizo lake. Basi nae mwenyekiti Tukajibizana mbovu sana, ugomvi karibu uibuke nimchape ngumi maana alianza kuminyooshe vidole. Baadhi ya Watu wakaamulia na kumtoa mwenyekiti eneo Lile akaondoka.

Wife akazidi kububujikwa na machozi anaomba yaishe, kelele zile Ikawa Kama nmeufunga mtaa sasa maana zilikuwa kelele kibao Sana pale. Sijakaa sawa nikaona ile fuso yenye mzigo wa duka inarudi na kusimama pale nyumbani. Kwenye fuso anatoka kijana wa dukani na baba mkwe. Sijakaa sawa taxi nyeupe nayo inafika iko na wale shangazi zake na wife wale walionitukana sana kipindi kile.

Baba mkwe kanifata na kuniomba radhi yaishe, chonde chonde nitulize jazba. Nikamwambia mzee kuwa unawaona hawa walokuja na taxi, walionitukana Sana nilivyokuja ukweni kusuluhishwa. Wakanitusi sifai na kusema niwarudishie binti yenu,Sina msimamo,mzee wa kusemelea nna kiherehere , najipendekeza kwenye ukoo wenu, binti yenu mzuri sana na matusi mengine lukuki.

Sasa mzee wangu nmeamua kutimiza haja yenu, nmemuacha rasmi binti yako na kila kitu hapa nampa Kama unavyoona ili akaishi kwa amani. Tena nampa mbele ya umati huu mtaa mzima unashuhudia Ili mbeleni uko Asije Sema nimemtelekeza, mimi ni katili Sana Kama shangaz zake walivodai.

Umati wote ule ukawageukia wale shangazi zake na mzee wao waliulizia ilikuaje. Ikabidi kuwasimulia matus yote na kejeli zote nilizotukanwa ukweli siku ile nilipofata suluhu.

Umati ule ukawa unawashangaa na kuwanyooshea vidole wale wakwe zangu, inakuaje mkwe wao anakuja wayazungumze kistaarabu mnamtukana matusi, kinachotokea Hapa mkwe wenu msimlaumu, mmeyataka weyewe na mmejidhalilisha Kama familia.

Baba mkwe akasema chonde chonde yeye hakuepo siku ya matusi, nisimjumlishe tuyaongee. Nikamwambia mzee Mimi hatuwezi kuongea chochote kama nawaona Hawa hapa walonitusi matusi ya nguoni mbele yangu. Ikabidi waambiwe warudi kwenye Taxi yao na kuondoka eneo Lile. Maana Hali ya hewa ishachafuka.

Wife akabaki analia machozi Hadi kamasi, kapiga magoti mbele ya umati kumuomba baba ake msamaha kakosea yaishe. Baba ake kwambia hajamkosea yeye kanisekosea Mimi.
Kaja anatambaa anaomba msamaha yaishe nnachofanya namdhalilisha yeye na familia yake pale. Amekiri makosa yake yote tuanze upya. Nikasema HAPANA Hapa mpk kieleweke.
 
HATUJAKAA SAWA
Kwnyw ule umati nikamuona jamaa mmoja Ni dalali namjua anapajua saiti kwangu, Nikamwambia nenda haraka sn katafute mteja Kwny ile nyumba yangu naijenga haijaisha, Nataka iuzwe leo leo pesa yote Mpatie huyu MKE wangu leoleo. Watu wakasema unachokifanya sio kizur.
Unamdhakioisha mkeo.

Nikawaambia huyu sio MKE wangu, ni muuaji ajae. Kwanza majirani mkisikia nmekufa ghafla fanyeni uchunguzi haraka, nmeuawa, nikimrudia huyu mwanamke atakuja kuniua ana tamaa sana na Mali. Bora niokoe maisha yangu kwanza, nimpe kila kitu aondoke, mimi bado kijana na Nguvu bado ninazo, ntatafuta tu vingine.

Hatukukaa Sana vijana wakawa wamemaliza kuijaza ile canter vitu vya ndani na wanarudishia turubai ili waondoke pale kuelekea Magomeni. Wife akaenda kumuinamia dereva anaomba Sana asitoe gari, amekosea saa, tena amekosea mno.

Nikamwambia dreva ngo'a gari usimsikilize huyo. Dreva kaiweka silencer kila akitaka kutoa wife anasimama mbele ya gari anasema Basi Leo Kama Gari hii inaondoka Hapa, basi nigonge na tairi nife kabisa. Sina maana kuishi. Basi dreva akawa anasita kuitoa gari.

Hatujakaa sawa,
Naona gari ya mzee wangu inaingia,
Mzee kashuka, kanifata na kunivuta mkono mpaka kwny Gari yake. Akanambia niingie kwenye Gari yake.
Nmeingia akaniuliza,
"Mimi Ni baba yako?" Nikasema "ndio"
Basi nakuomba usitoke humu ndani ya Gari mpaka ntakaporudi. Mzee akatoka na kwenda nje nikaona anazungumza na dreva wa Gari zote mbili canter na fuso.

Mzee akaenda kuzungumza na baba mkwe. Kisha akarudi ndani ya gari na kuwasha gari tukaondoka pale kuelekea Kimara nyumbani kwa mzee. Nikaona zile Gari mbili fuso na canter nazo kwa nyuma zinafata pamoja na gari nyngn mbili private na taxi Moja.

Tumefika nyumbani mzee kaingiza Gari yake ndani na kuamuru zile fuso na canter nazo ziingie ndani. Zile Gari nyingine zikataka kuingia, mzee akasema zibaki uko uko. Mzee akanifungulia na kunambia niende chumbani nikalale. Nikamwambia Wale vijana wa mizigo hawajalipwa bado.

Mzee akatoa pesa kawalipa vijana wa fuso na canter akawaambia watalipwa kesho, gari zao zitalala pale na ziko salama tuonane kesho asubuhi warudi na vijana wapakue mzigo wote Kisha watalipwa na usumbufu, wakasema POA wakaondoka.

Mzee kaenda nje kawaambia,
Kila mtu atawanyike aende nyumbani kwake anafunga geti lake hataki kuona mtu mazingira yake na kweli mzee akafunga geti Kisha kurudi kunishika mkono kunipeleka chumbani na kuniamuru nilale kwanza nipumzike. Kama kuna Chochote cha kuongea, basi tutaongea kesho, ikabid nitii amri ya mzee na kulala kutuliza kichwa pale pale nyumbani.

Kesho yake asubuhi nmeamka niko nakunywa chai, asubuhi nikaona dirishani kumbe baba mkwe kaja kuongea na mzee, wamekaa kwenye viti nje wanaongea Sana. Kisha nikaona baba mkwe anaondoka. Mzee nae Karudi ndani.

Nikamuuliza mzee alikuwa anasemaje huyo, akasema nipumzike kwanza Kama nmemaliza kunywa chai nirudi chumban kwangu kulala, sipaswi kutoka nje Wala kwenda popote pale bila ruhusa yake. Nikasema sawa mzee.

Kesho yake jioni,
Mzee kaiiita Kunisikiliza, nikamsimulia kila kitu. Mzee kasema kwa kilichotokea wameazimia na baba mkwe kuwa kila mtoto akapumzike nyumbani kwao. Mimi ntatulia Hapa kwetu na wife atarudi kwao. Kama kweli ndoa IPO basi itarudi Kama inafungishwa upya maana mpasuko uliokwishakuepo Kati ya familia hizi mbili Ni mkubwa sana, Ni Bora kila upande ukakae kivyake ukajitafakari kwa upya kwa kilichotokea.

Kweli ikawa nmerudi nyumban rasmi,
Baada ya wiki nikarudi normal na mzee akanisihi nikakae full-time kule duka kubwa, ofisi ijirudi kwanza ilipe madeni yake yote, ikitengamaa ndo niendelee na mirad Yake. Kwasasa nimuachie atapambana nayo mwenyewe. Kweli nikaanza kukaa duka kubwa mwnyw full time.

Gafla wife akaanza usumbuf anaomba sn radhi kwa yaliyopita.
Kila mtu wangu wa karibu anaemfahamu, anamfata anamwambia aniombee msamaha.
Anatuma Watu lukuki wanibembeleze.
 
IKAFIKA KIPINDI
Akawa anakuja dukan anakaa chini na mtoto mgongoni kibarazani analia anaomba msamaha sn nimsamehe sn kwa yote aliyonikosea. Anaahidi atajirekebisha Ni shetani alimpitia.simjibu chochote akichoka kuomba msamaha anaondoka zake.

Kuna siku kashinda dukan asbh mpk saa 11 jioni na mtoto mgongoni anabembeleza. Mpk nafunga anabembeleza anabubujikwa na machozi, nilivofunga nikaenda nyumbani. Usiku kaja, kakuta geti halijafungwa kasukuma kaingia ndani na kwenda dirishan kwangu chumban analia anabembeleza nimsamehe. Nikamkaushia.

Kaenda Hadi dirisha la bi.mkubwa analia kakosa anaomba asamehewe.
Bi mkubwa nae akakausha Ila alivoondoka nikashangaa na asivompenda huruma ikamuingia nae akawa ananisihi nimsamehe turudiane. Nikamwambia bi.mkubwa achana nae uyo,hafai.

Tumeenda ukimya juu ya ukimya,
Wife akadili na mzee, kumbe akawa Anaenda kuomba msamaha ofsin kwa mzee. Mzee alipoona imekua kero akaniita na kunambia uyu mwanamke kila Mara anakwenda ofsn kwake kumuomba msamaha na anadai shangaz zake ndo waliomponza anajutia kilichotokea. Naonaje suala la kumsamehe. Nikasema mzee Mimi simtaki tena. Mzee akasema sawa Kama nmeamua hivyo. Ikaisha.

Baada ya miez 3 tangu Lile vurugu. naendelea na shughuli zangu nishaanza msahau wife, mzee akanambia jumapili tutakua na kikao Cha familia saa 10 mchana usichelewe kurudi uwepo. Nikasema sawa. Nikajua yatakua mambo ya familia yetu tu. Kweli Nmefika nyumbani mapema.

Gafla Niko chumban bi mkubwa kaja nigongea kua MDA tayar nije seblen.
Ile Natoka nafika seblen,nawaona wale shangazi zake wameketi, ikanibidi kurudi zangu chumbani na kukaa kitandani nikajiinamia kwa uchungu. Ikawa Kama wamenitonesha upya kile kidonda .

Mzee kaja kaniinua na kunambia twende seblen kila kitu kitakua sawa.
Kweli nmeinuka kinyonge nmeenda seblen nmekaa na mzee kochi Moja kubwa la Watu watatu.

Gafla shangaz Yao mmoja aliekua na mdomo akaja niangukia chonde chonde nimsamehe kwa yaliyopita.
Mzee akaniangalia usoni, nikaona mzee kama anatuma ujumbe kua anajiskia viby jins mmama yule mtu mzima anavolia. Wale wengine wakawa wanasema samahani yaishe yaishe. Babamkwe nae akasema imefkia mahali wife mpk anataka kujiua nyumbani kwao, alishameza hadi vidonge Mara mbili kajifungia chumbani anataka kujiua yye na mtoto. Wakavunja mlango kumnusuru.

Kama familia wanaomba radhi, wametukosea Sana, wanaomba radhi Sana. Anawasiwasi wanakoelekea atampoteza binti Yake na mjukuu wake, binti yake anazurula kila siku mjini na mtoto mgongoni anasema anaaga kaja kuomba msamaha na hasamehewi na kichwa chake kishachanganyikiwa sahv kilivyo tusije kushangaa kagongwa na Gari yeye na mtoto wote wamefariki. Mzee kaniangalia usoni.

Sijakaa sawa, kumbe wife alijificha jikoni nae kaja analia Hadi kamasi macho yamevimba na mtoto wake mgongoni kaniinamia anaomba msamaha. Mzee kaniangalia Tena usoni Tena na kunipa ishara ya nimsamehe. Nikatikisa kichwa kukubali.

Mzee kamuinua wife na kumkalisha kushoto kwake, Mimi kulia kwake.
Akasema kua Hawa wote Ni wanangu. Nyie wote nendeni kila kitu kitakua sawa. Basi wageni wale wakatawanyika.

Tukabaki familia yetu, wife na mtt. nikawa ndani ya siku 2 simuongeleshi.
Bi mkubwa akanisihi yaishe niongee na mzazi mwenzangu, mzee nae akanisihi yaishe bhana. Basi siku ya 3 wife kaja chumbn kwangu kavaa kimitego analia anaomba msamaha.
Kwasababu moyoni nishamsamhe na nilivommiss siku nyng sijapiga show.
Basi ugomvi wetu ukaishia pale.

Baada ya wiki pale home,
Mzee akatutaftia nyumba nyingine kubwa zaidi na kutupangishia kua tukakae uko pale kwa wapangaji tuhame. Alivotupeleka kule tunakutana na vile vitu vyetu tulivosomba na canter vipo vimerundikwa TU sebleni. Wife akaanza kuvipanga upya na maisha yakarejea Kama zamani.

TANGU HAPO miaka mingi imepita na WIFE HAJAWAI TENA KUTAMKA KAULI ILE YA TUGAWANE MALI.

Na pia,
Tangu ugomvi huo alirudi kua mama wa nyumbani na Hadi leo hii nnapoleta Uzi huu hajawai tena kuuza duka langu lolote.

Pia,
Nilikata mguu kabisa na magomeni kule kwa mashangazi waswahili wale.
Japo wanadai ugomvi ulishaisha ila nmekua karibu na ndugu wa wife kule upande wa mama ake na upande wa baba ake, Maelewano mazur Nmebaki na baba mkwe wangu TU. wengine ni salamu TU,kila mtu kivyake.

Nihitimishe kwamba
kile kipind kilipita na kilikua Cha mafunzo sn kwetu kutukomaza na Siwez kumhukumu sn wife maana umri wake ulkua bado mdogo sn, afu mazingira ya uswahili alikokulia kwa mashangazi wale yalimharibu.
Nashkuru upande wa mama ake walinisaidia sn kumshape wife akatulia akawa mcha mungu na MKE mzur Sana.[emoji1431]

Kwasasa
MKE wangu kiumri na kitabia amekua sana. Naweza kusema Ni MKE bora kabisa maishani, naeweza kukaa mbele ya Wanaume wenzangu waliooa nami nakajivunia kua Nmeoa mke bora kabisa na pure wife material mama wa watoto wangu[emoji4]

Na huwa nawaza Sijui ningekaza ningempoteza kipind kile sijui ingekuaje maisha yangu, maana kila nnakogusa Ni chenga tupu. Michepuko wote nilonao, vichwa maji tupu, mamaJ inclusive.

KINGINE,
Najivunia Sana baba mkwe wangu nilie nae, Ni mkwe asiyependa mambo ya kipuuzi kabisa na alisaisaidia Sana kumshape wife miaka 5 ya changamoto ya ndoa yangu.[emoji1431]

SIKU NIKITULIA NTASHUSHA TENA KISA kingine KILICHONIFANYA NIJIVUNIE HUYU BABA MKWE WANGU KATIKA KUMNYOOSHA WIFE WANGU[emoji4]

ASANTENI SANA WAKUU[emoji1431]
#######mwisho######

NB:
Kuna la kujifunza Hapa wakuu
Uzi huu nmeuleta baada ya kuguswa na Uzi wa mdau mmoja mwenye kisa Kama changu, ugomvi wa kibiashara na mkewe, Kisha mkewe akadai talaka wagawane Mali.

NAWASILISHA[emoji1431]
 
IKAFIKA KIPINDI
Akawa anakuja dukan anakaa chini na mtoto mgongoni kibarazani analia anaomba msamaha sn nimsamehe sn kwa yote aliyonikosea. Anaahidi atajirekebisha Ni shetani alimpitia.simjibu chochote akichoka kuomba msamaha anaondoka zake.

Kuna siku kashinda dukan asbh mpk saa 11 jioni na mtoto mgongoni anabembeleza. Mpk nafunga anabembeleza anabubujikwa na machozi, nilivofunga nikaenda nyumbani. Usiku kaja, kakuta geti halijafungwa kasukuma kaingia ndani na kwenda dirishan kwangu chumban analia anabembeleza nimsamehe. Nikamkaushia.

Kaenda Hadi dirisha la bi.mkubwa analia kakosa anaomba asamehewe.
Bi mkubwa nae akakausha Ila alivoondoka nikashangaa na asivompenda huruma ikamuingia nae akawa ananisihi nimsamehe turudiane. Nikamwambia bi.mkubwa achana nae uyo,hafai.

Tumeenda ukimya juu ya ukimya,
Wife akadili na mzee, kumbe akawa Anaenda kuomba msamaha ofsin kwa mzee. Mzee alipoona imekua kero akaniita na kunambia uyu mwanamke kila Mara anakwenda ofsn kwake kumuomba msamaha na anadai shangaz zake ndo waliomponza anajutia kilichotokea. Naonaje suala la kumsamehe. Nikasema mzee Mimi simtaki tena. Mzee akasema sawa Kama nmeamua hivyo. Ikaisha.

Baada ya miez 3 tangu Lile vurugu. naendelea na shughuli zangu nishaanza msahau wife, mzee akanambia jumapili tutakua na kikao Cha familia saa 10 mchana usichelewe kurudi uwepo. Nikasema sawa. Nikajua yatakua mambo ya familia yetu tu. Kweli Nmefika nyumbani mapema.

Gafla Niko chumban bi mkubwa kaja nigongea kua MDA tayar nije seblen.
Ile Natoka nafika seblen,nawaona wale shangazi zake wameketi, ikanibidi kurudi zangu chumbani na kukaa kitandani nikajiinamia kwa uchungu. Ikawa Kama wamenitonesha upya kile kidonda .

Mzee kaja kaniinua na kunambia twende seblen kila kitu kitakua sawa.
Kweli nmeinuka kinyonge nmeenda seblen nmekaa na mzee kochi Moja kubwa la Watu watatu.

Gafla shangaz Yao mmoja aliekua na mdomo akaja niangukia chonde chonde nimsamehe kwa yaliyopita.
Mzee akaniangalia usoni, nikaona mzee kama anatuma ujumbe kua anajiskia viby jins mmama yule mtu mzima anavolia. Wale wengine wakawa wanasema samahani yaishe yaishe. Babamkwe nae akasema imefkia mahali wife mpk anataka kujiua nyumbani kwao, alishameza hadi vidonge Mara mbili kajifungia chumbani anataka kujiua yye na mtoto. Wakavunja mlango kumnusuru.

Kama familia wanaomba radhi, wametukosea Sana, wanaomba radhi Sana. Anawasiwasi wanakoelekea atampoteza binti Yake na mjukuu wake, binti yake anazurula kila siku mjini na mtoto mgongoni anasema anaaga kaja kuomba msamaha na hasamehewi na kichwa chake kishachanganyikiwa sahv kilivyo tusije kushangaa kagongwa na Gari yeye na mtoto wote wamefariki. Mzee kaniangalia usoni.

Sijakaa sawa, kumbe wife alijificha jikoni nae kaja analia Hadi kamasi macho yamevimba na mtoto wake mgongoni kaniinamia anaomba msamaha. Mzee kaniangalia Tena usoni Tena na kunipa ishara ya nimsamehe. Nikatikisa kichwa kukubali.

Mzee kamuinua wife na kumkalisha kushoto kwake, Mimi kulia kwake.
Akasema kua Hawa wote Ni wanangu. Nyie wote nendeni kila kitu kitakua sawa. Basi wageni wale wakatawanyika.

Tukabaki familia yetu, wife na mtt. nikawa ndani ya siku 2 simuongeleshi.
Bi mkubwa akanisihi yaishe niongee na mzazi mwenzangu, mzee nae akanisihi yaishe bhana. Basi siku ya 3 wife kaja chumbn kwangu kavaa kimitego analia anaomba msamaha.
Kwasababu moyoni nishamsamhe na nilivommiss siku nyng sijapiga show.
Basi ugomvi wetu ukaishia pale.

Baada ya wiki pale home,
Mzee akatutaftia nyumba nyingine kubwa zaidi na kutupangishia kua tukakae uko pale kwa wapangaji tuhame. Alivotupeleka kule tunakutana na vile vitu vyetu tulivosomba na canter vipo vimerundikwa TU sebleni. Wife akaanza kuvipanga upya na maisha yakarejea Kama zamani.

TANGU HAPO miaka mingi imepita na WIFE HAJAWAI TENA KUTAMKA KAULI ILE YA TUGAWANE MALI.

Na pia,
Tangu ugomvi huo alirudi kua mama wa nyumbani Hadi leo hii nnapoleta Uzi huu hajawai kuuza duka langu.

Pia,
Nilikata mguu kabisa na magomeni kule kwa mashangazi waswahili wale.
Japo wanadai ugomvi ulishaisha ila nmekua karibu na ndugu wa wife kule upande wa mama ake na upande wa baba ake. Maelewano mazur Nmebaki na baba mkwe wangu TU.
Hao wengine salamu TU,kila mtu kivyake.

Nihitimishe kwamba
kile kipind kilipita na kilikua Cha mafunzo sn kwetu kutukomaza na Siwez kumhukumu sn wife maana umri wake ulkua bado mdogo sn, afu mazingira ya uswahili alikokulia kwa mashangazi wale yalimharibu.
Nashkuru upande wa mama ake walinisaidia sn kumshape wife akatukia vizur Sana.[emoji1431]

Kwasasa
MKE wangu kiumri na kitabia amekua sana. Naweza kusema Ni MKE bora kabisa maishani, naeweza kukaa mbele ya Wanaume wenzangu waliooa nami nakajivunia kua Nmeoa mke bora kabisa na pure wife material[emoji4]

Na huwa nawaza Sijui ningekaza ningempoteza kipind kile sijui ingekuaje maisha yangu, maana kila nnakogusa Ni chenga tupu. mamaJ inclusive.

KINGINE,
Najivunia Sana baba mkwe wangu nilie nae,
Ni mkwe asiyependa mambo ya kipuuzi kabisa na huwa alinisaidia Sana kumshape wife miaka 5 ya changamoto ya ndoa yangu.[emoji1431]

SIKU NIKITULIA NTASHUSHA TENA KISA KILICHONIFANYA NIJIFUNIE HUYU BABA MKWE WANGU KATIKA KUMNYOOSHA WIFE WANGU[emoji4]

ASANTENI WAKUU[emoji1431]
#######mwisho######

NB:
Kuna la kujifunza Hapa wakuu
Uzi huu nmeuleta baada ya kuguswa na Uzi wa mdau mmoja mwenye kisa Kama changu, ugomvi wa kibiashara na mkewe, Kisha mkewe akadai wagawane Mali.

NAWASILISHA[emoji1431]
2023 umefunguliwa na Season Ya Mama G.....
Enyiwei Tugusie kidogo mkesha wa Mwaka Mpya wewe na Mama J ulikuwaje
 
Back
Top Bottom