TWENDE PAMOJA SASA,
Miaka hiyo baada ya masomo,
Mzee wangu aliniamini Sana akanipa biashara yake flan niisimamie na kweli niliisimamia vizur na ikafanikiwa kuzaa biashara nyngn mpya.
Mzee wangu hua sio mchoyo wa fadhila, alininunulia gari Kama zawadi na pia Kama usafiri kurahisisha mizunguko kwny hizo biashara zake nilizokua nasimamia. Nikawa nasimamia bishara za mzee uku nikiwa naishi nyumbani.
Changamoto za biashara ya mzee, ilikua inanikutanisha na warembo sana,wahuni na wapenda starehe wa kila aina hapa mjini. Kwaiyo Kama kijana nikaanza vijitabia flan hivi vya wanawake. Maana MDA mwingi nilikua natembea na pesa mfukoni afu kipind kile ukiwa na usafiri plus umaarufu walikua wanakuja wenyewe.
Biashara yetu Kuna MDA ilikua inadhamini fashion show na mashindano ya warembo n.k yote ilkua ktk kujitangaza,sometimes kupush uuzaji wa vinywaji.
Kwaiyo jina la biashara ya mzee ilikua kubwa,pia langu lilikua kubwa eneo lile maana ndo nilikua msimamizi mkuu.
Kwaiyo suala la kutembea na mrembo nnaemtaka Hata halikua issue maana sikuhitaji kujitambulisha Sana,nilikua nafahamika sana.
Sasa kuna kipind nilipita Kwan mdada flani maarufu sn alikua anagombea umiss ktk wilaya Moja Hapa dar na ile show,mazoezi na maandaliz yote yalilikua yanafanyika kwny ukumbi wetu. Nilivomuona nikampenda Basi tukaanza mahusiano. Mashindano yalivoisha Akawa nafas ya 3 na kwenda kushiriki mbele zaidi na kua maarufu sn hivyo kutokana na umaarufu wa yule dada mahusiano yetu yakajulikana sana town na mzee taarifa zile zikamfikia.
Mzee wangu sio mtu wa kukurupuka,
Aliniita na kuniweka chini kunishauri mambo kadhaa wa kadhaa na kunionya khs tabia niliyoianzisha na hatari niliyomo na pia kipind icho ukiskia ukimwi Ni ukimwi haswa akanipa mifano ya Watu walioangamia kwa Njia niliyoingia Mimi. Kisha akanishauri Kama nmeshindwa Ni Bora nitafute mwanamke nioe atagharamia mahali na kila kitu mwenyewe. Mahusiano Yale yafe haraka sn na hii tabia ya umalaya ife Mara Moja.
Always sipendi kumwangusha mzee wangu,nikamuahidi nitalifanyia kazi nipe MDA kidg. Mzee akasema sawa. Baada ya kukaa Nikachambua ktk list ya wanawake wengi nilokua nao,nikaibuka na binti mmoja mrembo sana, ila maisha yake ya kawaida Sana sio mtu wa Bata na umri wake miaka 19 na very submissive kwangu, ana heshima, adabu na utii Sana japo huwa namzingua sometimes ila nikiangalia moyoni mwake ananipenda Sana na kweli naona naweza kummudu na sio wale wa kwenye umiss,fashen show n.k
Basi nikaanza kumuweka karibu binti,
Nilipompa wazo binti kutaka kumuoa akakubali na kwenda kumtambulisha rasmi kwa wazee. Baada ya utambulisho Mzee na bi mkubwa walisita Sana maana binti hakua amesoma sana na alitoka mazingira flan ya kiswahili sana uko magomeni.
Bi mkubwa alimkataa Moja kwa Moja, ila mzee nikivomfafanulia akanielewa maana mzee wangu ananiamini Sana.
Bi mkubwa alimkubali binti tu kwa shinikizo la mzee, maana mzee akishasema ndio final say ya familia nzima na kweli mzee kalipa mahali, harisi na ndoa ikafungwa tukaanza kuishi pamoja na wife pale nyumbani.
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]