Mke aliyefiwa na mama yake mzazi lazima amuombe ruhusa mumewe kabla ya kwenda msibani? Je yapi ni masharti yanahusika?

Mke aliyefiwa na mama yake mzazi lazima amuombe ruhusa mumewe kabla ya kwenda msibani? Je yapi ni masharti yanahusika?

Yaani kama kuna dini ipo serious inatoa compendium yenye haya maelekezo sasa ninaamini maneno ya Carl Max kwamba Religion is opium of people! Huu ni wivu wa kipuuzi kabisa na umewekwa kwenye maandishi ili kuhalalishwa.
 
Ruhusa ya nn,ni anatakiwa mpa taarifa mmewe sio ruhusa.
 
Mods, hili siyo suala la kisiasa. Peleka kule kwenye jukwaa la social issues kuna wataalam wa masuala ya ndoa huko watamsaidia Mwanajamii mwenzetu.
 
Wadau hamjamboni nyote?

Kichwa cha habari chahusika hapo juu

Je ni lazima mke amuombe ruhusa mumewake Ili aweze kwenda Kwa msiba wa mama yake mzazi? Je Mumewe anayo haki ya kumkatalia ombi lake?

Masharti gani? Aya zipi?

Wenye ilimu na wanatheolojia mkuje mtupe madini
Kidini:Nzuri kuomba ruhusa,Kwa waislamu ukiolewa sahau kuhusu wazazi wako.Inatakiwa kumshirikisha alie kuoa kwa kila change Moto Japo si kila change Moto useme....
Wenza Mume na Mke kuombana ruhusa pia ni tabia njema na baraka..
 
Nadhani mtoa mada amekusudia kwenye mazingira ya kiimani zaidi.....

Nadhani suala hili ungeliuza kwa wanachuoni pahala unapoishi au viongozi wa kidini kutokana na itikadi yako....

Hapa jukwaani kwa siku hizi sio sehemu sahihi kwani kumekuwa uwanja wa kejeli hata kwenye mambo ya msingi hasa yanayogusa Imani.....

Katika upande wa uislamu.... mwanamke hatoi taarifa bali anomba ruhusa kwa mumewe....na mume anaweza kukataa kulingana mazingira ya jambo lenyewe au wao wenyewe ingawa kibinadamu na kiungwana haitakuwa na picha nzuri.......

NB:
Niko tayari kusahihishwa katika maelezo hayo......
 
Aiseee watu mnaishi dunia ipi. Huo muda na nguvu za kuomba ruhusa atapata wapi kwanza
 
Mke akifiwa na Mama yake ina maana Mme amefiwa na Mama mkwe na Watoto wamefiwa na Bibi.
Mara,nyingi Mke akifiwa na Mama anaelemewa na majonzi. Automatically Mme anakuwa na jukumu llisilokwepeka la kuhusuka na msibani kwa Mengi na si ruhusa tu.
MMe anapaswa kuchukua Majukumu ya msibani kwa nafasi yake akisaidiana na ndugu wengine .
Kwa mantiki hiyo nafasi ya kuombana ruhusa haionekaniki.

KUjibu swali mahusi lililoulizwa Inatakiwa mke aombe ruhusa.
 
Kutoa taarifa kwa mumewe yatosha - tena kawaida waondoke wote na mumewe kwenda msibani.
 
Hii nadhani hata Wamachame au Wamarangu wanayo. Hata ukipewa ruhusa kule kwenye msiba inabidi ukalale kwa upande wa watu wa mume wako na sio kwenu
 
Mke akifiwa na Mama Mzazi, huo msiba Mume unamhusu kabisa. Kwani naye amefiwa na Mama Mkwe..

Sijaelewa hiyo Ruhusa wanaombana ya nini wakati ni msiba unawahusu wote?
Huu mtego walifungwa wale wanawake viburi wenye vijicent vyao,wakifiwa hao tayari msibani hata bila taarifa kwa mume wake!!
 
Misiba hutukuta katika hali yoyote kunamsiba unaweza kuwakuta huku mkiwa mbali kifamilia mf. Mume yuko mbali kikazi hivo inakua si rahisi yeye kufika haraka msibani.hivo basi ikiwa mama watoto wako atawahi kupata tasrifa ya msiba wa baba yake nishart ahakikishe amekujulisha kabla yakufunga nyumba nakupandisha watoto kwenye gari kwenda msibani.
Hii nikanuni na desturi nzima yamaisha nasio vinginevyo.
Naikitokea hakuna mawasiliano baina yamume namke walio naubali kidogo yampasa mwanamke afanye subra walau siku3 huku akitafuta mawasiliano namumewe ilikumpa taarifa yakuondoka.
Nawewe mwanaume nihaki ya msingi kumpa ruhusu mkeo nakushiriki moja kwamoja kwenye majanga yatakayo wagusa wanafamilia wote.
mkuu siku tatu kwenye msiba wa mama yake? si atakuta wamezika? msiba wa mama mkwe ni wa wote mambo ya kuombana ruhusa yanayoka wapi, kama uko mbali sio ruhusa ni taarifa kwamba huku tumepatwa na msiba
 
Kwa Mujibu wa Dini ya Kiislamu Hairuhusiwi Na Ukinyimwa Ruhusa Huezi kwenda
 
Hapo inapimwa busara ya Mume!!
Hapana Kwa Dini Ya Kiislamu Ruhusa Ya Mwanamke Si Busara wala Ombi Ni lazima ndiyo Aqida yake na Ndiyo FiQHI inavyotaka na Sharia pia..

Nakumbuka Kuna Riwaya (Hadithi) Moja Nimeisahau Baadhi ya Vipengele.. Ila Inazungumzia Kuhusu Mke aliyezuiawa kwenda Popote na Mumewe Wazazi wake wakaumwa Sana..

Akaenda kaka yake Kumuambia Kuwa Mama anaumwa sana na Hajiwezi, akamjibu kaka Yake Kuwa Hawezi kuondoka Nyumbani kwakuwa Hajapewa Ruhusa hiyo..

Hali ikazidi kuwa Mbaya Na nyumbani mama Yake akawa anamuhitaji maana Alitaka Kukata Kauli kaka Mtu akaja Huku analia anamuomba Aende Binti akalia Sana ila Akasema Siwezi kuja Mume wangu hakunipa Ruhusa...

Ikabidi Waongozane Mpaka Kwa Mtume MUhammadi (S.W.A)...

walipofika kwa Mtume kaka mtume akamuombea ruhusa Dada yake kwa mtume (Maana Mumewe alikuwa Amekwenda Vitani)..

Mtume akawaambia Kama Mumewe ndo kamyima Ruhusa Hata yeye hana Mamlaka ya kuvunja Amri ya mumewe..

Kwahyo kaka mtu akasepa..

Yule Mzazi akafariki...Kaka mtu akarudi tena akamsihi bhasi twende hata tukamsitiri Mzazi ila msimamo ulikuwa Pale pale..

Yule kaka Akaenda kwa mtume Akalia na kumsihi sana ila mtume akamwambia Hana mamlaka hayo japo Na yeye anasikitika sana..

Walipozika Mtume akasema kuwa Wazazi wake wamesamehewa madhambi Kutokana na Imani kubwa na Heshima aliyo nayo Mwanawe
 
Mtoa mada analenga kitu kingine kwenye swali lake! Sema amekuwa si muwazi!

Hoja yake ni kuhusu utii wa mke kwa mume, hasa kwenye Uislam.
Yes, uislam unamtaka mke kuomba approval ya mumewe anapotaka kwenda popote!

Washereheshaji wakakazia kwa kusema hata kama ni msibani kwa mama yake!

Hoja kuu hapa ni utii wa mk kwa mume! Sio swala la msiba wa nani!

Kwa hali ya kawaida kukiwa na taarifa ya mama yake mke kufariki, kabla mke hamjafanya lolote lazima atamtaarifu mumewe, na hakuna mume atakataa hili!

Labda ikiwa ni ndoa ya washenzi!
Na si ajabu akajua hiyo taarifa kabla ya mkewe.
 
Back
Top Bottom