Mke aliyemuua Mwalimu huko Kilombero apandishwa kizimbani

Medecin

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
8,221
Reaction score
22,496
Mahakama ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro imewapandisha kizimbani na kuwasomea shtaka watu watatu akiwemo Jovina Steven Mwekya (33), mkazi wa Mang'ula ambaye ndiye mke wa marehemu Mwalimu Tungaraza, Musa Amani Mwakyoma (28), mkazi wa Mang'ula, na Tadei Sales Mwinuka (40), mkazi wa Mang'ula, kwa kosa la mauaji.

Wakisomewa shtaka hilo na mwendesha mashtaka wa serikali, Dastan William, mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Regina Futakamba, amesema mnamo usiku wa Juni 2, 2024, wakati marehemu akiwa amelala chumbani, watuhumiwa hao walipanga njama ya kumvamia chumbani kwake na kumpiga na kitu kizito kichwani, hivyo kusababisha kifo chake.

Aidha, baada ya kusomewa shtaka hilo, watuhumiwa hao wamerudishwa mahabusu mpaka tarehe 25 Juni, 2024, itakapotajwa tena.

PIA SOMA:
- Morogoro: Atuhumiwa kula njama kumuua mumewe ili ale raha na bodaboda


Team kataa ndoa wanazidi kupata points za kugomea kuoa au kuolewa.
 
Mbona ize tu, angemuambia ebwanaee mi sikutaki nimelipata bwana jingine la kunitimizia haja zangu we sepa. Jamaa angesepa tu kuliko kupoteza uhai. Siku hizi mwanamke akileta za kuleta wanaume huwa hatutaki makubwa huwa tunasepa na kwenda kuanza maisha kwingine upya japo inauma sana ila maumivu hupoa baada ya miaka mingi kupita ukikaa muda mrefu bila kupata mke mwingine. Wanawake wakianza kuonesha dalili mbaya ya kuhatarisha ndoa ni bora wakimbiwe mapema
 
hyo boda mwenyewe alivo na sura mbaya ila wanawake sijui wana shida gan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…